Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,370
- 39,186
Nimekuwa nikisubiri ripoti hii ya Human Development na hatimaye ndio imetoka. Ukiwasikiliza watawala wetu inaonekana kuwa Taifa letu linapiga hatua kubwa ya maendeleo na wananchi wafurahie! Mgogoro wangu na Lowassa ulianza pale alipodai kuwa Tanzania inapaa, na mimi nikasema kama inapaa basi waliopaa ni viongozi huku wananchi wakiwa wameachwa kipawa wameduwaa!
Mojawapo ya ripoti inayopima maendeleo ya watu (siyo vitu) ni ripoti hii ya Umoja wa Mataifa. Kati ya nchi 177 zilizoangaliwa Tanzania imetoka kuwa nchi ya 162 na kuwa 159.. Je huku ndiko kupaa alikozungumzia Lowassa?
Kwanini baada ya FDI tunazoingiza, sifa tunazopata toka wakubwa n.k mbona inapofika kwenye kupima vinavyopimika hatuonekani? Mbona Uganda wametoka kwenye "Low Human Development" na sasa wako kwenye "Medium Human Development"? What are we doing wrong? Au hizi zote ni njama za wapinzani ambao hawataki kutoa pongezi kwa viongozi wanapofanya vitu vizuri?
Angalia hapa ripoti hizo na ulinganishe mwenyewe