Warudisha chenji mna siri gani?

njeeseka

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
1,371
976
Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu mpangilio wa noti pindi ninavyorudishiwa chenji zangu ninaponunua bidhaa na bado naendelea na utafiti.

Kuna siku moja ghafla nilipata wazo la kuangalia chenji baada ya kufanya manunuzi; nilitoa elfu kumi na kununua bidhaa na nilirudishiwa elfu sita yaani elfu tano moja na elfu moja, yule aliyerudisha aliweka elfu tano juu na elfu moja chini. Baadae tena nilinunua vocha ya elfu moja baada ya kutoa elfu kumi, chenji chenji nilipewa elfu tano juu na elfu mbilimbili chini yake.

Nimeendelea na utafiti na jambo hilo.limejitokeza mara kwa mara nikitoa elfu kumi chenji zinarudishwa kwa mpangilio wa iliyo kubwa inawekwa juu na zenye thamani ndogo zinawekwa chini.

Leo nimefanya manunuzi nimerudishiwa elfu saba zikiwa ktk mpangilio km ninavyoueleza ( nimekuwekea picha chini). Mpangilio huu umenishtua kwani mimi kwa kawaida ninapangilia pesa kubwa chini na ile dogo naweka juu, sasa hii imekuwa kinyume chake ndio maana ninashtuka, sina hakika kama wanaorudisha chenji huwa wanakosea au mipangilio yao iko sahihi au kuna jambo lipo nyuma ya pazia.

Nimeleta hapa jamvini ili kama kuna mtu anaelewa lolote karibu tujuzane, km huelewi pia ruksa kuuliza au kuweka nyongeza/nyamanyama...
IMG_20171103_161640.jpg
 
Mimi mbona naenda sokoni daily na chenji narudishiwa kinyume chake..coincidence
 
Inawezekana ila wananitisha kwa nini kila mrudisha cheji ananijaribu? Mimi sijaribiwi....ha ha haaa
mkuu una sehemu umevurugwa si bure kwa kawaida pesa kubwa huonekana haraka so huwa wanatafuta ndogo halafu kubwa hufuata nadhani ndiyo maana mpangilio unakuwa tofauti ha ha ha ha
 
mkuu una sehemu umevurugwa si bure kwa kawaida pesa kubwa huonekana haraka so huwa wanatafuta ndogo halafu kubwa hufuata nadhani ndiyo maana mpangilio unakuwa tofauti ha ha ha ha
Ha ha haaa kwa uzoefu wako hii inawezekana, na huu ukata sisi wengine tumezoea ndogo inakuwa juu ili tuwahi kuitumia
 
Back
Top Bottom