Warning: Uzushi kuhusu hayati Chacha Wangwe na Deus Mallya ukome!

Kama kuna siri au Hakuna Siri juu ya marehemu chacha wangwe Mungu ndie anajua tu ! Na kama kuna Jambo la siri na la kweli ndugu rafiki au mtanzania yeyote analihisi lina ukweli alete hapa JF tulipime uzito wake kisha tunamwachia mungu tu

Mwulizeni Mtikila.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ni muda mrefu sasa umepita tangu tuondokewe na mwanasiasa maarufu aliyetikisa sana ndani ya chama chenu cha Chadema.Kinachonifanya nimkumbuke na niingiwe mashaka na sera zenu,ni namna mnavyokazana kueneza hasira na chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao na polisi.Siasa zenu ni kama zile za enzi za akina Musolin ambao walikuwa radhi kuangamiza bunge zima ili kupata uhalali wa kutawala na kutenda maovu dhidi ya maadui zao kisiasa.Chadema kila kukicha mnakuja na sera za ajabu ajabu! Mara mnaanzisha vikundi vya kujilinda,mara eti mmerushiwa mabomu! (kitu ambacho naamina mnaandaa wenyewe) yote haya kupata huruma ya wananchi na kupata kuungwa mkono kwa kutumia damu za watu wasio na hatia! Nalazimika kukumbusha kuhusu Chacha Wangwe kwa kuwa amekufa wakati amejiandaa kuja Dar kusema siri nzito dhidi yenu! Najiuliza je,mlimtoa uhai ili asiseme kuhusu haya yanayojiri sasa!? Na kama sivyo mbona mko bize sana kuligawa taifa? Mnatupeleka wapi? Siwaelewi!

Akili zako na chama zinafanana kwa kila kitu,kama unaweza kuandika upuuzi kama huu bila hata kushituka!nikushauri wewe una chama chako,unakiamini pamoja na kukipenda pamoja na maovu mengi yakiwemo,na wengine tuna chama tunachokiamini kuwa kitawaondoa watz kwenye dimbwi la ujinga,maradhi na umaskini kwa hyo unachokiamin we sisi hatuwez kukiamin baki na chama lako na siye na cha kwetu.
 
Kelele nyingi bila mpangilio wa sauti. Ni kama taarabu za Komba

Ni muda mrefu sasa umepita tangu tuondokewe na mwanasiasa maarufu aliyetikisa sana ndani ya chama chenu cha Chadema.Kinachonifanya nimkumbuke na niingiwe mashaka na sera zenu,ni namna mnavyokazana kueneza hasira na chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao na polisi.Siasa zenu ni kama zile za enzi za akina Musolin ambao walikuwa radhi kuangamiza bunge zima ili kupata uhalali wa kutawala na kutenda maovu dhidi ya maadui zao kisiasa.Chadema kila kukicha mnakuja na sera za ajabu ajabu! Mara mnaanzisha vikundi vya kujilinda,mara eti mmerushiwa mabomu! (kitu ambacho naamina mnaandaa wenyewe) yote haya kupata huruma ya wananchi na kupata kuungwa mkono kwa kutumia damu za watu wasio na hatia! Nalazimika kukumbusha kuhusu Chacha Wangwe kwa kuwa amekufa wakati amejiandaa kuja Dar kusema siri nzito dhidi yenu! Najiuliza je,mlimtoa uhai ili asiseme kuhusu haya yanayojiri sasa!? Na kama sivyo mbona mko bize sana kuligawa taifa? Mnatupeleka wapi? Siwaelewi!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ni kabisa jamaa alikufa akielekea dar kuja kusema siri zetu za gavana wa benki kuu daud balali kutangazwa amekufa huku akiendelea na maisha ktk kisiwa kimoja huko marekani.
 
wanataka kuleta ishu ya kwamba majaji hawakuwa fair walipotoa hukumu ilhali upande wa pili wanasema majaji wanauwezo na uzoefu wa kutosha ilimradi tu kupinga hoja ya lissu......hawa jamaa ni kizunguzungu sana.....
MBONA HAMTUAMBII ILIPOPELEKWA ILE computer mpakato(laptop) ya CHACHA WANGWE???
nadhani imepelekwa kulekule ilikopelekwa ya MWIGAMBA
 
Warning bila kuonesha hatua ama kuonesha madhara ya kukiukwa hilo onyo ina maana gani
 
Deus Mallya ameshindwa kuanzisha urafiki na Zitto Z Kabwe?!!

Body without head
 
hiyo onyo mbona huonyeshi kwa unaitoa kama nani au umetumwa na nani hasa funguka usione aibu kazi ni kazi
 
Salaam!
Mnamo Tarehe 5/03/2012 Mahakama ya Rufani Dodoma ilitoa hukumu ya Rufaa kati ya DEUS MALLYA v/s JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (Criminal Appeal no. 52/2010). Hukumu hiyo iliyopinga maamuzi ya Criminal Appeal no.34/2009 iliondoa Hatia na hukumu zote za awali zilizomtia hatiani Ndg.DEUS MALLYA juu ya makosa aliyoshtakiwa nayo na kutiwa nayo hatiani ambayo yalikuwa ni.

(i) Causing Death throug dangerous Driving
(ii) Driving a motorvehicle without a valid driving licence.
Hukumu hiyo ilitolewa na jopo la Majaji watatu ambao ni.
1.The Honourable Mr. Justice H.R. Nsekela - JA
2.The Honourable Madame Justice N.P. kimaro - JA
3. The Honourable Mr. Justice B.M. Luanda - JA

Kwa muda mrefu sasa tumeshuhudia wanasiasa uchwara wakiendelea kunasibu tatizo la kifo cha Hayati Wangwe (R.I.P) kwa namna wanavyotaka. Pia vijana wepesi wa hoja na masikini wa kufikiri wamekuwa wakitumia msiba ule hadi leo kwa mambo ya hovyo hovyo!..

Ni busara kama mtu akikosa cha kuandika ajisomee vitabu au alale badala ya kuendelea na upotoshaji usiokubalika katika jamii ya kistaarabu.

What is behind the curtains?
 
kama lilivyo jina lako hata kabla hujaonekana tu umeshajishtukia mwenyewe Jina lako tu loh? Ulitakiwa kutoa ufafanuzi tu kama ulivyoanza wewe ni msemaji wa familia hiyo? Au kama nikazi ya njaa pia sio makosa yako tutakuelewa tu kwamba hiyo yaweza kuwa miongoni mwa ajira za serikali sikivu na chama cha zamani
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom