WARNING:Ukipata Ujumbe huu tujulishe ASAP

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Kuna member ana nick ya "Sikazi" amekuja na njia moja ya Spamming ambayo niwafahamishe members wengine kuwa ikitumika kwenu bila hiari yenu tufahamishe HARAKA iwezekanavyo.

Ujumbe huo unakupa link ya kuweza kujaribu kuingia kuona "passwords" za watu wengine; Ukijaribu kufuata link hio inaweza kukufanya uoneshe password yako kwa yeye na hivyo kucompromise your privacy. JF haitauliza password yako au kutuma email ya kutaka kuoneshe password yako KWA SABABU YEYOTE ILE. Tunauwezo wa kureset password yako bila ya kuuliza password ya zamani.

Kwa wale ambao walienda kujaribu kufungua link hiyo hakikisheni mmebadilisha password zenu kupitia CP.

Spamming of any kind is strictly not allowed on JF! Katika pitia PM zangu nimekumbana na malalamiko toka kwa members wawili mchukia fisadi na Yebo Yebo ambao kusema kweli ndo wamenishtua nikaamua kufuatilia na kugundua katuma ujumbe wa aina hii kwa members wengi zaidi kama waonekanavyo chini hapa:

  • Sanda Matuta
  • Timtim
  • womenofsubstanc
  • Tonga
  • naimaomari
  • Kasheshe
  • Yebo Yebo
  • WildCard
  • QM
  • mchukia fisadi
  • Kana-Ka-Nsungu
  • Jasusi
  • Bubu ataka kusema
  • Alinda
Huyu simfungii. Namwacha ili kuona kama yeye ataweza kui-access account yake tena. Please do report such spammers thru your profiles and Private Messages to us so that we take action ASAP.

Banning is not the only solution for such people!

Kind regards
 
Last edited by a moderator:
I'll advice all members who accessed the link and tried to log with their password to immediately change their passwords.
 
.......sasa ina maana keshaingia na kutumia password za watu wengine?
 
Sidhani kama mtu anaweza kuingia unless kama kuna mtu amejaribu kuingia na kucheki passwords za watu.
 
Sidhani kama mtu anaweza kuingia unless kama kuna mtu amejaribu kuingia na kucheki passwords za watu.

.......sasa ina maana keshaingia na kutumia password za watu wengine?
..Hapana ndugu Ogah, hiyo aliyotoa Mkjj ni tahadhari. Just in case, hiyo link inampeleka mtu kwenye site nyingine ambayo inakuwa na remote server na kuna key stroke capture malware installed. Halafu huyo mtu anakuwa na traffic analyser na anakuwa amezi-index links zote alizowawekea watu hapa JF. Hivyo kama amedhamiria anaweza kabisa kusikilizia mtu ana type nini na ni member yupi, kisha baada ya log in kadhaa akagundua password ya mtu.

Ni exercise ngumu kufanya na mtu inabidi awe na mshiko mkubwa kuweza kufanya kitu kama hicho... Tahadhari ndiyoo muhimu zaidi. Mambo ya online huwa hayako assured by 100%.

Hivyo kama alivyosema Mkjj, iwapo mtu ame click hiyo link, basi ni bora tu kubadilisha password, iwapo alitembelea link kisha akalog out halafu aka log in tena JF hali hiyo site bado iko active, halafu cache na cookies zinakuwa bado hazijawa deleted.

Nyongeza:

Ikitokea kuwa umetembelea link fulani hivi hapa JF, halafu ghafla unajikuta automatically umekuwa logged out... basi ni muhimu KUTO-log in mara baada ya kuwa logged out. Ukikumbana na tukio kama hili ukiwa una surf JF ni bora kutoa taarifa mapema kwa: webmaster(at)jamiiforums.com. Hata kama una surf websites nyinginezo wasiliana na wamiliki wa sites hizo mapema. Kabla ya hivyo, hakikisha kuwa una clear cookies zako zote kisha unafunga browser yako mara moja. Hii ni tahadhari mojawapo katika kuepukana na washenzi wanaoweka key strokes capture software... hivyo wana ku-direct kwenye website zao kupitia hizo link, kisha scripts zinakuwa executed ambazo zinalazimisha ulog out kule uliko kuwa. Kwa vile ni natura instinct ku-log back on... basi hapo ndipo wanapokukamatia... maana wanakuwa wanaku-monitor wewe vizuri zaidi kwa kusikilizia yote unayotype.

Kingine ni kwamba, ni vizuri kuwa na tahadhari kuhusiana na sites mbalimbali ambazo unaweza ukakutana nazo na zinakuwa na link za websites ambazo wew ni member. Ifahamike kuwa nyingi ya websites zinazoweka links ni safe... na ukitaka kujua kwa haraka link iko okay, ni kuangalia kwenye window chini pale unapoweka mouse kwenye link hiyo full address ya link hiyo inakuwa inaonekana. Basi chukua tahadhari tu kuwa link unayoclick itakupeleka kule unako kusudia na si kwingineko. Maana wanaweza wakasema kabisa, tembelea jf kwa kubonyeza hapa..., badala yake kumbe link ile inakuwa inakupeleka kf (kifoforums.com)!! :(

Usiku mwema. Ngoja nijinyoshe kusubiria shamrashamra za kesho, suit yangu nimeshapiga pasi, mapanga yamejichonga hayooo hata inzi hathubutu kutua na kuacha kuumbuka.... :).
Kwa wale mlio click, Poleni kama mtakuwa mmekwazwa na huyo muhuni.

SteveD.
 
Shukran sana SteveD and have a nice weekend bro.
Sisi pia hapa tunatamasha la African World Festival na tutajimiksi na
nguvu hapo kesho.Subiri picha kama kawa!
 
Kwa nini huyu mtu asitajwe na wengine tumtolee uvivu. Watu wengine bwana....sijui wana mashetani gani. Poleni wote mliolengwa.
 
Yeah mimi nimeipata hiyo PM. Kitu cha kwanza kilichonijia akili kuwa inaweza kuwa ni mtego wa virus. Na kwa sababu nilikuwa natumia computer ya kazini, basi nikaogopa kufungua hiyo link.

Asanteni kwa tahadhari.
 
Mimi ninachouliza huyu mtu anataka nini? mimi ni mmojawapo niliyopata hiyo msg na nimeifungua sasa sijui what to expect next. Mi nashauri huyu mtu aonywe na kama anajulikana aumbuliwe tu, anachokitafuta kwenye account za watu ni nini kama sio uzushi! bwana Sikazi (whoever you are)mind you own damn business. Watu wengine hatustahili kuwa nao katika kundi hili.
 
Wakuu, msitie shaka. Hivi vitu vinaweza kuwachanganya wengi ila ukweli ni kuwa HAKUNA member hata mmoja anaweza kuingia kwenye account ya mwingine na kuitumia au kuitumia JF kuzima pc zenu ama kuwatumia virus kwa namna yoyote. Ni suala la kuwa-threaten watu na wala msihangaike kubadili passwords.

Anyway, kuna kitu zaidi nafanya maana wapuuzi kama hawa ni wengi. Kuanzia kesho kila kitu kitakuwa tofauti na alivyotarajia huyu.

Naomba muda kidogo tu...

There's nothing to worry about!
 
Nimepokea hiyo mail ila ni kama nyingi nyenginezo za wanaojifanya wajuaji nimeignore.

Asante mkuu
 
" Desclaimer: You are responsible for your own action. Don't blame this page if you get caught or sued"

This statement alone scared me .... alikolala ndiko nilikoamkia ... tena anakuambia kabisa "siri yako usimwambie mtu" sina haja ya kumchunguza yeyote yule ... ajaribu kwengine
 
Huyu ni mshamba sana tena anaharufu ya kifisadi maana nusu nimtapikie kwa kichefu chefu.
 
Huyu mtu anahangaika sana, hata mimi amejaribu sana wiki hii ila hakujua masikini ya Mungu kuwa nilijua kuwa hii ndio itakuwa his next step kwa hiyo toka juzi nimekuwa na mtaalamu wa IT hapa kwangu akimchezea yeye, najua huko uliko mkuu unachechemea na hiyo computer yako, pole sana maana JF umeikuta na utaicha kama vile na sisi tulivyoikuta,

JF mbele, wanachama nyuma ukijaribu kinyume utaishia kuchekesha.
 
Lakini hata nyie mliojaribu kwenda huko ili mujue passwords za wengine mulikuwa mnataka nini? kwi kwi kwi!!!

Naona umbea ulikuwa mbelembele kutaka kufahamu Mwafrika wa Kike ni nani? Invisible siku nyingine uwaache tu wakumbane na mkenge wa virus ndio wajue umbea haulipi kwi kwi kwi!!!
 
Bwana SIKAZI alikuwepo kwenye harusi ya MAX.

Tena alikuwepo toka kanisani mpaka ukumbini!

Sasa ndio mshindwe kushangaa, ila haina neno, tuna m monitor kwa karibu.
 
Back
Top Bottom