Warithi wa Tibaijuka, Mwijage, Rweikiza, Asumpta via CDM wajulikane mapema; Mukoba atamvaa Kagasheki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warithi wa Tibaijuka, Mwijage, Rweikiza, Asumpta via CDM wajulikane mapema; Mukoba atamvaa Kagasheki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Sep 7, 2012.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kuna maswali mengi miongoni mwa Wanachadema katika majimbo ya Muleba Kusini, Kaskazini, Bukoba vijijini, Nkenge na Bukoba mjini kuhusu nani wa kuwatoa wabunge walioko sasa katika uchaguzi wa 2015. Wanachama wanapenda kujua mapema nani ataweza kuwatetea vilivyo kupitia CDM hasa baada ya CCM kuanza kupoteza Muelekeo.
  Kule Kwenye jimbo la Nkenge haijulikani nani ataweza kuipeperusha bendera ya CDM, kuna jamaa mmoja alitaja jina la somebody Malinzi nisijue kama ni Jamal au Dioniz watu wakasema kuwa wale ni ccm damu.

  Upande wa Muleba Kaskazini, Kusini, Bukoba vijijini bado wanachadema hawajajua nani atatangaza nia ili maandalizi yaanze mapema na sio kuibuka mwishoni ghafla na kujitoa kama ilivyokuwa kwa Focus kule nkenge.

  Kwa Bukoba Mjini wadau wanasema Gratian Mukoba atapambana na Kagasheki na ana Mvuto kuliko Rwakatare Wilfred. Sijui wadau wengine wanalisemaje ili. Walau Mukoba akitajwa walio wengi wanakubali kuliko kumtaja Rwakatare tena.

  Kwa hiyo wale wote wenye lengo la kuwaondoa wabunge wa ccm walioko hivi sasa inabidi wawe na long term plan.....mje kwa wadau tuanze kuwapa mikakati mapema mjue wapi waliopo wamekosea ili mtumie nafasi hizo. mambo ya ghafla sio mazuri. Njooni mpime upepo muone mnakubalika vipi sio mnatoka mijini sijui nje ya nchi bila hata kuyajua mzaingira vizuri ati mnaomba kuchaguliwa njooni mapema tena kimya kimya then tuone kama tutawaondoa wezi wa raslimali za nchi hii madarakan hasa CCM.
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Wabunge wenyewe watachukia kusikia au kuona maandalizi haya lakini wajue boti iliyowabeba inatoa harufu ya uvundo hasa huku nje hata kama huko ndani ya Chama wamepulizia Nivea Deodorant ili wajifanye hawasikii uvundo. Kama group members wako ni wauaji ni ngumu wewe kukataa kuwa sio muuaji
   
 3. C

  CRITO Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ta Muganyizi nakuunga mkono juu ya kupata watu wanaijiandaa mapema. Nakuunga mkono pia kuwa Lwakatare asigombee bukoba mjini. Lakini nakuonya wewe na CHADEMA kuwa MUKOBA ni kibaraka wa serikali na hafai kuwa mgombea wa chadema. Andaeni vijana smart hatutaki mazee haya yamelelewa na mfumo. Mukoba ukimwona anafoka unaweza danganyika, lini umeona yeye binafsi amegombana na serikali? "Migomo huwa anaiitisha pale kunapokuwa na vuguvugu la uchaguzi na anapotaka kuondolewa kwenye nafasi aliyonayo kwenye chama cha walimu.

  Kwa ujanja sana mnakumbuka alivyoahirisha mgomo mara ya kwanza na kuwahadaa walimu? na mnakumbuka alivyoacha loopholes za kisheria juzi na kubatilisha mgomo? na mnakumbuka alivyokubali mara moja kutangaza walimu warudi shuleni?

  na unajua kuwa huyu ni fisadi anayedhulumu walimu bila huruma? kwa nini walimu wanalazimishwa kuwa wanachama wa cwt naye anakaa kimya? Huyu ni kibaraka.kwa nini bukoba nao wasijifunze kutoka kwa majimbo kama arumeru,arusha,kawe ubungo,nyamagana,mbeya,na kwingine. Kwani hakuna vijana wadogo wanaoweza kusaidiwa kugombea na kubadili wazee hawa? mukoba na lwakatare wote hawafai.tafuteni kijana bukoba mjini.

  Uchaguzi uliopita chadema ilishindwa hasa kwa sababu vijana hawakupiga kura.namna nzuri ya kuwafanya wapige kura ni kuweka kijana mwenzao na mkamuunga mkono. Shida nasikia ninyi wahaya ni wanafiki sana. Sijui mtafanyaje
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Teh teh teh, eti Gracia Mkoba amtoe Kaghasheki.
   
 5. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Mbona Rwakatare alikuwa mbunge wa CUF mapema huku bukoba kabla ya maeneo hayo uliyoyataja? Hilo unafiki kipimo chake sikijui. Sijui kule Dodoma ambako wabunge kibao ni CCM unafiki wao ni kiasi gani. Mie nilitegemea utataja nani anafaa badala ya huyo Mukoba unayemsema. Na nimesema waje au wajitokeze mapema ili mapungufu kama hayo uliyoyasema. Kama unafununu nani atatangaza nia wewe tutajie. Ila wale wapiga kura hapa wanampa chapuo.
   
 6. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Mwana umechekaaaa..............Mamaisara bana .....nani sasa atamrithi....Dr Bana au...tehetehete
   
 7. C

  CRITO Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ta muganyizi naelewa unachosema. Na wala usihadaike kudhani wewe tu ndiyo una access na hapo bukoba mjini.najua ni vipi jina la mukoba linatajwa hapo bkb mjini ni kweli. Lakini kwa nini kurisk kuweka kibaraka mtu asiyeaminika? Hebu ona watu kama prof kahigi kule shinyanga, alikuja chadema ili apate ubunge basi, lakini yeye amelelewa na ccm na kama siyo kuombwa na wananchi ahamie chadema ili wamchague,basi asingegombea. Na unaona alivyo, kama siyo mfuatiliaji huwezi hata kujua kama ni chadema.wapo akina selasini, ni masalia ya mifumo ya ccm,akina shibuda,eeh.

  Lwakatare kuwa mbunge kabla ya vijana niliowataja wa majimbo mengine ni sawa.lakini amezeeka,na anazo kasoro nyingi sasa zisizomuuza tena kwa wapiga kura.nakuhakikishia kama lwakatare atagombea,ccm watashinda saa 4 asubuhi. nMukoba anaweza kushinda ila hatakuwa mtu wa kuaminika, zaidi atakuja kuleta migogoro kwenye chama cha chadema.

  Sasa kwanini kujiweka katika hatari? imani yangu na kadri ninavyoona hali ya siasa jimbo la bukoba mjini,chadema inahali nzuri kupata mbunge,muhimu aletwe kijana asiyekuwa na makosa bado na anayeweza siasa za kizazi kipya.wewe ta muganyizi unataka kusema kuwa kwa hiyo zaidi ya hao wawili mukoba na lwakatare hakuna mtu mwingine yeyote anayetajwa,uwe unamjua au haumjui?

  Kagasheki anaweza asigombee ubunge.kama ataamua kugombea kwa sababu tu amepewa uwaziri basi kutakuwa na mpasuko wa pili kwenye kambi yao,wa kwanza ukiwa ni ule wa mzee wa pale juu,na sasa atafarakana na meya,na hiyo itasaidia kidogo upande wa chadema. Muhimu kwa sasa chadema wangekuwa na programu za kuwa karibu na watu hasa vijana na akina mama.pia madiwani wa chadema wasiendelee kuvuruga kwani tutahitaji kupata madiwani.

  Kuhusu unafiki ninaelewa maana ya relativism,lakini maoni yangu hayo ni objective kuwa wahaya na hasa hapo mjini ni wanafiki.wanasema hili wanatenda lile. Kama wewe ulikuwepo uchaguzi uliopita usingedhani Lwakatare angeshindwa ubunge. Unafiki wenu ulisaidia sana kumpa ushindi Kagasheki hata wewe Muganyizi kama kweli unawasikiliza watu wa kawaida huwezi kusema eti anayetajwa ni Mukoba tuuu, labda kama na wewe unataka kuanza kumpendekeza, maana ndo siasa zenyewe.
   
 8. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na mleta hoja kuhusu umuhimu wa wagombea kujitokeza mapema,na nakubaliana na CRITO kwamba baadhi yetu tuna tabia za kinafi,na niongeze roho mbaya! Nimewahi kuandika kwamba Kagera kama hatutachangamkia mageuzi,tusilalamike baada ya CCM kuangushwa kwamba tumetupwa pembezoni ya utawala utakaokuja!
   
 9. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hiyo title bana, teh teh teh teh... mi kudhani Tibaijuka ataka kuolewa tena na sasa anatafutwa nshikaji katika hao nshomile teh teh teeeeeeeh! Njoo nikuzawadie kipande cha ngolombe kilichokaushwa. Utapenda.
   
 10. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Wewe naye una mambooo tehteheteheteheteheteheteeeeee
   
 11. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Nidokeze basi kama una fununu watu wa kurithi watu hawa.
   
 12. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Hakuna unafiki pale .......Rwakatale alikuwa kapoteza kabisa mvuto. Mtu anakunywa Rubisi na Nkonyagi hadi anapoteza ....watu walikuwa wamesha mdharau. Pia tabia ya akina mama wa Kihaya wana tabia ya Kumchagua Kagasheki na Kikwete ati wana sura nzuri. Pamoja na hayo nahitaji wa kuleta mabadiliko..... niwajue mapema maeneo husika ili nitumie mwanya wa ofisi niliyopo ya kuzunguka maeneo yote nikusanye maoni ya wananchi juu yenu. Kama mnaogopa kujitaja basi mni PM
   
 13. C

  CRITO Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wa uchaguzi mkuu uliopita bukoba mjini kuna kijana alikuwa akihutubia kila mkutano wa chadema na watu walimpenda sana na ni machachari, kasoma sayansi ya siasa na utawala, ualimu na alisoma falsafa, mnamkumbuka lakini? Kijana alipambana uso kwa uso na kagasheki hadi siku ya mwisho. Alikuwa mratibu na msaidizi wa lwakatare wakati ule.

  Amewahi kuja hapa kuendesha mafunzo na halima mdee kwa vijana wa chadema wakati wa maandalizi ya mchakato wa katiba mpya, kwa wanaokumbuka alivyokuwa gumzo hapa akitafsiri barua zile za mheshimiwa kagasheki za ufisadi za kiitaliano,sema nimesahau jina lake.Nadhani atakuwa ameshamaliza chuo kikuu sasa.

  JE ta muganyizi hudhani kama vijana kama huyo wasio na kashfa yoyote wanaweza kusimama na kubeba chADEMA BUKOBA MJINI?
   
 14. C

  CRITO Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SASA lwakatare bado anaonyesha anataka kugombea.nani na wakati gani ataambiwa ukweli huu kuwa asigombee? maana ni kweli pia kuwa kwa nafasi yake ya sasa ya mwenyekiti mkoa na mkurugenzi wa ulinzi wa taifa anazo nguvu kwenye chama kiasi kwamba mgombea yeyote wa chadema ni lazima apate uungwaji mkono na lwakatare kama anataka kufaulu,maana bado watu wapo ambao wanaamini katika lwakatareeism,hasa aliotoka nao CUF.

  Ta muganyizi,unajua na lwakatare anaitwa muganyizi,je utatusaidia kumweleza mwajina ukweli huu?
   
 15. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kama ni kumchana ukweli tayari wa jina Tumemweleza hata Slaa siku moja alimwambia kuwa inabidi apambane sio kunywa rubisi tu. Huyo Kijana uliyemsema inabidi aje mapema tuanze kuandaa njia na kupima mtazamo wa wapiga kura juu yake. Waje mapema hili ni muhimu. Itakuwa ngumu M4C kuandaa wanachama wakati wakupigiwa kura hawajaeleweka. Kura zetu zinaweza kwenda kwingine. Huyu Kijana wa Political science aje maana tutashare common knowledge ili tujue tutumie mikakati ya Nicolo Machiavelli au la
   
 16. C

  CRITO Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini sasa nadhani unatia chumvi,wajina siyo wakunywa rubisi bwana au unaanisha kalinyaeeee.Ngoja nitafute jina lake huyu dogo nawewe hebu jaribu sasa kuulizia kwenye mjadala uwezekano wa vijana kama hawa.ni vigumu sana akina mukoba kuwa hawana kadi za ccm,wasingedumu hivyo kwenye nafasi zao
   
 17. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Tatizo la bukoba kuna unafiki mwingi kama mdau mmoja alivyosema hapa.halafu kuna katabia ka kuwazalau vijana hasa kama hujaoa na unakaa nyumbani kwa wazazi.kuna mzee mmoja (Mzee Ruangisa) ana miaka zaidi ya themanini,mwaka 2010 alikuwa anagombea na kijana mmoja wa chadema kata ya kitendaguro huyo mzee alishinda pamoja na kwamba ameongoza kata hiyo zaidi ya miaka 30 hajafanya lolote.kijana huyo alikuwa anajua kujenga hoja na watu walionyesha kumkubali lakini mwisho hawakumpigia kura.
   
 18. FOR 2015

  FOR 2015 JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 539
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanabodi,

  Nimekuwa nikisubiri hii kwa muda mrefu....Ta Muganyizi ahasante sana....binafsi sitatangaza leo ila niatweka nia by 2013 tuombe tu uzima...Jimbo tarajiwa ni kwa Mama Tibaijuka lazima nipambane nae!NO WAY.

  Mimi nina BSC na sasa nafanya MSC Agricultural Economics. Nimeajiriwa since 2008 baada ya kumaliza Chuo. Naomba Ta Muganyizi na wadau wengine mniunge mkono mara tu nikitia nia.....Nawasiliana na Mhe. Conjester Rwamlaza kupata pia ushauri wake
   
 19. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  mkuu sina fununu kuhusu akina nani wanataka kugombea. Inawezekana bado wanapima upepo ukizingatia vuguvugu la M4C halijafika huko.
   
 20. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #20
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kunywa rubisi wala kalinya si tatizo tatizo ni kupoteza ukaanzisha na ugomvi na mwishowe ukakamatwa kwa muda si vizuri
   
Loading...