Warioba: Wananchi wanahoji mamlaka ya Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba: Wananchi wanahoji mamlaka ya Rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Aug 10, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,812
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba amesema moja ya mambo yaliyohojiwa na wananchi wengi katika mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba Mpya ni mfumo wa uongozi na utawala, hasa mamlaka ya uteuzi.

  Amesema katika mikutano ya ukusanyaji huo wa maoni iliyofanyika katika mikoa saba ikiwamo Kusini Unguja na Kusini Pemba, wananchi walihoji madaraka aliyonayo Rais katika uteuzi wa nafasi mbalimbali zikiwamo za watendaji wakuu wa taasisi za Serikali.

  Kauli hiyo imekuja wakati Tume hiyo ikiwa imemaliza awamu yake ya kwanza ya kukusanya maoni ya wananchi huku ikitarajia kuendelea tena na zoezi hilo katika mikoa mingine saba, kuanzia Agosti 26 mwaka huu.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba alisema wananchi 188,679 walihudhuria mikutano ya Tume kati yao 46,620 walitoa maoni yao.

  Alisema watu 17,440 walitoa maoni kwa njia ya kuzungumza na 29,180 kwa njia ya maandishi.
  Alisema katika mikutano hiyo wananchi walihoji masuala mbalimbali likiwamo la mfumo wa uongozi na utawala wakielekeza katika kutaka mabadiliko katika utezi wa wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wengine wa Serikali.
  "Wananchi walihoji uteuzi wa nafasi mbalimbali ndani ya Serikali likiwemo suala la uteuzi wa wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wengine wa Serikali," alisema Jaji Warioba na kuongeza;

  "Wananchi wameonyesha wazi kwamba wanataka Katiba ya aina gani, wana uelewa mkubwa kuhusu maisha yao kuliko tunavyodhani, hata wasomi nchini wanatakiwa kutambua wazi kwamba, wakitaka kujua wanachokitaka Watanzania waende vijijini kuwasikiliza wananchi."

  Kwa mujibu wa katiba iliyopo wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wengine wa juu wa Serikali wakiwamo jaji mkuu, wakuu wa mashirika na taasisi nyeti za Serikali utezi wake hufanywa na Rais.
  Alisema kuwa mambo mengine ambayo wananchi hao walitaka yaingizwe katika Katiba Mpya ni pamoja na masuala ya ardhi, kilimo, elimu, huduma za afya, hifadhi za jamii, nafasi ya utoaji wa haki na madaraka ya wananchi.
  Alisema kuwa licha ya kuwa Watanzania wengi hawaijui Katiba ya sasa, lakini maoni waliyoyatoa yanaendana na vifungu vilivyomo katika Katiba hiyo.

  Alifafanua kwamba licha ya kuwa muda wa miezi 18 ambayo imepewa tume hiyo kuwa mdogo, ni lazima tume hiyo ifanye kazi kwa umakini ili uchaguzi wa mwaka 2015 ufanyike huku kukiwa na Katiba Mpya.
  "Tunapenda sana uchaguzi wa 2015 ufanyike wakati nchi ikiwa na Katiba Mpya na lazima tufanye kazi hii ndani ya muda uliopangwa" alisema Jaji Warioba.

  Onyo

  Katika hatua nyingine, Jaji Warioba alivitaka vyama vya siasa, mashirika ya dini, wanaharakati na asasi za kiraia kuacha kuingilia uhuru wa wananchi kutoa maoni kwa kuwataka wafuate misimamo ya vyama, taasisi na asasi zao.
  Jaji Warioba alitumia mkutano huo kuzitaka asasi za kiraia, vyama vya siasa, wanaharakati na mashirika ya dini kuacha tabia ya kuwaelekeza wananchi cha kuzungumza wakati wakitoa maoni.

  Alisema sheria ipo wazi kwamba makundi hayo yakitaka kutoa elimu kwa wananchi yanatakiwa kutoa taarifa kwa Tume, huku akisisitiza kuwa hata vikipewa nafasi hiyo viitumie vyema na sio hiyo kuwapangia wananchi cha kuzungumza.

  Aliongeza kuwa kutokana na waumini wa dini ya kiislamu kuwa katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kuwepo kwa sensa ya watu na makazi, tume hiyo imeamua kusogeza mbele tarehe ya ukusanyaji wa maoni, itaendelea na zoezi hilo kuanzia Agosti 26 mwaka huu.

  Alisema mikoa ambayo Tume itakwenda kukusanya maoni ya wananchi katika awamu hii ya pili ni Lindi, Mwanza, Kigoma, Mbeya, Katavi, Morogoro na Ruvuma.
  Katika awamu ya kwanza Tume hiyo ilikusanya maoni katika mikoa ya Pwani, Dodoma, Manyara, Kagera, Shinyanga, Tanga, Kusini Unguja na Kusini Pemba.
   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hapa wananchi wamelenga maana rais wetu anatumia urais kutuumiza huku akiwasaidia marafiki zake hata wasio na maana. Ukiangalia uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya na majaji utagundua hili. Wengi ni washikaji wake na wafadhili wake au watu wake aliowatumia kwenye wizi wa EPA. Lazima tupunguze madaraka ya rais maana siku akitokea chizi au msanii kama sasa nchi itayumba zaidi na inavyoyumba.
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,812
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  mbona sioni hoja yoyote kuhusu muungano hasa kutoka pemba wakati tume ilipokuwa huko??
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280
  Hapa Warioba sio mkweli wazanzibari/wapemba hawawezi kosa kutoa hoja ya muungano. ujue kuwa Warioba hatatenda haki hata kidogo. Hiyo ni dalili mbaya. hamna katiba mpya hapo ya watu bali ya CCM. This is a remarkable observation!
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,812
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo jaji warioba naye ameshajipaka tope la ccm la kuchakachua katiba ???mzee anazeeka vibaya au ???
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Tunapenda ikifika 2015 katiba mpya iwe tayari kwa uchaguzi mkuu!

  Hii tume ya Warioba tayari inajijengea mazingira ya kusema kuwa muda waliopewa ni mchache, ingiza na visingizio vya ramadhani,sensa, misiba...itafika 2015 watasema kazi haijakamilika.

  Hii ya buluu ilikuwa awataje tu CCM inayotaka wanachama wake waunge mkono serikali mbili, huku CCM ikisahau kuwa hawa wanachama pia ni wananchi wenye misimamo na mawazo yao huru.

  Hatutaki katiba ya vyama,tunataayarisha katiba ya nchi.

  Agosti 2012...2013, 2014, 2015 katiba mpya haijakamilika, tutafanya nini wadau?
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Hayo ya madarakabya rais si sana kule visiwani kulalamikia,suala la Muungano ndio kubw sana kule na muundo wake....pamoja na watendaji wa muungano na wa zanzibar na madaraka yao na nguvu zao.....(Mfano waziri mkuu na yule waziri kiongozi..mipaka yao ya utendaji na nani mkubwa zaidi)
   
 8. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,812
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  nguvu ya umma itaamua!!
   
 9. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Warioba asipindishe maneno. Wananchi wanahoji teuzi za Jakaya sio Rais, nchi yetu hajiwahi kupungukiwa na imani kwa rais wetu kama kipindi hiki.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Kweli Rais ana madaraka makubwa na kama akiamua kuweka marafiki zake, tunaopata shida ni sisi walipa kodi pale serikali inaposhindwa kufanya kazi. Teuzi za Rais ingekuwa bora ziwe zinathibitishwa na bunge.
   
 11. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ndio maana na yeye kaanza kuanguka anguka kwenye mikutano kwa kisingizio cha uchovu kumbe mipombe
   
 12. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Warioba amenza vibaya. Kitendo cha kuzungumzia maoni ya watz juu ya suala la Muungano ni dhahiri kwamba anatekeleza agizo la Jk la hakuna kuzungumzia muungano. Tumeanza kupungukiwa imani naye na maoni yetu. Mimi nimehudhuria mikutano ya Tume zaidi ya 8 na muundo wa Muungano lilikuwa suala muhimu kwao.
   
 13. T

  Tata JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,744
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280
  Sasa kama wananchi wa vijijini wana uelewa mkubwa kiasi cha jaji kuwashauri wasomi wakawasikilize inakuwaje tena anatoa onyo kwa vyama vya siasa, mashirika ya dini na asasi za kirais zisiingilie uhuru wa wananchi wa kuongea? Mimi nadhani wananchi hawa wananaweza kabisa kuainisha pumba na mchele toka kwa hizi asasi.
   
 14. only83

  only83 JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba amesema moja ya mambo yaliyohojiwa na wananchi wengi katika mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba Mpya ni mfumo wa uongozi na utawala, hasa mamlaka ya uteuzi.

  Amesema katika mikutano ya ukusanyaji huo wa maoni iliyofanyika katika mikoa saba ikiwamo Kusini Unguja na Kusini Pemba, wananchi walihoji madaraka aliyonayo Rais katika uteuzi wa nafasi mbalimbali zikiwamo za watendaji wakuu wa taasisi za Serikali.

  Kauli hiyo imekuja wakati Tume hiyo ikiwa imemaliza awamu yake ya kwanza ya kukusanya maoni ya wananchi huku ikitarajia kuendelea tena na zoezi hilo katika mikoa mingine saba, kuanzia Agosti 26 mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba alisema wananchi 188,679 walihudhuria mikutano ya Tume kati yao 46,620 walitoa maoni yao.

  Alisema watu 17,440 walitoa maoni kwa njia ya kuzungumza na 29,180 kwa njia ya maandishi.

  Alisema katika mikutano hiyo wananchi walihoji masuala mbalimbali likiwamo la mfumo wa uongozi na utawala wakielekeza katika kutaka mabadiliko katika utezi wa wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wengine wa Serikali.

  “Wananchi walihoji uteuzi wa nafasi mbalimbali ndani ya Serikali likiwemo suala la uteuzi wa wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wengine wa Serikali,” alisema Jaji Warioba na kuongeza;

  “Wananchi wameonyesha wazi kwamba wanataka Katiba ya aina gani, wana uelewa mkubwa kuhusu maisha yao kuliko tunavyodhani, hata wasomi nchini wanatakiwa kutambua wazi kwamba, wakitaka kujua wanachokitaka Watanzania waende vijijini kuwasikiliza wananchi.”

  Kwa mujibu wa katiba iliyopo wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wengine wa juu wa Serikali wakiwamo jaji mkuu, wakuu wa mashirika na taasisi nyeti za Serikali utezi wake hufanywa na Rais.

  Alisema kuwa mambo mengine ambayo wananchi hao walitaka yaingizwe katika Katiba Mpya ni pamoja na masuala ya ardhi, kilimo, elimu, huduma za afya, hifadhi za jamii, nafasi ya utoaji wa haki na madaraka ya wananchi.

  Alisema kuwa licha ya kuwa Watanzania wengi hawaijui Katiba ya sasa, lakini maoni waliyoyatoa yanaendana na vifungu vilivyomo katika Katiba hiyo.

  Alifafanua kwamba licha ya kuwa muda wa miezi 18 ambayo imepewa tume hiyo kuwa mdogo, ni lazima tume hiyo ifanye kazi kwa umakini ili uchaguzi wa mwaka 2015 ufanyike huku kukiwa na Katiba Mpya.

  “Tunapenda sana uchaguzi wa 2015 ufanyike wakati nchi ikiwa na Katiba Mpya na lazima tufanye kazi hii ndani ya muda uliopangwa” alisema Jaji Warioba.
   
 15. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  “Tunapenda sana uchaguzi wa
  2015 ufanyike wakati nchi
  ikiwa na Katiba Mpya na lazima
  tufanye kazi hii ndani ya muda
  uliopangwa” alisema Jaji
  Warioba...mmm! hii kauli ya walioba inatia mashaka...nadhani Lipumba alikuwa sahihi kupendekeza iudwe tume huru ya uchaguzi ili kama mchakato wa katiba mpya utakuwa bado haujamilika kufikia 2015,basi tuwe na tume huru ya uchaguzi itakayo simamie uchaguzi wa 2015...kwa kauli hiyo ya Walioba matarajio yangu ya kuuona uchaguzi wa 2015 ukifanyika kwa katiba mpya yameanza kufiia kwa kasi...
   
 16. p

  pembe JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hii tume imeshakuwa ya CCM sasa. Tunataka tunachotaka sisi sio inachotaka tume. Yako mengi tu yanatakiwa ktk katiba mpya (ingawa wao wasema marekebisho ya katiba) ila kuu ni mamlaka mkubwa ya rais na suala la muungano. Tume isikilize na itoe ripoti sahihi ili bunge la katiba liweze kupitisha kitu cha kweli. La sivyo nguvu ya umma itawaumbua.
   
 17. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280
  only83
  Na hii ni kutokana na abuse of power aliyoionyesha Mkuu wa nchi katika teuzi mbali mbali aprticularly wakuu wa Mikoa na wilaya. tazama Chiku Galawa tanga, she is a dictotor of the century!Unawapeleka wafanyakazi mahali hakuna nyumba na unasema mwende hata majumbani mlikozaliwa hakuna nyumba. So silly a statemtn to your fellow human beings!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Haya madaraka kwa enzi za Nyerere it was okey but hawa waliofuata hasa mwenzetu wa sasa sijui ni TISS wanamislead au yeye anakaidi ushauri wa TISS maana kuna viongozi wanateuliwa mpaka unashangaa ata UYU!
  Na ivi viti maalumu Warioba vip hawakuongelea wananchi maana watu wanavaa vikuku bungeni na kujishebedua tuu!
   
 19. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Huyu Mwenyekiti wa tume ya katiba anadai kuwa wananchi wanawekewa maneno midomoni mwao hasa kuhusu madaraka ya Rais. Je, yeye hajawekewa maneno haya mdomoni mwake? Je, tayari anavipengele ambavyo hataki vibadilike? Hivi sio kwamba wananchi wanatoa maoni yao kutokana na elimu waliopewa na wanasiasa na watu wengine kama activists? Sasa kuongea hivyo sio kuminya uhuru wa kutoa maoni?

  Sources: TanzaniaDaima 10/08/2012 and Mtanzania 10/08/2012.
   
 20. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Warioba hasemi kweli hapa baali anataka kuwazuga tu Watanzania.

  The Intelligent mind can clearly read from his tiny mind what he(Warioba)and Team members in their committee are planning for CCM Government and Tanzanians!.

  Kuna kauli moja ameitoa amabayo hakika inakera.Kwamba kuna vyama vya Siasa,NGOs na Wanaharakati wanawafundisha Wananchi mambo ya kwenda kusema kwa manufaa yao! Hapa simwelewi kabisa Warioba. Kuna ubaya au dhambi gani ya kufanya hivo???Warioba lazima ajue kuwa kuna Watanzania wengi sana hawaijui hata Katiba iliyoko kwa sasa. Kwa hiyo Watanzania wanatakiwa wafundishwe na hawahawa Wanasiasa,Wanaharakati na NGOs maana ndiyo wasomi na wenye kujua Katiba na Sheria zilizopo kwa sasa. Hawa ndiyo wanajua sheria ipi ni nzuri na mbaya na ipi ifanyiwe marekibisho! Kwa hiyo wana haki ya kuwafundisha watu ili wajue nini cha kuzungumza mbele ya Tume ya Warioba.

  Lakini inavyoelekea Warioba na Tume yake na CCM yake wana agenda ya siri hapa. Wao wanajua kabisa Watanzania wengi ni mbumbumbu wa Katiba kwa hiyo basi wanataka kutumia ujinga huo wa Watanzania kuchomeka na kuendeleza sheria zilezile za kipuuzi ili kuendelea kuwakandamiza na kuwanyonya Wadanganyika! Tumesikia Tume ikiwahoji maswali wananchi wanaowasilisha maoni yao kama vile ni Mahakamani. Hii ni kutaka kuwadadisi Wananchi ili kutaka kujua ufahamu wao na kama wamefundishwa cha kusema! Huu siyo utaratibu hata kidogo. Na katika hili watanzania tusikubali. Kazi ya Tume ni KUKUSANYA MAONI NA SIYO KUHOJI NANI KASEMA NINI NA KWASABABU GANI.

  Warioba aache Wananchi wafundishwe Katiba hii ya sasa waifahamu na wachague yepi mazuri na yepi mabaya hatimaye waamue namna Katiba yao Mpya inatakiwa iwe.
   
Loading...