Warioba - Viongozi waoga kutoa maamuzi magumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba - Viongozi waoga kutoa maamuzi magumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 25, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba
  Katika hatua nyingine; Jaji Warioba alisema kuwa kuna tatizo la baadhi ya viongozi kuogopa kutoa maamuzi magumu kwa kuogopa kulaumiwa.
  Alisema kuna wakati yanatokea mambo ambayo inaonekana dhahiri maamuzi magumu lazima yafanyike, lakini wahusika wanashindwa kufanya hivyo kwa kuogopa kulaumiwa. "Viongozi wanashindwa kutoa maamuzi magumu kwa kutaka kuwapendezesha baadhi ya watu, hapana unapofika wakati wa kuchukua uamuzi mgumu serikali inatakiwa kufanya hivyo bila kuogopa kulaumiwa, kuna mambo ya maendeleo yanayohitaji maamuzi magumu," alisisitiza Warioba.

  Alisema kuna dalili kuwa kampeni zimeshakuwa suala la kudumu kutokana na malumbano ya viongozi kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.

  “Mnamaliza kampeni badala ya kuanza kushughulikia masuala ya maendeleo watu wanaanza kampeni za uchaguzi ujao sasa hapo maendeleo yatapatikana sa ngapi,” alihoji Warioba.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kiongozi shupavu mwenye kujali haki na maslahi ya Taifa Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitakiwa kuchukua hatua za kashfa ya Jairo siku bunge lilipokosa imani naye na kuikataa bajeti.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  sidhani kama anastahili sifa hiyo uliyompa! PINDA NI JOKA LISILO NA SUMU!
   
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,822
  Likes Received: 2,302
  Trophy Points: 280
  Waziri mkuu ndiyo mtendaji number one wa serikali sasa ukiwa na waziri mkuu mwoga kama pinda andika maumivu. Amesahau wakati wa Kambarage operation vijiji vya ujamaa - Kawawa prime minister alifanya kazi kubwa sana.

  Kumbuka enzi za Kambarage wakati Moringe akiwa Waziri mkuu - zoezi la wahujumu uchumi lilikuwa ni zito sana ila lilifanyika.

  Sasa pinda wewe utakumbukwa kwa lipi? kulia bungeni mauaji ya albino? Kwanza juzi pale pale Bungeni ungemsimasiha kazi Jairo ili JK ajue ala kumbe kuna kifaa nimekiacha home kinaitwa Pinda.

  Hata kama haripoti kwako na protocal zinakuzia lakini mtu akija anga zako wewe unafagia tu - Unakumbuka Lowassa alivyomfagia yule mkuu wa wilaya aliyekaa na mahindi ya msaada ofisini kwake bila kuyapeleka kwa walengwa?
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,199
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Haya ni kweli kabisa. Hivi kampeni wanazofanya kina Nape sasa hivi uchaguzi utafanyika tarehe ngapi ya mwezi gani?

  .
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Dongo kwa Kikwete hilo.
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,199
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Haya ni kweli kabisa. Hivi kampeni wanazofanya kina Nape sasa hivi uchaguzi utafanyika tarehe ngapi ya mwezi gani?

  .
   
 8. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ingekuwa vema kama nae angefanya uamuzi mgumu wa kutuhabarisha ni kioongozi gani katika ishu ipi au zipi ameshindwa kufanya maamuzi magumu na kwa namna gani tumwajibishe........hapa ndipo ninaamini maamuzi magumu ni rahisi kutamani mwingine ayafanye na sio 'MIMI' kuyafanya
  mix with yours
   
 9. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hao viongozi waoga ni akina nani?......kila mtu viongozi waoga viongozi waoga....tumechoka.....kama nyie sio waoga tajeni majina kudadadeki
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,574
  Likes Received: 4,688
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee hajitakii mema ngoja Kikwete na misukule yake wamsikie uone watakavyomtukana.
   
Loading...