Warioba, Salim wazungumzia kumbo la upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba, Salim wazungumzia kumbo la upinzani

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kilimasera, Nov 4, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MAWAZIRI wakuu wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji mstaafu Joseph Warioba, pamoja na mwanadiplomasia wa Kimataifa, Dk Salim Ahmed Salim, kwa nyakati tofauti wametoa maoni yao kuhusu nguvu ya vyama vya upinzani kutwaa majimbo mengi ya uchaguzi.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mahojiano maalumu na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) juzi, Warioba alisema CCM imepoteza majimbo si kutokana na upinzani, bali ni matatizo yaliyojitokeza ndani ya chama chenyewe.

  “Nafikiri ndani ya CCM kura za maoni zilileta mgawanyiko.“

  Kwa mujibu wa Warioba, hivi sasa kuna mwamko pamoja na hamasa kwa wananchi ambao
  sehemu nyingine wamesikiliza sera za vyama hivyo na wamedhani wakiwapa ridhaa wanaweza kufanya mabadiliko.

  “Nadhani kuna mwamko…tulitokea katika historia ya chama kimoja na wananchi walielewa hicho chama, itikadi yake na sera zake na hasa vijijini walikuwa wamezoea hivyo,” alisema.

  Hata hivyo, mwamko wao wa kule kupata fursa ya kusikiliza hizo sera za vyama vingine,
  umewachukua muda mrefu kuchukua uamuzi wa kufanya mabadiliko.

  “Ninaona vyama vya upinzani wanavyoongoza, kwa mfano Mwanza, mahali pazito pale, wanaingia vijana waliozalizwa miaka ya 1970 …na hata ukiona kwenye mikutano, vijana wameamka na hii ni dalili nzuri kwani vijana ndiyo nguvu ya Taifa,” alisema.

  Warioba alisema kuwa vijana ndiyo wanaoleta mabadiliko na kwamba ukikuta mahali mawazo ya vijana na wazee yanafanana, ujue hapo pamedumaa.

  “Lazima vijana wawe na mtazamo mpya tofauti na wazee, watachukua uzoefu wao na kuanzia hapo, lazima pawe na mabadiliko,” alisisitiza Warioba.

  Naye Dk. Salim, akitoa maoni yake kupitia TBC juzi, alisema wakati umefika kwa CCM kujifanyia tathimini ya mambo mbalimbali.

  Alisema uchaguzi umekwenda vizuri, licha ya kuwepo kwa dosari za hapa na pale ambapo hata wachunguzi wa kimataifa waliokuwepo nchini, wameridhika na ulivyofanyika
  kwa utulivu na amani.

  Pamoja na kuzungumzia mambo mbalimbali juu ya uchaguzi huo, Dk Salim ameshauri CCM sasa ifike mahali ijitathimini na akaongeza kuwa upinzani kushinda katika baadhi ya majimbo si jambo baya.

  “Tunazungumzia demokrasia, kuiimarisha demokrasia, hilo halina wasiwasi wowote …kuna mahali vijana wetu wanashinda na maeneo mengine, pengine ndugu zetu upinzani wanashinda,“ alisema Dk Salim.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hawa ukitazama wanapoonge hivyo kwenye Tv, ujue ndani sana ya mioyo yao wana zaidi ya hayo waliyothubutu kuyatamka hadharani!
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni kweli wao ni kama wametoa mawazo yao lakini wameshindwa kuweka wazi kama CCM wataendelea na mwenendo huu kiama chao hakipo mbali!!!!!!!
   
Loading...