Warioba: Nchi Hivi Sasa Inayumba!

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,666
22,674
VIONGOZI wastaafu na wasomi nchini wamesema hivi sasa taifa linakabiliwa na viashiria vya uvunjivu wa amani hali inayosababisha nchi kuyumba.

Kutokana na hali hiyo wamesema ni muhimu kudhibiti amani hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Walikuwa wakizungumza Dar es Salaam jana katika mkutano uliandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere unaojadili amani na umoja wa nchi.

Jaji WariobaAkizungumzia hali ya amani, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba, alisema hivi sasa nchi imekuwa na viashiria vingi vya uvunjifu wa amani jambo ambalo linawezakuhatarisha maisha ya wananchi.

Alisema kuibuka migogoro baina ya wananchi na Serikali ni miongoni mwa sababu za dalili ya uvunjifu wa amani.

Jaji Warioba ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema viongozi wanapaswa kukaa pamoja na kujadili sualahilo.¡°Hivi sasa kuna baadhi ya watu wanapendakujitambulisha kwa ukanda, ukabila, udini na uongozi jambo ambalo ni hatari kwa wananchi kwa sababu linaweza kuleta ubaguzi.¡°

Hali hii ilikuwapo kabla ya uhuru ambako Serikali ya Mkoloni ya Uingereza iliweza kuwabagua wananchi jambo lililosababishaviongozi waasisi na wananchi waliokuwapokipindi hicho kupigania uhuru.¡°¡-baada ya kupata uhuru, Serikali ya awamu ya kwanza ilitunga sheria ya uraia ambayo iliweza kuondoa ubaguzi wa rangi,ukabila na ukanda na kuwaunganisha wananchi, kutafuta viongozi na kutumia lugha moja ya kiswahili,¡± alisema Jaji Warioba.

Alisema kuwapo vitendo hivyo ni lazima Watanzania wajue kwamba amani iliyokuwapo ilitafutwa hivyo wanapaswa kuienzi na kuidumisha iweze kudumu.

Amani ikitoweka kuirudisha ni kazi, hivyo basi tunapaswa kuienzi na kuhakikisha inadumu vizazi kwa vizazi,¡±alisema.Dk. SalimWaziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Dk. Salim Ahmed Salim, alisema Watanzania wengi wana hofu kuhusu uvunjifu wa amani hivyo ni lazima hatua zichukuliwe nchi isipoteze sifa ya kuwa kisiwa cha amani, umoja na utulivu.

Uvunjifu wa amani unatokana na migogoro ya siasa, hali ya uchumi, tofauti za dini na kabila na hata kutotenda haki kwa wote pamoja na kupuuza msingi mkuuwa usawa wa binadamu.

Hivyo tumeona umuhimu wa kufanya mkutano huu kwa sababu ya wasiwasi walionao Watanzania kuwa tusipochukua hatua zinazostahili sasa taifa letu litapoteza sifa za msingi ambazo zinaifanyaTanzania iwe kisiwa cha amani,¡± alisema Dk. Salim.

Akitoa mfano wa nchi za Afrika zilizopotezasifa ya kuwa na amani kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kondo (DRC), Libya, Sudan Kusini, Misri, Somalia, Burkina Faso na Burundi, alisema mifano hiyo inatosha kuwa funzo kwa Tanzania juu ya athari za uvunjifu wa amani.¡°

Tujifunze kutokana na matatizo yanayowakumba wenzetu. Haya yanaweza kutokea Tanzania kama hatutakuwa makini, viashiria vya uvunjifu wa amani vikiachwa viendelee taifa litaangamia na hakuna atakayepona,¡± alisema Salim.

Askofu NgalalekumtwaAkizungumza katika mkutano huo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, alisema amani ya nchi ni ya kila mtu endapo itavunjika kila mmoja atawajibika kwa nafasi yake.¡°

Kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kudumisha amani ya nchi, ikiwa tutaruhusu ivunjike hakuna atakayepona, hivyo basi kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha tunailinda na kuidumisha amani iliyopo,¡±alisema.

Alisema kutokana na viashiria vinavyoonekana hivi sasa ndani ya nchi ni ukweli usiopingika kwamba wananchi wasipokuwa makini nchi inaweza kwenda kubaya.

Alisema kutokana na hali hiyo, wanapaswa kutoruhusu viashiria hivyo viendelee katikajamii bali ni kuikemea na wananchi kuendelea kudumisha amani.

PROFESA SHIVJI Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Kavazi la Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji, alisema imefika wakati kama taifa, watu wajiulize viashiria vya kutoweka kwa amani vimefikaje?¡°

Tujiulize kama nchi ina viashiria vya kutoweka kwa amani tujiulize tumefikaje hapa na kama tukibaini kuna tatizo ni lazima tuanze kufikiria namna ya kupambana navyo kabla havijatufikisha kubaya.

¡°Hatuwezi kujifariji kuwa sisi ni kisiwa cha amani wakati leo kuna viashiria vya kuvunjika kwa amani nchini.

Ni jukumu letu kama taifa kusimama wote kwa pamoja na kusema hapana kwa wale wanaoweza kutugawa na kuiharibu amani yetu,¡± alisema Profesa Shivji.

Profesa LipumbaMwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba, alisema uvunjifuwa amani unatokana na vitendo vya Serikali kutotenda haki kwa wananchi jambo ambalo limesababisha kutoaminika kwa wananchi.

Alisema hadi sasa hakuna uwazi katika uwajibikaji wala utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayohusu jamii na taifa kwa ujumla, jambo ambalo limechangia kujitokeza migogoro baina yake na wananchi.

Serikali imeshindwa kutenda haki kwa wananchi jambo ambalo limesababisha kujitokeza kwa migogoro.

Kutokana na hali hiyo serikali inapaswa kuwa wazi na kuhakikisha kuwa inawashirikisha wananchi katika mambo mbalimbali ya taifa na jamii,¡±alisema.

Profesa BareguMhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Profesa Mwesigwa Baregu, alisema mchakato wa kutafuta Katiba mpya ulikuwa ni fursa ya kuweka mambo sawa lakini umekwama kutokana na matumizi ya ubabe badala ya maridhiano.

Viashiria vya uvunjifu wa amani vimekuwani vingi na tunatakiwa kuangalia tumefikajehapa tulipo na tunatokaje.

Kutafuta Katiba Mpya ilikuwa ni fursa ya kuweka mambo sawa lakini mchakato huo umeenda kwa ubabe badala ya maridhiano na ubabe ni chanzo cha mtafaruko,¡± alisema.

MbatiaMwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema dhana ya amani imebaki kuwa ni mtaji wa siasa kwa wanasiasa ambao wameishiwa sera huku wanasiasa hao hao wakishiriki kwa njia moja au nyingine katika uvunjifu wa amani.

Alisema amani ya Tanzania haitaweza kudumu endapo hapatakuwapo usawa katika nyanja zote za utoaji wa haki hasa kwa mahakama, polisi, utawala wa sheria na mgawanyo ulio sawa wa rasilimali za nchi.

ButikuMkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, alisema lengo la mkutano huo ni kukusanya wadau mbalimbali kujadili viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyojitokeza katika jamii.

Alisema mkutano huo unaweza kutoka na mapendekezo ya kuitaka serikali na wananchi nini kifanyike kuhakikisha amani inadumu.¡°Katika kipindi hiki kuna viashiria vingi vya uvunjifu wa amani, jambo ambalo linaweza kuwatia hofu wananchi, kutokana na hali hiyo, tumewaalika wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wakuu wastaafu, waliopo madarakani, wanasiasa na wadau mbalimbali,¡±alisema Butiku.

Chanzo : Mtanzania
 
Tuanze na Polisi kwa kung'ang'ania ukabila. Ukisikiliza matangazo yao kuwahusu waanga au watu wanaowatuhumu watatamka "kabila lake". Uniacha nikishangaa karne hii ambapo watu wengine hawajui hata kuongea hiyo lugha ya kikabila bado unataka kumtambulisha mtu kwa kabila lake!
 
Wewe Judge Warioba kaa kimya, hivi hujui wewe ni DILI kwa vijana wa UVCCM kupandishwa vyeo? Shauri lako, you have been warned.
 
amani ya nchi hii itavunjwa na ccm kwakucheza michezo michafu katika zoezi la uandikishaji wapiga kura na watakapogomea matokeo mwezi februari.hakika nchi itachafuka.
Kama Burundi ambapo misingi yote ya amani iko kwenye katiba lakini mtu mmoja anaamua kuwaingiza kwenye machafuko kwa lazima!
 
Serikali ya Kikwete si serikali ya Watanzania. Huwezi kumshauri lolote lenye maslahi kwa taifa akashaurika.

Mifano kama Katiba mpya, miswada gandamizi, na mapendekezo murua ya tume mbalimbali yalivyodharauria, inayodhihirisha pendekezo lolote lile lenye maslahi kwa Watanzania, kama halikinzani na maslahi kwa ccm fisadi, serikali ya ccm haiwezi kulitilia maanani.

Ninachelea hata wangeazmia jambo gani, serikali ya ccm haiwezi kulithamini isipokuwa kama litakuwa linaendeleza ubabe, na kulinda maslahi ya ccm na mafisadi.

Ninatamani wangekuwa na ujasiri wa kukemea wazi wazi tabia za Ccm na serikali yake kuhujumu uhai na uwepo wa Taifa, lakini nao wanazunguka zunguka mbuyu na kuishia kubembeleza zimwi liishi kwa amani na familia bia madhara. Uliona wapi wakati zimwi linaishi kwa damu za watu? Liishi kwa amani ili life? Zimwi habembelezwi!!!. Akikubali ni kwamba ameona akili zako zinaishia hapo na hivyo anakubali yaishe ili usimpigie kelele lakini haachi asili, kuishi kwa kula watu!. Hakuna salama!!!!!!!!
 
Yeye mwenyewe warioba na akina butiku na hao akina Askofu Ngalekumutwa wamnechangia sana hiyo hali.Anyway wasiwe na wasiwasi nchi itatulia tu
 
Wewe Judge Warioba kaa kimya, hivi hujui wewe ni DILI kwa vijana wa UVCCM kupandishwa vyeo? Shauri lako, you have been warned.

Ni nani kampa Mzee Warioba "warning" nadhani ni lazima atakuwa Mzee ki umri kuliko yeye Warioba na kama umri wake ni mdogo basi Mh.Kinana afanye kama vile alivyofanya kwa Nape.UVCCM/BAVICHA nawengine hawana matatizo na Mzee Warioba.... ninavyodhani.
 
Kibaraka mwinzi wa viungo vya albino wewe ndio kaa kimya and why you warned him who are you dude papuch.

swissme

Mkuu watu kama hawa ndiyo wanaotucheleweshea ukombozi wa hii nchi..
 
Ndio ni kweli inayumba na huenda ikayumba zaidi.....lakini huo ni upande mmoja wa sarafu. Upande wa pili ni je wewe na mimi tunafanya nini ili kuinusuru nchi na hayo (viashiria na matendo ya dhuluma na uvunjifu wa amani)?

Lazima tuombe, no question there. Lakini pia ni lazima matendo yetu na kauli zetu sisi huku chini vioneshe kuwa tunachukia rushwa, ufisadi, ukabila, udini na mambo kama hayo.
Lazima tukatae kurubuniwa, kununuliwa na kutumika (tena mara nyingine kinyume cha fikra, utu, taaluma na hisia zetu wenyewe).

Lazima tuwe mabalozi wa amani kwa kusema ukweli, kupenda na kuheshimu wengine na kutenda haki kwa wote. "It begins with us"
 
VIONGOZI wastaafu na wasomi nchini wamesema hivi sasa taifa linakabiliwa na viashiria vya uvunjivu wa amani hali inayosababisha nchi kuyumba.

Kutokana na hali hiyo wamesema ni muhimu kudhibiti amani hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Walikuwa wakizungumza Dar es Salaam jana katika mkutano uliandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere unaojadili amani na umoja wa nchi.

Jaji WariobaAkizungumzia hali ya amani, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba, alisema hivi sasa nchi imekuwa na viashiria vingi vya uvunjifu wa amani jambo ambalo linawezakuhatarisha maisha ya wananchi.

Alisema kuibuka migogoro baina ya wananchi na Serikali ni miongoni mwa sababu za dalili ya uvunjifu wa amani.

Jaji Warioba ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema viongozi wanapaswa kukaa pamoja na kujadili sualahilo.¡°Hivi sasa kuna baadhi ya watu wanapendakujitambulisha kwa ukanda, ukabila, udini na uongozi jambo ambalo ni hatari kwa wananchi kwa sababu linaweza kuleta ubaguzi.¡°

Hali hii ilikuwapo kabla ya uhuru ambako Serikali ya Mkoloni ya Uingereza iliweza kuwabagua wananchi jambo lililosababishaviongozi waasisi na wananchi waliokuwapokipindi hicho kupigania uhuru.¡°¡-baada ya kupata uhuru, Serikali ya awamu ya kwanza ilitunga sheria ya uraia ambayo iliweza kuondoa ubaguzi wa rangi,ukabila na ukanda na kuwaunganisha wananchi, kutafuta viongozi na kutumia lugha moja ya kiswahili,¡± alisema Jaji Warioba.

Alisema kuwapo vitendo hivyo ni lazima Watanzania wajue kwamba amani iliyokuwapo ilitafutwa hivyo wanapaswa kuienzi na kuidumisha iweze kudumu.

Amani ikitoweka kuirudisha ni kazi, hivyo basi tunapaswa kuienzi na kuhakikisha inadumu vizazi kwa vizazi,¡±alisema.Dk. SalimWaziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Dk. Salim Ahmed Salim, alisema Watanzania wengi wana hofu kuhusu uvunjifu wa amani hivyo ni lazima hatua zichukuliwe nchi isipoteze sifa ya kuwa kisiwa cha amani, umoja na utulivu.

Uvunjifu wa amani unatokana na migogoro ya siasa, hali ya uchumi, tofauti za dini na kabila na hata kutotenda haki kwa wote pamoja na kupuuza msingi mkuuwa usawa wa binadamu.

Hivyo tumeona umuhimu wa kufanya mkutano huu kwa sababu ya wasiwasi walionao Watanzania kuwa tusipochukua hatua zinazostahili sasa taifa letu litapoteza sifa za msingi ambazo zinaifanyaTanzania iwe kisiwa cha amani,¡± alisema Dk. Salim.

Akitoa mfano wa nchi za Afrika zilizopotezasifa ya kuwa na amani kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kondo (DRC), Libya, Sudan Kusini, Misri, Somalia, Burkina Faso na Burundi, alisema mifano hiyo inatosha kuwa funzo kwa Tanzania juu ya athari za uvunjifu wa amani.¡°

Tujifunze kutokana na matatizo yanayowakumba wenzetu. Haya yanaweza kutokea Tanzania kama hatutakuwa makini, viashiria vya uvunjifu wa amani vikiachwa viendelee taifa litaangamia na hakuna atakayepona,¡± alisema Salim.

Askofu NgalalekumtwaAkizungumza katika mkutano huo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, alisema amani ya nchi ni ya kila mtu endapo itavunjika kila mmoja atawajibika kwa nafasi yake.¡°

Kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kudumisha amani ya nchi, ikiwa tutaruhusu ivunjike hakuna atakayepona, hivyo basi kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha tunailinda na kuidumisha amani iliyopo,¡±alisema.

Alisema kutokana na viashiria vinavyoonekana hivi sasa ndani ya nchi ni ukweli usiopingika kwamba wananchi wasipokuwa makini nchi inaweza kwenda kubaya.

Alisema kutokana na hali hiyo, wanapaswa kutoruhusu viashiria hivyo viendelee katikajamii bali ni kuikemea na wananchi kuendelea kudumisha amani.

PROFESA SHIVJI Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Kavazi la Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji, alisema imefika wakati kama taifa, watu wajiulize viashiria vya kutoweka kwa amani vimefikaje?¡°

Tujiulize kama nchi ina viashiria vya kutoweka kwa amani tujiulize tumefikaje hapa na kama tukibaini kuna tatizo ni lazima tuanze kufikiria namna ya kupambana navyo kabla havijatufikisha kubaya.

¡°Hatuwezi kujifariji kuwa sisi ni kisiwa cha amani wakati leo kuna viashiria vya kuvunjika kwa amani nchini.

Ni jukumu letu kama taifa kusimama wote kwa pamoja na kusema hapana kwa wale wanaoweza kutugawa na kuiharibu amani yetu,¡± alisema Profesa Shivji.

Profesa LipumbaMwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba, alisema uvunjifuwa amani unatokana na vitendo vya Serikali kutotenda haki kwa wananchi jambo ambalo limesababisha kutoaminika kwa wananchi.

Alisema hadi sasa hakuna uwazi katika uwajibikaji wala utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayohusu jamii na taifa kwa ujumla, jambo ambalo limechangia kujitokeza migogoro baina yake na wananchi.

Serikali imeshindwa kutenda haki kwa wananchi jambo ambalo limesababisha kujitokeza kwa migogoro.

Kutokana na hali hiyo serikali inapaswa kuwa wazi na kuhakikisha kuwa inawashirikisha wananchi katika mambo mbalimbali ya taifa na jamii,¡±alisema.

Profesa BareguMhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Profesa Mwesigwa Baregu, alisema mchakato wa kutafuta Katiba mpya ulikuwa ni fursa ya kuweka mambo sawa lakini umekwama kutokana na matumizi ya ubabe badala ya maridhiano.

Viashiria vya uvunjifu wa amani vimekuwani vingi na tunatakiwa kuangalia tumefikajehapa tulipo na tunatokaje.

Kutafuta Katiba Mpya ilikuwa ni fursa ya kuweka mambo sawa lakini mchakato huo umeenda kwa ubabe badala ya maridhiano na ubabe ni chanzo cha mtafaruko,¡± alisema.

MbatiaMwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema dhana ya amani imebaki kuwa ni mtaji wa siasa kwa wanasiasa ambao wameishiwa sera huku wanasiasa hao hao wakishiriki kwa njia moja au nyingine katika uvunjifu wa amani.

Alisema amani ya Tanzania haitaweza kudumu endapo hapatakuwapo usawa katika nyanja zote za utoaji wa haki hasa kwa mahakama, polisi, utawala wa sheria na mgawanyo ulio sawa wa rasilimali za nchi.

ButikuMkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, alisema lengo la mkutano huo ni kukusanya wadau mbalimbali kujadili viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyojitokeza katika jamii.

Alisema mkutano huo unaweza kutoka na mapendekezo ya kuitaka serikali na wananchi nini kifanyike kuhakikisha amani inadumu.¡°Katika kipindi hiki kuna viashiria vingi vya uvunjifu wa amani, jambo ambalo linaweza kuwatia hofu wananchi, kutokana na hali hiyo, tumewaalika wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wakuu wastaafu, waliopo madarakani, wanasiasa na wadau mbalimbali,¡±alisema Butiku.

Chanzo : Mtanzania

Ingefaa na Mangula ahudhurie kikao hicho maana alituhumiwa kutaka kumwua dkt Slaa. Hicho pia ni kiashirio cha uvunjifu wa amani. Unafikiri ingekuwaje Mangula angefanikiwa kumwua Slaa? Viashiria hivi vibaya lazima vikemewe waziwazi na wahusika kwa vile wanajulikana lazima waonywe.
 
Tume ya uchaguzi ionywe mapema na kila mpenda amani, waache mipango ya kutaka kuiba kura Octoba kwa ajili ya ccm. Wakifanya hivyo tu amani lazima itayumba.
 
Kwani lini waliiba kura mzee hebu tukumbushe nasi tujue kura kiasi gani ziliibwa.
 
Mzee amepigika sana hizi zote ni porojo tu.

  • [*=center][h=2]EXCHANGE RATES[/h]
    blueline.gif

    icon_exchangerates.png
    Wed, 27 May 2015

    [*=center][h=2]1 USD
    BUY: 2065.95
    SELL: 2111.8
    [/h]
    [*=center][h=2]1 EUR
    BUY: 2196.05
    SELL: 2296.58
    [/h]
    [*=center][h=2]1 GBP
    BUY: 3109.14
    SELL: 3251.12
    [/h]
    [*=center][h=2]1 ZAR
    BUY: 170.993
    SELL: 174.898
    [/h]
    [*=center][h=2]1 KES
    BUY: 21.0917
    SELL: 21.9723
    [/h]
 
Kwani lini waliiba kura mzee hebu tukumbushe nasi tujue kura kiasi gani ziliibwa.
Simiyu,
Lazima kama Watanzania tujifunze kuona maslahi yetu kwa miwani ya Utaifa, usawa, maendeleo kwa wote nk.
Natatizika na miwani yako kushindwa kuleta taswira sahihi ya hali halisi ya nchi yetu na kuita viashiria dhahiri kama porojo. Lugha na tabia kama hiyo ndio iliyotufikisha hapa tulipo.

Kumbuka: "intellectuals solve problems, genius prevent problems". Wewe ni nani kati ya hao? Au uko kundi la tatu ndugu?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom