WARIOBA na rekodi yake akiwa Waziri Mkuu

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,402
54,878
..hii ni sehemu ya mahojiano ya Waziri Mkuu Mstaafu Sinde Warioba alipozungumza na gazeti la raia mwema.

..alianza hivi:

"Mwaka 1985 hatukuwa na akiba ya fedha za kigeni. Tulikuwa tunashindwa hata kulipia meli moja ya mafuta. Sasa kama akiba yetu ikipungua, bei ya mafuta imepanda, bei ya vyakula imepanda, tukajikuta hatuna akiba ya fedha za kigeni, tunafanyaje? "

Swali: Ulipata kuwa Waziri Mkuu. Kama leo ungeshika tena nafasi hiyo ni mambo gani ambayo ungeyashughulikia ambayo hukuyashughulikia?

Jaji Warioba: Kwanza, kwanza kabisa, sina mawazo ya kuwa Waziri Mkuu kabisa. Hilo halipo. Na kwa msingi huo hata nisingefikiria nitafanya nini kwa sababu hayo wakati wetu umepita. Hali imebadilika.

Wakati nikiwa Waziri Mkuu matatizo yetu yalikuwa tofauti kabisa na matatizo ya sasa. Wakati ule uchumi wetu ulikuwa umeporomoka. Ulikuwa haukuwi.

Mfumuko wa bei ulikuwa mkubwa, asilimia 36, 37 na hatuna fedha za kigeni. Hatuna vitu madukani. Ni wakati ule wa bidhaa adimu, nchi haina chakula.

Kwa hiyo, wakati ule jukumu letu kubwa lilikuwa kuirudisha nchi katika msingi ambao utatuletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na tuliweka priorities zetu.

Moja, ilifika tukasema tujitosheleze kwa chakula katika muda wa miaka mitatu. Tulifanikiwa vizuri sana, lakini tukapata tatizo la hifadhi. Ikabidi tujenge maghala kwa haraka sana, tumepata chakula kingi zaidi tukiweke wapi?

Tukasema lazima tu stabilise hali ya mafuta katika kipindi kifupi. Tukaweza. Tukasema lazima tuteremshe mfumuko wa bei. Hatukufanikiwa sana, lakini haukuendelea kukua.

Tumeukuta uko 36, tunatoka baada ya miaka mitano umekuwa 19. Tukasema haya yalikuwa ni mafanikio makubwa.

Tukasema tuwe na sera za msingi na ndipo tulipoanza. Mnajua matatizo tuliyopata wakati ule, tulipunguza sana matumizi kwenye huduma za jamii, elimu, afya, maji tukatia kwenye huduma za uchumi. Tukaanza kujenga miuondombinu, hatukukamilisha.

Vipindi viwili vya Rais Mkapa walikazania hii. Tukafika mahali unaweza kuona mafanikio fulani fulani. Mfumuko wa bei umepungua, miundombinu iliboreshwa sana, ukakuta huduma za jamii zimeboreshwa ikiwa ni shule na afya na nyinginezo.

Kwa hiyo, sisi ilikuwa ni kuweka msingi ule. Na ndiyo ilikuwa jukumu letu. Tulijitahidi. Tulijitahidi na ndiyo kipindi hicho sasa uchumi umeanza kukua.

Sasa hivi hali ni tofauti na siwezi ku-speculate kwa sababu haikuja mawazoni mwangu. Mimi nasema sasa ni mzee wa kushauri tu. Ya kufikiria ningekuwa Waziri Mkuu hata haimo, kwa hiyo hata sisemi ningefanya hiki na hiki hapana. Nakumbuka hali ilivyokuwa kule na tulifanya nini. Tulipata matatizo. Unajua hali ilikuwa mbaya sana kwenye afya?

Tulikuwa na matatizo lakini tulivumilia hivyo kwa yale makubwa, na hasa chakula, maana hata mazao ya biashara miaka ile ndiyo tulifikia rekodi ya kuvuna pamba, na ilikuwa ni kwa kufanya kazi na wananchi.

Swali: Kuna majuto? Ungetaka kufanya nini ambacho hukufanya?

Jaji Warioba: Siwezi kusema na regret kwa sababu hali ilivyokuwa mazingira yenyewe ni kwamba unatamani tu kwamba aah kwa jitihada ungekuwa umefanikiwa mengi zaidi lakini haikuwezekana.

Kwa kweli hali haikuwa nzuri sana. Kwamba matarajio yalikuwa miaka mitano tutakuwa tumefika hapa. Hatukuweza kufika huko, lakini tulijitahidi tulivyoweza.
 
naam wako wanaosema mzee ruhsa awamu yake hawajafanya kitu wajifunze between the lines
 
..huyu nafikiri alifanya kazi yake kwa kufuata sheria, bila makeke.

..pia inaelekea aliondoka na heshima zake. ndiyo maana hana uwoga kuizungumzia rushwa au kuwanyooshea kidole wala rushwa.

..najua kwa Tanzania si rahisi kukuta mwanasiasa asiye na mawaa, lakini kwa standards zetu, Sinde Warioba anaelekea kuwa msafi.

NB:

..IS HE THE BEST PRIME MINISTER WE HAVE EVER HAD?
 
He was one of the best Prime Ministers, not the best. Inabidi tuwapime hawa wazee kwa vigezo mahususi. JF inaweza kuanzisha thread maalumu ya kuangalia utendaji wa PMs wetu na kuweka vigezo kisha tukasema nani alikuwa bora kwenye nini na nini? Je tunaweza kuwapima bila kugusia marais wao?

Njia nyingine tumwombe Warioba awe online kwa saa moja tumuulize maswali hapa jamvini. Kisha afuate SAS, EL, MP, etc. Tujaribu kuwatafuta. Ninaweza kumtafuta Salim na Warioba!
 
Njia nyingine tumwombe Warioba awe online kwa saa moja tumuulize maswali hapa jamvini. Kisha afuate SAS, EL, MP, etc. Tujaribu kuwatafuta. Ninaweza kumtafuta Salim na Warioba!

Naamini itakuwa jambo la busara kama utaweza kufanikisha hilo. Tanzania bado tuna rasilimali ya Wazee wa Busara lakini cha kushangaza Mh. Kingunge anawaponda,.... mmmh.

Mkuu Mwanakijiji naamini ingependeza kama nawe unaweza kupata nafasi ya kuongea na hawa wazee kwenye radio yako ili iwe na manufaa kwa Watanzania wengine maana kwa Bongo still hawa wazee watazidi kuwapiga madongo kutoka SISIEMU kutokana na misimamo yao.
 
Indume,
Achana na Kingunge. Yeye alishageuka kuwa kigeugeu. Baada ya kupata mshiko wa parking pale Dar basi lazima awaponde wenzake ambao hakuandamana nao kisiasa. He is a Judas.
 
He was one of the best Prime Ministers, not the best. Inabidi tuwapime hawa wazee kwa vigezo mahususi. JF inaweza kuanzisha thread maalumu ya kuangalia utendaji wa PMs wetu na kuweka vigezo kisha tukasema nani alikuwa bora kwenye nini na nini? Je tunaweza kuwapima bila kugusia marais wao?

Njia nyingine tumwombe Warioba awe online kwa saa moja tumuulize maswali hapa jamvini. Kisha afuate SAS, EL, MP, etc. Tujaribu kuwatafuta. Ninaweza kumtafuta Salim na Warioba!

Ha ha haaaa hiyo ndio itakuwa siku ya nyani kuteleza kutoka kwenye mti, hawawezi kuthubutu kuja hapa kwa saa moja kwani wanajua joto ya jiwe iko hapa. Hasa wale wanafiki maana wataumbuliwa.

BTW wazo zuri jaribuni kuwakaribisha hapa halafu tupeane taarifa tuwahoji.
 
..huyu nafikiri alifanya kazi yake kwa kufuata sheria, bila makeke.

..pia inaelekea aliondoka na heshima zake. ndiyo maana hana uwoga kuizungumzia rushwa au kuwanyooshea kidole wala rushwa.

..najua kwa Tanzania si rahisi kukuta mwanasiasa asiye na mawaa, lakini kwa standards zetu, Sinde Warioba anaelekea kuwa msafi.

NB:

..IS HE THE BEST PRIME MINISTER WE HAVE EVER HAD?

La hasha!

Hapo umeongelea sifa moja tu, tena labda haifiki moja. Alikuwa msafi, alifuata sheria, hakula rushwa, na akaondoka na heshima yake. Kwa kifupi, Muadilifu.

Muadilifu ni sifa. Na inaweza kuwa sio sifa. Unapokula kiapo cha madaraka, zaidi ya kufanya kazi zako, cha chini kuliko vyote unachoahidi ni kufuata sheria, kutokutuibia. Ukitimiza hilo unakuwa umekamilisha wajibu, tena wa chini kuliko wote. Unapotimiza wajibu hupigiwi ngoma. Unapofika kazini katika muda unaotakiwa kila siku hupewi malipo ya ziada, unapewa mshahara. Hata kama wenzako wanachelewa kila siku. Ukiingizia kampuni mapato kuliko ulivyo tarajiwa ndio unaweza kudai bonus, au overtime payment kama umefanya kazi muda wa ziada. Hutakiwi kupewa chereko kwa kuwa muadilifu, hata kama kama unalinganishwa na Wachafu, wakina Mkapa.

Ndio maana nasema mazuri uliyo yataja hapo yanaweza yakawa au yasiwe sifa inayoweza kupima excellence - kwa sababu ni wajibu wa Waziri Mkuu kutokutuibia. Na kama ni sifa, ni sifa moja tu.

Jokakuu, sijui kama unakumbuka enzi za Warioba lakini Mkuu aliondoka na sifa mbaya ya kushindwa katika Utekelezaji. Dhihaka mpaka zikaenea kwamba Mwinyi alipo fire baraza la Mawaziri, Warioba akauliza kama yeye pia yuko fired!

Kwa hiyo, sio tu, hawezi kuwa the best, nadhani hata katika the best hayumo. Mawaziri wakuu wazuri kuliko wote nadhani ni Nyerere na Sokoine. Na watatu labda Salim.

Ahsante.
 
Naamini itakuwa jambo la busara kama utaweza kufanikisha hilo. Tanzania bado tuna rasilimali ya Wazee wa Busara lakini cha kushangaza Mh. Kingunge anawaponda,.... mmmh.

Mkuu Mwanakijiji naamini ingependeza kama nawe unaweza kupata nafasi ya kuongea na hawa wazee kwenye radio yako ili iwe na manufaa kwa Watanzania wengine maana kwa Bongo still hawa wazee watazidi kuwapiga madongo kutoka SISIEMU kutokana na misimamo yao.

Napenda sana kufanya mahojiano na hawa wazee, nilikuwa nimewaline up wengi tu.. but it cost money...!
 
..huyu nafikiri alifanya kazi yake kwa kufuata sheria, bila makeke.

..pia inaelekea aliondoka na heshima zake. ndiyo maana hana uwoga kuizungumzia rushwa au kuwanyooshea kidole wala rushwa.

..najua kwa Tanzania si rahisi kukuta mwanasiasa asiye na mawaa, lakini kwa standards zetu, Sinde Warioba anaelekea kuwa msafi.

NB:

..IS HE THE BEST PRIME MINISTER WE HAVE EVER HAD?

He sure is one of the greatest...but the best? Maybe the best living PM. Sokoine had a caliber of his own. Salim, well, he didn't serve long enough to have a good analysis of his Premiership. Warioba ni muadilifu lakini nafikiri he should have stood up for himself when Mzee Ruksa was being led astray with the Dirias and KK!
 
Huwa najiuliza kwa nini huyu Warioba hakuendelea kuwa waziri mkuu wa mzee Ruksa kwa kipindi cha miaka 10.

Anaongea vitu vinaeleweka kuhusu Muafaka kuliko Babu wa Kilwa na Mgosi,Je Ruksa aliogopa kuwa huenda angeweza kugombea Urais awamu ambayo ilifuata kama kawaida ya wanaomaliza uwaziri mkuu hugombea U rais?Huyu jamaa ndo waziri wa kwanza kuundiwa wizara hii ya TAMISEMI ambayo iliundwa kipindi cha Ruksa.

Hata kupata ubunge kule Bunda mkoani Mara kipindi fulani ilikuwa mbinde maana waliendeshana na Stephen Wassira alipokuwa amehamia NCCR-MAGEUZI.
Naona baada ya kukosa U waziri mkuu kipindi cha pili,mambo yalimwendea kombo sana ktk duru za siasa.

Hiki kichwa bado tunakihitaji kwa maendeleo ya Taifa hili
 
Kitila Mkumbo,

..amezungumzia mabadiliko makubwa ktk KILIMO/CHAKULA na UCHUMI/FEDHA. hivi haiwezekani kwamba wanaostahili sifa hapo ni mawaziri wa sekta hizo mbili kuliko yeye Sinde Warioba?

..ile kashfa ya Rio-Degeneiro ilitokea akiwa bado Waziri Mkuu? baada ya hapo ndiyo mambo yalianza kwenda mrama ktk serikali ya Mzee Ruksa.
 
CCM ya wakati wao sio ya sasa, maana sasa hivi hakuna msafi hata mmoja ndo maana kikwete anapata tabu kupata mawaziri, kila mtu ana kashifa yake inayosubiri kuibuka. Wakati wa mkutano wa Rio de Geneiro yeye alishaachishwa uwaziri mkuu nafikiri waziri mkuu alikuwa Msuya, mwananchi gold sinauhakika.
 
..huyu nafikiri alifanya kazi yake kwa kufuata sheria, bila makeke.

..pia inaelekea aliondoka na heshima zake. ndiyo maana hana uwoga kuizungumzia rushwa au kuwanyooshea kidole wala rushwa.

..najua kwa Tanzania si rahisi kukuta mwanasiasa asiye na mawaa, lakini kwa standards zetu, Sinde Warioba anaelekea kuwa msafi.

NB:

..IS HE THE BEST PRIME MINISTER WE HAVE EVER HAD?

JOKA KUU NILIKUWA NAJIULIZA HIVI KWA NINI WAZEE WENGINE WAKO KIMYA NCHI INALIWA WANALO JAMBO WAKISEMA TU WATAUMBULIWA WARIOBA HANA MAFINDOFINDO NDIYO MAANA ANA MA CONFIDANCE YA KUSEMA.
 
jamco said:
Wakati wa mkutano wa Rio de Geneiro yeye alishaachishwa uwaziri mkuu nafikiri waziri mkuu alikuwa Msuya, mwananchi gold sinauhakika.

jamco,

..cleopa msuya alikuwa waziri mkuu mwishoni mwa utawala wa mzee mwinyi. nafikiri kuanzia late 1994. mkutano wa Rio ulifanyika wakati wa waziri mkuu akiwa sinde warioba au john malecela. matumizi ktk mkutano ule yalikuwa ni kashfa kubwa kuliko ile ya safari ya sumaye marekani.

..hiyo kampuni ya mwananchi si inahusika na masuala ya kusafisha dhahabu. nadhani CCM wana hisa huko, na Sinde Warioba yuko kwenye bodi ya wakurugenzi.
 
pamoja na sifa zote hizo, tuliokuwa vyuo vikuu wakati ule akiwa pm naddhani mwaka 1989-1990, tutamkumbuka, alivyowateka akina matiko matare na kwenda kuwahoji kunako giza, nadhani anakumbuka vema alivyowashuhulikia wanafunzi wakati wule walipomchora mwnyi pale revoulinary square. atabaki kwetu kama mtu ambaye alijua maana ya state yaani...cohesive,...invisible, ..incognito,...inconquencocable....eheee, na kila aliyehoji kuhusu mwenye kwenda kucheza isambe pale uwanja wa taifa na bongo man wakati madaktari wakiwa wamegoma pale muhimbili montuary ikiwa inajaa, walikutana na definition ya state ya warioba...incognito, ehee.. invisible...endelea
 
Nami Nakubali Kuwa Sokoine Na Julius Kidogo Na Salim....ingawa Hakukaa Sana...warioba Hapana..........
 
Back
Top Bottom