..hii ni sehemu ya mahojiano ya Waziri Mkuu Mstaafu Sinde Warioba alipozungumza na gazeti la raia mwema.
..alianza hivi:
"Mwaka 1985 hatukuwa na akiba ya fedha za kigeni. Tulikuwa tunashindwa hata kulipia meli moja ya mafuta. Sasa kama akiba yetu ikipungua, bei ya mafuta imepanda, bei ya vyakula imepanda, tukajikuta hatuna akiba ya fedha za kigeni, tunafanyaje? "
Swali: Ulipata kuwa Waziri Mkuu. Kama leo ungeshika tena nafasi hiyo ni mambo gani ambayo ungeyashughulikia ambayo hukuyashughulikia?
Jaji Warioba: Kwanza, kwanza kabisa, sina mawazo ya kuwa Waziri Mkuu kabisa. Hilo halipo. Na kwa msingi huo hata nisingefikiria nitafanya nini kwa sababu hayo wakati wetu umepita. Hali imebadilika.
Wakati nikiwa Waziri Mkuu matatizo yetu yalikuwa tofauti kabisa na matatizo ya sasa. Wakati ule uchumi wetu ulikuwa umeporomoka. Ulikuwa haukuwi.
Mfumuko wa bei ulikuwa mkubwa, asilimia 36, 37 na hatuna fedha za kigeni. Hatuna vitu madukani. Ni wakati ule wa bidhaa adimu, nchi haina chakula.
Kwa hiyo, wakati ule jukumu letu kubwa lilikuwa kuirudisha nchi katika msingi ambao utatuletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na tuliweka priorities zetu.
Moja, ilifika tukasema tujitosheleze kwa chakula katika muda wa miaka mitatu. Tulifanikiwa vizuri sana, lakini tukapata tatizo la hifadhi. Ikabidi tujenge maghala kwa haraka sana, tumepata chakula kingi zaidi tukiweke wapi?
Tukasema lazima tu stabilise hali ya mafuta katika kipindi kifupi. Tukaweza. Tukasema lazima tuteremshe mfumuko wa bei. Hatukufanikiwa sana, lakini haukuendelea kukua.
Tumeukuta uko 36, tunatoka baada ya miaka mitano umekuwa 19. Tukasema haya yalikuwa ni mafanikio makubwa.
Tukasema tuwe na sera za msingi na ndipo tulipoanza. Mnajua matatizo tuliyopata wakati ule, tulipunguza sana matumizi kwenye huduma za jamii, elimu, afya, maji tukatia kwenye huduma za uchumi. Tukaanza kujenga miuondombinu, hatukukamilisha.
Vipindi viwili vya Rais Mkapa walikazania hii. Tukafika mahali unaweza kuona mafanikio fulani fulani. Mfumuko wa bei umepungua, miundombinu iliboreshwa sana, ukakuta huduma za jamii zimeboreshwa ikiwa ni shule na afya na nyinginezo.
Kwa hiyo, sisi ilikuwa ni kuweka msingi ule. Na ndiyo ilikuwa jukumu letu. Tulijitahidi. Tulijitahidi na ndiyo kipindi hicho sasa uchumi umeanza kukua.
Sasa hivi hali ni tofauti na siwezi ku-speculate kwa sababu haikuja mawazoni mwangu. Mimi nasema sasa ni mzee wa kushauri tu. Ya kufikiria ningekuwa Waziri Mkuu hata haimo, kwa hiyo hata sisemi ningefanya hiki na hiki hapana. Nakumbuka hali ilivyokuwa kule na tulifanya nini. Tulipata matatizo. Unajua hali ilikuwa mbaya sana kwenye afya?
Tulikuwa na matatizo lakini tulivumilia hivyo kwa yale makubwa, na hasa chakula, maana hata mazao ya biashara miaka ile ndiyo tulifikia rekodi ya kuvuna pamba, na ilikuwa ni kwa kufanya kazi na wananchi.
Swali: Kuna majuto? Ungetaka kufanya nini ambacho hukufanya?
Jaji Warioba: Siwezi kusema na regret kwa sababu hali ilivyokuwa mazingira yenyewe ni kwamba unatamani tu kwamba aah kwa jitihada ungekuwa umefanikiwa mengi zaidi lakini haikuwezekana.
Kwa kweli hali haikuwa nzuri sana. Kwamba matarajio yalikuwa miaka mitano tutakuwa tumefika hapa. Hatukuweza kufika huko, lakini tulijitahidi tulivyoweza.