Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,500
Tume ya Katiba inayoongozwa na Jaji Mstaafu Joseph Warioba imetangaza kuwa itakabidhi rasmi rasimu ya pili ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Desemba 30 mwaka huu kwa Rais Kikwete na Makamu wake Dr Billal pamoja na Rais wa Zanzibar Dr Shein.
Baada ya kukabidhi rasimu hiyo, Tume itakuwa imefikia ukomo wake rasmi baada ya Wabunge kushikia bango kuvunjwa kwa tume hiyo baada ya rasimu ya pili kukabidhiwa. Kwahiyo Tume itabunjwa rasmi mara baada ya makabidhiano hayo huku tukisubiri Bunge la Katiba kuteuliwa na kisha baadae Kura ya maoni kufanyika.