Warioba hakupaswa kumung'unya maneno kwenye suala la Chediel Mgonja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba hakupaswa kumung'unya maneno kwenye suala la Chediel Mgonja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bangusule, Oct 15, 2009.

 1. b

  bangusule Senior Member

  #1
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ndugu zangu,

  kipande cha habari nimekitoa kwenye gazeti la Raia Mwema na kinazungumzia uwezekano wa mgogoro wa kikatiba ambao ungeweza kutokea iwapo agizo la Mwalimu Nyerere kumteua Chediel Mgonja kuwa mkuu wa mkoa lingetekelezwa.

  tutaendelea kuweka historia wazi kila inapowezekana. Mwalimu Nyerere aliamini kwamba Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilimuonea marehemu Chedieli Yohane Mgonja kwa kumhukumu kutoshiriki siasa/uchaguzi kwa kipindi cha miaka 10 ktk kesi ya uchaguzi ya miaka ya 80.

  mwaka 1983 Mwalimu akamteua Mgonja kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanya kabla ya kumaliza adhabu yake. sasa hapo juu unaona Warioba anatumia maneno meeeengi kuelezea suala hili kimafumbo.

  kabla hajaondoka madarakani Mwalimu alimpunguzia Mgonja adhabu yake. Mgonja aligombea ubunge wa Same ktk uchaguzi wa 1985. wananchi wa Same walimpa ushindi Mgonja, kwasababu wao, kama ilivyokuwa kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,waliamini kwamba Mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu ile kimakosa.

  sikuona ulazima wa Warioba kuzungumzia suala hili kimafumbo wakati marehemu Chedieli Mgonja tayari ameligusia katika kitabu chake kinachoitwa "JOHARI YA MAISHA YANGU."

  kama suala dogo kama hili wenye kuifahamu historia yetu wanalificha vipi kuhusu masuala mengine muhimu?
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Warioba hakuwa na interest katika kutaja majina, kama unavyosema majina tayari yapo katika kitabu hicho. Warioba alikuwa na interest ya kumuonyesha Nyerere kama mtu anayeshaurika, ingawa kwa mbinde hiyo alivyoieleza hapo juu anaweza kuwa katuonyesha zaidi kwamba Nyerere alikuwa haambiliki zaidi ya alivyoambilika.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Bangusule,
  Siyo kuficha. Natamani kila mtu aliyefanya kazi na Mwalimu angepata wasaa wa kuandika
  experience zake na hii ingetupa picha ya Ikulu ya Mwalimu. Hicho kitabu cha Mgonja kinapatikanaje? Inaonekana Warioba kalizungumzia from his own perspective as an Attorney General.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Si kweli kwamba Nyerere alikuwa haambiliki ? Jaji Warioba

  [​IMG]
  Mwandishi Wetu​
  Oktoba 14, 2009 [​IMG] [​IMG]Asimulia jinsi Mwalimu alivyokuwa akiendesha vikao vya Cabinet
  Unafahamu siku ambayo Mwalimu Julius Nyerere alipotaka kuteleza na hatimaye kukiuka sheria? Je, unafahamu ni kwa namna gani alivyokuwa akiendesha vikao muhimu kwa mustakabali wa nchi? Katika makala haya, aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wake, na baadaye Waziri wa Sheria na Katiba, Jaji Joseph Warioba, anaelezea hayo ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya miaka 10 ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
  KATIKA mazungumzo yake aliyoyafanya mjini Dar es salaam na waandishi wa habari, hivi karibu, Jaji Warioba alizungumza mengi kuhusu hali ya sasa ya nchi, lakini pia alimgusia kidogo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.
  Alianza kwa kuzungumzia madai yanayoelekezwa kwa Mwalimu Nyerere kuwa alikuwa haambiliki; kwa maana kwamba hakuwa akisikiliza wasaidizi wake.
  Jaji Warioba anasema: "Unajua kuna watu walikuwa wanasema haambiliki, lakini Mwalimu Nyerere ni mtu aliyekuwa anasikiliza sana.
  "Mimi nimefanya naye kazi kwenye serikali. Nilikuwa kwenye cabinet (Baraza la Mawaziri), nimekuwa kwenye chama, niliingia kwenye Halmashauri Kuu ya TANU mwaka 1976. Wakati alipokuwa mwenyekiti (wa CCM-Taifa) baada ya kutoka kwenye urais, mimi ndiye nilikuwa Katibu wake wa Ulinzi na Usalama.
  "Staili ya Mwalimu, iwe kwenye cabinet, au iwe kwenye National Executive alikuwa na kakitabu kadogo. Mnaanza mjadala, mnanyoosha mikono tena anaandika… ataandika majina kisha ataita mmoja mmoja. Mnaweza kuendelea na mjadala siku nzima hamsikii akisema, anawasikiliza tu. Mkimaliza ana sum-up (anafanya majumuisho). Ni mtu ambaye alikuwa anajua, alikuwa mtaalamu kabisa wa kujenga consensus," alisema Jaji Warioba.
  [​IMG]

  Mwalimu Julius Nyerere
  "Unajua kila mahali kuna makundi. Sasa unaweza kuwa na kundi la viongozi hawa wanaona wale wenzao wanasema mambo ya ovyo ovyo hivi. Na kwenye cabinet mnaweza kumsikia mtu anazungumza, mnasema huyu anazungumza utumbo.
  "Lakini Mwalimu akija ku-sum-up anasema kama fulani alikuwa amesema hivi… wote mnatoka pale mnaona uamuzi ule ni wenu wote, na ndiyo maana unaona kipindi chetu kile ilikuwa akizungumza Rais, utakuta wengine wanaozungumza walikuwa wanazungumza namna ile ile, kwa sababu ni kitu kilichozungumzwa na mnakielewa."
  Kwa mujibu wa Jaji Warioba, kauli za viongozi kupishana hazikuwapo enzi za utawala wa Mwalimu. "Baadhi wanafikiri tulikuwa parrots (kasuku) wa kuimba wimbo wa Mwalimu, lakini unawezaje kuimba exactly kama hukuelewa?," aliuliza Jaji Warioba na kuongeza: "Ilikuwa ni kujenga ile consensus, ndiyo uongozi wake ulivyokuwa.
  Jaribio la kuvunja sheria
  "Na kinyume na wale wanaosema alikuwa haambiliki, si kweli. Alikuwa anakasirika kama mtu mwingine yeyote yule na aliweza kukufokea. Na wakati fulani alikuwa amemteua mtu katika nafasi fulani. Mimi kama Mwanasheria Mkuu wake nikaenda kumwambia: ‘Mwalimu hapa sheria inakataa, huwezi kumteua huyu.'
  "Nikamwambia kuna kikwazo cha kisheria hapa, kwa kuwa alikuwa yule mtu (aliyepaswa kuteuliwa) alikuwa ameonewa mambo fulani. Mwalimu akakasirika, akaniambia wewe ndiye kikwazo. Wewe umezoea kila ukija hapa ni kuniambia usifanye hivi kwa sababu sheria inakataa, hapana hili sikubali."
  "Nikamwambia Mwalimu, hili ni suala la Katiba, ukifanya hivi kutakuwa na crisis (mgogoro) kwenye Bunge. Akasema si ndiyo demokrasi? Ngoja iende huko. Nikamwambia kwamba ni suala la Katiba, na yeye ndiye guardian (mlezi) wa Katiba.
  "Nikaendelea kumwambia Mwalimu kwamba ikitokea crisis na yeye ndiye guardian; yaani imesababishwa na guardian, ni kitu serious. Akasema ndiyo demokrasi, haya mambo ya kufichaficha siyo mazuri; ngoja iende huko."
  Jaji Warioba anaendelea kulikumbuka tukio hilo na kusema: "Nikatoka pale, nikaenda kwa Waziri Mkuu, Sokoine (Edward) nikamwambia; ‘PM sasa kutakuwa na matatizo kwenye Bunge, boss hataki kubadili msimamo', akasema aah hebu twende bwana tumshauri angalau asimwapishe huyu mpaka tuwe tumetoka bungeni."
  Kwa mujibu wa Jaji Warioba, walipokwenda kumwona Mwalimu asubuhi nyumbani kwake, Msasani Dar es Salaam, yake mambo yakawa tofauti. Walikwenda kumwona Mwalimu Msasani, kwa kuwa alikuwa na ofisi yake ndogo aliyokuwa akiitumia na alikuwa akifika Ikulu kama kuna matukio rasmi, kama mkutano wa Baraza la Mawaziri au mengine.
  "Alipotuona tu akaanza kucheka, akasema; ‘Edward (Sokoine), nilimfukuza huyu jana; lakini aliniambia kitu kimenisumbua sana usiku. Sasa sijui kimekuleta nini hapa? Waziri Mkuu akaelewa na akauliza, sasa nini kimekusumbua?
  "Mwalimu akasema nimefuata ushauri wake. Akasema: ‘Joseph, wewe ni stubborn (msumbufu) eeh?'
  Chimbuko la tukio hilo ambalo lingemweka Mwalimu Nyerere katika mgogoro wa kikatiba, lilihusu uamuzi wake wa kumteua mkuu wa mkoa.
  Ilikuwa mwaka 1983, mtu huyo (jina linahifadhiwa), awali alikuwa na kesi mahakamani, na kwa mujibu wa sheria kwa wakati huo, ukifikishwa mahakamani unapoteza baadhi ya haki za kiraia kama kupiga kura kwa nyakati fulani.
  Kwa hiyo kwa kuwa Mwalimu alitaka kumteua mtu huyo kuwa mkuu wa mkoa, ambaye kwa wakati huo moja kwa moja angekuwa mbunge, mgogoro ungejitokeza kikatiba kwamba, mbunge ni lazima awe na sifa kamili za kiraia (zikiwamo za kupiga kura), ambazo kama mhusika huyo angeteuliwa asingekuwa nazo.
  Jaji Warioba anahitimisha simulizi ya tukio hilo kwa kusema: "Lakini sasa wakati mwingine kuwa stubborn kunasaidia; yaani usije ukaacha kusisitiza hoja yako kama unaamini uko sawa sawa. Kwa hiyo, ni kweli wakati mwingine Mwalimu alikuwa mbishi, lakini akikaa akitulia anajirudi.
  "Kwa hakika, ni mtu mmoja ambaye, kwa viongozi niliowahi kufanyanao kazi, alikuwa haoni aibu kuja kusema hapa nilikosea.
  "Mwalimu alikuwa giant kwenye intellectuals, no doubt about that, na he could stand his ground kwenye argument", anasema Jaji Warioba na kuongeza: "Lakini alikuwa ni mtu ambaye yuko tayari ku-compromise. Ni mtu ambaye pamoja na kwamba alifika kiwango hicho cha juu, kimsingi alikuwa ni mtu wa kawaida.
  "Kama ungefika Butiama ukakuta anacheza bao na wale wazee, na wewe humfahamu; na kisha wale wazee wakakuambia Rais yuko hapa, unaweza usiamini.
  "Mimi ni Muikizu, siwezi kuzungumza Kiikizu kwa ufasaha. Nitachanganya na Kiswahili tu, lakini Mwalimu alikuwa anakaa na Wazanaki wale huku akizungumza Kizanaki kwa ufasaha.
  "Alikuwa ni mtu wa kawaida. Mtaona hata msisitizo wake katika mambo ya maendeleo alipokuwa akisema people centred development ilikuwa ni hiyo ya kuwaweka mbele wananchi. Alikuwa akisema elimu ya Mtanzania ni primary school kwa sababu anawafikiria wale wananchi wa kawaida. Akisema afya ya Mtanzania ni zahanati, anamaanisha hivyo hivyo. Na alipata matatizo sana aliposema kuwa elimu ya Mtanzania ni primary school."
  Mbio za siasa baada ya Mwalimu
  Kwa mujibu wa Jaji Warioba, kisiasa hapa nchini kuna uhuru zaidi, na hilo ni lazima Watanzania walikubali. "Ule mfumo wa chama kimoja ulikuwa na nidhamu yake, sasa uhuru ni mpana zaidi wa kutoa mawazo, lakini tofauti mimi nafikiri chama na viongozi wakati ule walikuwa kweli wanajituma".
  "Kulikuwa na kujituma katika kuutumikia umma. Hivi sasa siasa zimekuwa za ubinafsi mno; yaani msisitizo kwenye utumishi kwa umma umepungua.
  "Unajua mazoea bwana ni magumu sana, unajua mimi siku hizi huwa nasahau. Wakati mwingine ninaposema sistahili kutukuzwa, ninaonekana kama wa ajabu hivi. Stahili siku hizi ni uheshimiwa. Kuna kupenda ukubwa, na hata wanapojitambulisha husema kuwa mimi ni mheshimiwa mbunge fulani.
  "Acha wengine wakuite mheshimiwa, siyo wewe mwenyewe ujiite hivyo. Kwa hiyo, nadhani uhuru wa mawazo umepanuka zaidi lakini ukichukua siasa kwa ujumla commitment yake ni kama imepungua.
  Mwalimu dhidi ya ufisadi
  "Kama kuna kitu Mwalimu alikuwa anachukia ni rushwa, ubadhirifu, wizi matumizi mabaya ya madaraka. Kuna wakati kuna mahali alisema kwamba pamoja na kujua kwamba kumchapa mtu mzima viboko ni kitu kibaya, lakini alikubali wala rushwa wakithibitishwa mahakamani wachapwe viboko."
  "Alikuwa na msemo wake: Caesar's wife must be above suspicion; yaani ile suspicion tu inatosha kwamba uongozi wako umefika mwisho. Siku hizi inabidi uthibitishwe na Mahakama, lakini yeye kwake uaminifu ni kitu kikubwa, kwa hiyo hata kutuhumiwa tu inatosha kupoteza sifa za uongozi.
  Kuhusu demokrasia, Jaji Warioba alisema hivi: "Nadhani demokrasia yetu (pamoja na malumbano yake yote) imepanuka. Nadhani mfumo wa vyama vingi umekuza demokrasia. Tatizo nadhani lipo kwenye vyama vyenyewe; yaani hakuna demokrasia.
  "Tunasisitiza demokrasia ya nchi, lakini ni kama vile tunafumbia macho demokrasia ndani ya vyama vyetu. Tumekuwa zaidi watu wa kanuni na taratibu, lakini kama tukiimarisha demokrasia, hasa katika vyama, tutafika mbali; maana sasa hivi inaonekana demokrasia ni kama kupingana hivi".

  [​IMG]
   
 5. b

  bangusule Senior Member

  #5
  Oct 16, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Bluray,

  labda watu wa sheria watamuelewa zaidi Warioba kuliko mimi ambaye napenda zaidi historia na kila kitu kuwekwa wazi. suala ambalo linaonekana dogo la sakata ya uteuzi wa Mgonja kuwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga linaweza kuandikiwa kitabu.

  kesi ya uchaguzi iliyomhusisha Chediel Mgonja naamini ni funzo zuri sana kwa wanafunzi wa sheria, siasa, na hata historia. hii ilikuwa ni kesi ya kwanza ya aina yake ambapo "wananchi" au wapiga kura walimshtaki Mbunge "wao." kesi hiyo iliunguruma Mahakama Kuu ya Arusha ambapo Mgonja alishinda. baadaye wapinzani wake walikata Rufani Mahakama Rufani ambayo ilitengua uamuzi wa Mahakama Kuu.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  I know all that, but still it doesn't change judge Warioba's focus and stress.
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  na Nyerere aliamini kuwa Mahakama ya rufani hakiutenda haki. Ndiyo maana alitaka kulipeleka swala hilo bungeni, mhimili mwingine wa nguzo za utawala.
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hapo ndipo kwenye crisis, Mahakama ndiyo imepewa kazi ya kusema nini ni haki na nini si haki. Na mahakama ya rufaa ndiyo ya juu kabisa, kwa hiyo Nyerere alikuwa hana jinsi ila kukubali.

  Kupeleka hilo swala bungeni maana yake ingekuwa marekebisho ya sheria/ katiba, ambayo hata hayo mahakama ingekuwa bado ina jukumu la mwisho la kuinterpret sheria.

  Katika nchi inayofuata utawala wa sheria mahakama ina nguvu sana, sema huyu Nyerere alitaka kupindisha rule of law hapa. Ingekuwa showdown Nyalali na Nyerere.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Blueray,
  At the end of the day Warioba's arguments prevailed, au siyo? Which shows Nyerere alisikiliza.
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  I am showing that Warioba's attempt to show Nyerere as not being haambiliki failed. In order to convince him he had to jump hoops and enlist Moringe and plead for such a straightforward issue.
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Blueray,
  For those who knew Nyerere that was the way he operated. He may not agree with you today but see him next morning on the issue you will get a different response. That does not mean that he was "haambiliki". It only showed that he was "hakurupuki".
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Oct 17, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Very well put Jasusi. Clearly, it seems like he liked to sleep on whatever the issue was before reaching a decision. I dig that kind of style.
   
 13. Chachu Ombara

  Chachu Ombara JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2016
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 5,117
  Likes Received: 5,043
  Trophy Points: 280
  ANNE KILANGO NA CHEDIEL MGONJA, UTENGUZI WA KAMBARAGE NA POMBE: KATIKA KUMBUKUMBU YA MIAKA 94 YA UZAWA WA MWALIMU NYERERE

  Chediel Yohane Mgonja ni Jina Mashuhuri Nchini, Ni Jina ambalo popote tunapotaka kuijadili Historia ya Taifa hili hatuwezi kuliepuka. Mgonja Ana Historia ndefu, tangu Chuoni Makerere Miaka ya Mwishoni mwa 1950 Mpaka Kuwa Mbunge Na Waziri Mwenye Umri Mdogo zaidi Mwaka 1965 kwa kumshinda Ndugu Elias Kisenge, aliyekuwa Katibu Mkuu wa TANU Katika Uchaguzi wa Jimbo la Same Katika Mkoa wa Tanga (Katika Wakati Husika Same ilikuwa Ni Sehemu ya Mkoa wa Tanga).

  Mgonja alikuwa Pia Rafiki wa Karibu wa Mwalimu Nyerere, pamoja Na Kuwa Kiongozi Mtiifu kwake. Itakumbukwa Ni Mgonja aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati tukitoa Msimamo Tata wa "Kuitambua Biafra" Mwaka 1968, Na Pia Ni Mgonja aliyesimamia Mapinduzi Makubwa ya "Kisomo cha Watu Wazima" wakati akiwa Waziri wa Elimu Miaka ya Mwanzoni mwa 1970.

  Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 1980 kulikuwa Na Ushindani Mkubwa Katika nafasi ya Ubunge kuliwakilisha Jimbo la Same, pamoja Na Ushindani huo Chediel Mgonja alishinda Uchaguzi Ule. Ushindi ule haukuwaridhisha washindani wake, Hivyo Mgonja alishitakiwa kwenye kesi ya uchaguzi kuwa aliiba kura za uchaguzi (election irregularities) na kwa hiyo ushindi wake wa ubunge haukuwa halali.

  Kesi Husika iliunguruma kwa Muda wa Miaka Miwili, kati ya 1980 Mpaka 1982, hatimaye Mgonja alishinda kesi dhidi yake Katika mahakama Kuu Arusha. Ushindi huo wa Mgonja Ukakatiwa Rufani Katika Mahakama ya Rufaa.

  Katika shauri hilo namba 84 la mwaka 1980 lililofunguliwa na William Bakari na mwenzake dhidi ya Mgonja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mahakama ya Rufaa Tanzania iliamua kuwa, mpiga kura ana haki kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo Tofauti Na Maamuzi ya Mahakama ya Arusha iliyosema Wapiga Kura Hawana Haki hiyo. Na Hivyo Walalamikaji walishinda Kesi Husika. Mahakama Pia ilimhukumu Mgonja kutokujihusisha Na Siasa kwa Muda wa Miaka 10.

  Mwalimu Nyerere hakuipenda Hukumu hiyo ya Mahakama Kuu, Yeye aliamini Rafiki yake Mgonja ameonewa tu. Hivyo Mwaka 1983 akamteua Mgonja kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga hali ya Kuwa adhabu yake ya kutojihusisha Na nafasi Za Kisiasa kwa Muda wa Miaka 10 haijatumikiwa hata kwa Mwaka Mmoja.

  Mwanasheria Mkuu wa wakati ule Ndugu Joseph Sinde Warioba anazikumbuka zaidi nyakati Husika, anaeleza yafuatayo;

  "Na kinyume na wale wanaosema (Nyerere) alikuwa haambiliki, si kweli. Alikuwa anakasirika kama mtu mwingine yeyote yule na aliweza kukufokea. Na wakati fulani alikuwa amemteua mtu katika nafasi fulani. Mimi kama Mwanasheria Mkuu wake nikaenda kumwambia: Mwalimu hapa sheria inakataa, huwezi kumteua huyu.

  Nikamwambia kuna kikwazo cha kisheria hapa, kwa kuwa alikuwa yule mtu (aliyepaswa kuteuliwa) alikuwa ameonewa mambo fulani. Mwalimu akakasirika, akaniambia wewe ndiye kikwazo. Wewe umezoea kila ukija hapa ni kuniambia usifanye hivi kwa sababu sheria inakataa, hapana hili sikubali.

  Nikamwambia Mwalimu, hili ni suala la Katiba, ukifanya hivi kutakuwa na crisis (mgogoro) kwenye Bunge. Akasema si ndiyo demokrasi? Ngoja iende huko. Nikamwambia kwamba ni suala la Katiba, na yeye ndiye guardian (mlezi) wa Katiba.

  Nikaendelea kumwambia Mwalimu kwamba ikitokea crisis na yeye ndiye guardian; yaani imesababishwa na guardian, ni kitu serious. Akasema ndiyo demokrasi, haya mambo ya kufichaficha siyo mazuri; ngoja iende huko.

  Jaji Warioba anaendelea kulikumbuka tukio hilo na kusema: Nikatoka pale, nikaenda kwa Waziri Mkuu, Sokoine (Edward) nikamwambia; PM sasa kutakuwa na matatizo kwenye Bunge, boss hataki kubadili msimamo, akasema aah hebu twende bwana tumshauri angalau asimwapishe huyu mpaka tuwe tumetoka bungeni.

  Kwa mujibu wa Jaji Warioba, walipokwenda kumwona Mwalimu asubuhi nyumbani kwake, Msasani Dar es Salaam, yake mambo yakawa tofauti. Walikwenda kumwona Mwalimu Msasani, kwa kuwa alikuwa na ofisi yake ndogo aliyokuwa akiitumia na alikuwa akifika Ikulu kama kuna matukio rasmi, kama mkutano wa Baraza la Mawaziri au mengine.

  Alipotuona tu akaanza kucheka, akasema; Edward (Sokoine), nilimfukuza huyu jana; lakini aliniambia kitu kimenisumbua sana usiku. Sasa sijui kimekuleta nini hapa? Waziri Mkuu akaelewa na akauliza, sasa nini kimekusumbua?

  Mwalimu akasema nimefuata ushauri wake (nimetengua Uteuzi wa Mgonja Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga), Akasema: Joseph, wewe ni stubborn (msumbufu) eeh?"

  - Masimulizi ya Jaji Joseph Sinde Warioba, Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mwaka 1983 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Julius Nyerere alipomteua Ndugu Chediel Yohane Mgonja Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

  Mwalimu Nyerere aling'atuka Madarakani 1985, Lakini kabla ya Kung'atuka alimpunguzia (kwa Mamlaka aliyonayo Kikatiba) Mgonja adhabu yake ya kutojishughulisha Na Siasa kwa Muda wa Miaka 10. Mgonja aligombea ubunge wa Same katika uchaguzi wa mwaka 1985, wananchi wa Same walimpa ushindi Wa Kishindo, Na Pia wakamchagua Tena Kuwa Mbunge wao Katika uchaguzi wa mwaka 1990, ambapo alistaafu Siasa Za Kibunge 1995.
   
Loading...