Warioba: Hakuna chama cha upinzani kinachoweza kuongoza nchi

bado sijaona chama cha upinzani chenye umakini wa kuiongoza nchi, chadema ni wahuni na wanywa viroba tu
 
Baada ya kile kilichoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi kusambaratika kwa kipigo kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kuna kila dalili kwamba bado tuna miaka 40 mbele kwa Upinzani(kama upo ) kuchukua Dola.
Sababu za kutochukua Dola kwa sasa ni pamoja na:-
(a) Kukosekana kwa ajenda wanayosimamia. Kila chama kiko bize kupigania maslahi binafsi ya Chama badala ya Taifa. Sera za baadhi ya Vyama haziwashawishi wapiga kura kuviamini;
(b) Ubinafsishaji wa Vyama Vya Siasa has a Upinzani ambapo Vyama vimekuwa Mali ya Viongozi badala ya Wanachama. Matokeo take ni migogoro isiyokwisha;
(C) Vyama kukosa misimamo ya Kisiasa na tabia ya ugeugeu. Leo wanasimamia hiki na kesho wanasimamia kingine;
(d)Kukosekana kwa Viongozi makini na ukosefu wa uzoefu wa kuongoza Nchi. Viongozi wengi waliokimbilia huko ni makapi ya CCM ambao hawana credibility mbele ya jamii.
Hizo ni sababu chache ambazo zitawafanya Wapinzani wasubiri hadi 2055
 
Katika dokezo la kipindi cha "Dakika 45" kinachotarajiwa kurushwa siku ya Jumatatu kuanzi saa 3:00 usiku,mzee Warioba anasikika akisema bado wakati haujafika kwa wapinzani kuongoza nchi.

Mtangazaji alimuuliza kama anaona wakati umefika kwa wapinzani kushika madaraka.

Jibu la mzee Warioba lilikuwa ni;

Wakati wa vyama vya upinzani bado na akaongeza kuwa hajaona chama chenye uwezo na kilichojiandaa kwa kila aina kuongoza nchi.

My take;
Mzee Warioba kwa hili hayuko sahihi kabisa na huenda kajibu vile akihofia jamaa wanaeweza kum-kolimba au kumfanyia mizengwe mingine.

Ungewaelekeza uongozi wa CCM waache kununu wapinzani uchwara.Leo Lipumba anapewa support na serikali ya CCM unamtengaje Lipumba na CCM?

Upinzani imara utakuwepo kama HAKI itatendeka kwa vyama vyote vya SIASA,kuanzia CCM hadi vingine.Hata CCM ni chama cha upinzani maan wapinzani wao ndiyo hao CUF na wengineo.

Ni bora vyama vyote viitwe vyama vya siasa tuondoe lile neno upinzani maana wenzetu wa CCM wanadhani tukiwa na mawazo tofauti nao basi ni wahaini,wakati wahaini wapo humo humo CCM
 
Tangia taifa hili lilipokubali kuingiza mfumo wa vyama vingi jitihada mbalimbali za vyama vya upinzani kuingia ikulu zimekuwa zikigonga mwamba kila chaguzi zinapofikia. Sijaona jitihada zozote zinazochukuliwa na vyama vya upinzania kutathmini ni wapi wanakosea na nini wafanye ili kujenga imani kwa watanzania kuwachagua kuongoza taifa hili. Kwa miaka mingi vyama vya upinzania vinajiuza kwa ajenda za kupambana na ufisadi na uzembe serikalini lakini njia wanazotumia kutuaminisha naona zinagonga mwamba. Mi nawashauri wapinzania kaeni chini jiulizeni mnakosea wapi, mikakati gani muichukue ili kujenga imani kwa watanzania wawachague kuongoza taifa hili. Bila mikakati thabiti mtaendelea kuchukia kuongozwa na ccm na kuendelea kujenga uhasama usio na manufaa kwa taifa hili.
 
Back
Top Bottom