Warioba atumika kufanya madudu ya kuibeba sera ya CCM ya Serekali 2


A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Messages
859
Points
0
A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2010
859 0
[h=1][/h]Written by Ahmed Omar Khamis // 12/12/2012 // Habari // 1 Comment


• CCM wanaufanya mchakato ni wao, mali yao.
• Serikali inawapa uso kutekeleza vitimbi viovu dhidi ya mchakato huo.
Utowaji wa maoni katika wilaya ya Mjini ratiba imepanga vituo vyote vya kutoa maoni jirani na matawi imara ya CCM ili kutoa urahisi kwa CCM kuuteka nyara
mchakato katika wilaya hii. Wakiwa katika matawi yao hayo kiasi cha wanachama 70 hivi hulala hapo tawini huku wakigharamiwa magodoro ya kulalia na vyakula. Kama hilo halitoshi CCM hulazimisha kutumika kwa vifaa vyao vya jukwaa na viti vya kukalia. Mara wakifika katika eneo la kutoa maoni hupanga viti vyao na mabenchi kwa utaratibu wao na kukalia viti hivyo. Baadhi ya viti hua vitupu na huwekwa ili kuwazuilia nafasi wenzao watakapokuja baadae. Haya ndio yaliyojitokeza leo asubuhi katika shehia ya M/Matarumbeta Jang’ombe.Hata hivyo wananchi ambao walidhaniwa kuwa ni wafuasi wa mkataba walifukuzwa na kupigwa huku wakiambiwa wende Pemba wakatoe maoni M/Matarumbeta pana wenyewe.
Baada ya wanamkataba kuchachamaa sheha akishirikiana na wana CCM walipiga simu polisi na ghafla gari mbili za FFU zilifika. Mara baada ya kufika waliwasikiliza wana CCM madai yao na ndipo wao waliposaidia kuwasogeza nyuma zaidi wanamkataba. Vijana wawili walijaribu kugoma na kuhoji kwa nini polisi wanafanya hivyo lakini walisombwa na kuingizwa katika defennder na kuchukuliwa na pingu mikononi.Hivi mchana wa leo kiasi cha saa 8:00 tume ya mabadiliko ya katiba itakuwepo katika shehia ya Jang’ombe. Nilifika katika kituo hicho kiasi cha 5:00 asubuhi ili kuona maandalizi yanavyoendeleav katika kituo hichi. Kinyume na kawaida nilikuta jukwaa ambalo ninatarajiwa kutumiwa na tume linaendelea kujengwa katika uwanja finyu ulio ndani ya skuli hiyo na kuachwa viwanja kadhaa vilivyopo nje ya skuli hiyo. Vifaa vya jukwaa na viti ni mali ya CCM. Lengo la kuliweka jukwaa ndani ya uwanja finyu wa skuli bila shaka ni kujificha ili wanamkataba wababaike wasijue kituo kilipo na wakifika wakimbilie katika uwanja wa nje wa skuli na hivyo wana CCM wawahi nafasi zote za mbele.Ghafla kundi la wanamkataba liliwasili katika eneo hilo na kuingia ndani ya geti la skuli ili kuwahi kukaa katika foleni. Mara tu sura za wanamkataba zilipofahamika, sheha wa shehia hiyo akishirikiana na wana CCM walitumia ubavu kuwasukuma huku wakirushiana makonde na wana mkataba na kufanikiwa kulifunga geti la skuli hiyo. Wanamkataba wachache waliwahi kupenya lakini wengi wao kubaki nje. Kama kawaida yangu nilisogea na kupiga picha ya tukio hilo lakini ghafla kundi la samaki lilinijia ghafla na makelele ya matusi na kutishia usalama wangu. Hali hadi sasa ipo hivyo katika kituo hichi
Zoezi la utowaji maoni ya katiba mpya linazidi kuingia dosari na kuelekea kuharibika kabisa. Mchana huu zoezi hili linatarajia kufanyika katika kituo cha skuli ya Kidongo chekundu. Katika kuendeleza vitendo vya ubabe na kuuteka nyara kila mchakato wa kidemkrasia, CCM kwa mashirikiano na sheha huku wakipata ulinzi na uungwaji mkono wa jeshi la polisi wameamua kuifunga milango ya geti la kituo hicho na kutowaruhusu kuingia wale wote wanaodhaniwa kuwa na maoni ya muungano wa mkataba. Sheha wa shehia ya Jang’ombe akishirikiana na wana CCM wamebaki ndani ya geti hilo wakiwatambua wale ambao wana mawazo kama yao na kuwaruhusu kupita.


Vijana wanaozuiliwa kuingia ndani ya geti hujaribu kuhoji na kutaka kuingia kwa nguvu lakini jeshi la polisi humvamia kila anaejaribu kuingia kwa nguvu, kumpa kipigo na kumpeleka kiuoa cha polisi na pingu mkononi. Hali ni mbaya sana na inatisha. Sijui kama huu ni utowaji maoni tena unaozingatia uhuru, haki na demokrasia.
 
A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Messages
859
Points
0
A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2010
859 0
Hofu ya ccm hivi sasa ni muelekeo wa maoni yalivyo, Upande wa Zanzibar Unataka Muungano wa mkataba yani Zanzibar iwepo na Tanganyika iwepo halafu wakae mezani.
Na upande wa Bara hivyo hivyo wanataka mfumo wa Serekali 3 yani ya Tanganyika iwe alive na Zanzibar halafu kuwe na ya Muungano kwa mambo ya nayohusu Muungano tu.

Kwahili pande mbili zote za Muungano linakubaliwa na wananchi wake, lakini ccm hili hawalataki wako tayari kuipoteza Tanganyika ili wafiche mazambi yao kwa ccm.

Kuibuliwa upya Tanganyika ndio kifo cha ccm Bara na zanzibar.
 
Tiba

Tiba

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2008
Messages
4,548
Points
1,250
Tiba

Tiba

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2008
4,548 1,250
Asante mkuu, nimefurahia jinsi ulivyoleta taarifa hii na kufanikiwa kupiga picha. Kwa kuweka sawa taarifa yako, nafikiri tuseme kwamba CCM inabaka utaratibu wa watu kutoa maoni ya katiba lakini sio kumlaumu Warioba kwani sina uhakika kama anajua hayo yanayoendelea. Lakini kwa taarifa hizi, na picha serikali inapashwa kuchukua hatua na kuacha ubabe wa kutotoa nafasi kwa uhuru watu kutoa maoni yao.

Tiba
 
M

Mandi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Messages
385
Points
0
M

Mandi

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2011
385 0
ccm na warioba wote wanajua wanalolifanya.ndo maana katika kutoa maoni ni vitisho tu kutoka ffu. ni wakati mwafaka sasa kuihuhisha tanganyika na kuifanya itambulike kimataifa.neno tanzania bara linaisaliti kilwa.pia muungano haukufanyika tanzania bara na tanzania visiwani ila ni zanzibar na tanganyika.ccm wanaulinda muungano ili waweze kulinda chama na sera zake kana kwamba nchi hii ni ya ccm peke yake.
 
kelao

kelao

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Messages
5,932
Points
2,000
Age
40
kelao

kelao

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2012
5,932 2,000
Mimi ninachokiona mbele ni uwezekano wa kupata katiba mpya ya kweli chini ya serikali ya ccm ni ndoto. za
 
mpemba mbishi

mpemba mbishi

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2011
Messages
1,132
Points
1,195
mpemba mbishi

mpemba mbishi

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2011
1,132 1,195
CCM ni Tanzania na Tanzania ni CCM, kufa kwa Tanzania ndio kufa kwa CCM na kwa HAKIKA ikiondoka Tanzania muda mchache sana utakaofuatia CCM itabaki katika vitabu vya kihistoria! Kule Pemba CCM haijuilani tena na hapa Unguja imebaki makapikapi ya mwisho. Sijui huko Tanganyika.
 

Forum statistics

Threads 1,286,211
Members 494,902
Posts 30,887,440
Top