Warioba aogopa serikali 3 asema ni changamoto.Hoja dhaifu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba aogopa serikali 3 asema ni changamoto.Hoja dhaifu.

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by GHIBUU, Jul 28, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Warioba anajichanganya mwenyewe, anasema “Serikali mbili malalamiko yanaendelea kujitokeza kila kukicha” , vilele anasema “wanaohitaji Serikali tatu wasijidanganye kuwa zikianzishwa kero za Muungano hazitokuwapo” . Amezungumzia kero kwa njia mblili zinazozungumzwa bila ya kutoa mawazo ya njia ipi itakuwa bora , au ndio “SIRI KALI”

  Sasa warioba kama anaogopa serikali tatu za changamoto jee muungano wa EAC hauna changamoto kwa TZ ?

  Mimi napinga nae kwa kaulizake kwa kusema kuwa viongozi ndio wanaotaka serikali 3 kwa maslahi yao ya kisiasa,sio kweli,wewe warioba kama wataka kujua nani anaetaka seriakli tatu lete kura ya maoni,zanzibar kuwe na chombo huru cha kukusanya maoni kwa upande wetu,na tanganyika vile vile,utapta jibu sahihi la muungano kama tunautaka au hatuutaki,kama ni serikali tatu au 2.

  Habari kamili hii hapa

  na Betty Kangonga. WAZIRI Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, amesema tatizo la Muungano linasababishwa na mamlaka zinazogombea madaraka na si wananchi.

  Warioba ambaye alikuwa akizungumza kupitia Televisheni ya Taifa (TBC), alisema kuwa muungano uliopo bado ni imara lakini wanaohitaji madaraka ndiyo wanaoufanya uonekane na matatizo.
  Alisema wale wanaogombea madaraka wanapaswa kuchukua hatua ili isifike sehemu matatizo hayo yakawaletea shida wananchi.
  Warioba alisema wapo baadhi yao wanatoa sababu kuwa kuanzishwa kwa serikali tatu kunaweza kumaliza kero ya muungano, jambo alilosema kuwa halina ukweli wowote.
  Kwa mujibu wa Warioba, uwepo wa serikali mbili malalamiko yanaendelea kujitokeza kila kukicha, hivyo alishauri kuwa wanaohitaji serikali tatu wasijidanganye kuwa zikianzishwa kero za muungano hazitakuwepo tena.
  “Wapo wanaohitaji serikali tatu na kwamba wanaona hilo ndilo jawabu, hawajiulizi juu ya je serikali tatu hazitakuwa na changamoto zake? Na kama zikija, hizo changamoto zinamalizwaje,” alihoji Warioba.
  Akizungumzia kuhusu Bunge, Warioba alisema Bunge la sasa limeanza vibaya na halitoi mfano mzuri, hata lugha inayotumiwa na viongozi hao alidai sio ya staha bali ni ya kukejeliana.
  Alisema Bunge limekuwa la fujo, hatua inayowafanya wananchi mitaani kuambiana kuwa iwapo unahitaji burudani basi ni bora uangalie Bunge.
  “Wananchi wanaambiana kuwa kama unataka burudani angalia Bunge maana unakuta malumbano hata vyama vilivyopo huoni msimamo wake…sijui linaonyesha mfano gani, lazima wachukue hatua,” alieleza.
  Warioba alisema kuwa anaamini wabunge watakuwa wamesikia maoni ya wananchi, hivyo wanachotakiwa ni kutumia vizuri kanuni ili kurudisha nidhamu iliyopotea.
  Alisema Bunge lazima lichukue maamuzi magumu pamoja na kufuata maadili na ikiwa watafanya hivyo, alisema watarudisha hamu kwa wananchi ya kulitazama Bunge hilo.
  Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema wakati wa chama kimoja wananchi walikuwa wanapenda kipindi cha Bunge kwani walitenga muda wao na kusikiliza kupitia redio, bali kwa sasa teknolojia imekuwa hivyo wanajua kinachoendelea.
  Alisema pamoja na kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi, lakini Bunge limeweza kufanyakazi nzuri, kwa madai kuwa matatizo ya nchi ni magumu lakini Bunge la mfumo huo limejitahid
   
 2. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa ni wale wale watanganyika hata mtu akisoma huwa hana akili.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Muungano unaenda halijojo mwenye masikio na asikiye neno hili.
   
 4. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Hawa wazee waksha choka huwa wanaingiwa na woga,wanaogopa kila ki2 hata vivuli vyao...let them go!
   
 5. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watanzania watu wa ajabu sana! Hivi sasa hata hizo serikali mbili tuna matatizo kibao yanayotaka fedha za kuwaletea Watanzania maendeleo wanayoyahitaji mno halafu watu wanadai kuwepo na Serikali tatu ambazo zitaongeza mzigo kwa Watanzania hao hao maskini wa kutupa. Tutakuwa na viongozi 3 wenye hadhi ya urais, huenda tutakuwa na maziri wakuu ama makamu 3, tutakuwa na ongezeko la mawaziri na manaibu mara tatu achilia mbali Makatibu Wakuu na watumishi wengine watakaotakiwa ku-cater for hizo Serikali tatu. Hivi ni akili kweli. Acheni hayo mambo ya Serikali tatu kuongeza tu mzigo kwa wananchi waliokwishapigika! Kwa ujinga wangu nilidhani either twende kwenye Serikali moja ili kusiwepo na huu msuguano wa nchi mbili pamoja na matumizi yasiyo ya lazima ama tuuvunje kabisa Muungano ili tusitegemeane tena kila mtu abebe mzigo wake! Kwanza tukiachana na Muungano ni kama tuna endorse tu hali iliyopo hadi hivi sasa kwa sababu tayari Zanzibar ni nchi iliyo na serikali yake fully fledged. Tusidanganyane!
   
 6. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  kaka umesoma wapi wewe ?

  Katika muungano wa Europian union,wabunge na mawaziri katika bunge lao ndio hao hao wanaotoka katika nchi zao ambazo tayari ni wabunge au mawaziri,kwa mfano mfumo ambao tunaohitaji wa serikali tatu.

  Haya ndio mapendekozo yangu na muono wangu.

  Kila upande tanganyika na zanzibar kutakuwa na serikali yake ambayo ni soveregn state,kila upande utajiendesha wenyewe kwa gharama zake,hata vyama vya siasa kila upande kuwe na vyama vyake vya siasa. sio mchanganyiko huu tulio nao.

  HAYA katika serikali ya muungano,nafikiri kutakuwa imepitwa na wakati kuwa na katiba,kutakuwa na tu na serikali ya shirikisho ambayo itakuwa ni ya mkataba wa mambo fulani tu ya kibiashara.

  Bunge la muungano liwe na mfumo huu.

  Wabunge watakao huzuria katika bunge la muungano watakuwa mawaziri tu,ambao watatoka katika pande mbili,zanzibar na tanganyika,na rais wa muungano atachaguliwa ndani ya bunge hilo kwa kupiga wenyewe kura,mawaziri hawa kutoka pande mbili kutakuwa na usawa kamili,idadi sawa sawa katika bunge.

  Hatutahitaji kupoteza mambilioni ya kupiga kura kwa kuteuliwa rais wa muungano,kura itatumika katika bunge la muungano,rais wa muungano hatakuwa na malaka yoyote ya kungilia nchi yoyote ile katika ya hizi mbili tanganyika na zanzibar. Maamuzi yatakayo toka katika bunge yatachukuliwa na viongozi wa pande mbili na kuyafanyia kazi bila ya kuingiliana ,yaani mbunge wa zanzibar kuingilia mambo ya tanganyika.au wa tanganyika kungilia zanzibar.

  Kwa upande mwengine nafikiri haina haja hata kuwa na muungano,naona sio lazima tena bora kila mtu achukue chake,EAC ipo na ndio itakayo tuunganisha tena.
  TUSIPOTEZEANE TIME.
   
 7. D

  Deo Mushi Member

  #7
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Warioba ni babu hana jipya wala haeleweke
   
 8. D

  Deo Mushi Member

  #8
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama wewe ni Msomi mzuri lazima ujiulize Huu Mungano ni wa nini? kwa faida ya nani? kwa unmuhimu gani? Kwangu mimi hauna faida bora kila mtu achukue chake tuachane kwa amanii kuliko kuja kuumizana badae
   
Loading...