Waraka wasambazwa kuitafuna CCM 2010, kanisa Katoliki laukana

Wana deal na wrong audience! watanzania hawana shida na nyaraka fulana, kofia, khanga, pilau nk mambo poa
 
JK hana sababu ya kuonewa huruma kwani yeye mwenyewe anajitosheleza kwa ukakamavu na uongozi thabiti,tatizo lenu mliomadogma mkipumbazwa tuu mmepambazishwa!Mtasema sana lakini ukweli utabaki palepale JK ndiye chaguo la watanzania wengi wenye kutaka amani na utulivu sasa kama nyie mnataka fujo(na tayari tunawajua kawaida yenu ni fujo hata mashuleni mlifahamika) ameni nchi na mwende kwa ndugu yenu M7 tuachieni nchi yetu

JK ni chaguo lako wewe na wenzio wenye mawazo yenye magengeza....na wewe unajiona ni mwenye nchi?pole sana
 
Kuibuka kwa mambo kama haya, yawe feki au siyo feki, ni ushahidi thabiti kuonyesha kuwa Kikwete hawezi kazi ya kuongoza Taifa hili.
 
Salva Rweyemamu kazi yake hiyo na huo waraka umeandaliwa na jamaa mmoja ktk ofisi ya akina salva na miongoni mwa aliyeupeleka same ni dogo mmoja hivi anaishi kigurunyembe moro.

Yawezekana nikakubaliana na namna hoja hii ilivyokaa. Lakini kama ni uongo nachelea kusema tutakuwa tumepoteza muda wetu na nguvu zetu kujadili hoja ambayo ama ilishapitwa sana na wakati au mtu tu kakurupuka nayo. Hata hivyo ninaona wazi kuwa hoja hii italeta kampasuko ambako ili kukaondoa la,zima ifanyike kazi ya wazi.

Napendekeza kanisa lijiondoe kwenye hii lawama kwa kutoa TAMKO rasmi nasi tuisute serikali ya CCM kwa kutengeneza cheap propaganda.
 
kanisa linatakiwa kuendelea kuelimisha wananchi jinsi gani wataondokana na umasikini kwa kupata watu wasio na choyo. Viongozi wa mifano na siyo Chadema au C.C.M. au udini. Nini ni haki ya Mtanzania?
 
Huo ni waraka wa CCM na si wa kanisa! CCM tu ndio wana muda wa kupandikiza chuki na majungu ili waendelee kuhodhi madaraka kifisadi na si kanisa kwani kanisa liko kuhubiri amani na umoja! JK atang'oka tu na hata akiiba kura tena mwisho wake utakuwa mbaya kama fisadi mwenzake mkapa. Hivi Mkapa anajisikiaje pale ambapo Mwinyi akipita mahali anashangiliwa na yeye akipita anazomewa!JK naye atazomewa sana kama tu bado akiwa madarakani ameanza kutupiwa mawe!
 
Mwandishi Daniel Mjema

IKIWA imebaki takribani miezi 10 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, waraka mzito unaodaiwa kuwa wa Kanisa Katoliki umeanza kusambazwa nchini ukiwahamasisha waumini wake kutoichagua CCM.

Waraka huo unadai suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi na serikali kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC) ni mambo yaliyokataliwa na kanisa, lakini serikali ya awamu ya nne imepuuza kauli hiyo ya kanisa.

Kadhalika waraka huo unaenda mbali na kudai kuwa vyama vya CCM na CUF kwa sasa havifai kwa kanisa kwa kuwa vimekuwa mithili ya mbwa mwitu aliyejivika ngozi ya kondoo, huku ukitahadhariha kuwa Mahakama ya Kadhi na OIC ni hatari kwa Ukristo.

Hata hivyo, rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Mhashamu Askofu Yuda Thadei Ruwa'ichi ameukana waraka huo akisema ni 'feki' na kutaka vyombo vya dola kuwatafuta na kuwakamata wanaousambaza.

"Oktoba mwaka huu lilishafanyika jaribio la kusambaza misikitini waraka feki kama huo, lakini sisi kama kanisa tunasema kama ni waraka wa Wakristo hauwezi kusambazwa misikitini bali makanisani," alisema Askofu Ruwa'ichi alipoongea na Mwananchi.

Askofu Ruwaichi alisema kama ulivyokuwa waraka ule wa Oktoba ambao aliuelezea kuwa haukuwa wa kanisa hilo, waraka unaosambazwa sasa pia si wa kanisa na kuwataka Watanzania kuwa makini na watu wasiolitakia mema taifa.

Rais huyo wa TEC alisema wapo watu wanaojaribu kuchezea waraka halali uliotolewa na kanisa hilo ambao mtu yeyote akiusoma ataona kanisa halina shida na mtu mmoja mmoja wala halina mgogoro na dini nyingine.

"Nawaomba wananchi ambao tayari waraka huo umefika mikononi mwao, wauchunguze vizuri na wamchunguze vizuri mtu anayewapitishia karatasi hatari kama hiyo, kwa sababu ana lengo la kuwapotosha kwa maslahi yake," alisema.

Waraka huo wenye kurasa tatu ambao Mwananchi imefanikiwa kupata nakala yake unatanguliwa na maandishi yanayosomeka: "Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). Huduma ya Kichungaji katika jamii kuelekea uchaguzi mkuu 2010."

Kwa mujibu wa maelezo ya waraka huo, ambao inadaiwa kuwa umetolewa na Tume ya Haki na Amani ya TEC, unasambazwa kwa siri kwa maaskofu, mapadre na wachungaji kote nchini na inadaiwa kuwa mtu wa kawaida haruhusiwi kuupewa.

Waraka huo ambao umesambazwa pia katika misikiti mbalimbali wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, umegusia suala la vita dhidi ya ufisadi ukisema kuendelea kuikumbatia CCM ni hatari kubwa kwa kanisa.

"Kama kanisa litakuwa kimya bila kulidhibiti, basi kanisa litachafuliwa kwa njia moja au nyingine," unasema waraka huo ukisisitiza kuwa huu ni wakati wa kanisa kushika hatamu ya uongozi wa nchi.

Waraka huo unaendelea kudai kuwa chini ya awamu ya tatu ya Rais Alli Hassan Mwinyi, kanisa liliweza kudhibiti na kurudisha heshima yake lakini katika awamu ya nne kumekuwa na udhalilishaji wa kanisa wa kiwango cha juu.

"Mwelekeo wa kanisa kwa sasa ni kuelekeza nguvu zetu kwa wakristo wote Tanzania kwa chama chetu cha CHADEMA katika uchaguzi ujao ili maslahi ya kanisa yarudi kama zamani,” unadai waraka huo.

Waraka huo umevuja zaidi katika misikiti mbalimbali ya Jimbo la Mwanga linaloongozwa na Profesa Jumanne Maghembe.

Habari za uhakika zilizopatikana jana zimelidokeza Mwananchi kuwa Desemba 20 mwaka huu, waraka huo ulisomwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti katika eneo la Tingatinga lililo Kifaru mkoani Kilimanjaro.

Hata hivyo, Prof. Maghembe anayedaiwa alikuwepo katika harambee hiyo amekana kuufahamu au kuuona na kuna habari kuwa sumu yake imeanza kutafuna kampeni za chini za ubunge wilayani Mwanga.

"Sijauona huo waraka kama uko Mwanga nitaupata," alisema Profesa Maghembe ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika ujumbe wake mfupi wa maandishi alioutuma Mwananchi alipoombwa ufafanuzi.

Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo jana alithibitisha kuuona waraka huo na kueleza kwamba umeshasambaa maeneo mengi ya wilaya ya Mwanga, lakini akasema anavyouona si waraka rasmi wa kanisa.

"Hata kama Kanisa litasema ni feki lakini 'damage' (uharibifu) ni mkubwa umeshasambaa na ni hatari sana… linatakiwa jicho la karibu sana kwa sababu mwelekeo huo ukiachiwa unaweza kusababisha umwagaji wa damu," alisema.

Mwenyekiti wa CCM mkoani Kilimanjaro, Vicky Nsilo Swai hakutaka kuzungumzia suala hilo alipoulizwa na Mwananchi kama ana taarifa na waraka huo, badala yake akataka Mwananchi iwasiliane na Kanisa Katoliki kwa kuwa ndilo linaguswa.

"Kauli ya kanisa katika hilo ni 'very important'(muhimu sana ); wakubwa hao ndio wanatakiwa waseme kwa sababu linagusa kanisa lakini ifahamike pia Tanzania haiendeshwi kidini tuna katiba na sheria zetu," alisema. Mpaka jana mchana ilikuwa haijaweza kufahamika sababu hasa za waraka huo kuanza kusambaziwa Mwanga, japo maudhui ya waraka wenyewe umeelekezwa kwa maaskofu, mapadre na wachungaji nchi nzima.

Source: Mwananchi

Kanisa Katoliki ni 'very organised institution'. Lina wasomi na wataalamu wa kila aina. Na hivyo, haliwezi kufanya kitu cha kipuuzi kama hicho. Ukiachilia mbali 'newsletters' ambazo zinaweza kuandikwa na kuchapishwa na parokia fulani kutokana na mahitaji yao au 'document' inayohusu taasisi mojawapo na maendeleo yake, nyaraka zote za Kanisa Katoliki zinaandikwa na (authorised by) maaskofu kwenda kwa Wakristo na mara zote huwa zina majina yao.

Hakuna waraka wowote wa Kanisa Katoliki ambao unasambazwa bila kuwa na majina ya waliouandika na kama waraka huu unasambazwa kwa maaskofu, mapadre na wachungaji nchi nzima, umeandikwa na nani? Note: Wachungaji si moja ya viongozi wa Kanisa Katoliki! Hapa inaonesha aliyeandika waraka huu hana uelewa wa safu ya viongozi wa Kanisa Katoliki.

Tetesi za waraka huu zilianza kusikika miezi kadhaa iliyopita na kama alivyosema mwenyekiti wa TEC, ni vyema vyombo vya dola viwakamate hao wanaousambaza ili waeleze wanautoa wapi na hapo ndipo ukweli utakapojulikana.

Sababu ni kwamba unaonekana kuwa waraka hatari na wenye lengo la kuwagawa Watanzania. Na pengine kwa vile umeonekana ukigawiwa msikitini, hao viongozi wa msikiti ndio wangeweza kusaidia vyombao vya dola kujua waliupata wapi. Binafsi, naona kuna watu wanacheza mchezo mchafu hapa ili kuleta mgawanyiko na migogoro ya kidini katika taifa letu.
 
Wakuu
Hapa inabidi kufikiri zaidi. CCM huwa kuna kamati ya Fitna. Na hii kamati kazi yake ndiyo hii ya kufitinisha ili kuchanganya watu.

Pamoja na haya, nafikiri zaidi ifuatavyo:
-Wilaya ya Mwanga, kuna Waislamu wengi kuliko Wakiristo
-Mbunge wao ni Mwislamu
-Anaonekana kukabwa koo na mgombea Mkristo
-Kawaida ya watu wa Mwanga hawana udini katika uchaguzi
-Watu wa Mwanga huwa wana ugonjwa wa "Ugweno" na "Usangi"

Kwa hiyo, waraka huu feki kautafuta Profesa Maghembe ili kumwaga fitna ili kuokoa jahazi.

BTW: Huu waraka feki ulishajadaliwa hapa jamvini kipindi tunajadili waraka wa Kanisa Katoliki. Kilizuka kikundi fulani DSM kikaandika huu feki ili kupotosha ule wa wazi. Profesa ameukimbilia ili umwokoe lakini si mpya na ndiyo maana umesomwa msikitini na msomaji alikuwa Profesa mwenyewe. Habari ndiyo hiyo.

Mbona Prof. kasema hajauona???
 
Acheni hizo fikra mgando Jee mmesahau katika uchaguzi uliyopita baadhi ya vikundi vya kiislamu vilipiga kampeni ya kutoichagua ccm na matokeo yake yalikuwaje? Mkumbuke kuna mamilioni ya watu ambao mnaweza kuwaita wajinga lakini pamoja na mimi bado tunaipenda ccm. Tatizo la nchi hii ni ubinafsi serikali haiajiri watu kutokana na muelekeo wa siasa hivyo kuna wengi ambao wapo kwenye ajira za umma ambao wanafanya mambo kifisadi hivi mnailaumu ccm???? Vinginevyo wawekwe makada katika sehemu hizo lazima mtalalamika. The only way forward ni kuwa na independent Ethic Code body yenye meno makali ili kuhakikisha kila kiongozi ambaye ana miliki mali iwe imepatikana kihalali vinginevyo kutaifisha
 
Lisemwalo lipo na kama halipo laja. Sasa CCM haifai, CUF haifai, Vp Chadema.

Inawezekana hata Chadema wana play hapo. Vipi waraka huo uonekane Mwanga wakati Dar sijasikia.

Lisemwalo Lipo. Chadema ....Vs......katoliki.
 
Wanataka kukimbia upuuzi wao, kanisa katoliki ndio limeandika huu waraka likazambaza kwa siri kuona joto linaendaje

Christian fundementalist at work! shame on them, wamezoea "Kupendelewa" hawataki justice lol

UKISIKIA KITU NA UKAKIKUBALI BILA KUFANYA UCHUNGUZI........ unaonyesha jinsi ambavyo unaendeshwa na hisia...... wenyewe wameukana halafu wewe unasema ni wa kwao.....MWAGA USHAHIDI.......

Waraka huu umeandikwa na wakatoliki kuendeleza mikakati yao kama kawaida,
Hawa jamaa wanamambo mengi ambayo mengine hivi karibuni yameshtukiwa na wa Tanzania, kamavile kusaini memorandam za siri na serikali, nk

Sasa dili lililo kuwa la siri kwa mapadre, limeshtukiwa sasa wanalikataa, mengi yatajitokeza na siri nyingi zitafumbuka, na mtawatamani sana viongozi waliokuwa wanailinda Catholic party warudi!!

This is transparency Gorverenment, ujinga wote utajulikana, na catholic mtakana mengi, unafiki unaanza kufichuka.

Yote yaliyoandikwa kwenye waraka yalikuwa tayari yanafahamika kwa watanzania anyway! sas wanakana nini? No more excuse!!!!!!

MWAGA USHAHIDI........
 
Mbona Prof. kasema hajauona???
sishangai viongozi wetu kukana walichotamka a.k.a kumeza maneno yao....
1. ZENJI KUJIUNGA NA OIC WALIKANA BAADAYE WAKAKUBALI (wakalifungia gazeti la motomoto)
2. LORIONDO KUUZWA, WALIKANA BAADAYE WALIKUBALI (wakalifungia gazeti la motomoto)
3. KIKWETE MWENYEWE KAANZA KUKANA BAADHI YA MAMBO ALIYOYAAHIDI WAKATI WA KAMPENI
 
Wakuu
Hapa inabidi kufikiri zaidi. CCM huwa kuna kamati ya Fitna. Na hii kamati kazi yake ndiyo hii ya kufitinisha ili kuchanganya watu.

Pamoja na haya, nafikiri zaidi ifuatavyo:
-Wilaya ya Mwanga, kuna Waislamu wengi kuliko Wakiristo
-Mbunge wao ni Mwislamu
-Anaonekana kukabwa koo na mgombea Mkristo
-Kawaida ya watu wa Mwanga hawana udini katika uchaguzi
-Watu wa Mwanga huwa wana ugonjwa wa "Ugweno" na "Usangi"

Kwa hiyo, waraka huu feki kautafuta Profesa Maghembe ili kumwaga fitna ili kuokoa jahazi.

BTW: Huu waraka feki ulishajadaliwa hapa jamvini kipindi tunajadili waraka wa Kanisa Katoliki. Kilizuka kikundi fulani DSM kikaandika huu feki ili kupotosha ule wa wazi. Profesa ameukimbilia ili umwokoe lakini si mpya na ndiyo maana umesomwa msikitini na msomaji alikuwa Profesa mwenyewe. Habari ndiyo hiyo.

Wacha kutumwagia Pumba! Hivyo unataka tuamini kamba zako? Wapi !
Unafikiri CCM au Profesor mzima haelewi elimu duni ya uraia walio nayo wengi wa Watanzania? Wengi wa Watanzania ni wa kufuata upepo na ukija kwenye masuala ya dini ni kabisa. Kitu kikishaandikwa au kutangazwa kinakuwa ndio hicho kwa wengi wa Watanzania na hata ufanye vipi huwezi kukisawazisha. Sasa Waraka uwe kwa jina la dini ukizungumzia mafarakano ya kidini iwe CCM au Maghembe autumie? Wana uwezo gani wa kuwabadilisha Watanzania wahisi kuwa hayo yanayosemwa dhidi yao si kweli? Mbona hivi sasa wana kazi ya kujisafisha na ufisadi na wanashindwa halafu wakalianzishe hili?
Samahani ! mwenye akili yake akiacha unazi hawezi kukubali utumbo uliouandika. Bado atafutwe mchawi kwa hili na kwa mujibu wa matukio mbali mbali inawezekana ikawa huu waraka ulikuwa siri na ukavuja na si rahisi mtu kujibebesha nao sasa lakini waliozoeya kufanya hivi ndio wenye fursa nzuri ya kutowa nyaraka kama hizi.
 
Haya ndio mazingira halisi ya nchi yetu. Kwangu si jambo la kushangaza kuusikia waraka kama huo. Na nyingi nyingine zitakuja, kwani tatizo ni kutoka kwa ule waraka wa kwanza wa katoliki.

Kuwa Katoliki liliikumbatia na kutawala kupitia CCM siku za nyuma, ni maelezo yanayojieleza wazi hapa chini. Soma nukuu hii kwa makini.

"Kadhalika waraka huo unaenda mbali na kudai kuwa vyama vya CCM na CUF kwa sasa havifai kwa kanisa kwa kuwa vimekuwa mithili ya mbwa mwitu aliyejivika ngozi ya kondoo, huku ukitahadhariha kuwa Mahakama ya Kadhi na OIC ni hatari kwa Ukristo."

Kama hivi leo havifai, ni lini vilifaa na kwanini?
Hebu angalia mapendekezo ya chama mbadala katika nukuu hapa chini. (Kwa bahati mbaya sijasikia tamko lolote lile juu ya kauli hii toka kwa viongozi wa CHADEMA) lAKINI HASA NI NINI MAANA YAKE?

"Mwelekeo wa kanisa kwa sasa ni kuelekeza nguvu zetu kwa wakristo wote Tanzania kwa chama chetu cha CHADEMA katika uchaguzi ujao ili maslahi ya kanisa yarudi kama zamani,” unadai waraka huo."

Je wewe mwananchi unakubaliana na hilo. Kuwa CHADEMA inamvuto wa kikatoliki si siri.Na ushahidi kamili unajitokeza pale ambapo CHADEMA ina ushirikiano wa moja kwa moja na chama cha CHRISTIAN DEMOCRATIC PARTY (CDU) cha ujerumani. Si hivyo tu bali hata msaada mkubwa wapesa za kampeni huchangiwa toka katika shirikishi la kanisa katoliki la ujerumani na matajiri wa kijerumani wenye mgusu na msimamo mkali wa kikatoliki.

Ni kweli watanzania tunahitaji kukikabidhi madaraka chama chenye maadili ya aina hiyo. Yote tisa lakini ni muhimu tujifunze toka kwa jirani zetu Rwanda, Burundi na hata Kongo.

Mpaka hatujapata vyama mbadala kwa CCM, NI VYEMA KUBAKI NA ZIMWI LIKUJUALO.
 
JK hana sababu ya kuonewa huruma kwani yeye mwenyewe anajitosheleza kwa ukakamavu na uongozi thabiti,tatizo lenu mliomadogma mkipumbazwa tuu mmepambazishwa!Mtasema sana lakini ukweli utabaki palepale JK ndiye chaguo la watanzania wengi wenye kutaka amani na utulivu sasa kama nyie mnataka fujo(na tayari tunawajua kawaida yenu ni fujo hata mashuleni mlifahamika) ameni nchi na mwende kwa ndugu yenu M7 tuachieni nchi yetu

Mawazo mfu
 
Huo ni waraka wa CCM na si wa kanisa! CCM tu ndio wana muda wa kupandikiza chuki na majungu ili waendelee kuhodhi madaraka kifisadi na si kanisa kwani kanisa liko kuhubiri amani na umoja! JK atang'oka tu na hata akiiba kura tena mwisho wake utakuwa mbaya kama fisadi mwenzake mkapa. Hivi Mkapa anajisikiaje pale ambapo Mwinyi akipita mahali anashangiliwa na yeye akipita anazomewa!JK naye atazomewa sana kama tu bado akiwa madarakani ameanza kutupiwa mawe!

Sipendi mengi ya CCM lakini sipendi pia kuwa mnafiki. Siamini kuwa CCM wana haja ya kupandikiza jungu kama hili kwao wao itakuwa ni very cheap.

Tuwe wakweli na kuangalia tangu lini CCM wakakimbia kivuli chao badala ya kutetea matendo yao hata yawe mabaya? Tangu lini CCM wamewakataa wanaotajwa kwa ufisadi badala yake ndio wanawatetea.
Yanayoelezwa kwenye Waraka ni mambo ambayo CCM imekuwa ikishutumiwa nayo na wao wamekuwa mbele kuyatetea sasa wakurupuke na kujivika nayo kwa lengo gani?
Tunajidanganya tukifikiri kuwa CCM wanateteruka na vijineno vyetu humu JF, wao wanaamini kuwa wananchi wako nyuma yao. Naomba tujuulize hao tunaowaita wapiganaji wako wapi? Ni CCM na hao mafisadi wako wapi ? ni CCM kwa hivyo kwao wao ni moja baya au zuri linakaribishwa CCM.
Waraka huu bado una harufu ya Kanisa au kikundi fulani ndani ya Kanisa, suwala ni kuwa jee Kanisa kama Kanisa lina msimamo gani na waraka huo? Na iwapo linajivuwa na waraka huo basi tamko la kulaani yaliyoandikwa kwenye waraka huo ndio itakuwa kujinasua lakini kuanza kutafut mchawi bila ya kupinga lililotamkwa hakusaidii.
 
Unataka watamke na kuukataa mara ngapi ? Wao wamesema waraka wao wa mwanzo umesimama na ndiyo waraka pekee . Mbona hamuuleti hapa tuanmgalie kuanzia majina na sahihi ? Maana ukiwa hapa kila kitu kitaonekana waandishe waweke ngoma hapa badala ya kuandika habri tupu . Kanisa Katoliki hawawezi kukimbia maandiko yao hawana uoga huo. Kama huamini ngojea rungu la Pengo maana amekaa anautafuta ukweli then utamsikia
 
Lisemwalo lipo na kama halipo laja. Sasa CCM haifai, CUF haifai, Vp Chadema.

Inawezekana hata Chadema wana play hapo. Vipi waraka huo uonekane Mwanga wakati Dar sijasikia.

Lisemwalo Lipo. Chadema ....Vs......katoliki.

Kama hujasikia ni tatizo lako mwenyewe. Tetesi za waraka huu kuwepo zilianza kusikika mara tu baada ya kusambaa kwa Waraka wa Katoliki mwezi wa 7 au 8. Hata kiongozi fulani wa kisiasa aliwahi kusema anajua hata jina la msikiti unaousambaza na akasema akihitajika kuutaja atautaja.
 
Sipendi mengi ya CCM lakini sipendi pia kuwa mnafiki. Siamini kuwa CCM wana haja ya kupandikiza jungu kama hili kwao wao itakuwa ni very cheap.

Tuwe wakweli na kuangalia tangu lini CCM wakakimbia kivuli chao badala ya kutetea matendo yao hata yawe mabaya? Tangu lini CCM wamewakataa wanaotajwa kwa ufisadi badala yake ndio wanawatetea.
Yanayoelezwa kwenye Waraka ni mambo ambayo CCM imekuwa ikishutumiwa nayo na wao wamekuwa mbele kuyatetea sasa wakurupuke na kujivika nayo kwa lengo gani?
Tunajidanganya tukifikiri kuwa CCM wanateteruka na vijineno vyetu humu JF, wao wanaamini kuwa wananchi wako nyuma yao. Naomba tujuulize hao tunaowaita wapiganaji wako wapi? Ni CCM na hao mafisadi wako wapi ? ni CCM kwa hivyo kwao wao ni moja baya au zuri linakaribishwa CCM.
Waraka huu bado una harufu ya Kanisa au kikundi fulani ndani ya Kanisa, suwala ni kuwa jee Kanisa kama Kanisa lina msimamo gani na waraka huo? Na iwapo linajivuwa na waraka huo basi tamko la kulaani yaliyoandikwa kwenye waraka huo ndio itakuwa kujinasua lakini kuanza kutafut mchawi bila ya kupinga lililotamkwa hakusaidii.

Lugha ya huo waraka ina 'harufu' ya wafitini wa Kanisa Katoliki. Sijawahi kuona Kanisa Katoliki likiandika waraka unaosambazwa kwa maaksofu, mapadre na wachungaji na usio na jina la mwandishi wala publisher. Ni lini Kanisa Katoliki likawa na wachungaji? Ni akina nani hawa? Na mwandishi ni nani: maaskofu, mapadre au wachungaji?

Ila tukinusanusa tutakuja kugundua kwamba walioutunga ni wale wanaousambaza pia!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom