Waraka wasambazwa kuitafuna CCM 2010, kanisa Katoliki laukana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wasambazwa kuitafuna CCM 2010, kanisa Katoliki laukana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Selous, Dec 28, 2009.

 1. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwandishi Daniel Mjema

  IKIWA imebaki takribani miezi 10 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, waraka mzito unaodaiwa kuwa wa Kanisa Katoliki umeanza kusambazwa nchini ukiwahamasisha waumini wake kutoichagua CCM.

  Waraka huo unadai suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi na serikali kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC) ni mambo yaliyokataliwa na kanisa, lakini serikali ya awamu ya nne imepuuza kauli hiyo ya kanisa.

  Kadhalika waraka huo unaenda mbali na kudai kuwa vyama vya CCM na CUF kwa sasa havifai kwa kanisa kwa kuwa vimekuwa mithili ya mbwa mwitu aliyejivika ngozi ya kondoo, huku ukitahadhariha kuwa Mahakama ya Kadhi na OIC ni hatari kwa Ukristo.

  Hata hivyo, rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Mhashamu Askofu Yuda Thadei Ruwa'ichi ameukana waraka huo akisema ni 'feki' na kutaka vyombo vya dola kuwatafuta na kuwakamata wanaousambaza.

  "Oktoba mwaka huu lilishafanyika jaribio la kusambaza misikitini waraka feki kama huo, lakini sisi kama kanisa tunasema kama ni waraka wa Wakristo hauwezi kusambazwa misikitini bali makanisani," alisema Askofu Ruwa'ichi alipoongea na Mwananchi.

  Askofu Ruwaichi alisema kama ulivyokuwa waraka ule wa Oktoba ambao aliuelezea kuwa haukuwa wa kanisa hilo, waraka unaosambazwa sasa pia si wa kanisa na kuwataka Watanzania kuwa makini na watu wasiolitakia mema taifa.

  Rais huyo wa TEC alisema wapo watu wanaojaribu kuchezea waraka halali uliotolewa na kanisa hilo ambao mtu yeyote akiusoma ataona kanisa halina shida na mtu mmoja mmoja wala halina mgogoro na dini nyingine.

  "Nawaomba wananchi ambao tayari waraka huo umefika mikononi mwao, wauchunguze vizuri na wamchunguze vizuri mtu anayewapitishia karatasi hatari kama hiyo, kwa sababu ana lengo la kuwapotosha kwa maslahi yake," alisema.

  Waraka huo wenye kurasa tatu ambao Mwananchi imefanikiwa kupata nakala yake unatanguliwa na maandishi yanayosomeka: "Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). Huduma ya Kichungaji katika jamii kuelekea uchaguzi mkuu 2010."

  Kwa mujibu wa maelezo ya waraka huo, ambao inadaiwa kuwa umetolewa na Tume ya Haki na Amani ya TEC, unasambazwa kwa siri kwa maaskofu, mapadre na wachungaji kote nchini na inadaiwa kuwa mtu wa kawaida haruhusiwi kuupewa.

  Waraka huo ambao umesambazwa pia katika misikiti mbalimbali wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, umegusia suala la vita dhidi ya ufisadi ukisema kuendelea kuikumbatia CCM ni hatari kubwa kwa kanisa.

  "Kama kanisa litakuwa kimya bila kulidhibiti, basi kanisa litachafuliwa kwa njia moja au nyingine," unasema waraka huo ukisisitiza kuwa huu ni wakati wa kanisa kushika hatamu ya uongozi wa nchi.

  Waraka huo unaendelea kudai kuwa chini ya awamu ya tatu ya Rais Alli Hassan Mwinyi, kanisa liliweza kudhibiti na kurudisha heshima yake lakini katika awamu ya nne kumekuwa na udhalilishaji wa kanisa wa kiwango cha juu.

  "Mwelekeo wa kanisa kwa sasa ni kuelekeza nguvu zetu kwa wakristo wote Tanzania kwa chama chetu cha CHADEMA katika uchaguzi ujao ili maslahi ya kanisa yarudi kama zamani,” unadai waraka huo.

  Waraka huo umevuja zaidi katika misikiti mbalimbali ya Jimbo la Mwanga linaloongozwa na Profesa Jumanne Maghembe.

  Habari za uhakika zilizopatikana jana zimelidokeza Mwananchi kuwa Desemba 20 mwaka huu, waraka huo ulisomwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti katika eneo la Tingatinga lililo Kifaru mkoani Kilimanjaro.

  Hata hivyo, Prof. Maghembe anayedaiwa alikuwepo katika harambee hiyo amekana kuufahamu au kuuona na kuna habari kuwa sumu yake imeanza kutafuna kampeni za chini za ubunge wilayani Mwanga.

  "Sijauona huo waraka kama uko Mwanga nitaupata," alisema Profesa Maghembe ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika ujumbe wake mfupi wa maandishi alioutuma Mwananchi alipoombwa ufafanuzi.

  Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo jana alithibitisha kuuona waraka huo na kueleza kwamba umeshasambaa maeneo mengi ya wilaya ya Mwanga, lakini akasema anavyouona si waraka rasmi wa kanisa.

  "Hata kama Kanisa litasema ni feki lakini 'damage' (uharibifu) ni mkubwa umeshasambaa na ni hatari sana… linatakiwa jicho la karibu sana kwa sababu mwelekeo huo ukiachiwa unaweza kusababisha umwagaji wa damu," alisema.

  Mwenyekiti wa CCM mkoani Kilimanjaro, Vicky Nsilo Swai hakutaka kuzungumzia suala hilo alipoulizwa na Mwananchi kama ana taarifa na waraka huo, badala yake akataka Mwananchi iwasiliane na Kanisa Katoliki kwa kuwa ndilo linaguswa.

  "Kauli ya kanisa katika hilo ni 'very important'(muhimu sana ); wakubwa hao ndio wanatakiwa waseme kwa sababu linagusa kanisa lakini ifahamike pia Tanzania haiendeshwi kidini tuna katiba na sheria zetu," alisema. Mpaka jana mchana ilikuwa haijaweza kufahamika sababu hasa za waraka huo kuanza kusambaziwa Mwanga, japo maudhui ya waraka wenyewe umeelekezwa kwa maaskofu, mapadre na wachungaji nchi nzima.


  Source: Mwananchi
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  huu waraka ndio uliompeleka methodius kilaini BUKOBA!........STUKA
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwenye hilo feki atuletee hapa tafadhali
   
 4. kibanzi

  kibanzi Member

  #4
  Dec 28, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli hilo feki alilete hapa tusemenalo maana hizi habari bwana
   
 5. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jamiiforums haishindwi kitu,mwenye nao aulete
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hii ni janja ya CCM, waraka huo umetolewa na Makamba na Makala pasi kumsahau Chiligati. Lengo lao kuwapumbaza watz waone kuwa JK anaonewa hivyo aonewe huruma apewe kura 2010. jk na serikali yake ni useless wametuthibitishia hilo kwa miaka 4 waliyotawala.
   
 7. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,424
  Likes Received: 3,786
  Trophy Points: 280
  Hii statement ya "peace maker" nahisi nayo ni feki.................
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huu waraka lazima umeandikwa na propaganda machinery ya CCM ili kuwadumaza wananchi waone kana kwamba Kanisa linamuonea Kikwete kwa hiyo apate sympathy ya waislamu na ndio maana umesambazwa misikitini!! Waraka wa wakisto husambazwa kanisani na unawahusu wakisto na si vinginevyo; hizi spin za watu wa aina ya Salva Rweyemamu!!
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280

  Dhuu.... Kwa hiyo ulishayajua haya mapema. Mbona hukusema kabla???
   
 10. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  JK hana sababu ya kuonewa huruma kwani yeye mwenyewe anajitosheleza kwa ukakamavu na uongozi thabiti,tatizo lenu mliomadogma mkipumbazwa tuu mmepambazishwa!Mtasema sana lakini ukweli utabaki palepale JK ndiye chaguo la watanzania wengi wenye kutaka amani na utulivu sasa kama nyie mnataka fujo(na tayari tunawajua kawaida yenu ni fujo hata mashuleni mlifahamika) ameni nchi na mwende kwa ndugu yenu M7 tuachieni nchi yetu
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Nimeamini kuna watu wame-register humu kwa malengo maalumu.

  Sasa kwa nini unataka wenzako waende kwa M7. Kwani nchi ni ya waliomchgua JK peke yao?? Fikiri kabla ya kuandika!!!
   
 12. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huruma gani? Wa-TZ hatuhitaji nyaraka! Filana, Pilao na Pombe za kienyeji zinatosha! Bila hizo hata alie machozi ya damu, hapati kura!!
   
 13. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,424
  Likes Received: 3,786
  Trophy Points: 280
  Swala si kuwatimulia nchi nyingine kwani wanaweza wakalianzisha huko huko........ si unakumbuka 1979 kilitokea nini na hao wa huko kwa M7........ TAFAKARI.TUCHUA HATUA kabla ya kuandika wazo lisilofaa.......
   
 14. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo unataka tuwashughulikie humu humu?
   
 15. e

  echonza Senior Member

  #15
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utulivu na amani pekee kwa watanzania ni bure. Tunataka mtu anayesimamia ustawi wa nchi hii. Mtu anayeweza kusimamia maamuzi yanayowafanya watanzania kujivunia nchi yao na rasilimali nyingi zilizopo ndani ya ardhi ya nchi hii nzuri.

  Utulivu na amani vinasaidia nini ukisikia mwezi huu mtu kafa na njaa, wakati tuko na rasilimali zote hizo (maji ya kutosha, ardhi yenye rutuba, madini, wataalamu nk); ila tunakosa kiongozi wa kutufanya tunufaike kwa matunda ya vyote hivyo. Hivi hiyo ni amani mtu anapokufa na njaa? Tofauti ni nini kati ya afaye kwa njaa na afaye kwa kupigania haki ya wote? Hizo ni fikira mgando kabisa.

  Mimi sina shida na majina ya viongozi waliopo madarakani leo bali ni staili ya uongozi wao hauna tija kuweza kutuletea mabadiliko na maendeleo ya kweli tunayoyataka watanzania maana mifano mingi ipo; kwamba hilo limeshindikana ndani ya uongozi wao.
   
 16. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180

  Duhh, Mkuu umejuaje? yaani 100% bila kukosea.....Big shame Salva[​IMG]
   
 17. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  Huu waraka umeandikwa na wabaya wa CHADEMA iwe ni CCM, NCCR au vikundi fulani vya waislam nk, lakini lengo kubwa si kuchafua kanisa katoliki bali kuchafua chadema. Hisia zinaniambia Mhe. Makamba anajua huu waraka unatoka wapi. Tungekuwa na vyombo vya upelelezi makini kama FBI ni wiki moja mchawi angepatikana.
   
 18. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hapa hakuna cha Methodius Kilaini wala nani...ni machinery ya ccm at peak of work!

  Wanatafuta legitimacy kwa mbinu ya kijinga hawa., na bahati mbaya imestukiwa...Hizo ni alama za nyakati kwao, na wakae wakijua kwamba wakati wao wa kuwepo unahojiwa na watu...!

  Mwenye macho na aone!
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Pia Kanisa Katoliki wangehusika na waraka huu wangesema wazi, maana hawana tabia ya kujificha, hasa inapokuja orientation yao ya masuala ya hatima ya nchi hii. These guys are bold and they never operate in darkness for a sensitive matter like this!
   
 20. P

  Penguine JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  pengo lete mawazo ujenge nchi yako. JF siyo uwanja wa matusi. hapa unatakiwa umwage points kwa hoja zipi unafikiri waraka huo siyo propaganda za hao wanaosemwa. hapo utaonekana kuwa mwana tafakuri na hujawa personally dogmasified.
   
Loading...