GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,518
- 108,793
ANGALIZO
Waraka huu nautoa kama GENTAMYCINE na siyo GENTAMYCINE mwana CCM au Mpinzani na Mtani Mkuu wa CHADEMA ( anavyojulikana na wengi humu ) na nautoa huku nikimtanguliza Kwanza Mwenyezi Mungu mbele, Unafiki pembeni na nikiiweka Mama Tanzania mbele yangu ili tuendelee kuifurahia Tanzania yetu.
Nawasilisha.

- Nawaomba Wanasiasa wa Tanzania wasameheane upesi kama siyo haraka sana
- Nawaomba Wanasiasa wa Tanzania wakatubu yale yote mabaya waliyosababisha
- Nawaomba Wanasiasa wa Tanzania waache chuki ambazo naona zinatupeleka kubaya
- Nawaomba wana CCM muonyeshe mfano wa Siasa bora na zenye Utu pamoja na Upendo
- Nawaomba wana CHADEMA muonyeshe Uungwana na Ukomavu wenu wa Kidemokrasia
- Naviomba Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Tanzania vitende haki
- Nawaomba Wanasiasa wote mfutane makovu ya Hasira na Vinyongo
- Nawaomba Viongozi wote Wastaafu waingilie kati afya ya wasiwasi ya Kidemokrasia nchini
- Naviomba Vyombo vyote vya Habari nchini vidumishe Upendo na Amani daima
- Namwomba Rais Dr. Magufuli aige busara na hekima za Yesu Kristo / Mtume Mohammed
- Naomba Watanzania wote tusali sana, tupendane na tugange yajayo kwa matendo mema
Nawasilisha.