Waraka wangu Kwako, Mpendwa Mtanzania

MGuccI

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
1,480
1,139
Wasalaam mpendwa natumai u mzima wa afya na kama una maradhi na upone haraka kwa kunywa dawa za mitishamba kwa sababu uwezo wa madawa ya kisasa huna, kama hauko hai Mwenyezi Mungu akurehemu sina uhakika kama walikuzika ama walikufukia nisamehe sana maana nilishindwa kufika katika msiba wako, ni mbali mimi nilipo ni mengi sijazungumza mbele yako lakini kwa kalamu na karatasi leo nakuandikia usijiulize kwa nini nimekimbia kijiji chetu tafadhali lakini tambua kuwa nawakumbuka kila siku.Nahofia sana kulitaja dhumuni la barua hii maana huenda si moja ama mawili mpendwa lakini nakusihi isome barua hii japokuwa ni ndefu sana

Kama hukupata nafasi ya kuingia darasani tangu nilipoondoka kwa sababu ya kukosa pesa ya kulipa ada katika shule tuliyojenga kwa mikono yetu, michango tuliyochangishwa tena kwa kulazimishwa, michango iliyosababisha tufedheheshwe mbele ya wake na watoto wetu, basi mpelekee Athumani yule mtoto wa mwenyeketi wa mtaa aliyebahatika kusomeshwa kwa pesa zetu za kodi akusaidie kuisoma japo najua atakudanganya maneno mengine kwamba nimeandika ndio kumbe nimeandika sio na penye neno elimika atasema danganyika, sikulaumu wewe hata kidogo na yeye pia simlaumu, kijiji chetu sisi ni wapole sana hata tukivuliwa nguo mbele ya wake na watoto wetu bado tutasema tunadumisha amani kijijini kwetu na tutakaa kimya na hasira zetu zikiwa zimejificha.

Nisamehe mpendwa wangu John japo kielimu ulinizidi lakini bado nilipata ajira wewe hukupata, hukuwa na pesa ya kumuhonga mwajiri kama nilivyofanya mimi na mwajiri akasema

"Uzoefu nitaupata kazini".
Mpendwa dada Maria ulikuwa na akili sana darasani na ulitamani sana kuendelea kusoma, ulifurahia mwenyekiti wa kijiji aliposema elimu bure kwa wote lakini hawakunipa pesa za kukununulia sare ya shule na ulipigwa sana kama hukuvaa kiatu cheusi mguuni ndio maana kaka yako alipotaka kuoa ilibidi uolewe wewe ili mali utakayotolewa aitumie yeye kuoa hukupenda kuolewa lakini ilibidi, nisamehe mwanangu kwa kukufanya bidhaa. Nisamehe kwa sababu ni mfumo mbovu ulionisukuma na sasa nimekukimbia unabaki kuteseka mwenyewe kwenye ndoa

Mpendwa Charles sijisikii vyema wanapokuita anti chaz lakini utafanyaje iwapo waarabu waliwafanya hivyo babu zetu, tazama we si mwanaume rijali tena na unalilia haki ya ndoa ya jinsia moja, iko wapi serikal yenu? iko wapi? inasahau upuuzi waliotutendea hao rangi nyeupe tena wasiokuwa na asili ya hapa kwetu inawashangilia wakitoa hoja bungeni, bunge limekwisha thamani yake, bunge limekuwa tena lao na wala si letu!!! Na wananichekesha kweli eti huwa wanakuja kusimamia uchaguzi wenu pale mnapokuwa mnamchagua mkubwa wa kijiji, hivi huwa wanakuja kufanyaje?? Au walishaacha kuja siku hizi?? Hichi kijiji nilichopo wala siwaoni wakija, mwenyekiti ni mkali sana hana uoga dhidi yao.
Nafurahia maisha yangu ya kuwa mkimbizi, nisamehe kwa hilo!!!

Mpendwa Musa ualimu wako umekufikisha wapi? maana nilivyoondoka ulikuwa ndo una mwezi wa kwanza kazini. Vipi bado unavaa nguo zilizochanika matakoni? au viraka kila kona? tazama ofisi yako tazama na familia yako, looh!! ama kweli heshma na sifa ya mwalimu iliyobaki ni ‘SHIKAMOO' nyingi kila kona, yuko wapi huyo mwenyekiti wako aliyekuahidi mshahara mnono kisha akakutukana eti huna maana katka jamii tena akakukejeli kwa mgomo wako baridi? ni wap imepotelea heshima ya jina Mwalimu? zamani ilikuwa sifa leo hii ni aibu kujulikana wewe ni mwalimu. Ualimu na walimu unathaminika sana huku kwetu lakini nasikia huko kwenu wale waliofeli pekee ndio kimbilio lao, kwani nani ambaye anapanga kuwa mwalimu huko kijijini kwenu?? Eti nasikia mwenyekiti wako mpya alioa mwalimu lakini tangu amuoe akaacha ualimu!! Ya kweli hayo ama ni tetesi??? Kama ni kweli rafiki yangu akili za kushikiwa ongezea na za kwako, ujiulize kisha upate jawabu.

Mpendwa nina mengi ya kukuuliza kuhusu kijiji chetu lakini koroboi inafifia na mafuta yanazidi kupanda bei, yule mbunge niliyemchagua hadi leo hajauleta huo umeme aliohaidi maskini kura yangu haijanifaidisha, nimeibiwa kura yangu. Nikiamka salama asubuhi nitaendelea kukujulia hali.

*****

Najua waraka wangu huu haujakuchosha bado, na kalamu yangu bado ina wino na karatasi yangu bado ina nafasi kiasi fulani kuweza kuendelea kuzungumza na wewe.

Mpendwa bibi, nilifurahshwa na barua yako uliyomwambia Athumani aniandikie, ukasema una kiremba kipya ambacho kimefanana na blauzi yako lakini hukusema kuhusu sketi wala kiatu looh! bibi! unanipa raha japo machozi yananitoka kwa udhalilishaji niliosikia unafanyiwa, hivi walipoziba nywele zako zenye mvi na kifua chako kilichonyonyesha watoto kumi na sita lakini wakasahau kukuficha uchi wako, na wakaidharau miguu , sitakulaumu kamwe kwa kufurahia vazi lako hujui ni kwa nini na kamwe hutajua, sina la kukusaidia naogopa kurudi kijijini hapo sijawatenga lakini naogopa kuwa mfungwa huru. Kiremba chako na hilo blauzi yako inayosifia chama tawala hakika ni fedheha. Lakini angalau wamekuvika kwa muda, lakini kwa nini wasikupatie kila mwaka, marafiki gani hao wanafiki wanakuchekea kila baada ya miaka mitano?? Marafiki wanafiki, lakini kwa kuwa umewaamini mimi sina cha kukushauri.

Mpendwa rafiki yangu wa utotoni Lesika, hayo mayai unayouza na maji ya kufunga kwenye mifuko ni lini utakidhi mahitaji yako? ni lini utakuwa na familia yako au una mpango wa kuwa padri?? kama una mpango huo fanya haraka kuijibu barua yangu hii nikutumie maombi kwa wamisionari labda watakuchagua na ulivyo na rangi ya mikosi wanataka rangi nyeupe eti wanasema rangi ya Mungu.

Usiwadharau bali jidharau wewe, wao ndio wametunga sheria na kuweka masharti ili wewe uungue na jua na ufe mapema uwe mbolea kwenye mazao yao. Lesika ndugu yangu akili yako imeganda na wa kuiyeyusha hayupo amefichwa, usijidanganye eti wewe na ukapuku wako utamjua alipo? ukijaribu tu!! nitakutana na wewe ahera.

Wapendwa mama zangu, nimesikia vinywa vyenu vimeyaruhusu meno yenu, yamecheka kwa furaha eti kwenye baraza wameongezewa wawakilishi, najua hamkukaa mkafikiri laiti mngefikiria na kutafakari majina ya hao kina mama hao ni walewale wacheza ngoma wenzake enzi za utoto na baadae kumbi za starehe huko mjini leo hii amewaleta ikulu wacheze nae tena huku wanakula jasho lenu bila huruma, mama kuna ulazima wa kutabasamu? mi nakuandikia haya si kwa ubaya, usinichukie mwanao. Japo ni aibu kubwa sana nimekimbia kijiji changu.

Mpendwa katika elimu Nshomile ndio jina lako niliambiwa huko kwenu unaitwa Rubani na kwenye kile kijumba chako cha udongo kilichozungukwa na migomba hawaish wazee kuja kufanya matambiko tangu uchaguliwe kujiunga darasa la 13 mchepuo wa Fizikia, Kemia na Hisabati. Sina uhakika sana na Urubani wako labda usubiri katiba ibadilishwe na Nyungo za Wachawi ziruhusiwe kupasua anga ya Tanga kwenda Shinyanga na wewe uwe mmoja wa marubani Sikutukani Nshomile lakini soma umalize na siku moja utaniita Mtabiri. Lakini kwa hasira kubwa najua waweza kuniita mchawi wako.
Rafiki wa wa ujanani Fredrick wanajiuliza kimekusibu nini hadi hauendi kanisani ngoja nikusaidie kuwapa jibu, utakuwa mjinga hadi lini? mchungaji anaishi nyumba nzuri na kula kuku kama ilivyo kawaida yako kula mlenda pori na utumbo wa kuku mara moja moja.

Huyo huyo mchungaji anakupangia sadaka ya kutoa Wasalaam mpendwa natumai u mzima wa afya na kama una maradhi na upone haraka kwa kunywa dawa za mitishamba kwa sababu uwezo wa madawa ya kisasa huna, kama hauko hai Mwenyezi Mungu akurehemu sina uhakika kama walikuzika ama walikufukia nisamehe sana maana nilishindwa kufika katika msiba wako, ni mbali mimi nilipo ni mengi sijazungumza mbele yako lakini kwa kalamu na karatasi leo nakuandikia usijiulize kwa nini nimekimbia kijiji chetu tafadhali lakini tambua kuwa nawakumbuka kila siku.Nahofia sana kulitaja dhumuni la barua hii maana huenda si moja ama mawili mpendwa lakini nakusihi isome barua hii japokuwa ni ndefu sana

Kama hukupata nafasi ya kuingia darasani tangu nilipoondoka kwa sababu ya kukosa pesa ya kulipa ada katika shule tuliyojenga kwa mikono yetu, michango tuliyochangishwa tena kwa kulazimishwa, michango iliyosababisha tufedheheshwe mbele ya wake na watoto wetu, basi mpelekee Athumani yule mtoto wa mwenyeketi wa mtaa aliyebahatika kusomeshwa kwa pesa zetu za kodi akusaidie kuisoma japo najua atakudanganya maneno mengine kwamba nimeandika ndio kumbe nimeandika sio na penye neno elimika atasema danganyika, sikulaumu wewe hata kidogo na yeye pia simlaumu, kijiji chetu sisi ni wapole sana hata tukivuliwa nguo mbele ya wake na watoto wetu bado tutasema tunadumisha amani kijijini kwetu na tutakaa kimya na hasira zetu zikiwa zimejificha.

Nisamehe mpendwa wangu John japo kielimu ulinizidi lakini bado nilipata ajira wewe hukupata, hukuwa na pesa ya kumuhonga mwajiri kama nilivyofanya mimi na mwajiri akasema

"Uzoefu nitaupata kazini".
Mpendwa dada Maria ulikuwa na akili sana darasani na ulitamani sana kuendelea kusoma, ulifurahia mwenyekiti wa kijiji aliposema elimu bure kwa wote lakini hawakunipa pesa za kukununulia sare ya shule na ulipigwa sana kama hukuvaa kiatu cheusi mguuni ndio maana kaka yako alipotaka kuoa ilibidi uolewe wewe ili mali utakayotolewa aitumie yeye kuoa hukupenda kuolewa lakini ilibidi, nisamehe mwanangu kwa kukufanya bidhaa. Nisamehe kwa sababu ni mfumo mbovu ulionisukuma na sasa nimekukimbia unabaki kuteseka mwenyewe kwenye ndoa

Mpendwa Charles sijisikii vyema wanapokuita anti chaz lakini utafanyaje iwapo waarabu waliwafanya hivyo babu zetu, tazama we si mwanaume rijali tena na unalilia haki ya ndoa ya jinsia moja, iko wapi serikal yenu? iko wapi? inasahau upuuzi waliotutendea hao rangi nyeupe tena wasiokuwa na asili ya hapa kwetu inawashangilia wakitoa hoja bungeni, bunge limekwisha thamani yake, bunge limekuwa tena lao na wala si letu!!! Na wananichekesha kweli eti huwa wanakuja kusimamia uchaguzi wenu pale mnapokuwa mnamchagua mkubwa wa kijiji, hivi huwa wanakuja kufanyaje?? Au walishaacha kuja siku hizi?? Hichi kijiji nilichopo wala siwaoni wakija, mwenyekiti ni mkali sana hana uoga dhidi yao.
Nafurahia maisha yangu ya kuwa mkimbizi, nisamehe kwa hilo!!!

Mpendwa Musa ualimu wako umekufikisha wapi? maana nilivyoondoka ulikuwa ndo una mwezi wa kwanza kazini. Vipi bado unavaa nguo zilizochanika matakoni? au viraka kila kona? tazama ofisi yako tazama na familia yako, looh!! ama kweli heshma na sifa ya mwalimu iliyobaki ni ‘SHIKAMOO' nyingi kila kona, yuko wapi huyo mwenyekiti wako aliyekuahidi mshahara mnono kisha akakutukana eti huna maana katka jamii tena akakukejeli kwa mgomo wako baridi? ni wap imepotelea heshima ya jina Mwalimu? zamani ilikuwa sifa leo hii ni aibu kujulikana wewe ni mwalimu. Ualimu na walimu unathaminika sana huku kwetu lakini nasikia huko kwenu wale waliofeli pekee ndio kimbilio lao, kwani nani ambaye anapanga kuwa mwalimu huko kijijini kwenu?? Eti nasikia mwenyekiti wako mpya alioa mwalimu lakini tangu amuoe akaacha ualimu!! Ya kweli hayo ama ni tetesi??? Kama ni kweli rafiki yangu akili za kushikiwa ongezea na za kwako, ujiulize kisha upate jawabu.

Mpendwa nina mengi ya kukuuliza kuhusu kijiji chetu lakini koroboi inafifia na mafuta yanazidi kupanda bei, yule mbunge niliyemchagua hadi leo hajauleta huo umeme aliohaidi maskini kura yangu haijanifaidisha, nimeibiwa kura yangu. Nikiamka salama asubuhi nitaendelea kukujulia hali.

*****

Najua waraka wangu huu haujakuchosha bado, na kalamu yangu bado ina wino na karatasi yangu bado ina nafasi kiasi fulani kuweza kuendelea kuzungumza na wewe.

Mpendwa bibi, nilifurahshwa na barua yako uliyomwambia Athumani aniandikie, ukasema una kiremba kipya ambacho kimefanana na blauzi yako lakini hukusema kuhusu sketi wala kiatu looh! bibi! unanipa raha japo machozi yananitoka kwa udhalilishaji niliosikia unafanyiwa, hivi walipoziba nywele zako zenye mvi na kifua chako kilichonyonyesha watoto kumi na sita lakini wakasahau kukuficha uchi wako, na wakaidharau miguu , sitakulaumu kamwe kwa kufurahia vazi lako hujui ni kwa nini na kamwe hutajua, sina la kukusaidia naogopa kurudi kijijini hapo sijawatenga lakini naogopa kuwa mfungwa huru. Kiremba chako na hilo blauzi yako inayosifia chama tawala hakika ni fedheha. Lakini angalau wamekuvika kwa muda, lakini kwa nini wasikupatie kila mwaka, marafiki gani hao wanafiki wanakuchekea kila baada ya miaka mitano?? Marafiki wanafiki, lakini kwa kuwa umewaamini mimi sina cha kukushauri.

Mpendwa rafiki yangu wa utotoni Lesika, hayo mayai unayouza na maji ya kufunga kwenye mifuko ni lini utakidhi mahitaji yako? ni lini utakuwa na familia yako au una mpango wa kuwa padri?? kama una mpango huo fanya haraka kuijibu barua yangu hii nikutumie maombi kwa wamisionari labda watakuchagua na ulivyo na rangi ya mikosi wanataka rangi nyeupe eti wanasema rangi ya Mungu.

Usiwadharau bali jidharau wewe, wao ndio wametunga sheria na kuweka masharti ili wewe uungue na jua na ufe mapema uwe mbolea kwenye mazao yao. Lesika ndugu yangu akili yako imeganda na wa kuiyeyusha hayupo amefichwa, usijidanganye eti wewe na ukapuku wako utamjua alipo? ukijaribu tu!! nitakutana na wewe ahera.

Wapendwa mama zangu, nimesikia vinywa vyenu vimeyaruhusu meno yenu, yamecheka kwa furaha eti kwenye baraza wameongezewa wawakilishi, najua hamkukaa mkafikiri laiti mngefikiria na kutafakari majina ya hao kina mama hao ni walewale wacheza ngoma wenzake enzi za utoto na baadae kumbi za starehe huko mjini leo hii amewaleta ikulu wacheze nae tena huku wanakula jasho lenu bila huruma, mama kuna ulazima wa kutabasamu? mi nakuandikia haya si kwa ubaya, usinichukie mwanao. Japo ni aibu kubwa sana nimekimbia kijiji changu.

Mpendwa katika elimu Nshomile ndio jina lako niliambiwa huko kwenu unaitwa Rubani na kwenye kile kijumba chako cha udongo kilichozungukwa na migomba hawaish wazee kuja kufanya matambiko tangu uchaguliwe kujiunga darasa la 13 mchepuo wa Fizikia, Kemia na Hisabati. Sina uhakika sana na Urubani wako labda usubiri katiba ibadilishwe na Nyungo za Wachawi ziruhusiwe kupasua anga ya Tanga kwenda Shinyanga na wewe uwe mmoja wa marubani Sikutukani Nshomile lakini soma umalize na siku moja utaniita Mtabiri. Lakini kwa hasira kubwa najua waweza kuniita mchawi wako.
Rafiki wa wa ujanani Fredrick wanajiuliza kimekusibu nini hadi hauendi kanisani ngoja nikusaidie kuwapa jibu, utakuwa mjinga hadi lini? mchungaji anaishi nyumba nzuri na kula kuku kama ilivyo kawaida yako kula mlenda pori na utumbo wa kuku mara moja moja.

Huyo huyo mchungaji anakupangia sadaka ya kutoa anasema kima cha chini ni noti anaona haya kusema 500 na waumini wanapga makofi na vigelegele, vya nini hvyo? wakati ni kumuhudumia mwanaume anayejiweza? anakudanganya kwa kutoa mashetani na kuponya vilema, hata umasikini ni kilema basi angekuponya na wewe Fred. Nadhani hapo ningekiri kuwa huo ulokole upo. Vinginevyo nakupa pole.

Jua limewaka natakiwa kwenda shambani nikirudi nitaendelea kukuulizia kuhusu wamasai wanaofahamu eti rais aliyeko madarakani anaitwa "Nyerere" halafu nasikia kila uchaguzi wanashiriki sina uhakika sana kama huko kijijini kwenu neno linaloitwa kampeni mnalifahamu na nina wasiwasi sana huenda kura zenu anaenda mwenyekiti wa kitongoji kuwawakilisha looo!! bwana mkubwa ananichekesha sana yaani uwakilishaji hadi kwenye kupiga kura?? Heri yao Wakurya hawajui tofauti kati ya KURA na KULA.Wakiombwa Kura wanajua ni Kula.Na ndio maana miji yao ni mibovu na miundo mbinu hakuna, magari tabu kufika pale inapita misafara ya wasichana wanaoenda Kukeketwa kwa hiari yao wakiwa na furaha. Wanasahau madhara yaliyopo mbeleni.

anasema kima cha chini ni noti anaona haya kusema 500 na waumini wanapga makofi na vigelegele, vya nini hvyo? wakati ni kumuhudumia mwanaume anayejiweza? anakudanganya kwa kutoa mashetani na kuponya vilema, hata umasikini ni kilema basi angekuponya na wewe Fred. Nadhani hapo ningekiri kuwa huo ulokole upo. Vinginevyo nakupa pole.

Jua limewaka natakiwa kwenda shambani nikirudi nitaendelea kukuulizia kuhusu wamasai wanaofahamu eti rais aliyeko madarakani anaitwa "Nyerere" halafu nasikia kila uchaguzi wanashiriki sina uhakika sana kama huko kijijini kwenu neno linaloitwa kampeni mnalifahamu na nina wasiwasi sana huenda kura zenu anaenda mwenyekiti wa kitongoji kuwawakilisha looo!! bwana mkubwa ananichekesha sana yaani uwakilishaji hadi kwenye kupiga kura?? Heri yao Wakurya hawajui tofauti kati ya KURA na KULA.Wakiombwa Kura wanajua ni Kula.Na ndio maana miji yao ni mibovu na miundo mbinu hakuna, magari tabu kufika pale inapita misafara ya wasichana wanaoenda Kukeketwa kwa hiari yao wakiwa na furaha. Wanasahau madhara yaliyopo mbeleni.

By George Iron
0655 727325
 
Una shule ndogo lakini unajitahidi! Ila kama wewe huna kazi sisi wengine tunazo; uwe unaandika kwa kifupi na uzingatie vituo!

Umeelewa? Haya
 
Back
Top Bottom