Waraka wangu kwako mmiliki mtarajiwa,mmiliki mpya na mmiliki wa zamani wa biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wangu kwako mmiliki mtarajiwa,mmiliki mpya na mmiliki wa zamani wa biashara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kitomai, Nov 2, 2009.

 1. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,037
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145

  Rejea kutoka katika matangazo madogo madogo ya tarehe 27th october 2009 yenye kichwa cha matangazo kisemacho'' Je, unahitaji kupata kipato cha ziada?''. Sasa chukulia tayari umefungua biashara yako. Ukiwa kama mmiliki unatafuta njia za kuiboresha ili iendelee kustawi. Tayari una orodha ya majina ya watu 120, sasa unataka kusonga hatua moja mbele kuelekea kwenye ustawi. Unahitaji kufuta au ku ''delete'' virus au kuufanyia ''format '' mfumo mzima wa akili na ku-''install'' mfumo mpya uanoendena na mazingira mapya ya biashara unayoimiliki. Kumbuka zama hizi za chuma kuna watu wanafanya biashara kubwa na kujipatia mamilioni ya fedha ukiangalia vitendea kazi anavyovitunia utaona ana, ''laptop, meza, kiti na internet''. Sasa tunaaza safari kuutengeneza au kuuboresha mfumo mzima wa kufikiri. Mfumo huo ukiboreshwa mtu aweza kufanya kazi, kiwango chake cha ''performance'' kikawa juu
  .


  Mara nyingi sana unakutana na maoni yanayozungumzia namna ya kuanzisha na kumiliki biashara na kisimamia, matharani njia muafaka za kutunza vitabu vya mahesabu, namna ya kutunza majarada na namna ya kuwanasa wateja.

  Binafsi nitakuwa nikitoa mfululizo wa maoni yatayogusa katika eneo moja muhimu katika ustawi wa biashara ambayo sasa unaimiliki. Eneo hilo linahuska na mahusiano ya ufahumu wa akili zako na biashara unayoimiliki sasa. Awali ya yote unatakiwa kujua kwamba hatma ya ustawi au kutostawi kwa biashara yako iko mikononi mwako. Wewe ndiyo mwezeshaji wa kuifanya biashara istawi au idumae. Hakuna mwingine zaidi yako.

  Unatakiwa uendelee kuwa na msisimko huo katika maisha yote ya biashara bila kujari mafanikio utakayokuwa umeyapata awali. Ninayokawaida ya kubadirishana uzoefu mara kwa mara watu wanaomiliki biashara zao. Ninayo hazina ya kutosha kubadirisha na wewe uzoefu huo mfululizo kwa kipindi cha muda mrefu na nitakuwa nikikumegea kidogo kidogo. Uzoefu huo utakuwa mwenza unayetembea naye siku zote katika maisha ya hiyo biashara unayoimiliki. Utakufanya usijisikie mpweke ''lonely'' au '' Isolated''. Tambua utajikuta wewe mwenyewe unafanya kazi kama ofisi meneja, mhasibu, karani wa kutunza kumbu kumbu, mkurugenzi, unalo jukumu la kuandaa mpango wa biashara,┬ů.

  Jifunze namna ya kujihamasisha
  Kumbuka siku zote hatma ya ustawi wa biashara unayoimiliki ipo mikononi mwako wewe pekee. Hivyo basi, jijengee nia ya kutaka kufanikiwa kwa kujihamasisha kuwa wewe unaweza kufanya biashara yako ikastawi, wadau wengine wanaweza kutoa mchango kwa wewe kufanikiwa lakini jukumu kubwa linabakia mikononi mwako na hii itatokana na namna unavyoichezesha akili yako katika kuistawisha biashara yako. Nini unajiambia? Utasikia mtu analopoka biashara bwana hauewezi kufanya hivi hivi tu lazima uende kawa fundi akakutengeze!Au mimi sina karama sijajariwa na yeye aliye juu! Hivyo siwezi! Basi bora useme kama alivyojisemea mtume Paulo,'' Ninayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu''. Zaidi vipi unajihamasisha, nitakuwa ninakumegea kidogo kidogo katika mfululizo wa mawaidha yatakayofuata baada ya leo. Kwa kifupi mfululizo huu utawahusu sana wafuatao. (i)Wale ambao wana mawazo ya kumiliki biashaza zao.(ii) Wale ambao tayari wanamiliki biashara zao lakini wanahitaji kuziboresha (iii) Wale ambao wanatatizo la kujihamasisha (iv)Wale ambao wamesoma vitabu vya namna ya kuendesha biashara lakini hawajapata tiba ya mihemko''emotions".(v) Mwisho, wale ambao wanafanya kazi katika makampuni lakini wangependa kuwa na ubora walionao wale wanaomiliki biashara zao.

  INAENDELEA┬ů


  ADVERTISIMENT

  PROPERTY
  For Lease and Sale
  If you wish to lease or sale a shop, beach plot, office, showroom, bungalow, commercial plot, townhouse, apartment, warehouse, please call 0171114409/0784225000/0755312233 or email:emanuel@gmail.com
  MOTOR VEHICLES
  If you wish to sale or buy a used motor vehicle, please call:0717114409/0784225000/0755312255 or email:emanuel.kayinga@gmail.com
   
Loading...