Waraka wangu kwako Mh Rais John Pombe Magufuli

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Rais wangu Daktari John Pombe Magufuli, ninakuandikia maneno haya machache kama furaha yangu kuwa na rais kama wewe ambaye taifa lilimsubiri kwa miongo kadhaa, Wakati nikikupongeza kwa ustahimilivu na uchapakazi wako hasa kwakutowasikiliza wapiga kelele dhidi ya msaidizi wako mpendwa mkuu wa mkoa wa Dar, nashawishika kukwambia kwamba video hii hapa chini ni ya mkuu wa mkoa wa Dar iliyorekodiwa kwa kutumia kamera za kiusalama (cctv).

Video inaelezwa hapo ni kituo cha tv cha Clouds na kwamba mkuu wako wa Mkoa alivamia kituo hicho kwalengo alijualo yeye, yaani amevamia kwatumia jeshi letu linalotumia kodi za wananchi kwa mambo yanayodhaniwa ni binafsi. Kibaya zaidi amevamia kituo chako pendwa kabisa cha tv hasa kile kipindi cha Shilawadu.

Mimi nakutazama lakini nina akili timamu nafahamu kwamba vyeti feki vya Daudi Bashite anayejiita Paul C. Makonda KAMWE havitamtumbua, na njia sahihi ni hii ya "kuleta vurugu uraiani", naitafakari simu yako kwa Shilawadu, yule anakutamaza, wale wanakutazama na Dunia inakutazama mh rais, watanzania wanakutamaza mh rais, Katiba imekupa mamlaka ya nusu uungu rais wangu, fanya jambo watu wa tanzania na dunia wajue wewe ni nani. Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mpo wapi? Ninani katika ardhi ya jamhuri hii ambaye yupo juu ya sheria na katiba za nchi yetu?

Kama tukio hili ni uvamizi bila shaka runinga ya clouds itafungua kesi dhidi ya wavamizi, na hilo tunalisubiri...Lakini kwa mamlaka ya kirais, Mh Makonda amepoteza sifa za kuwa msaidizi wa Rais kwa nafasi yoyote ile....

Ikupendezavyo mheshimiwa rais, katiba inakupa nguvu kwamba hutatenda kazi yako ya urais kwakulazimishwa kushauriwa na mtu yeyote au kikundi chochote.

Wewe ndiye rais wetu, uliwazalo na ulitendalo lidumu daima mheshimiwa rais.

Nikutakie jumapili njema!

Na Yericko Nyerere
 

Attachments

  • VID-20170319-WA0275.mp4
    3 MB · Views: 47
Yaani jamaa hasikilizi wala nini.yule ni mtoto mpendwa tena wa kabila lake kanda moja wapi na wapi?? Tusahau tu.maana haki ya mnyonge hiari ya mwenye nguvu.
 
Halafu whistle blowers kama akina Mange eti ndio wamewekwa kwenye "the most wanted list" ya vyombo vyetu vya usalama! Sijui huwa tunataka nini yarabi! Hawa ndio watu muhimu wa kuzisaidia mamlaka na vyombo husika kutekeleza majukumu yao. Hapo ndipo umuhimu wa mitandao ya kijamii ulipo na sio umbea wa kijinga wa Lumumba.

Mimi huwa nashangaa sana wanaojidai kila siku eti "mwananchi mwenye taarifa za kuvisaidia vyombo vyetu" azilete; wapi mafichoni? Ili nini? Wala habari zenyewe hazihusu usalama wa taifa bali fraud za baadhi ya viongozi. Niltegemea Mange apokelewe kama shuja na kupewa ulinzi wote badala yake ndio anageuziwa kibao; anageuzwa yeye ndiye mhalifu!
 
huyo uliyemwandikia barua tayari, kabadili katiba ya chama ili agombee tena kiurahisi maana alishaona hapiti
 
  • Thanks
Reactions: 999
Katika nyakati ambazo Makonda/Daud kamshushia heshima Rais ni kipindi hiki, imani ya Rais inaporomoka mpaka ndani ya chama chake, watu wanatamani watumbuliwe wao ili wajiite majasiri wa kusimamia haki, hakuna hata mwana ccm mwenye akili zinazomtosha amefurahia hili la kukaa kimya.
Ukiona ccm wanaamua kusema hadharani ujue hawahofii tena kufujuzwa kwani hiyo ndio njia itakayowafanya kufunua madhaifu ya Rais wetu.
Kama Makonda angekuwa na adabu kidogo tu basi angejiuzulu kupisha uchunguzi wa hizi tuhuma zinazomuandama, nia iwe kulinda heshima ya Rais wetu na si vinginevyo.
 
unajua maana ya kuvamia? ingekuwa UVAMIZI ungeona wale askari aliokuwa nao wangerusha mabomu na kupiga risasi ovyo ovyo...lakin kwenye video umemuona Makonda anaingia kistaarabu na askari wake kuwasalimia clouds alienda kuwapa hi tu
Umekua mpole
 
unajua maana ya kuvamia? ingekuwa UVAMIZI ungeona wale askari aliokuwa nao wangerusha mabomu na kupiga risasi ovyo ovyo...lakin kwenye video umemuona Makonda anaingia kistaarabu na askari wake kuwasalimia clouds alienda kuwapa hi tu
Seriously kuna utafiti ulifanywa ukaonyesha watanzania tunatumia asilimia 1% kufikiri na mwingine ukatusifia tunaongoza kwa kuwa wanafiki naafiki kwa 100% hizi tafiti
 
Back
Top Bottom