WARAKA WANGU KWA WIZARA YA NISHATI NA WIZARA YA MAJI

XI JIN PING II

Senior Member
Mar 8, 2017
125
110
Habari wana Jamii Forum, leo nimeona nivema nikaweka mawazo yangu kwenye jukwaa hili, hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya watendaji waliopewa dhamana na serikali yetu kusimamia taasisi mbalimbali kwaajili ya maendeleo ya Taifa wapo humu na kwa namna moja ni wasomaji wa mwaswala mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwekwa kwenye mitandao ya kijamii hususani Jamiiforum.

Nianze kwa kutoa orodha ya taasisi ambazo leo napenda kuzimulika:

(1). TANESCO

(2). Mamlaka za maji za mikoa/Miji/Wilaya etc

Kwa ufupi tu, hizi ni taasisi mbili muhimu katika maisha ya kila siku ya Mtanzania. Kwa namna moja au nyingine watendaji wa taasisi hizi wamekuwa wakitimiza majukumu yao ya kusimamia utoaji na upatikanaji wa huduma kwa watanzania, huu ni ukweli usio pingika. Lakini bado hofu yangu ni juu ya uwezo wao wa kuzitambua na kuzifanyia kazi fursa mpya katika maeneo yao ya kazi. Nitatoa mifano michache hapa ili kuweza kuakisi uhalisia wa hali na mwenendo wa taasisi hizi. Kwa Tanzania hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa saana la watu ukilinganisha na miaka ya nyuma kidogo. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 idadi ya watu ilikuwa 44,929,002 Milioni (NBS,2012) lakini leo hii imefikia takribani watu 50,144,175 Milioni (NBS,2017) yaani ongezeko la watu (5215173milioni).Hii ina maana kwamba kwa kipindi cha miaka mitano tu (2012-2017) Tanzania imeongezeka idadi ya watu sawa na takribani nusu ya wananchi wote wa nchi ya Rwanda ambayo ina watu 11.61 million (NISR, 2015). Hoja ninayohitaji kuiweka mezani hapa jamiiforum ni kwamba; Idadi hii ya watu inayoongezeka inaenda sambamba na ongezeko la uhitaji wa makazi mapya na huduma kama Umeme na maji.

Kwa miaka ya hivi karibuni maeneo mengi katika mikoa mbali mbali yamezidi kupanuka kwa kujengwa makazi mapya na kujengwa taasisi za utoaji wa huduma kama shule na hospitali. Pamoja na ukuaji huu wa miji kupitia ujenzi wa makazi mapya na miundombinu ya kutolea huduma kwa jamii kama shule na hospitali bado mamlaka husika hazijafanikiwa kusambaza huduma muhimu kama UMEME&MAJI. Hapa ninajaribu kuweka mifano michache ya maeneo ambayo katika pitapita zangu kwenye mitaa mbalimbali ya baadhi ya mikoa nimebaini kwamba watendaji wa taasisi hizi za umma wanahitaji kupewa maarifa ya ujasiriamali ili waweze kusimamia taasisi hizi za umma kwa kumaslahi mapana ya Watanzania kwa kusajili wateja wapya ili kuweza kuongeza wigo wa utoaji huduma kwa jamii. Mifano ya mikoa ni: Morogoro (Kihonda,Mkundi,Kiegea, n.k), Dsm (Chanika, n.k), hii ni mifano michache tu lakini yapo maeneo mengi ambayo yanamakazi mapya kwa takribani miaka mpaka mitano hayapelekewi huduma hizi za umeme na maji au kwa kuwa pesa hizo zinazo kusanywa zinaingia kwenye mifuko ya serikali?? Hivi wangekuwa ndio wanamiliki na kuendesha hizo taasisi kama mali zao wangeweza kuona fursa kama hizo za kuongeza wateja na kipato kama mzigo au kama fursa??? Ipo haja ya mameneja wote wa taasisi hizi za umma kuwawekewa (Targets) ili kuweza kuchochea ufanisi na uwajibikaji wa taasisi kama hizi. Wananchi wanapata taabu kwa kushindwa kupata huduma muhimu kama Maji na umeme ninyi mko mnakula viyoyozi tu kwenye maofisi ya umma hapa ndipo Rais Magufuli anapoomba tumuombee inabidi tumuombee kweli kweli. Kwasababu hata swala dogo kama hili ambalo liko ndani ya uwezo wa meneja linasubiri Rais,Makamu wa Rais au Waziri mkuu ili kuweza kutekelezwa???? MKITUMBULIWA mnaona kama mnaonewa kumbe mnashindwa kutambua kuwa VIATU MLIVYOKUWA MMEVAA HAVIWATOSHI. HEBU BADILIKENI TOENI HUDUMA KANA KWAMBA NINYI NDIO WAMILIKI, TAMBUENI WAHITAJI WAPYA WASAMBAZIENI HUDUMA ILI NANYI MUWEZE KUONEZA MAPATO NA HATIMAE TAIFA LISONGE MBELE


Asanteni

Wenu katika ujenzi wa taifa Xi Jin Ping II
 
Kuna baadhi ya Taasisi zinaitaji kuwa na mkono wa Chuma kama pale Tanesco na Water Company awa walitakiwa kwanza waoorozeshwe katika SOKO LA HISA LA DAR-ES-SALAAM. Kwa sababu izi kampuni zinapiga pesa na watu wanaweka kibindoni. Kwanzaa hesabu za haya mashirika zilitakiwa zionekane sawa, ili watu wawe na percent yao wafanye biashara na waachane na janja janja maana huduma ya maji na umeme ina muhusu kila mtanzania
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom