Waraka wangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Waraka wangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza kabisa nianze kwa kukusalimu na kukupa pole kwa majukumu yako ya kila siku katika kulijenga taifa letu.

Ninaandika waraka huu kwako nikiamini ndio njia pekee ya kukufikishia ujumbe wangu ukiwa kama rais na mkuu wa nchi yetu kwani ni vigumu sana kuonana na wewe ana kwa ana ili nikueleze haya nitakayokueleza katika waraka huu.

Ninaamini utaupata waraka wangu huu, kama sio kuusoma wewe mwenyewe basi wasaidizi wako na hata usalama wa taifa watakupa taarifa kwani ninaamini watausoma kupitia mitandao ya kijamii.

Ni ukweli kwamba nchi yetu ipo katika hali tete kuliko wakati mwingine wowote kisiasa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi ndani ya nchi yetu. Hali hii tete inatokana na sintofahamu iliyopo kwenye mchakato wa kuipata katiba mpya ya nchi yetu.

Sikuwahi kudhani ama kufikiri kuwa ipo siku nchi yangu inayosifika kama kisiwa cha amani itakuwa imejawa askari kila kona ikiwa ni katika maofisi mbalimbali pamoja mabarabara ya miji na ofisi za chama chako wakiwa na silaha nzito, farasi, mbwa na magari ya maji ya kuwasha.

Siku hizi kuona maaskari polisi wakiwa wamevalia kivita imekuwa ni jambo la kawaida. Ninatamani ulinzi huu ungekuwepo kila siku labda ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi wangekuwa salama. Natamani ulinzi huu ungekuwapo kila siku labda rasilimali za nchi zisingetoroshwa mchana kweupe kupitia viwanja vyetu vya ndege.Natamani ulinzi huu ungekuwepo kila siku labda tembo wetu wangekuwa salama. Natamani ulinzi huu ungekuwapo kila siku labda kaka zetu na dada zetu wasingeathirika na madawa ya kulevya.

Inashangaza na kusikitisha kusikia kuwa askari wanaoranda mitaani wakiwa na silaha nzito, mbwa, farasi, magari ya kuwasha na mengine yakiwa na bendera nyekundu vyote hivi ni kwasababu ati mchakato wa kupata katiba ya nchi yenye amani. Kiukweli inaumiza na kusikitisha sana mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Rais, katika mchakato wa kupata katiba ya nchi ni hatari sana kudharau uhitaji wa kundi fulani hata kama ni dogo. Majadiliano na maridhiano ndio msingi wa kupata katiba wa kupata katiba bora nchi yetu na sio mitutu ya bunduki na maji ya kuwasha.

Mheshimiwa rais, ninajua unajua kuwa swala la katiba halikuwa kipaumbele chako wakati ulipokuwa unaomba ridhaa ya kuliongoza taifa letu na ndio maana halikuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama chako. Ninajua na wewe unajua kuwa uliamua kuanzisha mchakato wa katiba labda kwa mapenzi mema uliyo nayo kwa nchi ama kwa kulazimishwa au kusukumwa na kelele kutoka kwa wanaharakati na vyama vya upinzani.

Mheshimiwa Rais, najua unafahamu kuwa viongozi mbali mbali katika chama serikali yako walikataa kata kata kwa nchi yetu kuanza mchakato wa kupata katiba mpya, rejea kauli ya mwanasheria mkuu ambaye ndiye mshauri mkuu wa maswala ya kisheria kwa serikali yako. Pia rejea kauli ya aliyekuwa waziri wa katiba na sheria mh.Celina Kombani. Hii ilikuwa ni dalili na ishara kuwa viongozi na wanachama wa chama chako kuwa hawako tayari kuipa nchi yetu katiba mpya.

Mheshimiwa Rais, nchi kuandika katiba mpya huwa ni njia pekee kwa taifa kutibu majeraha, kujisahihisha pamoja na kuimarisha umoja na utengamano katika nchi na taifa. Kwanini mheshimiwa Rais katiba mpya inakuwa ni sababu kwa taifa letu kuingia kwenye mafarakano na kutokuelewana.

Ni ukweli kuwa katika misingi ya kupata katiba ya nchi, uhalali wa kisheria, kisiasa na kijamii huwa ni msingi na nyenzo ya kuhakikisha uhai wa katiba husika mh.Rais. Mheshimiwa Rais, mimi binafsi sitaki kuamini kuwa ni kweli kwamba huoni kuwa mchakato unaoendelea umepoteza uhalali wa kisheria kwani bunge maalumu limekusanya maoni tofauti na yale ya tume ya jaji Warioba? Huoni kuwa mchakato umekosa uhalali wa kisiasa kwani vyama vya kisiasa vingi vimejitoa kwenye mchakato? Hivi ni kweli mheshimiwa rais hujui kuwa mchakato huu umekosa uhalali wa kijamii kwa sababu maoni ya wananchi yamesiginwa?

Mheshimiwa rais, unafahamu kuwa haiwezekani mtu kuhukumu kesi yake mwenyewe. Sasa kama unafahamu hilo unadhani inawezekana kwa wanachama wa chama chako na wasio wa chama chako ambao ni wajumbe wa bunge maalumu kukubaliana na mapendekezo yaliyokuwa yanaingilia ulaji ama nafasi zao?

Mheshimiwa rais, wahenga wamepata kusema kuwa "mjinga anaposhupaa mpumbavu huduwaa". Ni ukweli kuwa watanzania wameduwaa kushangaa kinachoendelea ndani ya bunge maalumu la katiba kwa hawaamini kinachoendelea.

Mheshimiwa Rais, watanzania wa leo sio wale wa jana na juzi. Ukimuona kobe kainama ujue anatunga sheria, na dibwi lililotulia ndilo huzamisha. Usije ukajaribu kudhani kuwa watanzania wa leo watauza utu wao, uhai wa uzao wao na urithi wa vizazi vyao kwa gharama ya upumbavu wao sababu hawaamini uwezo wa nguvu zao kulipigania taifa lao kwa kigezo cha kutii utawala wa nchi yao hata kama ni wa hovyo.

Mheshimiwa Rais, nitajisikia faraja sana kama utatuachia nchi yenye amani na mshikamano pindi utakapomaliza kipindi cha utawala wako. Nitafurahi na kufarijika endapo utaacha jina lako likikumbukwa kwa wema na haki katika nchi yetu. Ninatamani jina lako liendelee kuishi ndani ya tabasamu na cheko na sio ndani ya vilio na kumbukumbu za makovu ya majeraha na makaburi juu ya ardhi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Rais, maneno ninayoyasikia huku mtaani kwetu na kwenye vijiwe vya kahawa ambapo wewe hufiki juu ya mchakato wa katiba vinanikosesha usingizi juu ya kesho yangu ndani ya nchi yangu.

Mheshimiwa Rais, unapokuwa umepotea njia huwa ni busara kurudi ulipotoka kuliko kwenda usipopajua. Mheshimiwa Rais.kwa mchakato huu tumepotea njia na ni bora turudi tukaanze upya. Wahenga walisema "kuanza upya sio ujinga".

Mheshimiwa Rais. Ninakumba uitumie ile busara iliyotumika kuahirisha bunge maalumu ili kuruhusu bunge la bajeti itumike sasa kuliahirisha bunge maalumu ili kutafuta maridhiano kwa mustakabali wa ustawi wa nchi yetu.

Mheshimiwa rais, wakati ninapomaliza waraka huu ninapenda kukushauri juu ya uwepo wa askari wengi mitaani. Ni ukweli kuwa ulinzi ni jambo nuhimu sana kwa usalama wa taifa. Ila ulinzi unapoonekana ni wa kulinda kundi fulani dhidi ya raia wa nchi hujenga na kuleta maana nyingine. Huku mtaani kwetu nimesikia watu fulani wanasema "inakuwaje polisi wanalinda wezi" sikuelewa ni nini maana ya kauli hii ila mheshimiwa rais ukikaa ukatafakari kauli hii najua utapata maana yake na wewe pengine tofauti na hii yangu iliyonisha.

Kurandaranda kwa magari ya kuwasha, mbwa, farasi na askari waliovalia kivita mitaani kutawafanya wananchi wazoee hiyo hali na mwisho wake hawataogopa tena kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa nchi yetu.

Mheshimiwa rais. ninajua wewe ni rais msikivu kama inavyokika ukisifiwa mara kadhaa na ninaamini bado ni msikivu na umenisikia mtukufu rais.

Ninakutakia kazi njema na afya tele katika ujenzi wa taifa letu ila kumbuka na kutafakari msemo huu wa wahenga kuwa "MJINGA AKISHUPAA MPUMBAVU HUDUWAA"

Ni mimi mwananchi wako
 
ujumbe mzito sana, ila hawasikii hao jeuri imeziba maskio yao, haina shida tutakutana tu ktk uwanja wa vita.hao wanajeshi na baadhi ya polisi wana akili timam, watajiunga na nguvu ya umma, ingawa tutakufa lakini habari yao wataipata, hakuna linaloshindikana
 
....


Kurandaranda kwa magari ya kuwasha, mbwa, farasi na askari waliovalia kivita mitaani kutawafanya wananchi wazoee hiyo hali na mwisho wake
hawataogopa tena kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa nchi yetu.....

hapo kwenye red.. Ref Arusha Mbeya na Mwanza
 
'Ujumbe mzito'; Ndugu yangu haya yamepangwa, km huamini angalia Kinana na Nape wanafanya nini mitaani!
 
'Ujumbe mzito'; Ndugu yangu haya yamepangwa, km huamini angalia Kinana na Nape wanafanya nini mitaani!

kuna uwezekano mkubwa hawa jamaa wana plot kitu kibaya kwa maana hawasikii kabisa na pia hawa stuki kabisa i think wanataka vita
 
Mimi najaribu kuwaomba watanzania amkeni wacheni kupiga domo mitaani kwani leo hii mkiamua kutoka road mtashindwa kama mnaweza fanyeni wecheni uoga hakuna dhambi mbaya kama uoga. Jitokezeni kwa wingi chakula maji tutachanga mahospitali yataandaliwa tomtoe mkoloni mweusi kk
 
Kwa hiyo ulitaka polisi wasijiandae ilhali nyie wahuni wa CHADEMA mlikuwa mnahatarisha amani ya nchi? Kosa mmelifanya wenyewe pale mlipotangaza maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima ndo maana jeshi la polisi likajiandaa nchi nzima kwa silaha zote ambazo wanazo na ambazo wanapaswa kuzitumia kwa mujibu wa taratibu zao za kazi
 
'Ujumbe mzito'; Ndugu yangu haya yamepangwa, km huamini angalia Kinana na Nape wanafanya nini mitaani!
Hakuna kipya alichokiandika. Ni yale yale tu ambayo anaandikaga Godbless Lema. Naona kamtuma sasa Mungi au kaingia kwa ID nyingine kupost utumbo huu
 
Hakuna kipya alichokiandika. Ni yale yale tu ambayo anaandikaga Godbless Lema. Naona kamtuma sasa Mungi au kaingia kwa ID nyingine kupost utumbo huu

Pamoja na kejeli zako hizi, naamini huwezi kusoma nilichokiweka, utabaki na upofu wa akili hivyo hivyo

Tunaamini ujumbe utamfikia Jk
 
Waraka huu utatujenga wengine ila si kwa raisi huyu!hapo kasoma kacheka cheka basi ila time will tell.
 
Mh Rais naomba usisikilize kelele za hawa vijana na polisi naomba waendelee kulinda amani tulio nayo huko mtaani na hasa Arusha ndio polisi wana paswa kuongeza!

Sisi wakazi wa Arusha tumefurahishwa sana na ulinzi unaodumishwa na tuna kushukuru sana!

Mh Rais kwa lugha nyingine bwana Mungi amekiri jeshi la polisi limefanya kazi nzuri na limelinda amani na ndio maana kapata wasaha wa kuandika na hasinge andika haya kama wasinge dhibitiwa!


Mh Rais huyu aliye andika waraka kama haukuandikiwa na mbunge Fulani yule ambaye anasema kila Leo hakuna dhambi iliyo kuu kama uoga lakini cha kushangaza anaogopa magari na mbwa wa polisi basi atakuwa pacha wake!

Mh Rais hawa watu hawataki majadiliano wala maridhiano ndio maana wameamua kuingia barabarani baada ya kuona wamedhibitiwa sasa wamekuja na style ya waraka!

Mh Rais wewe ni mvumilivu sana na umekuwa ukiwasikiliza Sana sasa inatosha!

Mh Rais mwandishi wa huu waraka ni bingwa wa kuku kejeli hivyo husimsikilize Bali endelea kuhakikisha ulinzi una dumishwa!

Mh Rais naomba upuuze huu waraka maana wanayo yasema wao hawawezi kuyatenda hata kama chama chao ndio kingekuwa kimetoa Rais!

Mh Rais naomba umpuuze bwana Mungi!

Mungu ibariki Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Laiti kama ukawa wangekubali kwenda kwenye meza ya majadiliano na wakaona umuhimu wa majadiliano basi hali isingetufika. By the way yaliyopita si ndwele ukawa watashiriki kwenye kampeni ya kura ya maoni, kama na hukoo watasusia basi hata kwenye upigaji wa kura ya maoni watashiriki .... Na hii yatosha kwamba mchakato umemshirikisha kila aliyetaka kushiriki.
 
Pamoja na kejeli zako hizi, naamini huwezi kusoma nilichokiweka, utabaki na upofu wa akili hivyo hivyo

Tunaamini ujumbe utamfikia Jk
Hizi si kejeli bali ni uhalisia. JK kasikia na anaona mengi sana kuliko haya. Mshauri boss wako Mbowe akijenge chama badala ya kukimbilia maandamano ambayo wananchi sasa wanayapuuza. Kudoda kwa Maandamano ya kupinga katiba mpya kuwe fundisho kwenu
 
Mh Rais naomba usisikilize kelele za hawa vijana na polisi naomba waendelee kulinda amani tulio nayo huko mtaani na hasa Arusha ndio polisi wana paswa kuongeza!

Mh Rais huyu aliye andika waraka kama hakuandikiwa na mbunge Fulani yule ambaye anasema kila Leo hakuna dhambi iliyo kuu kama uoga lakini cha kushangaza anaogopa magari na mbwa wa polisi!

Mh Rais hawa watu hawataki majadiliano wala maridhiano ndio maana wameamua kuingia barabarani baada ya kuona wamedhibitiwa sasa wamekuja na style ya waraka!

Mh Rais wewe ni mvumilivu sana na umekuwa ukiwasikiliza Sana sasa inatosha!

Mh Rais mwandishi wa hii wa huu waraka ni bingwa wa kuku kejeli hivyo husimsikilize Bali endelea kuhakikisha ulinzi una dumishwa!

Mh Rais naomba upuuze huu waraka maana wanayo yasema wao hawawezi kuyatenda hata kama chama chao ndio kingekuwa kimetoa Rais!

Mh Rais naomba umpuuze bwana Mungi!

Mungu ibariki Tanzania.
Japo umeandika mistari wastani wa mistari 7 iliyojaa, umejibu hoja zote za Mungi na kundi zima la CHADEMA
 
Back
Top Bottom