Waraka wangu kwa mitandao ya simu na TCRA

nelvine

JF-Expert Member
Nov 8, 2015
1,109
1,855
Happy workers days

Tujilinde na tuwalinde wengine dhidi ya corona.

Napenda kuishukuru mitandao yetu ya simu kwa kuajiri vijana wengi sana mtaani, vijana nao wamepata ajira ya kusajiri laini nao wana itwa freelancer/wakala/balozi au msajili laini.

Mmeajiri vijana wengi wasomi na wasio wasomi wana dhurula mtaani kutoa huduma kwa wananchi, uku wananchi wakiwaita wafanyakazi wa mtandao.

Je huyu kijana freelancer ana thaminiwa kwa kazi anayoifanya? Anapewa haki zake sahihi? Ndiyo siyo mfanyakazi wa kampuni yeye ni kibarua tu, lakini naye ana haki zake za msingi.

Freelancer ndiyo amebeba soko la mtandao husika, iwe Vodacom au Tigo bila freelancer ni kazi bure, lakini mbona uyu mnyonge hathaminiwi? Mbona ananyonywa? Mnajua taabu wanazozipata hawa vijana uko mtaani?

Licha ya mlipuko wa ugonjwa wa corona vijana hawa wanapiga kazi si mjini wala vijijini wao wanaita door to door, hawana barakola wala sanitaiza, hawajikingi dhidi ya cotona hawana vifaa, kampuni hata mishahara yao hazijawalipa, na kama wamelipwa hayupo aliyezidi 100,000, wengine wanapigwa kwa kuitwa wezi.

Dada zetu wanabakwa na kudharirishwa huko mitaani, licha ya vijana hawa kujitoa kindakindaki kuhakikisha soko la mtandao wake halishuki lakini mitandao na TCRA haiwatambui wala kuwajari kabisa hawana msemaji, wapi wakalalamike? Kila wanakolalamika wanaambiwa wao ni vibarua tu.

Kama hawa vijana hawana thamani basi ninyi mtoke maofisini mje uku vijijini msajili hizi laini, bila hawa freelancer hakuna Vodacom, Tigo, Airtel, TTCL, Halotel wala Zantel mitaani, lakini mbona mnawanyanyasa?

Najua serikali yangu ya awamu ya tano chini ya jembe Magufuli ni sikivu na haipendi kuona mnyonge anaonewa, na naami ujumbe huu utakufikia Mheshimiwa.

Vijana hawa wanapitia mengi sana hawana wakuwasemea, sasa katika siku hii ya wafanyakazi duniani acha nao wapate msemaji wao maana wamechoka.

Vijana hawa wanalipwa kwa njia ya kamisheni, yaani wana kadiliwa malipo licha ya taabu zotee wanazozipata uko sokoni. Wanalipwa kwa % tena 25% kijana ana sajiri laini 100 analipwa 6000? Hii ni haki kweli?

Changamoto za freelancer.

Malipo

Kama nilivyoyaandika hapo mwanzo vijana wanalipwa kwa kamisheni tena 25% kwa mwezi, kwa hesabu rahisi kijana akisajiri laini 100 wateja wakaweka vocha ya 1000(100*1000=100,000) vijana hawa watalipwa 25000 nayo ni ya maandishi, kiuhalisia wanalipwa 5%, malipo mengi yapo kwenye makaratasi na si uhalisia.

Wengine hata hawalipwi stahiki zao, watasemea wapi matatizo yao kama TCRA nayo tu ina wakandamiza? Hawana msemaji wao wala chama, japo ndiyo wamebeba hizi kampuni vichwani mwao, wakifikiria wana wategemezi wanawategemea aende wapi? Akaibe?

Vifaa vya usajiri
Vijana hawa hawana tshirt wala kitambulisho cha kibarua chake, yaani wana uziwa tshirt, miamvuli, na hata vifaa vya kusajilia, jamani hawa ndiyo wanao wawakilisha kwa wananchi lakini bado una muuzia tshirt ya mtandao wako ambayo anavaa anakutangazia soko lako, huu ni ukatili wa kiasi gani?

Kijana ana tshirt ina miaka minne ana vaa hiyo hiyo, afanye nini? Akiulizwa anajibiwa wewe ni freelancer tu huna mkataba na kampuni, kama hana mkataba mbona anashitakiwa na TCRA kama hana mkataba, yeye si mfanyakazi huru awe huru kila sehemu.

Mazingira hatarishi ya kazi
Vijana hawa wanahangaika angalau wapate kodi za pango na watoto wao wapate mkate wa kila siku, wanaenda kufanya kazi vijijini na kila sehemu, sehemu zingine hatarishi hata kwa uhai wao, lakini kwa kuwa kampuni na serikali haziwatambui wanaitwa wezi, vibaka, dada zetu wana bakwa, wanadharirishwa kingono na maneno kibao ya kashfa, watasemea wapi? Watamwambia nani? Hawatambuliki.

Wabebaji wakuu wa lawama
Huko mtaani freelancer akikutana na mteja aliyeweka vocha ikachukuliwa bila taarifa na mtandao husika basi yeye ndiyo atabeba kesi ya kampuni, ataitwa tapeli, kibaka.

Kijana huyu akifanya kosa kidogo tu kwenye mtandao, anafyekwa kamisheni yake, anafungiwa laini yake ya uwakala, uku rungu la TCRA nalo lipo nyuma yake, akimbilie wapi freelancer, nani amsemee mnyonge huyu?

Wana mengi sana freelancer ndiyo hawa wanao mshawishi mteja anunue laini ya mtandao fulani ina vifurushi vizuri, na wanajari na kusikiliza wateja, lakini ni dekio tu kwa mitandao, wakisha deki wanakanyagwa wana sahaulika kabisa, huku mtandao unasifiwa kwa kupeleka huduma kijijini kumbe hata hawakujui Ihimbo huko.

Ombi langu kwa mitandao ya simu na TCRA

Mitandao;

Vijana hawa wakumbukwe, nao ni wafanyakazi kama wafanyakazi wengine wa kampuni zenu hata kama ni vibarua lakini ndiyo wanao wafanya nyie masoko yenu yakue, muwaajari kama wafanyakazi wenu bila hawa msingekuwa hapo mlipo, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, hakikisheni mnayafanya haya;

  • Walipwe kamisheni halali na ziboreshwe.
  • Wapewe vifaa bure, tshirt, kofia, miamvuli, laini na vifaa vyote wavipate mara kwa mara.
  • Wapewe vitambulisho ili kupunguza uhalifu.
  • Kuwe na vikao na semina mara kwa mara.
  • Wawe na mikataba huru na ya wazi.
  • Wasikilizwe na kupokea maoni yao.
  • Wapewe vipaumbele ili kuwatofautisha wao na watu wengine, wazijue vyema bidhaa za mtandao kabla ya kufika kwa mteja.
  • Wapewe nafasi za kuwa viongozi.
  • Wapewe hamasa za kazi.
Serikali (TCRA)

Serikali yetu ni sikivu sana hasa katika awamu hii ya tano chini ya mheshimiwa Magufuli. Kama ilivo ada yeye ni Raisi wa wanyonge na freelancer hawa ni wanyonge, na mitandao imewaajiri vijana wengi sana.

Serikali myasimamie na kuyachunguza haya makampuni ya simu, vijana wapate:-

  • Vifaa bure
  • Wawe na vitambulisho
  • Walipwe stahiki sawa sawa na kima cha chini cha serikali kamisheni iwe ni motisha ya kufanya kazi.
  • Muwashirikishe katika mikataba yao na kampuni husika, wajue haki na wajibu wao.
  • Wajue misingi ya kazi zao, usalama wao na jinsi ya kulinda haki za faragha za wateja wao.
  • Watambulike na kampuni na serikalini hili kupunguza utapeli na wizi na si lawama zote ziende kwao.
Hawa wasipo thaminiwa ni hatari sana kwa usalama wa taifa letu. Wanajua vingi sana

Freelancer tuungane kudai maslahi yetu na haki zetu, sisi ndio mgongo wa kampuni.

Tujilinde na corona, tuwalinde na wengine.

Msemaji wa kujitolea wa wasajili laini Tanzania.

Freelancer Mwakijebele

Sent using jamii forums mobile app
 
TCRA nguvu yao yote wameamishia kwenye usajili wa alama ya vidole.

Mengine yote wamesahau kweli tupo kwenye nchi masikini.
 
Back
Top Bottom