Waraka wa wazi kwa wana MMU kumhusu “The Great”! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa wazi kwa wana MMU kumhusu “The Great”!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HorsePower, Apr 16, 2012.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Habari za leo wana MMU?

  Kwanza, naomba msamaha kwa wote ambao kwa namna moja au nyingine wasingependa kuzisikia tena habari za ‘The Great’. Si nia yangu kuwatonesha kidonda bali kuwashirikisha yale ambayo nimeona tunawezakujifunza kama watanzania wenye nia na mapenzi mema, ili yakafanyike kuwa msaada kwetu na kwa wanajamii wenzetu.

  Pili, kwa takriban wiki moja sasa, vyombo vya habari nchi Tanzania vikiwemo redio, magazeti na TV vimekuwa vikiripoti tukio la kumpoteza ndg yetu mpendwa ‘the great’! Binafsi, na mimi pia ni mmoja wa watanzania walioumizwa na kutoweka kwa ndg huyu. Naamini ni wengi ambao waliguswa sana na kifo hiki kutoka na ukaribu na ukarimu wa huyu ndg kwenye maisha yao ya kila siku. Wapo pia walioguswa na hili tukio ili kujipatia maslahi yao binafsi kwa kuuza habari na kuzusha mambo mengi yasiyo ya kweli ili kujipatia kipato cha udhalimu. Na pia wapo waliotumia msiba huu kama sehemu ya kwenda kufahamiana na wasanii na watu wengine mashuhuri. Kwa wote waliguswa kwa nia njema, nawapa pole sana na Mungu awafute machozi na kuziondoa huzuni zao!

  Kwa nini nimeandika waraka huu?
  Pengine ni kwa sababu ya kuguswa na hisia za maumivu ya mioyo ya watu juu ya tukio hili la kumpoteza ndugu yetu ‘the great’. Vyombo vya habari bado vinatukumbusha kila siku. Hotuba za viongozi wetu bado zinamtaja! Hata Juzi kwenye Kili Awards kauli za waliohojiwa bado wanashindwa kusema lolote bila kuacha kumtaja Kanumba. Nilikuwa kwenye sherehe moja Jana, nikamsikia binti mmoja akimwambia mwenzake kuwa siku hizi anaogopa kulala usiku pekee yake akihisi 'the great' anaweza kumtokea! Hizi ni dalili za wazi kuwa jeraha hili bado ni bichi na tunahitaji kufarijina ili tuweze kurudi katika hali ya kawaida.

  Nini tumejifunza?
  Tukiwa na maisha ya amani na watu, tukaondoa chuki na ubinafsi tukaacha tamaa pia, basi tunaweza kuishi maisha ya kuwa mfano.Kanumba kazikwa kishujaa kwa sababu ya aina ya maisha aliyochagua mwenyewe kuishi. Kwa sisi wana MMU tuliobaki, hatma ya maisha yetu ipo mikononi mwetu. Bado tuna nafasi ya kuishi maisha ambayo yanaweza kukumbukwa na vizazi vyetu vijazo badala ya kuwa na maisha ya kifisadi yatakayotuletea hukumu siku ya mwisho. Tubadilike!

  Hitimisho
  Nafikiri ifikie wakati sasa, watanzania wote tukubali kuwa huyu ndg hatuko naye tena duniani. Ni wakati wa kutambua kuwa yeye aliyetoa ndiyo huyo huyo pia aliyetwaa. Ni vizuri sasa kuukubali ukweli huu ili kuzinusuru akili na fahamu zetu ziweze kufikiria katika kuimarisha na kuenzi kazi zake badala ya kutumia muda mwingi kuendelea kulia na kuomboleza. Tukubali kuwa tumelia sana, tumeumia sana na pia tumehuzunika sana na sasa ni wakati wa kuyajaribu maisha bila ya kuwa na shujaa huyu wa tasnia ya filamu. Ningetamani vyombo vya habari visaidie kuwafariji watu na kuwaondoa majonzi badala ya kuendeleza hbr za huzuni, uchochezi na kujenga chuki baina ya wanajamii waliotuzunguka. Ni vigumu kumpata mtu kama huyu tena, ila yeye aliyemtwaa anafahamu ni kwa kiasi gani watanzania wameumia ni nini cha kutufanyia ili kuweza kuikabili hii hali.

  Nawaombea Mungu wa amani awafariji kwa faraja na baraka zake kuu. Tuamini kuwa sisi ni binadamu, na hii dunia si sehemu yetu ya kudumu na hivyo tujitahidi kutenda mema na kuishi na watu vizuri kujiwekea thawabu kwa maisha yetu baada ya haya ya duniani na kuacha kumbukumbu kama ya ‘the great’. Tupinge na kusaidiana kukemea maovu. Tuamini ya kuwa kazi ya Mungu haina makosa. Tudumu kutenda mema.

  RIP ‘the Great’ na wengine wote ambao bado mioyo yetu inawakumbuka kama Sokoine, JK Nyerere, Fanueli Sedekia, Angela Chibalonza, Rehema Mwakangare, Damian Kanuti, James Dandu, na wengineo wengi.

  Poleni Watanzania,

  HorsePower
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,480
  Trophy Points: 280
  mimi mama yako ndo bado nina machungu mengi,
  tena 'password' yangu moja ni ya jina lake
  na nimekaa nayo kwa zaidi ya miaka minne,
  nilikuwa simkubali sana ila nilikuwa namwona kama
  kijana anayejitahidi sana kusogeza gurudumu la maisha mbele (japo lisingenigusa kwa namna yeyote ile),

  je wewe unajua ni rahisi sana kumsahau mtu kwa kuwa katangulia mbele za haki,
  kama ni rahisi unavyowaza wewe hebu niambie fomula ya kumsahamu Kanumba (R.I.P).
   
 3. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145

  Ni ngumu sana mama yangu,hata mimi inanipa shida! Ila inatakiwa tufike wakati tukubali kuwa huyu ndg, pamoja na kuwa tumempenda sana, hatukonaye tena na hatuna namna ya kumrudisha kwenye mikono yetu hivyo na tujitahidi kuyaanza maisha mapya bila yeye.

  Pole sana.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Haya, ngoja nirekebishe memmory nisahau.

  Ila tutasahauje wakati DSTV ndio imeanza kuonesha Movie zake channel 127?
   
 5. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  meona maandishi mengi nikadhani nitapata jambo la maana humo lkn nilichoambulia ni kichefuchefu cha kumfananisha Kanumba na Sokoine. Wewe huna tofauti na yule mchungaji aliyeongoza ibada ya kumuombea marehemu iliyoandaliwa na wasanii wenzake ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa mtumishi wa Mungu.

  Mtanisamehe Pro-Kanumba, mimi huwa sipendi unafiki. Huyu mtu ndio kafa na anastahili heshima kwa mazuri ambayo mimi BINAFSI siyajui. Lkn inapofikia sasa tuanze kuaminishwa kuwa alikuwa mtakatifu kwa kuwa tu mliishi kwa kumsujudia, mimi sioni mantiki. Rejea maandishi yako mtoa mada
  Mimi si Mungu wa kuwahukumu watu, lkn na wewe ni nani wa kuwasafisha tena bila hata aibu?

  Wote tumesikia mazingira ya kifo cha Kanumba. Sasa unaupata wapi ujasiri wa kujaribu kutuaminisha na kututamanisha kuomba kifo kama cha Kanumba? Lets stop this illusions. Hakuna mazito ya kulisaidia hili taifa kutoka kwa Kanumba (kwa mtizamo wangu), makubwa katika kazi zake (na wenzake) ni uharibifu wa jamii yetu. Bongo muvies na wanachama wake ni taswira mbaya kwa Taifa lkn kwa kuwa sisi tunaathiriwa na utandawazi kwa namna mbaya, basi Kanumba kwetu ni nabii na tunaamua kumuabudu. Tena mbaya zaidi, tunapofuka macho na kushindwa hata kuona kuwa mwisho wake kimaadili haukuwa mzuri.

  Mimi simkatazi mtu kuamini anachoamini, lkn punguzeni kauli mjumuisho. Kusema Taifa limepoteza mtu muhimu, maana yake ni kunilazimisha hata mimi ambaye ninaamini kuwa Kanumba na wenzake ni wapotoshaji wa jamii yetu tuamini mnavyoamini nyinyi msiojua zamani tuliishije na sasa tunaumiaje.

  Juzi (kama sio jana), kwenye JAMII PHOTOZ, kuna mtu alipost picha ya watu wawili wakiwa kitandani wanapapasana mapaja. Kilikuwa kipande cha picha kutoka kwenye moja ya maigizo yetu ya Bongo. Je hicho ndio tunachokililia kwa Kanumba kufa? Haya ya Lulu, umri wake, jinsia yake na uhalisia wa mazingira ya yeye kuhusika na kifo cha Kanumba uliyazingatia kabla hujaandika huu waraka wa kumtuza marehemu?

  Binafsi nafikiri umefikia wakati sasa tuishi kwa malengo. BONGO MUVIES na waigizaji wake ni uchafu. Haya mabadiliko yanayotukumba tukiwa hatuna elimu ni sumu kwa taifa. Watoto wetu wako bize na Kanumba na Shigongo kiasi hawana muda wa kusoma vitabu bora na magazeti yenye msaada kwao na hilo linachangia yale tuliyoyaona kwenye matokeo ya kidato cha 4 na kujifanya tunajali na tumeumia. Hivi kwa akili tu ya kawaida, wapi kwenye gazeti la Uwazi unaweza kusoma makala ya uchumi au historia zaidi ya Ray kampa mimba Amina, Lulu kabakwa kolabo, Anti seche katoa mimba ya kigogo, wema sepeku abamizwa makofi na mke wa buzi lake,.....n.k?!

  Najua haya maoni yangu yatawakera wooote wanaoishi kwa hisia. Lakini mimi ni Mtanzania kama ulivyo wewe na haya ndio maoni yangu. Huu unabii wa Kanumba mimi naukataa. Wote tutakufa lkn hicho sio kigezo cha kukienzi kifo kichafu cha Kanumba kwa wewe kutuasa tuepuke ufisadi na tufe vizuri na kwa amani kama Kanumba. Tafakari mwisho wake halafu jiulize kama kweli upo sahihi
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ni vyema sana maana hapo sasa tutakuwa tunamuenzi 'the great'!. Kikubwa ni kuifanya akili ikubali kuwa hatuko naye tena ili kukwepa magonjwa kama 'msongo wa mawazo' na mengineyo yafananayo na hayo. Na hii pia itatusaidia watanzania turudi ktk hali ya kawaida maana hata mimi ki ukweli nimeguswa mno ..., msiba huu naweza kuufananisha na ule wa hayati Sokoine au JK Nyerere, Loh!
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Haya ni maoni yako na asante pia kwa mtazamo wako huu. Kwa upande wangu mimi naona kuna mengi ambayo tunaweza kujifunza kutoka na msiba huu. Wingi wa watu na majonzi ambayo yameonekana na pia media coverage imeonyesha ni kwa kiasi gani alikuwa mtu wa watu. Siko interested na personal life ya mtu ya mahusiano, maana walio wengi kwenye maisha yao binafsi ya mahusiano ni wachafu kuliko! Point yangu ni kuwa, tunaweza kuwa wapiganaji wakubwa kama yeye na kujipatia kipato kwa njia ya halali badala ya ufisadi na pia kuwa wenye mioyo na roho za kusaidia badala ya kuwa na chuki na mtazamo hasi unaofanana na huu wako. Aliianzia kwenye maisha ya chini akapigana na kufanikiwa na ameondoka kama shujaa, taka usitake. Ni hili ndilo jambo la kujifunza toka kwake ya kwamba nasi tunapaswa kuwa wapiganaji.
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,480
  Trophy Points: 280
  Unajitahidi sana kuchukua nafasi ya Mungu
  ya kuhukumu, je siku ukamkuta paradiso na wewe
  ukawa jehanamu itakuwaje.

   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Hivi unadhani watu wana msongo honestly???

  Watu wanajaribu kutengeneza pesa kwa jina la marhem
  Chezeiya wajasiriamali, na litatumika kwa muda mrefu sana ukizingatia na mazingira ya kifo chake.

  Hebu kumbuka hata Amina Chifupa, aliuza magazeti ya udaku kwa muda mrefuu sana, sembuse huyu.

  Hakuna cha msongo wala nini, people are making money, Period!

   
 10. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145

  Hapo penye bold sina cha kuongeza!
   
 11. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #11
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,285
  Likes Received: 808
  Trophy Points: 280
  Usiwalazimishe watu wamsahau Kanumba
  Ww ni mcheza filamu za Bongo? Nakuhakikishia hamtamkuta kwa umaarufu hata mkizindika
  Unamkumbuka Bruce-Lee mpaka leo Jack Chan wala Jet-Li hawatamkuta
  Pia wana MMU msijemlinganisha na wanasiasa JK Nyerere anasubiriKuwa Mwenye Heri
  Diana wa Prince nae kivyake
  Kanumba hatasahaulika na kizazi cha vijana hawa hata km alikutwa na Lulu au pombe
  Km tumezeeka na kizazi cha Ujamaa waacheni bba kizazi cha .com ndio kioo chao
   
 12. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hauko interested na personal life ya mtu, mmh! Very pathetic! Rudia kusoma ulichoandika halafu ujiridhishe kuwa hauko interested na personal life za watu. Kwako wewe, kutokana na udhaifu wa nafsi yako juu ya Kanumba (na unaamini wote tuko hivyo) unaona kuwa umaarufu wa Kanumba unajustify hata matendo machafu aliyoyafanya dakika za mwisho.

  Hebu angalia mawazo yako halafu pima usahihi wake:
  Lulu tunaruhusiwa kumtamani, si ndiyo?!
  Kwangu mimi maovu ni pamoja na kufanya vichocheo vya maovu yenyewe. Na hapa hukunielewa pia, nilizungumzia BONGO MOVIES kwa ujumla wake nikasema zinaiharibu jamii. Nikakupa na mfano wa picha iliyowekwa juzi/jana hapa ya watu wakishikana mapaja kitandani, lkn wewe kwa mtazamo wako ukaona najadili maisha ya Kanumba. Haya hebu niambia, ni nini alichokifanya Kanumba ambacho wewe unakichukulia kama kukemea maovu?
  Kama Kanumba alikuwa mfano, basi ni kwako si kwangu. Amani ni zao la ridhiko na matarajio mema. Simu aliyokuwa anagombania ni kielelezo cha amani na imani kwako? He was desperate to death, lkn bado wewe unaniomba huo uwe mfano kwa maisha yangu; HOW!

  Kwa kifupi nikuweke wazi, mimi sina tatizo na Kanumba as a person (kama unavyojiaminisha kwa kutotaka kusikia ukweli) lkn ni nipo completely against tabia zake. Haya mahubiri yako yana mapungufu mazito ndio maana sikubaliani na wewe.

  Kushindwa kwetu kuelewana ni sababu ya utofauti wetu linapokuja suala la kutumia akili kupata majibu. Kanumba kuzikwa na watu wengi ni zao la UMAARUFU na sio UBORA. Magazeti ya UDAKU hapa DSM yanauzwa zaidi mitaani, je huo ndio ukweli kwamba UWAZI na IJUMAA wikienda ni magazeti bora zaidi ya The Guardian na The Citizen?

  Mtu mwenye busara na hekima hashangilii kuungwa mkono na watu wengi bila kutafakari hao watu wanaomuunga mkono ni wa tabia na mtizamo gani kwenye maisha. Ukipanda kwenye daladala angalia wanawake woote waliojichubua kama hutawaona na UWAZI na IJUMAA lkn si Daily News na Nipashe. Nenda kwenye ofisi serious halafu uangalie kama kutakuwa na UWAZI au The Guardian. Hapo utajua tofauti ya kushabikiwa na kuwa bora.

  Mawazo yako ni kichekesho sawa na kudhania kuwa ipo siku kwenye meza ya wageni pale kwenye ofisi ya ILO utakuta gazeti la SANI badala ya The Citizen.
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  I can see a lot of energy kwenye hii sred.
   
 14. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kongosho nami nakubaliana na wewe, naona hapa nisiongeze neno!
   
 15. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hata mwanzo nilisema mimi si Mungu wa kumuhukumu, lkn nyie ni nani wa kumsafisha na kutuambia eti tuige mfano wa maisha yake? Siku zote tunawahukumu watu hapa jamvini, Chenge mwizi, Lowassa fisadi n.k. Tofauti hapa ni kuwa huyu kafa, na kama tulivyo, marehemu siku zote ni mwema. Je ni mwema na kwa Baba Lulu?

  Na nikukumbushe kuwa nimewasema wasanii wa maigizo kwa ujumla wao kuwa haya mapaja na maisha ya kuandikwa magazetini leo wamefuamniana, mara fulani ana mimba ya mume wa mtu si kitu cha kuiga. Shida ipo kwa Kanumba tu ambaye mnataka na mimi nikiwa na akili zangu timamu nimuone mtakatifu kwa kuwa kafa?

  Simjui wala hanijui lkn tabia zake si za kuigwa. Kama hamjui, kamuulizeni Baba Lulu ni vipi anajisikia saa hizi.

  Na kuhusu Jehanam, I deserve. Lkn sitawashauri watu kuiga tabia zangu mbivu na kuniita mtakatifu siku nitakayokufa. Stop being pathetic
   
 16. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  aluuu...kuna mapoint hapa...kuna mtu namuona yuko beyond great thinkers...umetishaaa...
   
 17. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  ...mamae!
  Ukitoka JF pitia dukani kwa Mangi uchukue kiroba kimoja, mwambie aandike kwenye bili ya Mphamvu.
   
 18. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Shizukan mdogo wangu, punguza jazba! siku zote huwa tunachukua na kujifunza yale yaliyo mazuri tu, mabaya tuna achana nayo baada ya kutusaidia kujua ubaya wake ndani ya jamii. Kwenye waraka wangu, sijataja baya lolote nikasema tujifunze kutokana na hilo, nimetaja kwa ufupi tu yale mazuri yanayotuhusu. Hayo mabaya kama unayafahamu wewe kaa nayo na yakusaidie usiyatende ndani ya jamii.
   
 19. R

  Rukwa21 Senior Member

  #19
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kila binadamu ana mapungufu yake hakuna aliyekamilika. Tufuate mazuri alioyafanya tuyaache mabaya aliyofanya. RIP Kanumba
   
 20. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kitu ambacho nimeshindwa kuelewa na huenda nisikielewe kabisa mpaka siku ya ahadi yangu ni jinsi baadhi ya Watanzania wanavyoacha kuangalia pande zote za shilingi za maisha ya "Mwendazake" mtu anakazana kutumia kigezo cha Mwendazake kusindikizwa na halaiki ya watu katika safari yake ya mwisho kama sababu ya kukaribia kumtangaza kama Mtakatifu au Mwenye Heri pasipo kufanya uchunguzi wa kina kuhusu aina ya watu waliotengeneza halaiki ile.
  Hivi kweli jamani tunaweza kuwaweka katika rank 1 hayati Baba wa Taifa,hayati Sokoine na Kanumba? yaani nikijichukulia mfano wangu binafsi..mimi na akili zangu timamu inichukue muda mrefu zaidi ku'recover majeraha yaliyosababishwa na msiba wa huyo mnayemuita "the great" kuliko majeraha yaliyosababishwa mathalani na msiba wa Baba yangu mzazi(R.I.P Baba) jamani kweli kabisa mtu anazimia na mwingine anakunywa sumu kabisa ksbb ya Kanumba!!!!!,ningepata fursa ya mathalani kuonana uso kwa uso na Mhanga hata mmoja wa kuzimia ningemuuliza kama amewahi kupata msiba wa mtu anayemhusu kabisa mfano mzazi,na kama ndiyo ningemuuliza kwanini hakufa...eenh kama mtu unaweza kuzimia kwasababu ya Kanumba basi inabidi ufe kabisa pindi unapopata msiba wa Mzazi wako.
   
Loading...