Waraka wa wazi kwa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu

Philipo Mwakibinga

Senior Member
May 13, 2013
111
175
Waraka wa Wazi wa Mwalimu Shukia kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan.

Wazo kuu: Elimu Bora ni Zao la Walimu Bora

1. Niungane na Watanzania wenzangu kwanza; kukupa pole kwa kuondokewa na mpendwa wetu, Hayati Rais John Pombe Magufuli; pili NIKUPONGEZE kwa kuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya sita kwa dhati na kukutakia kila lililojema katika kutekeleza majukumu yako. Wengi wamezungumzia juu ya utendaji wako mahiri. Nami naungana nao katika kushadadia hilo.

2. Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa hotuba zako. Ninapenda sana ‘tone of voice’ yako katika hotuba zako. Ni ‘tone’ ya chini lakini ujumbe ulio ndani yake ni ujumbe wa nguvu, uliobeba upendo, maono, wenye kuonya, wenye kuleta upatanisho, wenye kuleta uponyaji, wenye maelekezo, wenye kupambanua ujasiri wako, utu wako, na ujumbe uliojaa matumaini.

3. Pamoja na mafanikio makubwa katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoto wa kiTanzania wanaopata fursa ya elimu kutokana utekelezaji wa Elimu pasipo ada, kuna changamoto ya utoaji elimu bora kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na walimu wetu kukosa morali ya kazi kwa sababu ya mazingira magumu ya kazi wanayokabiliana nayo. Kuna idadi kubwa ya wanafunzi katika madarasa yetu. Mfano, takwimu za TAMISEMI za mwaka 2020 zinaonesha wastani wa uwiano wa mwalimu mwenye sifa-wanafunzi katika elimu ya awali kwa shule za Serikali ni 1:193 na kwa shule za msingi ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi sitini na mbili. Ni kwa muda sasa walimu hawajapata nyongeza STAHIKI ya mshahara ya kila mwaka. Kuna changamoto katika upandaji wa madaraja. Hali hii inafifisha morali ya walimu ya ufundishaji. Nchi nyingi duniani zilizofanikiwa katika elimu ziliwekeza vya kutosha kwa walimu.

4. Rai yangu kwako, Mheshimiwa Rais, kwa heshima na taadhima, pamoja na kuendelea kuboresha miundo mbinu ya elimu unaofanywa na serikali, nakuomba uangazie sekta ya ‘WALIMU’ katika ngazi zote za elimu nchini. Waangalie WALIMU wako kwa jicho la pekee. Mipango ya elimu ielekee katika kuboresha mazingira ya kazi ya walimu, kuboresha maslahi yao, kuwatia moyo walimu na kuwapa matumaini. Katika kuboresha mazingira ya walimu kuna haja ya kuendelea kuajiri walimu wenye sifa kwa kuzingatia idadi ya mikondo shuleni na si idadi ya wanafunzi.

5. Sambamba na uboreshaji wa mazingira ya kufundishia na maslahi ya walimu, jitihada za kuimarisha ubora wa walimu ziendelee ikiwa ni pamoja na kuanzisha Stashahada ya Ualimu wa shule za msingi kama Ilani ya CCM ya mwaka 2020 inavyopendekeza katika ukurusa wa 129, kipengere ‘n’.

Mheshimiwa Rais, nikutakie kila lililojema katika utekelezaji wa majukumu yako.

Ndimi, Mwalimu Richard Yesaya Shukia, Shule Kuu ya Elimu, Chuo Kikuu Dar es Salaam
 
😂😂Ila mwendazake alikuwa na mbinu kali sana, kila meimosi anakuja na sound mpya "ooh mke wangu mwalimu,sijui waziri mkuu mwalimu, tunawapenda sana" Hadi miaka mitano ikakatika kisanii kabisa. Duu tulikuwa na rais jiwe kwelikweli!
 
Mama samia alipohitimu f4 hakufanya vzr, maana yake alilamba bashite, akajikongoja jadi masters na kajisajili PhD.

Unataka walimu wa cheti wafutwe ili iweje,
Mama atakaeleta walaka huu mtengue siku hiyo hiyo.
 
Waraka wa Wazi wa Mwalimu Shukia kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan.

Wazo kuu: Elimu Bora ni Zao la Walimu Bora

1. Niungane na Watanzania wenzangu kwanza; kukupa pole kwa kuondokewa na mpendwa wetu, Hayati Rais John Pombe Magufuli; pili NIKUPONGEZE kwa kuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya sita kwa dhati na kukutakia kila lililojema katika kutekeleza majukumu yako. Wengi wamezungumzia juu ya utendaji wako mahiri. Nami naungana nao katika kushadadia hilo.

2. Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa hotuba zako. Ninapenda sana ‘tone of voice’ yako katika hotuba zako. Ni ‘tone’ ya chini lakini ujumbe ulio ndani yake ni ujumbe wa nguvu, uliobeba upendo, maono, wenye kuonya, wenye kuleta upatanisho, wenye kuleta uponyaji, wenye maelekezo, wenye kupambanua ujasiri wako, utu wako, na ujumbe uliojaa matumaini.

3. Pamoja na mafanikio makubwa katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoto wa kiTanzania wanaopata fursa ya elimu kutokana utekelezaji wa Elimu pasipo ada, kuna changamoto ya utoaji elimu bora kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na walimu wetu kukosa morali ya kazi kwa sababu ya mazingira magumu ya kazi wanayokabiliana nayo. Kuna idadi kubwa ya wanafunzi katika madarasa yetu. Mfano, takwimu za TAMISEMI za mwaka 2020 zinaonesha wastani wa uwiano wa mwalimu mwenye sifa-wanafunzi katika elimu ya awali kwa shule za Serikali ni 1:193 na kwa shule za msingi ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi sitini na mbili. Ni kwa muda sasa walimu hawajapata nyongeza STAHIKI ya mshahara ya kila mwaka. Kuna changamoto katika upandaji wa madaraja. Hali hii inafifisha morali ya walimu ya ufundishaji. Nchi nyingi duniani zilizofanikiwa katika elimu ziliwekeza vya kutosha kwa walimu.

4. Rai yangu kwako, Mheshimiwa Rais, kwa heshima na taadhima, pamoja na kuendelea kuboresha miundo mbinu ya elimu unaofanywa na serikali, nakuomba uangazie sekta ya ‘WALIMU’ katika ngazi zote za elimu nchini. Waangalie WALIMU wako kwa jicho la pekee. Mipango ya elimu ielekee katika kuboresha mazingira ya kazi ya walimu, kuboresha maslahi yao, kuwatia moyo walimu na kuwapa matumaini. Katika kuboresha mazingira ya walimu kuna haja ya kuendelea kuajiri walimu wenye sifa kwa kuzingatia idadi ya mikondo shuleni na si idadi ya wanafunzi.

5. Sambamba na uboreshaji wa mazingira ya kufundishia na maslahi ya walimu, jitihada za kuimarisha ubora wa walimu ziendelee ikiwa ni pamoja na kuanzisha Stashahada ya Ualimu wa shule za msingi kama Ilani ya CCM ya mwaka 2020 inavyopendekeza katika ukurusa wa 129, kipengere ‘n’.

Mheshimiwa Rais, nikutakie kila lililojema katika utekelezaji wa majukumu yako.

Ndimi, Mwalimu Richard Yesaya Shukia, Shule Kuu ya Elimu, Chuo Kikuu Dar es Salaam
Dawa ya Mwalimu mwenye kidomodomo kama wewe ni kukuletea Mkuu wa Wilaya mmoja tu akucharaze bakora za kutosha, huu utopolo ulikuwa wapi kumwandikia mwendazake?
Si ndio wewe uliyekuwa ukimuabudu na kumsujudia mwendazake ukidhani utapewa uteuzi?
 
Mbona hukumwambia haya Rais wenu mzalendo aliyemaliza kipindi kimoj? O

Issue ya kuwaboreshea maslahi sijui kama itawezekana, pesa haitoshi, na hasa mazingira ya sasa ambayo wizara ya fedha inashinikizwa mafungu yaelekezwe Zanzibar
 
Back
Top Bottom