Waraka wa wazi kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa wazi kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwamola, Jul 26, 2012.

 1. m

  mwamola Senior Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza, heshima yako na pole kwa majukumu ya kila ya ujenzi wa taifa hili.\

  Pili, Uniwie radhi kama nitakayosema yatakuwa mambo ya kawaida sana kiasi chakutostahili waraka huu. Hata hivyo nimeona yaweza kuwa ni ya muhimu kwangu/kwetu wahanga wa tatizo hili.

  Mheshimiwa Rais mimi na wenzangu wafanyakazi wa UDOM tulikuwa promoted November 2010 na November 2011 kutoka ngazi moja ya utumishi kwenda nyingine. Kwa wale wa November 2010 tulikaa pasipo kulipwa mshahara wa ngazi mpya ya mshahara kwa miezi 13 pasipo kulipwa mshahara huo mpya hadi hapo December 2011 tulipolipwa.

  Baada ya kulipwa tulijaza salary arrears claim forms mwezi February 2012 lakini hadi leo hatujalipwa malimbikizo hayo. Cha kusikitisha zaidi ni pale tulipokuwa tunajaza form hizo tuliambiwa tujaze mshahara wa chini ya stahili yetu kwa maelezo kuwa Hazina wangetulipa pasipo kujali kile tulichojaza (stahili yetu).

  Naandika waraka huu kukuomba mawili;
  i) Kuomba utusaidie tulipwe mapunjo (arrears) yetu kwakuwa imechukua muda mrefu sasa.
  ii) Kuomba ofisi yako kupitia utumishi utupeleke kwenye ngazi stahili ya mshahara yaani PUTS 2/3 badala ya PUTS 2/1 ambayo tumekuwa tukilipwa tangu November, 2010

  Tuna imani ofisi yako itatusadia kupata haki yetu hii cheleweshwa ama tuliyopunjwa kwa muda mrefu sasa.

  Ndimi katika ujenzi wa taifa
  Mtumishi katika nchi hii.
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,068
  Trophy Points: 280
  ''katika nchi hii''..!!
   
 3. o

  oyaoya JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Fuatilia ngazi husika mkuu, si kila jambo latatuliwa na rais. Nna hakika hata ngazi ya wizara hutaifikia na hiyo ishu itakuwa solved easily.
   
 4. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Unamjua anaewafanyia hvyo..a.k.a P.F.A.
   
 5. C

  Careboy wamuntere Senior Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi hii ina urasimu kaka, utakuta hata hwenye board husika hizo hela watu wanagawana na ukionekana unafuatilia basi huenda kibarua kikaota mbawa, hii ndo Tanzania bwana, sio UDOM tu hata ofisi zingine za Umma hayo mambo yapo, tena wale wenye kuchapa kazi vizuri ndo wanaodidimizwa sijui ni kwanini. kwa hiyo naomba binafsi kama rais ameliona hilo alifanyie kazi kwani watu siku hizi hawafanyi kazi zao kiuadilifu mpaka wasukumwa aibu sana hii.
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,783
  Likes Received: 36,779
  Trophy Points: 280
  Kama mnataka kulipwa vizuri, acheni kazi muende huko mnapopaamini- by JK

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 7. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Kama ulilipwa hiyo ngazi mpya ya mshahara shukuru Mungu, kawaulize walimu wa sekondari na shule za msingi wanamadai ya kuanzia lini na wamejaza CLAIM FORMS mara ngapi......! Shukuru kwa japo hilo serikali na hazina haina hela hata za kulipa/kurejesha mabilioni yaliyokopwa PPF,NSSF, PSPF ili kukijenga chuo cha UDOM. Na ndio maana wamepitisha waraka kupitia SSRA kuzuia ulipwaji wa mafao hadi 60yrs kwa kua kufanya hivyo mifuko itafilisika mwaka 2013.

  Agalizo ni kupima uwezo wa utendaji wa serikali ya CCM na kuchukua hatua 2015. Karubu kundini tumtafute kondoo aliepotea tangu uhuru mwaka 1961.......
   
 8. b

  bogota the king Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kibaya ni kwamba Rais wako huwa hasomi waraka ndani ya JF. Umeingia chaka! Vinginevyo mambo mazito yanachambuliwa humu yangesikilizwa hii nchi isingefika hapa tulipo!
   
 9. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Myopic thinking! unafikiri RAIS ni mtu mmoja? URAIS NI TAASISI, make no mistake kila siku wasaidizi/washauri wa RAIS husoma michango ya JF and when neccessary humpatia briefing.

  Kwa mfano suala SSRA na mafao yetu, kelele za JF zimeshafika IKULU na RAIS ameshakuwa briefied. Inategemea tu pressure yetu itakuwaje wafanyakazi.

  kama wewe unai underate JF kwanini kila siku inasemwa Bungeni? Mama Rwakatale, Dr. Nkya na jana Ngamia.

  FYI, mitandao ya kijamii ndiyo iliratibu Arab springs ktk nchi za Algeria, Egypt, Libya!
   
 10. M

  Maga JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Pole sana mwananchi
   
 11. peri

  peri JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Fuatilia kweneye ngazi husika na kuwa na subra ndugu, haki ya mtu haipotei.
  Kuna watumishi wamedai muda mrf sana lkn baaade wakalipwa.
   
 12. m

  mwamola Senior Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wafanyakazi hawa wamefuatilia sana tena kwakupitia vikao halali vya ndani ya chuo vingi kadiri ilivyowezekana na kumekuwa na lugha mbalmbali tangu july 2011 kwa kupitia barua mbalimbali za PFA na Director HRM kuwa serikali imefikia pazuri na uongozi na muda wowote tutalipwa. Cha ajabu ni kuwa hadi sasa hatujalipwa na nimeomba ofisi ya Rais na kwa uwezo wa Rais mwenyewe watumishi hawa walipwe hii ni kutokana na kauli za waziri wa utumishi kuwa zikishajazwa tu hizo claim forms watalipwa lakini leo ndoto hizo zimezima. Zaidi ni kwamba hazina, utumishi na wizara ya elimu zimekuwa zikitajwa na maafsa wa UDOM kuwa ndio wakwamishaji wakubwa wa malipo haya. nimemwomba rais kwa kuwa yu zaidi ya wizara zote
   
 13. s

  sawabho JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mkuu, kama umeishafuatilia kwa HR, Wizarani na Utumishi ikashindikana, nakushauri uandike barua kwa Rais na kuambatisha mawasiliano ambayo yamekuwa yakifanyika. Maana hapa JF huwezi taja wewe ni nani kwa majina.
   
 14. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Naunga mkono hoja!
   
 15. M

  Mwangendage Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wewe Jambo la kumalizwa n a UDOM unapeleka kwa Rais? hana muda huo na siyo kazi yake. kama management ya chuo imeshindwa kukusaidia appeal kwenye bodi ya chuo. I mean kwa Charman of board of Directors.
   
 16. M

  Mwangendage Member

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  umeonana na katibu wa wizara mara nagpi kuhusu jambo hili? au mwenyekiti wa bodi? au mkurugenzi wa wizara anayeshughulika na HR za vyuo?
   
 17. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mambo ya huko UDOM yanatisha. Unaweza ukaajiriwa ukamaliza hata mwaka mzima bila kuthibitishwa kazini wakati sheria za kazi zinasema ukimaliza miezi 6 uthibitishwe!
   
Loading...