Waraka wa wanafunzi wa elimu ya juu kwa rais jk. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa wanafunzi wa elimu ya juu kwa rais jk.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaga Michael, May 8, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,888
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ufuatao ni waraka wa wanafunzi
  wa elimu ya juu nchini kwa
  Serikali, kuhusu migomo na
  maandamano ya mara kwa mara
  hapa nchini. Umeandikwa na
  jopo la viongozi wa wanafunzi
  wa vyuo vikuu na wameupeleka
  serikalini. Wanatoa ushauri
  maridhawa wa namna ya
  kukomesha migomo kwa
  kuboresha sekta ya elimu, hasa
  kwa kuwapa fursa wanafunzi
  wote bila ubaguzi. Waraka huu ni
  mrefu na JAMHURI itauchapisha
  wote kuanzia leo. Endelea…
  Tunapenda kuchukua fulsa hii
  kwanza kuomba msamaha na
  kuwataka radhi wazazi wetu
  mliotutuma kwenda kutafuta
  elimu vyuo vikuu hapa nchini,
  kutokana na vurugu, migomo na
  maandamano ya mara kwa mara.
  Mambo hayo mmekuwa
  mmekuwa mkiyasikia au
  mkiyaona kupitia vyombo vya
  habari yakitokea katika vyuo
  mbalimbali hapa nchini.
  Pia tunaomba radhi kutoka
  mioyoni mwetu kwa walimu
  wetu (lecturers) kwa adha
  inayowakuta inapotokea
  migomo na maandamano.
  Pia tunawaomba msamaha
  viongozi wetu wa dini ambao
  kwa namna moja ama nyingine,
  wamekuwa wakitulea kiroho na
  kimaadili. Lakini tutakuwa
  hatujawatendea haki Watanzania
  ambao kodi zao ndizo
  zinazogharamia elimu yetu hapa
  chini.
  Bila shaka walitarajia kutuona
  tukisoma kwa bidii na kufaulu
  vuzuri, ili tutakaporudi katika
  jamii zetu tutumie elimu
  tuliyoipata kuwakomboa
  Watanzania wenzetu, ambao
  hadi sasa wanalia na kuangamia
  na vita kubwa ya Ujinga,
  Umaskini, Maradhi na Ufisadi,
  lakini wameendelea kushuhudia
  migomo na maandamano ya
  mara kwa mara yasiyo na
  kikomo.
  Baada ya kutafakari kwa kina
  kama wasomi, tukaona kama
  hatutakaa chini na kufanya utafiti
  (research) wa vyanzo na sababu
  zinazotufanya tuwe na migomo,
  tuandamane na kufanya vurugu
  za mara kwa mara vyuoni.
  Hatutaeleweka na tutaonekana
  kweli sisi ni wahuni, au
  tunatumiwa na watu ama
  wanasiasa wakati hizi ni tuhuma
  ambazo hazina ukweli hata
  chembe ndani yake.
  Lakini tunapenda kuwataarifu
  viongozi wetu, wazazi na
  Watanzania kwa jumla, kwamba
  matatizo haya yanatokana na
  vitendo vichafu vya baadhi ya
  watumishi pamoja na sera
  mbovu za kikandamizaji,
  kibaguzi, manyanyaso na uonevu
  uliovuka mipaka kwa wanafunzi
  wa elimu ya juu (vyuo vikuu).
  Na hatutaeleweka kwa walimu
  wetu waliojitolea kwa uzalendo
  wao wa hali ya juu, kutufundisha
  japo masilahi yao ni madogo
  ukilinganisha na kazi kubwa
  wanayoifanya.
  Pia kama tungekaa kimya,
  viongozi wetu wa dini ambao ni
  walezi wetu wa kiroho na
  maadili wasingetuelewa. Vilevile
  hatutaeleweka zaidi kwa
  Watanzania ambao wanatozwa
  kodi kwa ajira ya kugharamia
  elimu yetu ya juu, ili tusome kwa
  bidii ili turudi kulitumikia taifa.
  Tumefanya utafiti huu wa
  migomo, vurugu na
  maandamano ya mara kwa mara,
  ili tutoe taarifa ya upande wa pili
  wa wanafunzi, kwani kumekuwa
  na desturi au utamaduni wa
  vyuo kutoa taarifa zisizokuwa na
  ukweli kwa wananchi (umma),
  kwa kuwasingizia wanafunzi
  kwamba wanatumiwa na
  viongozi wa siasa kufanya fujo,
  vurugu na migomo matatizo
  haya yanapojitokeza.
  Taarifa hizi zisizokuwa na ukweli
  zimekuwa zikitolewa na baadhi
  ya watawala wa vyuo, ili
  kukwepa kutekeleza madai yetu
  ya msingi kwa kisingizio hiki
  kisicho na ukweli ndani yake,
  kama ilivyonekana katika gazeti
  la Mtanzania toleo namba na
  5842 la Jumapili Januari 15,
  2012.
  Kuna makala yenye kichwa cha
  habari kilichoandikwa kwa
  herufi kubwa na kusomeka:
  Vurugu UDSM: Uongozi wa chuo
  wadai waliofukuzwa ni
  wanasiasa.
  Habari kama hiyo ilichapishwa
  katika gazeti la Uhuru ilisomeka,
  “Vurugu za: Chama cha …
  cashukiwa kuwa nyuma ya
  mgomo’. Gazeti la Mzalendo la
  Januari 15, 2012 lilikuwa na
  makala yenye maudhui kama
  hayo.
  Kwa bahati mbaya, kwa upande
  wa wanafunzi hatukupata nafasi
  ya kukanusha madai hayo kwa
  ushahidi wa wazi kwa wazazi,
  walimu, viongozi wetu wa dini
  na Watanzania waliolipa kodi
  zinazotusomesha, wakaamini
  madai yaliyotolewa na Serikali na
  utawala wa chuo kuwa ni sahihi.
  Wakatuhukumu na kuwafukuza
  chuo wenzetu kwa kutuhusisha
  kutumiwa na vyama vya siasa,
  kitendo ambacho si kweli.
  Walifanya hivyo ili kukwepa na
  kupinga hoja na madai yetu ya
  msingi kwa majibu mepesi eti
  tumetumwa, ni ajabu kweli!
  Namna hii siasa zinavyoingizwa
  katika chuo, matokeo yake chuo
  kinakuwa sehemu ya kisiasa,
  jambo ambalo si sahihi. Chuo ni
  taasisi inayojitegemea, hivyo
  inapaswa kuendesha mambo
  yake bila kuingiliwa na taasisi
  nyingine.
  Hali hii ikiachwa iendelee kama
  Serikali haitatekeleza
  mapendekezo yetu ambayo ni
  njia sahihi ya kupunguza vurugu,
  migomo na maandamano, vyuo
  vikuu nchini kama siyo kumaliza
  kabisa, tutaomba wazazi wetu,
  walimu wetu na Watanzania
  walipa kodi mtuelewe kwa
  uamuzi mgumu tutakaochukua
  kama itakavyoonekana inafaa.
  Lakini vyuo vikuu vitapoteza sifa
  yake ya ndani na nje ya nchi.
  Vitabaki ni vyuo vya migogoro ya
  migomo, vurugu na
  maandamano miaka nenda rudi.
  Kufukuza wanafunzi si
  mwarobaini wa tatizo kwani
  maandamano, vurugu, migomo
  itaendelea kuwapo endapo
  madai na mahitaji ya wanafunzi
  hayatatekezwa.
  Yapo madhara makubwa
  ambayo yanatokana na migomo
  vyuoni, yakiwamo ya kuharibiwa
  kwa rasilimali za chuo, kuharibu
  ratiba za masomo, Serikali
  kuingia hasara na gharama za
  ziada chuo kinapofungwa kwa
  mgomo, kwani bajeti ya chuo
  inakuwa ilishapitishwa, na
  gharama za kupeleka polisi na
  magari ya maji ya kuwasha na
  mabomu ya machozi zinakuwa
  mzigo.
  Kibaya zaidi ni kwa wanafunzi
  kufukuzwa na kusimamishwa
  masomo, ambao
  wamegharamiwa na kodi za
  Watanzania wakitarajiwa
  kuhitimu na kurejesha mikopo
  na kulitumikia taifa letu.
  Tunaomba wazazi, walimu,
  viongozi wetu wa dini na
  Watanzania walipa kodi, kwa
  pamoja mtumie fursa hii
  kuishauri Serikali kutekeleza
  mapendekezo yetu, ili kuinusuru
  sekta mama ya elimu nchini
  isiyumbe na kuporomoka kwa
  kasi ya ajabu.
  Ni matumaini yetu kila kundi
  litatumia nafasi yake kuishauri
  Serikali kupokea mapendekezo
  yetu.
  Ili binadamu aweze kuzikabili
  changamoto za maisha na
  kujikomboa katika lindi la
  umasikini, lazima awe na elimu.
  Elimu ndiyo msingi wa
  kujitambua, kuyatawala na
  kuyatumia mazingira anamoishi
  binadamu ili kuboresha maisha
  yake na kujiletea maendeleo ya
  haraka.
  Ni wazi kuwa elimu ndiyo
  ukombozi wa binadamu kuiona
  kesho iliyo bora zaidi na
  kuogelea katika bahari ya
  utandawazi, ambayo inamtaka
  kila mmoja aogelee kwa namna
  awezavyo.
  Kwa kutambua ukweli huo,
  Serikali ya Tanzania imetoa fursa
  kwa wadau wa elimu kuwekeza
  katika sekta hiyo, ili kujenga taifa
  la watu wenye maarifa, ujuzi na
  uwezo wa kuzalisha.
  Dira ya Taifa ya Maendeleo ya
  mwaka 2025, Mkakati wa Kukuza
  Uchumi na Kupunguza Umasikini
  Tanzania (MKUKUTA) pamoja na
  Sera ya Elimu na Mafunzo, vyote
  vinaeleza umuhimu wa elimu ili
  kuiwezesha nchi kusonga mbele.
  Watanzania na wazazi kwa
  ujumla wanatarajia kuona
  watoto wao wanapata maarifa
  na uwezo, ili wachangie juhudi
  za Watanzania na wazazi wao
  kutatua changamoto zilizopo
  katika jamii.
  Wanafunzi wenye maarifa na
  ujuzi huwa na uwezo wa
  kufanya mambo mengi mapya
  kwa usahihi na kuwaongoza
  wenzao. Katika maendeleo ya
  ukweli katika jamii tunamoishi,
  matendo ya wasomi, kazi zao,
  majukumu yao na shughuli
  wanazofanya zinapaswa
  kudhihirisha matunda ya elimu
  waliyonayo.
  Zao muhimu la elimu kwa mtoto
  ni kuwa na uwezo mkubwa wa
  kufikiri kwa makini. Uwezo huu
  ndiyo unaohitajika sana katika
  jamii ya leo. Mtu mwenye uwezo
  wa kufikiri ndiye mwenye nguvu
  ya kuibua dhana mpya na
  kutafuta njia mbadala za kutatua
  matatizo.
  Watu walioibua teknolojia
  tulizonazo waliongozwa na upeo
  wa kufikiri ndipo wakaibuka na
  dhana mpya. Tendo la kufikiri
  lipo ndani ya akili na utashi wa
  mtu. Bila kufikiri matokeo ya
  juhudi za mtu mara nyingi huwa
  anguko au hasara.
  Serikali pamoja na wadau wa
  elimu nchini, wana mchango
  mkubwa wa kuibua taifa la
  wasomi na kutekeleza Dira ya
  Taifa ya Maendeleo ya Mwaka
  2025, MKUKUTA na Sera ya Elimu
  na Mafunzo ambavyo vyote
  vinaeleza umuhimu wa elimu ili
  kuiwezesha nchi kusonga mbele.
  Kukua kwa uchumi pamoja na
  mambo mengine hutegemea
  uwekezaji hasa wenye manufaa
  kama elimu, ili kupata wataalamu
  ambao ndiyo watakaoinua
  uchumi wetu. Kimsingi, uchumi
  hauwezi kukua bila wasomi. Nchi
  lazima iandae rasilimali watu
  wanaohitajika ili kuinua uchumi
  wa nchi yetu na kusaidia familia
  zao masikini.
  Rais wa Kwanza wa Tanganyika
  (Tanzania Bara) aliwahi kusema
  maneno yafuatayo katika hotuba
  zake kwa wananchi kwamba:
  “Hakuna Serikali yoyote duniani
  inayowawekea wananchi wake
  hela mfukoni, bali “the only best
  way to enrich a poor people is to
  educate their children” yaani njia
  pekee ya kuwasaidia wananchi
  masikini ni Serikali
  kuwasomeshea watoto wao.
  Kwa hili alikusudia kwamba
  ukimsomesha mtoto wa maskini,
  atakapopata hiyo elimu ataitumia
  kuinua familia yake kiuchumi na
  taifa kwa jumla. Ndiyo maana
  baada ya kupata Uhuru, Mwalimu
  Julius Nyerere alitambua maadui
  watatu- Maradhi, Umaskini na
  Ujinga.
  Lakini ili ukabiliane na maadui
  hawa, lazima uanze na adui
  ‘ujinga’ kwa kutoa elimu bora
  kwa wananchi ili waondoe
  umasikini na maradhi. Lakini
  tumeshuhudia Serikali kwa sasa
  inavyosuasua katika sekta hii
  muhimu ya elimu nchini.
  Katika Katiba ya Jamhuri ya
  Muungano wa Tanzania ibara ya
  9 kifungu kidogo cha (i), inasema
  hivi: “Matumizi ya utajiri wa Taifa
  yanatilia mkazo maendeleo ya
  wananchi na hasa zaidi
  yanaelekezwa kwenye jitihada ya
  kuondosha umasikini, ujinga na
  maradhi.”
  Kama tulivyosema, baada ya
  Uhuru wa Tanganyika mwaka
  1961, na baadaye Muungano wa
  Tanganyika na Zanzibar mwaka
  1964, Mwalimu Nyerere
  alitangaza vita kwa maadui
  watatu - Ujinga, Maradhi na
  Umasikini.
  Mwalimu alihakikisha
  anafanikiwa katika mapambano
  hayo. Alianza kuweka mikakati
  mbalimbali ikiwa ni pamoja na
  kukazia elimu ili kufuta ujinga,
  kupatikana madaktari wa
  kupambana na adui maradhi na
  wataalamu wa uchumi wa
  kupambana na adui umasikini.
  Fikra hii ya Mwalimu ilidumu hadi
  kufikia maziko ya Azimio la
  Arusha na kuanzishwa Azimio la
  Zanzibar Februari 1991 lililoamua
  kufuata mfumo wa kibepari
  uliokusudia kumilikisha rasilimali
  ya Tanzania kwa wachache.
  Baada ya hapo, maadui hawa
  waliwavamia Watanzania. Ujinga
  ulianza kuongezeka (idadi ya
  watu wasiojua kusoma na
  kuandika iliongezeka), maradhi
  yakaongezeka - vifo kwa mama
  na mtoto; uchumi ukadorora,
  umasikini ukaongezeka, shilingi
  ya Tanzania ikashuka thamani
  siku hadi siku huku mfumuko wa
  bei ya bidhaa ukiwaumiza
  wananchi wa kipato cha chini.
  Hilo ndilo Azimio la Zanzibar.
   
 2. T

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,746
  Likes Received: 513
  Trophy Points: 280
  Waache siasa wasome,

  Na ndio maana tunapata watendaji wabovu na wezi kwenye idara zetu, mitoto imekuwa mivivu kila kukicha inataka kugoma
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Waache siasa ili iweje. Au hujui maana ya siasa. Ukiacha siasa unakuwa mfu ndani ya jamii. Au bado unafikiri siasa ni uongo. Siasa ni Art and Science of social life. Is a way of life.
   
 4. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 945
  Likes Received: 283
  Trophy Points: 80
  mhn! napita tu
   
 5. T

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,746
  Likes Received: 513
  Trophy Points: 280
  Jifunze tofauti ya viunganishi and na or, usije aibika! ukisema art and science ni tofauti na kusema art or science!

  Kaangalie upya tafsiri ya siasa!
   
 6. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mchana migomo, usiku masomo
   
 7. M

  MAKAWANI Senior Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  "No person shall be condemed unheard" Wasiposikilizwa wakigoma msiseme wametumwa! Huo ni mwanzo mzuri!
   
 8. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwanza watuambie kama wao sio miongoni mwa waliondama kwenda kwa Nape kuipongeza CCM na JK siku chache zilizopita au?
   
 9. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Migomo duniani kote wanafunzi wanafanya sema Rais asake njia ya kuipunguza tu
   
 10. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kichwa chako kina shida sana....you don't even spend a second to think before you write your s.t.u.p.i.d.i.t.y....JK alianzia wapi siasa? Nyerere alianzia wapi siasa? Nkwame alianzia wapi siasa? Mbona hawa waliondamana juzi kuupongeza uamuzi wa cc ya ccm kuwaondoa wabunge wa ccm wezi haukusema kuw waache siasa wasome???? I do not think if you really make your BRAIN participate in your decision making? Bado unaamini kuwa ccm itatawala milele na ndiyo mbinu za ccm kusema kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu waache siasa vyuoni wasome huku wao wakitafuna nchi...kama wasomi watakaa kimya nani atasema? Ilikuwa enzi zile....kitabu tunapiga na siasa kama kawa....imekula kwenu...!!!

  STK ONE,
   
 11. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 4,983
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  hiyo ni double standard ya nchi yetu. Wanapenda kusikia kwamba wanachuo wote wanaipenda ccm basi! Wakisikia kuna wanaodai haki zao wanasema ni wafuasi na wamechochewa na cdm. Miaka ya nyuma sita aliwahi kuongoza mgomo udsm mpaka akachapwa viboko na jkn,sijui ni cdm gani ya wakati ule iliwachochea.
   
 12. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 4,983
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  serikali nyingi duniani ambazo ni dhaifu zimeangushwa/ziliangushwa na migomo ya wanachuo mf venezuela. Tanzania sio nchi ya kwanza kuwa na maandamano hayo.
   
 13. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,524
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  wamenena. tuwasikilize na kufanyia kazi dukuduku zao.

   
 14. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,391
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 160
  Acha kukurupuka, fanya utafiti kwanza.
   
 15. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 376
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  wale wa nape ni uvccm wa Bagamoyo, hakuna mwanachuo taahira
   
 16. b

  bdo JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,679
  Likes Received: 1,557
  Trophy Points: 280
  Ngoja nilale kwanza halafu nirudi kumalizia kuusoma huu waraka, ...
   
 17. b

  busar JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 485
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Seen. ..
   
 18. Mfarisayomtata

  Mfarisayomtata JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 410
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Usiseme walaka wa wanafunzi wa vyuo vikuu. Taja chuo husika sisi wengine mbona hatuujui huo?? Na utakuwa walaka wa wanafunzi wa UDOM.
   
Loading...