Waraka wa Waislam Kuelekea Uchaguzi

Mfumwa

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
1,456
42
Sina uhakika kama ulishawekwa hapa, mods kama ulishawekwa naomba muunganishe thread. Nimeu attach kwa hii msg.
 

Attachments

  • WARAKA WA WAISLAM.doc
    239 KB · Views: 601
Kwa upande wa Waislamu, zoezi la uchaguzi ujao linaweza kuwa Ibada na hatua muhimu ya kuwakomboa na hatimaye kuwapatia fursa muhimu kama ilivyo kwa raia wenzao Wakiristo. Haya yatategemea maamuzi na umakini wao wakati wa kuchagua wagombea udiwani, ubunge na urais. Ni kwa sababu hii basi, Shura ya Maimamu Tanzania inaona ni wajibu wake kutoa muongozo huu kwa Maimamu kwa lengo la kuwaandaa Waislamu kote nchini kushiriki uchaguzi ujao kwa kuzingatia maslahi ya Waislamu na Uislamu wao.

Hii ndiyo elimu ya uraia!
 
(17) HITIMISHO

Kwa kulitambua hilo, Shura kupitia kamati zake za siasa ambazo ni, kamati kuu, kamati za Mikoa, Wilaya/Majimbo na kamati za Kata, zimejitwisha dhima ya kuhakikisha kuwa Waislamu wa Tanzania kama Waislamu wanaingia katika uchaguzi ujao Kuingia katika uchaguzi kama Waislamu hakuna maana ya kupigia kampeni chama chochote cha siasa, kwani katika vyama vyote vilivyopo hakuna chama kilicho sajiliwa kama chama cha Waislamu wala cha Kiislamu.

Hii ndiyo elimu ya uraia katika nchi ya demokrasia.
 
Nimejitahidi kuusoma waraka huu kwa haraka haraka kwa kuwa sikuvutia kutumua muda wangu mwingi. Waraka unaonyesha uwezo mdogo walionao waandaaji hasa katika masuala ya siasa, dini na ushawishi kwa ujumala.

Waraka huu umekaa kama mhadhara wa kawaida kama ile ambayo huwa inatolewa ktk baadhi ya misikiti hapa bongo. Waraka umetumia kurasa nyingi kumlaumu Nyerere, Kanisa katoliki na ukristo kuliko mlengwa ambae ni Serikali.

Waraka haukujikita kuchambua sera bali umeonyesha baadhi ya yale yanayoonekana ni kero hasa kutokana na kutofuata sheria zilizopo. 35% unaongelea Kanisa Katoliki, 35% Uislam na waislam, 20% wakristo na 10% tu ndo inaongelea Serikali, Sera na uchaguzi 2010.

Binafsi waraka huu umenionyesha 'uwezo' wa wahusika katika kuyajua na kuchambua mambo.
 
Katika taarifa ya habari ya kituo cha luninga cha ITV, saa 02:00 usiku wa kuamkia uchaguzi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (wakati huo) Bw. Omari Mahita alihitimisha kampeni za vitisho kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu na kuwanasibisha wapinzani hususani CUF na visu kuwa ni silaha walizojiandaa nazo kwa ajili ya kuhatarisha amani nchini. Hauta hii ya mahita ilikuwa ni moja kati

Kamati Kuu ya Siasa ya Shura ya Maimamu Tanzania, ilimuandikia Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuomba kuruhusiwa kuweka waangalizi katika majimbo yote ya uchaguzi nchini

sasa hii shura mbona ipowazi kuwa wao wanaitetea CUF? hawa ndio mnaoifanya CUF kuwa chama cha waislamu na ndo tatizo kubwa lililopo sasa,CUF imefulia kwa kukosa mwelekeo,mnapiga domo tuu wenzenu znz wanaumizwa,kisa mumekaa kidini dini,naapa CUF haitakaa ije kushika dola kwa kosa hili!!
 
chaguzi zote za nyuma Waislamu wamekuwa wakipiga kura kwa kuzingatia zaidi umoja wa kitaifa na kile walichoamini kwamba ni maslahi ya Taifa. Pamoja na kuwa wao ndiyo kundi kubwa la kidini kuliko yote, mtizamo na msimamo huu umesababisha nguvu yao kisiasa kuwa dhaifu mno na hivyo kuathirika mno kijamii. Tofauti na Waislamu, Wakristo wao wamekuwa wakizingatia sana maslahi yao ya kidini kila wakati wa uchaguzi. Kutokana na mazingatio haya karibu viongozi wote wanaochaguliwa, hata wale ambao ni Waislamu wamejikuta wakiendesha shughuli za kila siku za nchi kwa kuzingatia maelekezo na maslahi ya kanisa na Wakristo. Kwa ujumla, kuna vielelezo vingi mno vinavyoashiria kuwa japo nchi yetu ni ya kisekula kikatiba, lakini kiutendaji inatawaliwa na ‘Mfumo Kristo'

JKikwete ushindi wa kishindo/tsunami-Dini mkristo, cheo-kidogo kuliko vyote tanzania
Shein-dini-mkristo,cheo kidogo kuliko vyote tz
pambaf waandishi nyie wa huu waraka, so tumchague mtu kwa kigezo kipi?Je ni wangapi waliwaruhusu watoto wao waende shule enzi hizo?Madrassa ilikuwa ya kumuinua muislamu kutoka wapi na afike wapi? mfumo wa nchi tumetawaliwa na wakristo Waingland + Germans, hamuoni znz kuna waislamu na udunya wa mawazo sababu wametawaliwa na Waarabu? haya mambo yapo wazi hakuna upendeleo hapa,shule,elimu,uelewa wako,kukubalika kwako kutakupa uongozi. thats why hata Bakwata wameliona hili wakaamua kuwakana shura ya manini sijui. utumbo mtupu! kwanza samahani ninakosea kuwalaumu waislamu, naomba niwalaumu hawa mashura waliouandika huu waraka wenye mtazamo na mawazo finyu, na uelewa mdogo kabisa kabisa kuwahi kuonyewshwa na taasisi ya kkitanzania!!puuh shame on you
 
Some this issue is crazy let pray election is something else let learn from our loverly brother and sister Kenyanan what happen
 
Nimejitahidi kuusoma waraka huu kwa haraka haraka kwa kuwa sikuvutia kutumua muda wangu mwingi. Waraka unaonyesha uwezo mdogo walionao waandaaji hasa katika masuala ya siasa, dini na ushawishi kwa ujumala.

Waraka huu umekaa kama mhadhara wa kawaida kama ile ambayo huwa inatolewa ktk baadhi ya misikiti hapa bongo. Waraka umetumia kurasa nyingi kumlaumu Nyerere, Kanisa katoliki na ukristo kuliko mlengwa ambae ni Serikali.

Waraka haukujikita kuchambua sera bali umeonyesha baadhi ya yale yanayoonekana ni kero hasa kutokana na kutofuata sheria zilizopo. 35% unaongelea Kanisa Katoliki, 35% Uislam na waislam, 20% wakristo na 10% tu ndo inaongelea Serikali, Sera na uchaguzi 2010.

Binafsi waraka huu umenionyesha 'uwezo' wa wahusika katika kuyajua na kuchambua mambo.


Unafiki mtupu! kama ulisoma kwa haraka haraka hizo % ulizi compute wakati gani?

Ili uwe waraka mzuri lazima utoke kwa wakatoliki sio? mlishalikoroga subirini mlinywe sasa.
 
Unafiki mtupu! kama ulisoma kwa haraka haraka hizo % ulizi compute wakati gani?

Ili uwe waraka mzuri lazima utoke kwa wakatoliki sio? mlishalikoroga subirini mlinywe sasa.

Sina muda mrefu Jf lakini hata bila kutumia akili nyingi utaona JF sio kama inavyotakiwa iwe.Tunapinga ili mradi umepinga hata kama unaona mwenyewe sio sahihi unalotetea.Tuwe tunaangalia maslahi ya nchi na uzalendo kwanza na sio kushabikia dini.Sioni mimi maslahi ya nchi katika waraka huu zaidi ya uchochezi.
Ohh my God where are great thinkers?
 
Mi na wasiwasi na uwezo wa hawa watu kufikiri!
Hivi hawa jamaa wanajua wanachofanya kweli?
Hawa jamaa hawajui wanachofanya kaka. Na hii inatokana na uwezo mdogo wa elimu "DUNIA", kama wanavyoiita, walionao. Fikiria yafuatayo........

1. Ili kuwa shehe mkuu, shura mkuu wa maimamu, imamu wa msikiti unahitaji elimu kiasi gani??? Nadhani unahitaji madrasa kadhaa, juzuuu za kumwaga na kiasi fulani cha Mashetani na uwezo mkubwa wa kushawishi wenzio wafanye fujo. And I think hii ya mashetani ndiyo sababu WAGANGA WA KIENYEJI KARIBU WOTE NI WAISLAMU, WATABILI WA NYOTA KARIBU WOTE NI WAISLAM, YOU NAME THEM....

2. Ili kuwa askofu unahitaji yafuatayo.........Pri-fomu wani unahitaji wani yia; Fomu wani hadi fomu foo unahitaji foo yeaz, hai skuul unahitaji twu yeaz, seminari unahitaji seveni yeaz. Yaani you need at leas 14 years to be in school before you become PADRE. SASA HUYU PADRE MMOJA ALIYEKO KULE PAROKIA YA KISHUMUNDU AU LITEMBO MBINGA UTAMLINGANISHA NA SHEHE MKUU WA TANZANIA KIELIMU..???? Hawa akina Kundecha, Gologosi na wengine mnajuwa elimu zao?? Most of them form four ya Kinondoni Muslim school NA JUZUU KADHAA. Nani anajuwa elimu Methodius Kilaini anitajie????

3. Kwa waislamu kujuwa sana Vitabu vyao vya dini ndiyo kunakomfanya mtu ajione anafaa kuwa shehe, imamu kwao elimu "DUNIA" siyo tatizo. Wakati kwa wakristu wa kikatoliki hata kama unajuwa Biblia kiasi gani ni lazima uende shule na utangazwe kanisani kwa muda wa at least wiki moja na waumini wakubali huna kasoro ndiyo utaupata huo upadre

KWA HIYO KIMSINGI TOFAUTI YA ELIMU WALIYONAYO VIONGOZI WA KIISLAMU NA KIKRISTU, INAONEKANA HATA KWENYE WARAKA NA MWONGOZO. KUNDI MOJA LINAZUNGUMZIA MATATIZO YA NCHI, LINGINE LINAZUNGUMZIA KUONEWA KWAO.
 
Unafiki mtupu! kama ulisoma kwa haraka haraka hizo % ulizi compute wakati gani?

Ili uwe waraka mzuri lazima utoke kwa wakatoliki sio? mlishalikoroga subirini mlinywe sasa.

Pole sana naona upo offended. Mimi nasema nimesoma na nimejadili baadhi ya aya. Sasa na wewe soma na utuletee ulichokiona kama kinapingana na nilichosema mimi ni tutajadili. Mbona waraka upo hapo? ubishi wa nini? Waraka wa Kanisa Katoliki tuliuchambua hapa. Hata huu tunaendelea kuuchambua na umeonyesha kuwa ni mbumba si mchele lakini bado tutachambua ili akina Shekhe Ponda waone pumba zao.

Eddie, si kweli kwamba ili waraka uwe mzuri lazima utoke katoliki. Maneno haya yanaonyesha uwezo wako wa kufikiri. Hapa tunachambua nini kimo kwenye waraka, nini lengo la waraka, manufaa ya waraka kwa nchi na wananchi. Hapa hatupendi kanisa wala msikiti, tunaipenda Tanzania.

Karibu tuendelee kujadili na kama pumba hizi hazijadiliki basi tuachane nazo na ijulikane kwamba ni pumba zisizojadilika.
 
Hao ndio maimamu, sasa sijui waumini wakoje !! Lakini siwasemi waumini wote, ila wale waliousoma na bado wakaendelea kuushabikia.
 
Tutajadili vipi waraka ambao baraza la waisilamu mbalo ndilo linalotambuliwa na serikali hauutambui
 
Tutajadili vipi waraka ambao baraza la waisilamu mbalo ndilo linalotambuliwa na serikali hauutambui

Waraka umezinduliwa kwenye mkutano wa hadhara. Umesambazwa na unaendelea kusambazwa. Huenda ukaendelea kusambazwa mpaka kipindi cha kampeni na uchaguzi mkuu mwakani. Pia huenda ukawaunatolewa hata ktk chaguzi zijazo.

Sasa kwanini tusijadili?

Kwani masuala ya waislam yanayojadiliwa hapa ni yale yaliyopitishwa na BAKWATA tu?

Hivi hiyo Shura ya maimamu ipo chini ya BAKWATA? kama haipo chini yake kwanini maamuzi ya BAKWATA yazuie mjadala?

Nadhani Shy unakimbia kivuli chako, hili lazima lijadiliwe ili kurekebisha palipokosewa na kuunga mkono palipo sahihi nk.
 
Asanteni, Tumeusoma. Halafu mbona Mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwiru haja comment? Au anawaogopa Waislamu? Mbona yeye anakomment za Wakatoliki tu? Mimi namwomba mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwiru (kwa heshima na taadhima zote tulizo nazo kwake) atoe kommenti pia. mheshimiwa uko wapi? Toa kommenti. Kazi kwako Mheshimiwa Kingunge!
 
Last edited:
Asanteni, Tumeusoma. Halafu mbona Mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwiru haja comment? Au anawaogopa Waislamu? Mbona yeye anakomment za Wakatoliki tu? Mimi namwomba mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwiru (kwa heshima na taadhima zote tulizo nazo kwake) atoe kommenti pia. mheshimiwa uko wapi? Toa kommenti. Kazi kwako Mheshimiwa Kingunge!

Huyo naye muislam.
 
Back
Top Bottom