Waraka wa siri wavujishwa: Marekani ilikusudia kuishambulia China kwa silaha za nyuklia

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,563
32,530
 Daniel Ellsberg
Daniel Ellsberg

Waraka wa siri uliotoroshwa kutoka Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) umefichua kwamba, jeshi la Marekani lilitoa pendekezo la kufanya mashambulizi ya anga ya silaha za nyuklia dhidi ya China hapo mwaka 1958 ili kuihami Taiwan mbele ya majeshi ya utawala wa kikomunisti wa China.

Kwa mujibu wa waraka huo uliofichuliwa katika mtandao wa intaneti na mvujishaji mashuhuri wa siri za Pentagon, Daniel Ellsberg.

Waratibu wa vita wa Kimarekani wakati huo walikadiria kuwa, Umoja wa Kisovieti utaisaidia China na kujibu mashambulizi kwa kutumia silaha za nyuklia, na kwamba shambulizi la nyuklia dhidi ya China lilikuwa thamani inayokubalika kwa ajili ya kuihami Taiwan.

Daniel Ellsberg mwenye umri wa miaka 90 ambaye ni mchambuzi wa zamani wa masuala ya kijeshi ameliambiia gazeti la New York Times kwamba, alidukua nakala ya siri sana kuhusu mgogoro wa Taiwan mwanzoni mwa miaka ya 70 na ameichapisha sasa wakati mgogoro wa nchi hizo bili umepamba moto kuhusu kisiwa hicho.

Baadhi ya yaliyomo katika waraka huo wa siri yaliondolewa katika hali ya usiri mwaka 1975.
Mwaka 1971 Daniel Ellsberg alipata umashuhuri mkubwa kwa kufichua waraka wa siri kupita kiasi wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani kuhusu vita ya Vietnam ambao ulijulikana kwa jina la "Pentagon Papers."
4by1aed6c56f051vlk1_800C450.jpg

Waraka wa siri uliofichuliwa na Daniel Ellsberg unamnukuu mkuu wa majeshi ya Marekani wakati huo, Kanali Nathan Twining akisema, iwapo kutatokea vita Marekani itatumia silaha za nyuklia dhidi ya vituo vya anga vya China ili kuzuia shambulizi la anga la nchi hiyo.

Kanali Twining aliongeza kuwa, iwapo shambulizi hilo halitasitisha vita, Marekani haitakuwa na njia mbadala ghairi ya kushambulia maeneo mengine ya China kwa kutumia silaha za nyuklia hata mji wa Shanghai.

Mgogoro huo ulimalizika mwaka 1958 baada ya majeshi ya utawala wa Kikomunisti wa China kusitisha mashambulizi ya mizinga dhidi ya visiwa vilivyokuwa vikidhibitiwa na Taiwan.

China inaitambua Taiwan kuwa ni jimbo lililoasi ambalo italirejesha kwa ardhi mama ya nchi hiyo hata ikilazimu kwa kutumia nguvu za kijeshi.

Chanzo: Waraka wa siri wavujishwa: Marekani ilikusudia kuishambulia China kwa silaha za nyuklia
 
Hiyo ilikuwa zamani miaka ya 1958. Wakati huu Marekani hawawezi kujaribu au kufikiria huo ujinga mbele ya taifa kubwa la China
Uko sahihi lakini ukweli ni kwamba, kwa wakati huu wote wanaogopana... Hivyo hakuna vita kubwa itakayoibuka kati ya mataifa haya mawili yenye nguvu duniani.

Wote kila mmoja anajitahidi kuepusha vita ya moto
 
Miaka 50 ijayo tutaletewa taarifa za namna ambavyo wamarekani walikuwa wanapanga kuishambulia Iran kwa mizinga ya nuklia na wakafeli baada ya kuugundua katika mioto ya kuotea mbali Iran Ni mojawapo.
Nb.
R
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom