Waraka wa siri wanaswa na Dr. Slaa kutoka CCM, juu ya katiba mpya kuelekea kwa wakuu wa Mikoa,Wilaya


Mkuu OKW BOBAN SUNZU,
Mimi nipo Makao ya CHADEMA. Taarifa zote za vikao vya ndani ya CCM kuanzia vikao vya Sekretarieti, CC, NEC hadi Mkutano Mkuu huwa tunaletewa na baadhi yao wenye nia njema na Taifa letu. Na kuna kipindi walikuwa wanatuletea hadi Muhtasari wa Kikao, ajenda na copy of signed list of attendance. Yani ukiwa CHADEMA Makao Makuu ni kama upo Makao Makuu ya CCM. Siri zao zote tunazipata.

Mkuu Tumbiri

Unatuwekea Mazingira magumu ya jinsi ya kunyofoa taarifa Sasa hivi tutaanza kuogopa kwa kuwa macho yataanza kuwa mengi!
 
mzee kweli ni mnafiki , chekeleeni2 kauli zake na uzushi wake ipo cku nchi hii itakuwa damu.

Pumbaf!

Wewe jinga kwelikweli. Yaani unaona watu wanaopigania HAKI YA WATANZANIA ni wanafiki? Kwanini usiseme CCM ndo wanafiki maana UFISADI wao ndiyo umewafanya Watanzania hali zao na nchi yao KIUCHUMI iwe mbaya kuliko!

Rais wako Kiwete alipoingia madarakani aliahidi Maisha Bora kwa kila Mtz,JE,UNAWEZA KUTUONYESHA HAYO MAISHA BORA KWA KILA MTZ?Najua hayapo.

Dr.Slaa wakti wa kampeni aliwaahidi Watz kuunda Katiba Mpya mara akichukua Madaraka. Pamoja na CDM kutochukua Madaraka bado ililisimamia hilo jambo la KATIBA MPYA bila hata ya kuchukua nchi na sasa linafanyika!!!

Sasa hapa mnafiki kati ya Kiwete na Dr. Slaa ni nani? Acha uzezeta wewe!
 
Yaani CCM bwana ivi wanadhani Tz ni yao milele!
Dr ebu tuwekee haadharani huo waraka tuuprint na kuwapa wananchi!
 
umeshaambiwa source itv kaka.

Mkuu hatujakataa hiyo hoja ila ni muhimu pia kuuweka wazi hapa ili na sisi tujue kilichomo kati ya mistari as we know tunatofautiana sana jinsi tunavyosoma na kupata maana kutoka katika maandishi as compared to kuambiwa kwa kinywa. Ni muhimu huo waraka kama upo uwekwe wazi
 
Huyu mtu anazeeka vibaya, ina maana wakuu wa mikoa ndo watakaotoa maoni kuhusu katiba mpya hadi wapewe maelekezo ya vitu gani CCM wanataka kwenye katiba mpya?
 
Hivi Mnambowa ni Lusinde nini Manaake hoja zake! Damu kwa kuupata ukweli juu ya mikakati ya CCM na katiba? Mbona hamna uhusiano, Itakuwa ni Lusinde huyu!
 
Hapa tunajadili hewa tu hii aina tofauti na ile habari ya TUNTEMEKE ya Mbowe na ukaskazini...watu hata hawajaona huo waraka wanasifia tu sababu katamka Slaa..

Kumbuka Slaa, alishawahi kusema wamekamata Kontena la futi 40 kule Tunduma likiwa na kura.

Leo tena analeta usanii kaona neno ufisadi halina tena mvuto kaamua kuja kwa mtindo wa waraka wa siri.

Hao wakuu wa mikoa ndio wataunda katiba ya Tanzania?

Slaa, wewe endelea kuwadanganya wafuasi wako lakini watu makini huwezi kuwapata.
 
Kutokana na tukio hili la kupatikana kwa huo waraka basi bila shaka tumepata jibu kwa nini WABUNGE WA MAGAMBA WALING'ANG'ANIA SANA WAKUU WA WILAYA WAHUSIKE KATIKA MCHAKATO WA KUKUSANYA MAONI kipindi cha kupitishwa muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba. Kinara wa hili jambo alikuwa mbunge wa Same mashariki Anna Kilango mpaka ilifikia wakati mbunge wa Kawe Mh.Halima Mdee kuuliza wabunge wa MAGAMBA waseme wazi, kuna agenda gani ya SIRI dhidi yao na wakuu wa wilaya mpaka kuwang'ang'ania hivyo? ambapo wakurugenzi wa Halmashauri walitosha kabisa kusimamia zoezi sababu wao ni viongozi wa serikali pia.
 
Dr.Slaa Akiwa kwenye ziara ya Kujenga Chama shy amesema Kamati kuu ya ccm,imetuma waraka maalum kwa wakuu wa wilaya na mikoa yote nchini kuhusu katiba mpya wakielekeza juu ya yale mahitaji,na mambo mbalimbali ambayo wanahitaji kwenye katiba yao,waraka huo unaonyesha mahitaji mbalimabali ya ccm na lazima yasimamiwe kama ilivyoonyeshwa !!!!!!!!Dr.SLaa Amesema kuwa waraka huo unamaslahi binafsi na unaweza kuhatarisha hali ya amani na utulivu hapa nchini.Wana Jf Je ! Tunatengeneza katiba yenye maslahi ya ccm ama ya watanzania wote !!!!!!!!!!!!Sorce:ITV HABARI SAA MBILI USIKU



Mfa maji haachi ........ watz wa 2012 siyo wa 1961 hawadanganyiki.
 
Wakuu wana jf, wana CDM na wote wanaoitakia mema nchi yetu huu ni wakati wa kuungana pamoja kuielimisha jamii ya wa TZ hasa vijijini kuhusu mambo mabaya yafanywayo na serikali ya magamba ili 2015 CDM ichukue hatamu ya nchi hii, hivyo basi hata ccm wakipitisha katiba mbovu sasa, itarekebishwa tu chini ya uongozi tukuka wa CDM. M4C.
 
Dr.Slaa Akiwa kwenye ziara ya Kujenga Chama shy amesema Kamati kuu ya ccm,imetuma waraka maalum kwa wakuu wa wilaya na mikoa yote nchini kuhusu katiba mpya wakielekeza juu ya yale mahitaji,na mambo mbalimbali ambayo wanahitaji kwenye katiba yao,waraka huo unaonyesha mahitaji mbalimabali ya ccm na lazima yasimamiwe kama ilivyoonyeshwa !!!!!!!!

Dr.SLaa Amesema kuwa waraka huo unamaslahi binafsi na unaweza kuhatarisha hali ya amani na utulivu hapa nchini.

Wana Jf Je ! Tunatengeneza katiba yenye maslahi ya ccm ama ya watanzania wote !!!!!!!!!!!!

Sorce:ITV HABARI SAA MBILI USIKU

Haya anayoyazungumza Dr.Slaa yana mashiko.Hatutaki kujua amepata huo Waraka lakini nina amini kuwa kuna Watu ndani ya CCM HAWAFURAHISHWI NA UTENDAJI WA CHAMA HIKI CHA MAFISADI KILICHOPOTEZA MVUTO KWA WATANZANIA.

Kwa watu ambao ni Great Thinkers wanaweza kuona sasa NI KWANINI WABUNGE WA CCM WALING'ANG'ANA SANA BUNGENI KUWA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAWE NDIYO WASIMAMIZI WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA KWENYE MAENEO YAO. Kila mtu mwenye akili timamu anajua kabisa kuwa CCM walijua kuwa hawa ma-DC/RC watasimamia vizuri KUCHAKACHUA MAONI YA WATANZANIA ILI MWISHO WA SIKU KATIBA MPYA IWE IMEBEBA MTAZAMO WA CCM KWA MASLAHI YAO.
Pengine ndiyo maana WAJUMBE WENGI WA TUME YA KATIBA MPYA NI WANA-CCM! Warioba-M/kiti ni CCM,Sallim Ahmed Salim-CCM,Palamagamba Kabudi-CCM,Augustino Ramadhani-CCM,Esther Mkwizu-CCM, Maria Malingumu Kashonda-CCM, Al-Shaymaa Kwegyir-CCM-Mbunge, Mwantumu Jasmine Malale-CCM, Joseph Butiku-CCM na wale wa kutoka Visiwani wengi ni CCM.TUNAWEZA KUSEMA KARIBU 80% NI WANA-CCM



Mimi napenda tu kuwaasa CCM kuwa NAFIKIRI WANATAKA KUCHEZEA AKILI ZA WATANZANIA AMBAO KWA SASA HAWATAKUBALI UJINGA NA UPUUZI HUU. TUNATENGENEZA KATIBA YA NCHI SIYO YA CCM!Sasa kama wanafanya ujanja ujanja wa kutaka Katiba iwe ya CCM,Nchi hii katika miezi hii 18 ITALIPUKA!!!!
 
umeshaambiwa source itv kaka.
Alichoomba mdau ni nakala ya huo waraka,sio chanzo cha habari. Ni kweli inakuwa ngumu kidogo kwa watu makini kuingia kwenye mjadala wenye hoja nzito kama hii pasipo kuuona huo waraka wenyewe. Kama ni kweli, basi tunaomba uwekwe hapa ili tuwe katika nafasi nzuri ya kuuchambua huo waraka.
 
Dr.Slaa Akiwa kwenye ziara ya Kujenga Chama shy amesema Kamati kuu ya ccm,imetuma waraka maalum kwa wakuu wa wilaya na mikoa yote nchini kuhusu katiba mpya wakielekeza juu ya yale mahitaji,na mambo mbalimbali ambayo wanahitaji kwenye katiba yao,waraka huo unaonyesha mahitaji mbalimabali ya ccm na lazima yasimamiwe kama ilivyoonyeshwa !!!!!!!!

Dr.SLaa Amesema kuwa waraka huo unamaslahi binafsi na unaweza kuhatarisha hali ya amani na utulivu hapa nchini.

Wana Jf Je ! Tunatengeneza katiba yenye maslahi ya ccm ama ya watanzania wote !!!!!!!!!!!!

Sorce:ITV HABARI SAA MBILI USIKU

Si Muubandike tu hapa, bado mnawaogopa hao CCM. Tuwachambue mpaka kieleweke. itatusaidia kutoa elimu ya uraia kwa wananchi nao wajue cha kufanya.
 
mzee kweli ni mnafiki , chekeleeni2 kauli zake na uzushi wake ipo cku nchi hii itakuwa damu.[Kabla haijawa damu, nyinyi kwanza ndo mtaanza kuwa damu, hakuna faida yoyote kwa wananchi watano kuwa na uhakika wa kula katikati ya kundi la watu milion 40.
 
Nimeshukuru sana prof baregu hakuapa kwa kutumia biblia wala Quran amehisi hakuna mpango mzuri wa kutengeneza katiba ya wananchi bali ni ya ccm
 
Back
Top Bottom