Waraka wa Profesa Anna Tibaijuka kuhusu Maendeleo ya Mkoa wa Kagera. "Kagera Twafa"

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,156
4,510
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wazalendo wote nchini na Duniani kwa Ujumla

Nimeambatanisha Waraka Kutoka kwa Profesa Anna Tibaijuka kuhusu uduni wa Maendeleo kwa Mkoa wa Kagera

---
KAGERA ,TWAFA

Anaandika Profesa Anna Tibaijuka
20220117_141656.jpg

Kagera. TWAFA. Tumuombe Rais Samia atuangalie kwa jicho la huruma, la mama mzazi.

1. Mwaka 1961 tukipata uhuru Kagera ulikuwa mkoa wa pili kwa maendeleo baada ya Kilimanjaro. Sasa hivi miaka 60 baada ya uhuru ni mkoa wa mwisho Tanzania Bara. Nambari 25.

2. Taarifa rasmi za Benki kuu..(Consolidated Zonal Economic Performance Report) Inaorodhesha pato la taifa kwa kila mkoa kwa kila mwananchi au kichwa (per capita GDP) kwa Tanzania bara.

3. Kwanza ni Dar es Salaam. Shs 4,678,751. Mwisho namba 25 ni Kagera Shs 1,168,661.

4. Kwa asilimia kipato cha mwananchi mkoa wa Kagera ni asilimia 44% tu ya kipato cha Taifa.

5. Na asilimia 25% au robo ya kipato cha wakazi wa Jiji Kuu la Dar es Salaam.

6. Ukilinganisha na Makao makuu Dodoma (Shs 1,759,347) Kagera ina asilimia 66% au theluthi mbili.

7. Hali ni tete. Kaya maskini nyingi hata mlo ni wa kubahatisha katika hali ya kawaida. Ukiingiza ukame inakuwa zahama.

8. Tukubali mkoa slowly but surely umefilisika. Tunahitaji kufanya tathmini ya kina kuona tunajikwamua vipi. Nini kazi ya Serikali? Nini jukumu la WanaKagera. Na kipi Mhe Rais wetu Mama Samia atuwekee nguvu?. Mambo yalipofikia tunahitaji mbinu zote na mikakati mipya kubadilisha hali hii isiyopendeza.

9. Lazima kumwangalia adui umaskini machoni na kupambana naye.
Tukikata tamaa au kulaumu hatutafanikiwa.

10. Kinachohitajika ni utambuzi na uelewa wa pamoja wa sababu za kufilisika kiasi hiki ili kurekebisha mambo. TUNAWEZA. KUJIKWAA SI KUANGUKA. Ila lazima tujipange. Kila mtu kwa nafasi yake.

11. Mwalimu Baba wa Taifa alisema. "It can be done. Play your part".

12. Ninawapongeza waheshimiwa Rais Samia na Waziri Mkuu Majaliwa kwa kupanga safu ya uongozi upya. Tumeshuhudia maboresho makubwa. Tunawapongeza Mawaziri na Makatibu Wakuu na Manaibu wote walioaminiwa na kupewa majukumu ya kuongoza sekta mbali mbali. Ninaomba nao waangalie hii hali tete ya Mkoa. Twafaaa... Tunahitaji msaada.

Na wenzetu wa Kigoma nambari 24.( Shs 1,479,389); Singida nambari 23. (Shs 1,622,891) sina budi kuwasemea pia. Kwa ujumla wetu: TWAFAAA.

KAZI IENDELEE katika mwaka huu wa OTAGWISA MUKONO.

Mama T

Chanzo: Bukoba Wadau
 
Tibaijuka Yeye amekua Waziri katika Serikali, mbona hatujawahi kusikia anawasemea wana Kagera, amekuwa mbunge miaka 10, hatukuwai kuona hata akisemea zao kuu la biashara kahawa, wakati Nchi jirani Uganda kahawa ni bei ni zaidi ya mala 3, mpaka kagera tunatamani kuuza Uganda. Tibaijuka alichokifanya alipopata ubunge na uwaziri ni kujimilikisha aridhi tu,akuna alichosaidia chochote, Sasahivi eti anapiga kelele.
 
Mkoa wa Kagera unapaswa kuwa moja ya mikoa tajiri sana kwani upo katika eneo nyeti (strategic position) kwa kupakana na Uganda na Rwanda. Kinachotakiwa ni kufungua mipaka na kufanya biashara bila vikwazo.

Kwa sasa mkoa umefungwa kwa kisingizio cha usalama na wakimbizi. Viongozi na hasa wana Kagera wanapaswa kupigania uhuru zaidi wa kufanya biashara kwa kuuza na kununua toka kwa majirani.
 
Kilichorudisha nyuma maendeleo ya Kagera ni usafiri. Wahaya walipokuwa wakifika Dar au Mwanza, usafiri wa kurudi kwao unakuwa ni mgumu sana ndipo wengi wao wakahamishia makao yao Dar na Mwanza. Serikali ya Magufuli ilijitahidi kujenga tena infrasturucture ya kwenda Bukoba kwa kufufua meli, usafiri wa ndege wa uhakikia, na jitihada za kuimarisha barabara kati ya Mwanza na Bukoba kupitia Busisi na hakuwahi kushukuru serikali hiyo.

Leo hii mama huyu kulilialia huku ni unafiki tu kama alikuwa hajui hili. Yeye ana hela ya mboga nyingi tu hapo Dar.
 
Nyie wana kagera wengi wasomi walikimbilia nchi za nje mmojawapo ukiwa wewe mama, mkaisahau nchi yenu.

Magonjwa makubwa makubwa yalianzia huko kwenu yakaimaliza nguvu kazi pia.

Waliopata visenti kama wewe na wengine inaonesha mlizikimbiza nje.

Mwendazake akaikuta kagera imetepeta akasema anajenga ili aishi hapo, ndo hivyo tena.

Mkubali tu mkoa uingie chato.
 
Mbona yeye hata shule zake amewekeza Mwanza, badala ya Bukoba.

Huyu mama amepagawa baada ya kuona bibi kizee mwenzake Muramura amepewa ulaji wakati yeye akisahaulika ingawa naye alikuwa huko UN-HABITAT.

Huo ndio ukweli,hakuna lingine wala nini?

Yeye si anakula za Museveni kidogo kidogo, shida yake nini?

Bado za mboga kutoka kwa Rugemalira!

Bado malori semi trailers zinapishana barabarani zikisomba cement,kwa mgongo wa Texas!

Kweli mama ana tamaa ya FISI.
 
Tibaijuka Yeye amekua Waziri katika Serikali, mbona hatujawai kusikia anawasemea wana kagera, amekuwa mbunge miaka 10, hatukuwai kuona hata akisemea zao kuu la biashara kahawa, wakati Nchi jirani Uganda kahawa ni bei ni zaidi ya mala 3, mpaka kagera tunatamani kuuza Uganda.Tibaijuka alichokifanya alipopata ubunge na uwaziri ni kujimilikisha aridhi tu,akuna alichosaidia chochote, Sasahivi eti anapiga kelele.
Unamwonea bure, umesahau msema wa kupsnua na kupanuliwa?
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom