Waraka wa pongezi kwa Makaburu wa Afrika ya Kusini

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Enyi Makaburu watukufu, nichukue fursa hii kuwapongeza kwa kukamata ndege inayosemekana ni ya Tanzania. Nasema inayosemekana ya Tanzania kwa kuwa sisi raia wa nchi hii wala kupitia wawakilishi wetu Bungeni hatujui gharama za ununuzi wa Ndege hiyo wala mkataba ulio tumika. Ni genge la Matapeli na majizi mtu na mpwa wake walikutana chumbani na kufanya maamuzi yao kisha wakatusingizia sie wana Watanganyika eti tumeamua kununua Ndege kwa Cash.

Mimi siwapongezi kwa kukamata Ndege iwe ya Serikali au mtu binafsi bali nawapongeza kwa Kuchukua hatua inayo jali misingi ya Utu, haki na ubinadamu dhidi ya raia wema.

Kuna kiongozi mmoja amesikika akisema eti kesi ya ndege itakapo isha serikali itawafungulia mashitaka ya uhujumu uchumi watu wote walio husika kufanya ndege yao ikamatwe. Hii serikali ndio imekuwa ikihubiria raia UTII wa SHERIA bila SHURUTI. Hivi leo mtu kudai haki yake ninyi mnakimbilia kushitaki watu ili muwafungulie Kesi za kuhujumu uchumi zisizo dhaminika waozee gerezani.

Makaburu mnaweza kuona sisi huku Tanganyika tuna viongozi wa aina gani na jinsi tunavyo teseka kuliko ninyi wakati ule wa ubaguzi wa rangi. Ni watu wanao tumia nguvu kuliko Akili.Wanahubiri Amani huku wao wanawamiminia Marisasi raia wema majumbani kwao kisa umesema ukweli. Eti hawa ndio watupeleke ktk uchumi wa kati na viwanda?

Pia hao watu waliojifanya kuandamana kuja Ubalozini Afrika ya kusini sio raia wema wa Taifa hili tunaomba muwapuuze.

Hao ni kikundi cha UHARIFU huku kwetu tunawaita MAZOMBI. Kundi hilo ndio hutumiwa Kupoteza watu, kuteka, kupiga na kuuwa.Sisi Watanganyi tunapenda HAKI, UHURU, AMANI na DEMOKRASIA. Tuliwasaidia kupigania uhuru wenu kwa kuwa tulijali Misingi ya Utu wa Binadamu wala hatukuhitaji mkipata uhuru wenu mje kutulipa fadhira sisi mtakapo ona serikali ya Tanganyika inakandamiza haki za Binadamu ninyi Mtuunge mkono hapana.

Mwisho nasikia kuna Wanasheria wamekuja huko Afrika kusini wakitokea Tanganyika. Kama mlivyo shikilia Ndege hata hao pia washikilieni tuu wasirudi huku itapendeza. Hao ndio wanao tubambikia sisi raia wema Kesi za Bandia ili tuteswe magerezani. Kuna raia wanatekwa wanalawitiwa na kuuawa.

Kwa hali ya sasa raia yeyote mwema ana imani zaidi ya kutendewa Haki na Makaburu au Mabeberu kuliko vibwengu hawa makatili ya awamu hii. Mungu awabariki sana Makaburu kwa kuikumbusha Serikali hii katili kuwa inayo wajibu wa kutenda haki japo ni sisi tulio wapigania ninyi mpate HAKI zenu.
Wasalaam.
Cc.Jacobe Zouma

Cc.Thabo Mbeki
 
Ahsante KWA kutuwakilisha.

Shida hatujui kitu kinaitwa ubinafsi, ukidadavua utagundua kiasili wanadamu wote n wabunafsi sasa ili uoneshe wewe n MTU mzima lazma ushinde ubinafsi tofauti ba mtoto,
Ndege imenunuliwa na mtu bila kushirikisha watu waandamiz ndan ya serikali sembuse watanzania utasema hicho n cha wote!

Eti baba kajenga nyumba bilaa Mke kujua wala watoto anasema surprise hivi mtamwelewa?

Jiwe acha ubinafsi n hizo za nchi nasi tunazitaka sio kila siku mpwa anatoa tu mnatumia hovyohovyo tu.
 
Back
Top Bottom