Waraka wa Pili wa Mbunge kwa Wananchi wa Jimbo la Ubungo na watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa Pili wa Mbunge kwa Wananchi wa Jimbo la Ubungo na watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Dec 26, 2011.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Katika waraka wangu wa kwanza kwenu niliwapa mrejesho kuhusu uwakilishi wa Mbunge katika mkutano wa pili wa Bunge. Nawaandikia waraka huu "Uhuru na Mabadiliko" katika mwaka 2011 wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo sasa inaitwa Tanzania bara.

  Lengo la waraka huu wa pili (Tazama Kiambatanisho) ni kuungana nanyi katika mwaka huu kutafakari kila mmoja wetu kuhusu taifa letu lilipotoka, lilipo na tunapotaka liende katika kipindi cha miaka 50 toka Uhuru na kutumia fursa hiyo pia kutafakari kuhusu jimbo letu katika kipindi cha mwaka mmoja toka uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2012.

  Waraka huu wote, isipokuwa aya ya kwanza na aya hii ya tatu, niliuandika tarehe 9 Disemba 2011; hata hivyo sikuutoa siku hiyo kutokana na ‘macho na masikio' ya wengi kuelekezwa katika ‘sherehe' za siku hiyo pamoja na matarajio kuhusu hotuba ya Mkuu wa Nchi kugusa masuala mapana kuhusu mwelekeo wa taifa. Nimeona niutoe waraka huu katika kipindi cha kuelekea mwisho wa mwaka, na ni wakati muafaka wa kutafakari zaidi baada ya ‘sherehe' kwa kuwa mpaka sasa Rais Jakaya Kikwete hajatoa hotuba nyingine ndefu kama alivyoahidi tarehe 9 Disemba na pia taifa linamaliza majonzi yaliyotokana na maafuriko yaliyoleta maafa katika mkoa wa Dar es salaam.

  Kwa hali hii ni wakati muafaka wa kurudi nyuma na kutafakari kiwango cha fedha tulichotumia kwenye ‘sherehe' za uhuru; huku taifa likiwa halina hata vifaa vya msingi vya uokoaji wakati wa maafa. Ni wakati muafaka wa kutafakari, ‘mafanikio' ya miaka 50 ya uhuru, tukiwa na matatizo ya mipango miji na kutetereka kwa misingi ya utawala wa sheria katika mkoa wa Dar es Salaam ambao ulitangazwa kuwa jiji mwaka huo huo wa uhuru.

  Nimeutoa waraka huu leo katika kata ya Mabibo jirani na Loyola eneo ambalo linabeba kumbukumbu ya kihistoria kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa Jimbo la Ubungo. Hivyo waraka huu umedokeza baadhi ya wajibu wa msingi ambao mbunge ameutekeleza katika Jimbo la Ubungo katika kipindi cha mwaka mmoja.

  Naelewa kwamba wapo wengine ambao walitumia mwaka huu wa 2011 wa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kufanya ‘sherehe' ama kufanya ‘maonyesho ya kijeshi', lakini binafsi nimeona pamoja na yote niwaandikie tutumie kutafakari. Ni wakati wa kila mmoja wetu kujiuliza ameifanyia nini nchi na pia kujiuliza nchi na wananchi wenzake wamemfanyia nini katika miaka 50 ya uhuru wetu. Tafakari hii haiwezi kuwa ya siku moja ya tarehe 9 Disemba bali ni mchakato endelevu wa kujitambua na kuchukua hatua. Tuna kila sababu ya kukumbuka na kuadhimisha siku ya uhuru, lakini hatuna sababu nyingi za kusherehekea tena kwa gharama kubwa tukilinganisha baina ya umri, rasilimali na mafanikio tuliyoyapata.

  Tunaelezwa kwamba Tanganyika ilipata uhuru bila kupigana vita hivyo maonyesho ya kijeshi ni ishara tu ya kujipanga kwetu katika kulinda uhuru wa mipaka yetu; lakini ilipaswa sikukuu ya leo iwe ni ya kuonyesha matunda ya miaka 50 ya uhuru.
  Mwaka 1958 wakati Mwalimu Julius Nyerere akihutubia Umoja wa Mataifa (UN) kutaka Uhuru wa Tanganyika dhidi ya mkoloni alieleza kwamba tunapodai uhuru kutoka kwa Waingereza sio kwamba tunataka ili watupe tu utawala, bali ni kwa sababu wameshindwa kuondoa umaskini, wameshindwa kuelimisha Watanganyika na pia wameshindwa kutoa huduma za afya.

  Tarehe 9 Disemba 1961 kupitia hotuba zake mbili kwa nyakati na matukio tofauti Nyerere akarudia kuwatangaza maadui watatu wa taifa- umaskini, ujinga na maradhi na akataka kila mmoja awapige vita. Siku hiyo hiyo, Nyerere akatangaza kuwa adui mkubwa ni umaskini! Miaka michache baada ya uhuru akarejea kumtaja adui mwingine mkubwa zaidi ambaye aliwahi kumweleza hata wakati wa kudai uhuru; naye ni ufisadi. Kwa hiyo vita yetu kwa sasa ni ya maadui wanne; ufisadi, umaskini, ujinga na maradhi. Katika kutathmini tulipotoka, tulipo na kupanga tunapotaka kwenda ni muhimu tukawatazama maadui hawa miongoni mwetu wananchi na katika nchi yetu kwa ujumla.

  Nawashukuru tena kwa kunipa heshima ya kunituma kuwawakilisha na kuwatumikia kwa kadiri nilivyowaomba kupitia uchaguzi ili kuunganisha nguvu za pamoja katika masuala ya kitaifa bungeni lakini pia tukiweka mkazo katika utekelezaji wa ahadi jimboni kwa kuweka kipaumbele kwenye; Akili, Ajira, Miundombinu, Maji, Uwajibikaji, Usalama, Ardhi na Afya (AMUA).

  Kimsingi kazi tatu kuu za mbunge ambazo zinatokana na mamlaka ya bunge kwa mujibu wa ibara ya 63 ya katiba ni; Mosi kuwakilisha (representation) wananchi, pili ni kutunga sheria (legislative) na tatu ni kuisimamia serikali (oversight) kuweka mazingira bora ya maendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

  Kama sehemu ya uwakilishi na usimamizi mbunge ana wajibu pia wa kuunganisha nguvu ya umma jimboni kuhamasisha maendeleo kupitia mfuko wa maendeleo ya jimbo na wadau wengine.

  Mwishoni mwa mwaka tutatoa Jimboni Ubungo taarifa ya kina ya utekelezaji ya kata kwa kata lakini katika waraka huu nitaeleza baadhi katika muktadha wa kutafakari mabadiliko ya nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii miaka 50 baada ya Uhuru wa Tanganyika.

  Waraka huu ni kwa ajili ya wote wenye kuamini kwamba uhuru wa kweli, si uhuru wa bendera bali ni uhuru dhidi ya umasikini, ujinga, maradhi na ufisadi. Uhuru wa kweli, ni uhuru wenye kuleta maendeleo kisiasa, kijamii na kiuchumi. Uhuru huu ni wenye mabadiliko ya kweli, yenye kuhimili misukosuko ya ukoloni mamboleo; na kujenga taifa lenye kutumia vizuri rasilimali katika kutoa fursa kwa raia wake.

  Ili uhuru wetu uweze kuwa wenye matokeo kwenye maisha yetu na ya taifa letu tunahitaji kuungana kufanya mabadiliko ya kweli. Changamoto kubwa ambayo nimeiona ni kwamba kuna udhaifu katika mifumo yetu ya kiserikali kwenye ngazi mbalimbali hali ambayo inakwaza hatua za haraka za kuleta mabadiliko.

  Kwa pamoja tunapaswa kuendelea kulitoa taifa letu katika kufilisika kimaadili na kiitikadi na kukubaliana tunu za kitaifa zenye kuwezesha misingi ya uwajibikaji. Uhuru wa kweli wa kisiasa utakuja kwa kuwa na uongozi wenye maono (vision) na maadili (values) na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha kuanzia sasa na kuendelea kutuwezesha kunufaika na rasilimali zetu: iwe ni vipaji vyetu, kodi zetu au maliasili za nchi yetu.

  Binafsi, jambo kubwa ambalo nimelifanya katika kipindi cha mwaka mmoja ni kutimiza majukumu ya kibunge ya uwakilishi, usimamizi na kutunga sheria kwa kuwa na utaratibu wa kufanya mikutano na wananchi, kuwa na ofisi ya mbunge inayohudumia umma na kuwasilisha masuala husika kwa kwa mamlaka mbalimbali bungeni, maofisini, manispaa na kwa njia nyingine mbalimbali. Ni dhamira yangu kuendeleza uwajibikaji tunapokwenda ili kuunganisha nguvu ya umma kila mmoja aweze kutimiza wajibu kwa nafasi yake.

  Nihitimishe kwa maneno ya Nyerere kwa taifa siku ya uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Disemba 1961 akiwaeleza wananchi kuhusu utendaji kazi wa baraza lake dogo la mawaziri 11 tu: "..mimi na wenzangu ni watumishi wenu ninyi mnaonisikiliza. Tunajua kuwa mnatuamini, nanyi tunawaamini. Na ni ninyi mnaotupa nguvu zetu tunazozihitaji kwa kazi kubwa iliyo mbele yetu…Na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu tutajitahidi kuwatumikieni bila kujitafutia faida zetu wenyewe au fahari ya cheo". Uhuru na Kazi, Uhuru na Mabadiliko.

  Nawatakia heri ya mwaka mpya wenye upendo, furaha na mafanikio tukiweka mstari wa mbele ukweli, uadilifu, na uwajibikaji katika maisha yetu.

  Wenu katika utumishi wa umma,

  John Mnyika (Mb)
  Jimbo la Ubungo
  26/12/2011
   

  Attached Files:

 2. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hongera mbunge. Mungu na akutie nguvu na hekima ili ufanikishe malengo yako kwa watu wa ubungo.
   
 3. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 488
  Trophy Points: 180
  Na Tanzania kwa ujumla.
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nashukuru Ndg Mnyika kwa kuwathamini watu waliokuthamini na kukuchagua.
   
 5. k

  king11 JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KAFULILA SI MBUNGE , Nawewe nyika , slaa , mboe ,pengo , shivji, malasusa na zitto kuna muswada umefika kwa rais wa kuwavua uraia na kuwafukuza nchi. rais akisaini tu mjue mmeisha na mtapelekwa kuwa wakimbizi
   
 6. S

  Stany JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Bro mnyika nakushukuru sana,much respect to you! You are a real responsible leader!
   
 7. b

  busar JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Nyaraka sawa, but maneno matupu hayavunji mfupa
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  hongera kwa waraka mzuri sana
   
 9. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  I am once again inspired, motivated and feel appreciated by someone special. Thank you a lot. Sasa ningetegemea ufafanuzi kwa uliyosema hasa kwenye yale uliyokwishafanya kwa mwaka huu mmoja kata kwa kata. Tunajitofautishaje na wabunge wa magamba kiutendaji pamoja na ugumu wa mifumo ya kiutekelezaji ya serikali? Nini matarajio yako kwetu sisi wananchi wa jimbo lako? Ni asilimia ngapi ya uliyoahidi umefshafanya? Nafahamu JK alituahidi mengi awamu yake ya kwanza na ameshindwa kutekeleza na nadhani hata mengine hakumbuki kama aliahidi....wewe je, uliahidi mangapi na utekelezaji wake ukoje? Happy New Year shujaa wa vijana Tanzania
   
 10. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,672
  Likes Received: 2,207
  Trophy Points: 280
  Kaza but. Ndoo Kwanzaa asubuh! But nyota njema huonekana tangu morng! Big up man!
   
 11. j

  jigoku JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mh Mnyika nashukuru kwa waraka,na nadhani kama utakuwa una system nzuri ya kuweka records huenda kwenye activities completed utakuwa na cha kuzungumza au kuandika kama kweli huja ainisha kwenye waraka uliouweka kama attachment,binafsi huo sijausoma nitasoma kesho ila nimesoma tu ile summary.
  Ushauri kwa wabunge wengine wa chadema wafanye kitu kama hiki,kama unaweza kumfikishia salamu hizi rafiki yangu Mh Higness kule Mwanza Ilemela,Na kwa wabunge wengine wa Chadema.
  Long live Mnyika,keep it up,tuko pamoja usichoke kupata mawazo yetu pia.
   
 12. k

  kijukuu kindo Member

  #12
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Mnyika big up kwa sana. Bado tunaomba ufuatilie suala la kibosile wa dawasco kujiunganishia maji kata ya Mbezi Lois mtaa wa Makabe baada ya kufanikiwa kuuzima mradi wa maji uliokuwa unatekelezwa na wachina, na kwa sasa amekua suplier mkubwa wa maji eneo hili kwa bei ya tsh 200 kwa ndoo.

  Anawezapia kusambaza maji usiku na kujaza matenki na visima majumbani kwa garama kubwa kwa kuunganisha mipira/mabomba marefu inayosemekana ameyafisadi hukohuko dawasco. Plse Mnyika do something, maana jitihada za kuwaona viongozi wengne wa eneo akiwepo diwani zimegonga mwamba. tunashindwa kujua labda nao wamebloo kwa huyo jamaa "jimama" la dawasco.

  Huduma ya Maji kwa wapiga kura wako ni miongoni mwa ahadi na vipaumbele vyako. Fika ujionee misururu mireeeefu ya raia na ndoo za maji. Daah, safari mbado ndefu.
   
 13. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #13
  Dec 27, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  This seem to be a good start of creative leader.
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Dec 27, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  so inspiring,Hongera sana kamanda ......
   
 15. m

  majogajo JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hv haiwezekani mbunge kutumikia majimbo mawili? naomba mnyika awe mbunge wa jimbo langu..........au nhamie ubungo? ila naogopa mafuriko........big up mnyika
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  He was supposed to be the second after ........................................... and the first after ..........................................
  CHADEMA imejaa majembe ya kufa mtu!
   
 17. BORNCV

  BORNCV JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa majukumu yako!
  Nakuombe Mungu akupe hekima na maarifa ya kulitumikia taifa na watu wake.
  Mungu ibariki TZ, Mungu ibariki CDM
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nafahamu uzito wa shughuli zako ni Ubungo kwanza. Ubunge ni zaidi ya Ubungo. Ni nini msimamo wako juu ya haya:
  -Posho. Kokote ziliko. Bado unazichukua?
  -Mikopo. Tuichukue sote kwenye mabenki au ninyi mpewe mingine kwa Ubunge wenu?
  -Ruzuku. Umasikini wote huu wa NCHI yetu vyama vya SIASA vinachotewa mapesa haya kwa wingi namna hii?
  -Udini. Huu unainyemelea NCHI yetu taratibu lakini kwa uhakika.
  -Bunge. Bunge letu sasa ni kubwa sana. Dar peke yake ina majimbo 7 ya uchaguzi! Ya nini yote haya. Kudai maji toka DAWASCO?
  -VITI MAALUM vya Ubunge. Hizi gharama zinazoambatana na viti hivi na uwingi wa viti vyenyewe na jinsi wanavyopatikana unalionaje?
  -Ikulu mlifuata nini hasa baada ya muswada ule kupita Bungeni? Mlitarajia Rais afanye nini hasa.
  etc.,etc.
   
 19. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Duh! Aise huu Waraka mtamu sana!
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  John Mnyika ni kichwa namkubali ni mmoja wa wabunge vijana wanaojua Tanzania/Wananchi wanataraji nini toka kwake.
   
Loading...