Waraka wa onyo kwa waganga wa Jadi nchini

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Siku za hivi karibuni kumekuwa na matamko ya watu wanao jiita waganga wa jadi wakitishia watu kutoshiriki katika michakato mbali mbali ya uchaguzi hapa nchini.

Kwa bahati mbaya mamlaka zinazohusika na usalama wa raia zimekaa kimya richa ya matamko hayo yanayo hatarisha usalama na Amani kutolewa hadharani na watu hao.

Waganga wa jadi huko Iringa walikuja na Azimio kuwa mtu yeyote atakaye mpinga Magufuli watamshugulilia kimazingara na kumpoteza.

Hivi karibuni pia Waganga wa jadi huko Kahama walikutana ktk ukumbi wa bwalo la Polisi na kutoa matamko kuwa mpinzani yeyote atakaye jitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa watamshugulikia.

Kwa jinsi hali inavyo kwenda naona sasa Wachawi mnataka kutwaa Madaraka ya uongozi kwa Nguvu. Na kwakuwa hamja kemewa, mnaweza kutoa maagizo mengine mkazuia watu Kuoa, kucheka, kwenda makazini, kufanya ibada na mengine mengi maana mmeanza kunogewa kutoa matamko yenu.

Sisi wapenda Amani tunawaonya Ninyi mnao jiita Waganga wa Jadi mnao tisha raia wasishiriki mambo ambayo ni haki yao ya kikatiba. Tunawambia mkome kabisa kutoa matamko yenu ya Kijinga kwa raia wa nchi hii ya Tanganyika. Hamna nafasi hiyo na kamwe hamta pewa nafasi ya kuendesha taifa hili kichawi.

Tunawajua ninyi nyote mnako ishi, familia zenu, ndugu na jamaa zenu pia na Mali zenu zilipo. Tunao uwezo wa kuwashugulikia ninyi nyote iwe mchana au usiku ili kudumisha Amani mnayo taka kuichokonoa.

Hivi kweli sisi raia wema tuwaachie ninyi Wachawi mtuamlie hatma ya nchi hii? Mtuchagulie nani awe kiongozi na nani asiwe kiongozi! "If you think you have a such freedom of speaking, but not to that extent"

Nazani wachawi mbakie na Kazi yenu ya Kuroga, hii ya Siasa hamuiwezi tuachieni raia wenyewe. Na kamwe hatutawaachia ninyi Mashetani kazi ya kutuchagulia sisi watu wa Mungu viongozi.

Maana tunajua ninyi mashetani hushirikiana na Mashetani wenzenu. Na kiongozi wenu mkuu ni IBIRISI joka lile la Zamani. Kazi yenu ni uasi, uovu umwagaji Damu na kuvuruga Amani. Kamwe hatuta ruhusu Mashetani kutupangia nini cha kufanya.
Wasalaam.
Cc. Meco

Cc.Wapenda Amani.
 
Enzi za nabii Mussa huko Misri nyakati za ufalme wa Farao, wachawi kama hawa walikusanyana makundi kwa makundi, lkn hawakuweza kukabiliana na Mkono wa Mungu kupitia kwa nabii huyu. Ukubwa wa pua si wingi wa kamasi, GOD's time is the best, kusudio la Mungu halipindishwi kwa kuwa hekima na njia zake si za kibinadamu.
 
Ondoa hofu, maneno ya chura hayawezi kumzuia tembo kunywa maji...

Wameagizwa kufanya wanachofanya, ila hakuna lolote...



Cc; mahondaw
 
Hao hao waganga wangemchimba beat Jpm wakisema kuwa ole wake apitilize muhula wa utawala kama ilivyo kwenye katiba kesho yake baada ya tamko kungetokea msako mkali wa hao waganga wa kienyeji.
 
Kwa jinsi hali inavyo kwenda naona sasa Wachawi mnataka kutwaa Madaraka ya uongozi kwa Nguvu. Na kwakuwa hamja kemewa, mnaweza kutoa maagizo mengine mkazuia watu Kuoa, kucheka, kwenda makazini, kufanya ibada na mengine mengi maana mmeanza kunogewa kutoa matamko yenu.
 
Na bado, jiwe noma, linapogonga lazima paonenekane. Safari hii hadi freemason watajitokoza kulitetea jiwe.

Uchumi wa kati huo ndugu.
 
Back
Top Bottom