Waraka wa Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Ndg Absalom Kibanda kwa Rais Jakaya Kikwete

Katika nchi zenye demokrasia ya ukweli serikali haina mamlaka ya kufungia magazeti au chombo chochote kile cha habari.

Hata kama yanatangaza nje ya maadili? kama ngono au kuhamasisha uzinzi, chuki (vs Upendo), kuhamasisha ukeketaji, ...?????? yaachwe tu sababu ya demokrasia au ????
 
Naona malalamiko tu kibao, sijapata point kabisa. Naona kama ana bifu na Waziri, sia angeenda tu mahakamani akamshtaki badala ya blaa blaa nyingi kiasi hiki.

utapataje point ikiwa umechomwa?
 
Hata kama yanatangaza nje ya maadili? kama ngono au kuhamasisha uzinzi, chuki (vs Upendo), kuhamasisha ukeketaji, ...?????? yaachwe tu sababu ya demokrasia au ????
Idea hapa si kuacha tu, bali ni kumshitaki mtu binafsi ambaye ameandika habari zisizo na ukweli. Kwa mfano mtu binafsi amepeleka makala yake kwenye gazeti, makala hii imeonekana kubeba sura za uchochezi, hivi unahitaji kulifungia gazeti zima? Si unamshitaki tu mhariri na huyo mwandishi? Je katika hizo adhabu, hakuna adhabu ya faini hadi, kila adhabu iwe ni kufungia tu?
 
"Kwa waraka huu mheshimiwa Rais, wakati tukikuahidi kwa dhati kabisa wewe binafsi na Watanzania wenzetu kwamba, tutaendelea na kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya uandishi wa habari, sambamba na kuheshimu sheria zilizopo, tunapenda kuliweka hili bayana kwamba, tutakuwa wa mwisho kuwatii viongozi dhalimu, madikteta, waliokosa utu na ambao kwao hila ndiyo msingi mama wa kupotosha na kupindisha mambo kwa sababu tu ya kulinda maslahi na malengo yao binafsi au yale ya makundi yenye hila"....Hapa Kibanda umenena.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza kabisa napenda kuamua kwa hiyari kujitoa jamii forums,naona vitu vingi vinaandikwa humu si vi elewi,nimejaribu kwa mwaka mzima sijapata mwelekeo,pili kuna kamati ilianzishwa ambayo ilikuwa chini ya waandishi wa habari kwa ajili ya kifo cha Mwangosi mimi sikuweza kuelewa ilikuwa na jambo gani,inawezekana labda ni mimi ni mwenye mapungufu ila nimeona ni ngumu kuwa amini waandishi wa habari-Kwaheri ya kuonana
 
Yaani haueleweki, umeandikwa kwa hasira ya watu fulani ili wafukuzwe kazi.

Uandishi mbovu, kujaza paragraph tu!

Hv nani atasoma waraka mrefu kama bajeti ya wizara fulani hadi unasahau yalioandikwa mwanzo?

Msomi anaandika mawazo makuu kwa paragraph chache na anaeleweka!

NO POINT AT ALL ACHA HABARI ZA UCHOCHEZI!

Nafikiri haya yanaweza kua majibu ya Mh.Rais anayoweza kutoa!

​Tikiti maji hiloooo!!
 
Nafikiri kaka yangu Kibanda ungemuomba Mh Rais awatume mawaziri wapeleke muswada bungeni wa kurekebisha sheria ya vyombo vya habari, Waziri sio kikwazo kabisa maana aliyefungia ni yeye kwa mamlaka aliyopewa na Sheria mbovu kabisa, Waziri hana tatizo na kwangu mimi ningesema Mama Amefanya vizuri sana kuliko hata watangulizi wake, mtu aliyekuwa kikwazo pale ni katibu mkuu aliyeondoka (Kamuh**)
 
Yaani haueleweki, umeandikwa kwa hasira ya watu fulani ili wafukuzwe kazi.

Uandishi mbovu, kujaza paragraph tu!

Hv nani atasoma waraka mrefu kama bajeti ya wizara fulani hadi unasahau yalioandikwa mwanzo?

Msomi anaandika mawazo makuu kwa paragraph chache na anaeleweka!

NO POINT AT ALL ACHA HABARI ZA UCHOCHEZI!

Nafikiri haya yanaweza kua majibu ya Mh.Rais anayoweza kutoa!



Join Date : 16th November 2013

siyo kosa lako naona una mwezi mmoja tu jf ndo maana hata comment yako iko weak sana rais hawezi kuwa na mawazo dhaifu na potofu kama yako. Anyway ukikomaa ndani ya jf comments zako zitaleta maana.
 
Absolum Kibanda-ACHA UNAFIKI ,WEWE NI mjasiliamali wa HABARI NA SII mwanahabari wa kustahili sifa NA VYEO ulivyonavyo,labda CHA kukusaidia,ukipata MDA mzuri NJE ya stress ZAKO,kasome MAANDISHI YAKO MIAKA ILE ya 2006-2009,KAYASOME UJIONE ULIPOPOTELEA,KASOME NAMNA ULIVYOKUWA UKIMCHAMBUA DR.NCHIMBI NA SAGA LA AMINA CHIFUPA,KASOME ULIVYOKUWA UKIWAANDIKA WANAMTANDAO BAADA YA KUINGIA IKULU,KIBANDA KAJISOME KWANZA BASI NDO UJE NA HUU UNAFIKI WAKO,UMEKUJA NEW HABARI SABABU YA NJAA ZAKO NA WATU UNAOWAANDALIA HOTUBA,WEWE NI MWANAHABARI WA MTU,UNAMILIKIWA,UNA BEI,HUNA HADHI YA KUANDIKA WARAKA KWA RAIS KWA NIABA YA UMMA,KAZI HIYO WAACHIE AKINA JENERALI ULIMWENGU,MBWAMBO,MAGID MJENGWA,JOHN BWIRE,EZEKIEL KIMWAGA,NA BAADHI YA WACHAMBUZI WA HABARI,NA SII WEWE KANJANJA WA HABARI,WEWE NI MWANDISHI SAWA NA VIDONGE VYA RANGI MBILI,LABDA TUKUULIZE,WARAKA HUU BOSS UNAYEMUANDALIA SPEECH KAUSOMA??-AU KAKUPA MISTARI KIJANA UKAANZA KUTIRIRIKA?? TARATIBU UTAKUKUMBUSHA ULIKOTOKA KATIKA HABARI CHAMBUZI MPAKA HAPO ULIPO KWENYE HABARI GALASA.
 
OngwaluMapesa, unauhakika kwamba huu ni Waraka wa Kibanda? Kwani Kibanda hamjui Kikwete? Kikwete anapenda kushabikia vitu vya blabla mambo serious kama hayo hana habari nayo.

Kwanza Kikwete hata hajui MwanaHalisi lilifungiwa kwasababu gani (Rejea hotuba yake kule Addis, Ethiopia) mambo yaliyoandikwa na TanzaniaDaima ndiyo yalifungia gazeti la MwanaHalisi huwezi kuamini. Viongozi kama Waziri wa habari, waziri wa mambo ya ndani (aliyeondoka), Waziri wa Elimu na Naibu wake, Waziri wa Kitoweo Mathayo, Sophia Simba, Kombani, Wasira, Lukuvi, Muhongo ndiyo wanapendwa na Kikwete.

Viongozi wanaofanyakazi zao vizuri zenye manufaa kwa Taifa hawapendwi na Kikwete wanahujumiwa na aliyewateua maana yeye yuko kipesa zaidi (Rejea Magufuli alipokuwa anatekeleza sheria ya hifadhi ya Barabara alishambuliwa na Kikwete na Pinda kama siyo Waziri. Eti ametengua uteuzi.... nyoo, Kikwete ni MSANII, matatizo yote yanayotukabili yanatokana na Kikwete hatuna Rais tungekuwa naye asingemteua Kinana kuwa Katibu mkuu wa CCM wala Mwigulu kuwa Naibu alijua anataka nini kutoka kwao.

Kama kweli huu waraka ameandika Kibanda ajue wanakuja kumalizia mifupa iliyobaki, Kaa kimya Kibanda umalizie siku zako zilizobaki. Angalia deni la Taifa lilipofikia mpaka sasa utachoka...!! Atabadilisha na kuweka walewale washikaji ambao kwao kuua siyo tatizo kikubwa ni kumfurahisha Boss wao.
 
Back
Top Bottom