Waraka wa Mswahili kwa Waswahili (I) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa Mswahili kwa Waswahili (I)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Felixonfellix, Apr 7, 2011.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa WAAFRIKA wote ukianzia na Tanzania, Nchi nzuri, chachu ya ukombozi wa Bara la Afrika, kimbilio la wakimbizi wa vita, tamanio la wabakaji wa uchumi.
  Nakala hii kwanza iwafikie kwanza watanzania wote kupitia vyombo vya habari, kwaajili ya Bara la Mungu, enyi baadhi ya wanahabari wanafiki, wekeni unafiki wenu pembeni mmjiunge na wenzenu wasio wanafiki kuijuza Dunia Mswahili anaiambia nini Afrika na watu wote.
  “Naapa kwamba sitamdhuru kiumbe wako huyu MSWAHILI kwa ujumbe ninao usoma leo hapa, na hata kama maneno yake yatakuwa shubiri kwangu, nitayatumia kwa manufaa ya nchi yangu na watu wangu nikijaribu kufanya kinyume na kiapo changu dhamira yangu mbaya inidhuru. Mungu nisaidie!”
  Ndugu,
  Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Waziri mkuu, Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mawaziri wote wa kawaida, Mawaziri Vivuli na viongozi wote wa kiimani na kisiasa.
  Heshima yenu popote mlipo!
  Mswahili nawasalimia!
  Mimi ni Vitali Maembe, mwanamuziki, Mswahili, Mwalimu na mtumishi mwenzenu wa waafrika.
  Mnamo tarehe 03/02/2011 nilianza ya kugawa chanjo ya Rushwa, ubinafsi na uvivu kwa kutumia muziki kwa watu wote. Bila kutumwa wala kushinikizwa na mtu wala shirika, wala chama, nilianzia Bagamoyo, mitaani, viwanjani na katika shule njiani kuelekea Dodoma. Ilinichukua siku na wiki kadhaa kufika huko, namna ya kusafiri kutoka kituo mpaka kituo, ruhusa ya kufanya maonesho, vitisho, njaa vilikuwa vikwazo vikubwa.
  Hatimaye jumatano tarehe 16 februari 2011 saa nne kasoro dakika kumi natatu mimi na rafiki zangu wawili tulifika Dodoma kituo kikuu cha mabasi. Lengo likiwa ni lilelile kuiokoa nchi yetu kwa jasho letu, akili yetu yote, moyo wetu wote na uwezo wetu wote kwa kadri tulivyoaminiwa na waswahili wenzetu, kwa kufikisha Waraka wa Chanjo wenye kurasa tano wenye ushauri na unaowaomba mawaziri na wawakilishi wafikirie namna ya kufanya marekebisho kadhaa yatakayoboresha huduma muhimu katika jamii. Ukosefu na uhaba wa huduma na haki unapelekea watanzania wengi kushiriki na kushirikishwa katika Rushwa. Hali ambayo inafanya waswahili tunatukanwa, tunatukana, kutukanishwa na kujitukanishwa, thamani ya utu wetu kutoonekana ndani ya nafsi zetu na nje katika kuishi kwetu, kwa kifupi sisi waathirika wa rushwa tunajiona kama mifugo tu kwenu nyinyi na wakati wowote mkiamua lolote mnatufanyia, tena mmeshafanya mengi kwa manufaa yenu na mifumo yenu bila kujali uwepo wetu”
  Pia lengo lilikuwa ni kuwasilisha ujumbe kwa njia ya muziki, ujumbe ambao niliagizwa na watanzania wa kawaida.
  Pamoja na kufika Dodoma hiyo jumatano ya tarehe 16 februari, hatukwenda moja kwa moja bungeni, tulipumzisha akili zetu, tukasema na njaa zetu, baada ya muafaka tarehe 17 asubuhi tulienda bungeni kuomba ruhusa kumuona Spika wa bunge ili kukabidhi waraka na kopi za albamu ya muziki ya Chanjo. Siku hiyo hatukufanikiwa kupata ruhusa, baada ya usumbufu mkubwa na vitisho getini kutoka kwa askari na wahusika wengine wa mlangoni jioni iliingia na siku ikaisha bila ruhusa. ‘haya ninayoyoyasema naamini mnayajua au mna taarifa nayo’ Hatukukubali kuondoka mpaka tulipopata ruhusa ya kukutana na msaidizi wa Spika Bw. Berege, hatukuweza kumkabidhi barua zetu sitini na nne zinazotakiwa kuwafikia mawaziri wote, wawakilishi wa vyama bungeni, spika na katibu wa bunge kwa kuwa msimamo wetu ulikuwa ni kumfikishia Spika na kumkabidhi ili kuhakikisha ujumbe unawafikia wahusika. Siku iliyofuata yaani tarehe 18 februari 2011, tulifika mapema asubuhi, mara hii tulipata ruhusa ya kuingia katika ofisi ya spika, haikuwa rahisi kuonana naye lakini tuliridhika na ukweli, hivyo tulikutana na Katibu wa spika Bw. Eliufoo na kumkabidhi ujumbe wetu aliupkea saa nne na dakika kumi na sita na akaandika na kuweka sahihi kwenye katatasi yetu nyeupe ya A4 aliyoamua kuikunja katikati kwa mapana baada ya kuandika kwa kalamu yake ya wino wa buluu kuwa amepokea ujumbe wetu.
  Awamu ya kwanza ya Chanjo iliishia BASATA Baraza la Sanaa la Taifa. Watu wasiopungua Elfu Ishirini wamekwishapata Chanjo ya Rushwa, Ubinafsi na Uvivu.
  Pamoja na hayo yote mpaka sasa sijapata matokeo ya ujumbe wangu Dodoma kutoka kwenu walengwa wote yaani wawakilishi wa vyama na Mawaziri wote. Spika na katibu wa bunge pia mmekaa kimya.
  Sasa nawauliza hiyo ni dharau, kiburi au chuki? Na kama ni hasira au chuki mmeniwekea mimi au wananchi wenu?
  Sikilizeni niwaambie,
  Mnaweza kujiuliza kwanini nitumie gharama nyingi ya muda, pumzi na pesa yangu masikini kama mie na kung’ang’ania kuimba nyimbo za namna hii na kuwafikishia watu moja kwa moja, kueleka bungeni. Kwanini natumia pesa ambayo ingebidi niitumie kuwatunza wanangu wadogo nyumbani wanaosubiri msaada wangu, mimi ni mjinga? Mimi siijui raha ama sina haja ya kustarehe? kwanini nisifanye biashara ya muziki nikawa tajiri kama hao wanamuziki wengine mnao wafagilia? Kwanini nisiwapigie kampeni niwe mmoja kati yao wanaoahidiwa viwanja ili wawadanganye masikini waswahili hali wakijua ukweli ni upi? Sina kingine zaidi ya mapenzi kwa nchi yangu na Afrika yangu, tumia akili na umri wako sasa kuelewa mambo mengine.
  Lazima ufahamu kuwa Rushwa ndio asili ya mateso wanayoyapata watu wenu, amua leo, sema neno moja tu na watu watapona. Kwa taarifa yako mkuu, watu wanakuficha mimi nakuambia ukweli, Waswahili wanasema huwezi kuwafanya lolote wala rushwa na wezi wa nchi hii kwa kuwa wewe ni mwenzao mimi siamini hayo lakini waswahili wana misemo yao kama vile ‘Lisemwalo lipo…’ au ‘ngoma ikivuma sana…’ nk.. Wewe waswahili unawajua naomba uyatilie thamani maneno yao.
  Wakuu!
  Nilipoona kuwa kazi yenu ya kuongoza ni ngumu nikaona niwasaidie kurahisisha mambo fulani, lakini mnaniona mpumbavu kabisa, angalieni matusi mnayotukanwa, watu wanailaani siku waliyoenda kupiga kura kuwachagua. Mimi na waswahili wenzangu tumegundua kuwa nyinyi ugumu wa maisha haya ndio raha yenu, mateso ya watu hawa wanyonge ndio matumaini yenu ya maisha bora kwenu, na watoto wenu siku za mbeleni..
  Nasema haya maneno yanayoshabihiana na lawama kwenu kwa kuwa naiona juhudi yenu ya kuwafanya watanzania wasisikie muziki wetu, muziki wa mswahili, muziki unaoeleza maisha halisi kabisa ya muafrika na kutoa ufumbuzi.
  Tazama! Unawaunga mkono watu ambao wanaonekana wazi hata kwa macho ya kitoto kuwa hawana mapenzi ya kweli nasi, unatuuza watu wako kwa ushawishi wa vitu vidoogo kabisa katika maisha, Makaratasi, makaratasi tu ndiyo yanayokufanya utuone bidhaa, unampa shetani damu ya wanao! Unaiunga mkono kauli ya yule punguani mmoja wa Afrika ya kusini miaka 1980! Umesahau kabisa KIAPO chako kwa Mungu mbele ya Muumba na waswahili wote, umewasahau wazee wetu walivyoteseka na kudhalilika katika kuijenga Afrika hii?
  Nakukumbusha!
  Yule punguani wa Afrika ya kusini alivyosema,
  “The black is the raw material for white man. So Brothers and Sisters, let us join hands together to fight against this Black devil. By now every one of us has seen it practically that the Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other. They are good in nothing else but making noise, dancing, marrying many wives and indulding sex. Let us all accept that the Black man is the symbol of poverty, mental inferiority, laziness and emotional incompetence”
  Je, kwa haya mnayotufanyia leo hali mkiwa wasomi na mnajua yote haya mnafikiri uongozi wenu haukubaliani na huyu bwana? Je, mnawezaje kumshawishi mswahili akawaelewa kuwa hamtumii msimamo huu kuwaongoza waswahili?
  Mswahili haitaji majibu ya ahadi bali vitendo na kauli thabiti itakayompa uhuru wa kweli katika ardhi ya babaake.
  Tumewapa nguvu ya kutosha itumieni kutuokoa!
  Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri mkuu, Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano Tanzania, Mawaziri wote halisi na vivuli.
  Najisikia vibaya kukupa ushauri huu lakini inabidi nikupe ingawa ni aibu kwangu na watanzania wote tuliokuweka madarakani, haya mambo ilibidi uwe umeyapitia na kuyafahamu miaka mingi iliyoita na kuyatumia kama ufahamu kukurahisishia nakuiboresha kazi yako ya kuwaongoza watu ambao wameletwa kuishi Afrika ili wasipate taabu, wafurahie maisha katika nchi waliyopewa na Mungu wao.
  Sikiliza Mzee wangu!
  Uliamua kuiongoza afrika na ukapewa ridhaa na waafrika, usikurupuke tu ukaanza kuongoza bila kujua wapi afrika inatokea, achana na hayo mavideo za ulaya na misimamo ya kigeni, acha kujiamini na elimujoho TANZANIA NI MOJA NA HAKUTAKUJA KUWA NA TANZANIA NYINGI ZAIDI YA HII YA WASWAHILI. Tanzania ndio Afrika, Afrika ndio dunia. Kama utafanya watanzania wakuone bora basi wewe utakuwa bora kuliko viongozi wote Duniani kwakuwa watanzania ni waswahili na waswahili wanafikiria mara tatu ya mtu wa kawaida.Tuliza akili mkubwa unisikilize.
  kwa kukusaidia tu ni kwamba ujue kuwa huna uwezo wa kuiongoza hata sehemu ndogo ya waafrika pekeyako, tena bila kujua haya nikwambiayo leo ndiyo kabisaa.
  Niwie radhi mkubwa wangu kama utaona nakukosea kukwambia haya. Sikwambii haya kukushusha cheo chako, la, haya ni mapenzi tu. Nakuomba uupe heshima umri wangu, na kazi yangu kama mwanamuziki, mwalimu na mswahili kwa kusikia mafundisho yangu.
  Kuna kitu kinaitwa Pan-africanism.
  Ndani ya hiyo tafuta kujua kuhusu wanasiasa wake, viongozi, wanamuziki na watu wengine waliohusika na afrika kwa moyo wao wote. Mwanao nakuomba uyashike haya, kama huwezi kuhifadhi kichwani shika kalamu na uandike haya. Wengi wa hawa walifanya mambo mazuri lakini mimi nawewe hatujui nia za moyoni mwao, pia wapo wliofanya mabaya, kwa kuangalia walikoanzia mpaka wanakoishia utajua lipi linalokufaa.
  Nenda ukamsome.
  Nnamdi Azikiwe, Robert Mugabe, Amílcar Cabral, Muammar al-Gaddafi · Marcus Garvey, David Comissiong, Kenneth Kaunda, Samora Machel, Jomo Kenyatta, Patrice Lumumba, Thabo Mbeki, Abdias do Nascimento, Gamal Abdel Nasser, Oliver Tambo, Kwame Nkrumah, Julius Nyerere, John Nyathi Pokela, Haile Selassie, Robert Mangaliso Sobukwe, Ahmed Sékou Touré, Abdulrahman Mohamed Babu, I.T.A. Wallace-Johnson
  Usiache kumsoma.
  Molefi Kete Asante, Steve Biko, Edward Wilmot Blyden, John Henrik Clarke, Cheikh Anta Diop, W. E. B. Du Bois, Frantz Fanon, John G. Jackson, Yosef Ben-Jochannan, Maulana Karenga, Fela Kuti, Bob Marley, Malcolm X, Ibrahim Hussein, Zephania Mothopeng, George Padmore, Motsoko Pheko, Runoko Rashidi, Walter Rodney, Burning Spear, David G. Mailu, Henry Sylvester-Williams, Stokely Carmichael, Omali Yeshitela
  Tuliza akili yako ujue wamefanya nini na wamefanyiwa nini kwaajili ya afrika yao na kwaajili yao binafsi.
  Usije ukawaongoza waafrika bila ufahamu mkubwa kuhusu haya yafuatayo, hapa ndipo kuna malengo, nia, utu na heshima yetu. Kuchanganyana na kuchanganyikana.
  United States of Africa, Afrocentrism, Kwanzaa, Pan-African colours, Pan-African flag, Négritude ,African nationalism, African socialism, African Century · Africanization, Kawaida, Ujamaa, Harambee, Ubuntu, Zikism, Black nationalism.
  Jua na uelewe kuhusu muungano, mabadiliko, umoja wetu na kudumu kwetu kama waafrika.
  African Union, Organization of African Unity, Uhuru Movement, UNIA-ACL · African Unification Front, International African Service Bureau.
  Hayo mambo mengine ni urembo tu, ni njia ya kutafuna rasilimali za waafrika tu. Nakuamini sana na ninaamini kuwa maneno yangu yatawasaidia watanzania na waafrika wenzangu kupitia busara zako, hayatakuwa chanzo cha wewe kunitesa au kugeuka sababu kuniua masikini mie ninayejaribu kuwakoa watanzania na waafrika wenzangu. Najua nimekupa nguvu ya kufanya lolote utakalo lakini naomba usinidhuru kwani wanangu na wapenzi wangu bado wananihidaji.
  Mimi ni wanamuziki nisingependa haya yafikie huku lakini imebidi nitumie njia hii maana nimeimba sana lakini redioni hawapigi, wengi wao wanasema wanahofia utawala wenu, hautafurahia nyimbo za mafunzo, lakini labda ni uoga wao tu, nakuomba uwaruhusu basi wapige nyimbo za Vitali Maembe.
  Mkuu,
  Katika kuongoza yashike hayo yote lakini langu mimi ni moja tu kama si mawili, usiupe nafasi ubinafsi, ubaguzi wa rangi, dini, kabila na jinsia.
  Mwisho,
  Usiache muziki ukadhalilishwa, usiupromoti muziki ambao unaona wazi unawapeleka watu wako pabaya, nchi italaaniwa, Muziki mzuri ni ule unaotoa elimu njema na kuwasaidia watu, ule mwingine usiuue pia uache uwepo tu ili kutofautisha kizuri na kuzuri sana. ‘pasipo ndicho kilichopo ndicho?’
  Mswahili anakutakia uongozi mwema na mafanikio katika mema!
  ‘Mungu ulisha ibariki Tanzania, Mungu ulisha ibariki Afrika! Tunaomba usituondolee Baraka hii!’
  “Hakuna kuogopa, hakuna kuongopa!”
  Vitali Maembe. 2011
   
 2. Pawaga

  Pawaga JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 686
  Trophy Points: 280
  mmmmh!
   
 3. k

  kituro Senior Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nikweli habari ni nzuli lakini naogopa kuisoma kwani nikiisoma sitasoma habari zingine! fupisha basi ili hata wale wanaotumia simu waweze kuisoma!.
  nakutakia kila kheri na kazi njema!
   
 4. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Msingi wa post yako ili usichoshe wengine ni huu. Nimeupenda sana kwa jinsi unavyo mkumbusha Mswahili aka Mjomba JK arudie historia nayeye awe miongoni mwa mashujaa wa Afrika. Ahsante Mkulu Vitali Maembe!
   
 5. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana Mswahili mwenzangu kwa mwendo mrefu wa kwenda kuwakilisha mswada pale DOM Bungeni.Hata kama kuanzia MJOMBA,ADERA NA MBUZI WA KAFARA hata kama hawakukujibu lakini sisi wanamabadiliko tuna imani ujumbe ulifika.
   
 6. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  heshima yako maembe.!
   
Loading...