Elections 2010 Waraka wa Lowassa kwa vyombo vya habari

The Informer

Senior Member
Jun 14, 2010
119
29
TAARIFA RASMI KWA VYOMBO VYA HABARI NOVEMBA 5, 2010

Novemba 3, 2010 mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa aliwatuhumu makada 30 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa walifanya kikao cha kupanga mipango ya kumwibia kura mjini Mwanza. Kati ya makada aliowatuhumu ni pamoja na
mimi.

Napenda kuufahamisha umma kuwa habari hizi si za kweli kwa sababu mwezi wote wa Oktoba, nilikuwa jimboni kwangu nikifanya kampeni za kuwania kiti cha Ubunge katika Jimbo la Monduli. Sikupata kusafiri kwenda Mwanza hata siku moja, na siku aliyoitaja ya Oktoba 19, nilikuwa katika vijiji vya Mfereji na Enguiki nikifanya kampeni siku nzima.

Ukiacha tuhuma hizo, pia upo uvumi uliosambazwa kwamba nilishiriki kikao cha mikakati ya kuchakachua kura, mjini Arusha kumsaidia mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Batilda Burian aweze kushinda kiti hicho. Nasema uvumi huu ni uzushi na si wa kweli.

Kutokana na yote haya, ninakwazika kwamba inaonekana katika nchi yetu umeanza kuingia utamaduni mpya wa kufanya siasa za uongo, uvumi, uzushi na kila aina ya hila kwa nia ya kujipatia ushindi. Kwa uzoefu wa mataifa mengi yaliyotuzunguka, ndani ya Afrika na sehemu nyingine duniani, amani hupotea kutokana usambazaji wa taarifa za uongo.

Mwasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alituachia amani na utulivu ambavyo ni tunu ya taifa hili.

Dalili zinazoonekana, kuna watu wanaelekea kuchoshwa na amani iliyopo.

Wanajiandaa kufanya vurugu, kuliingiza taifa hili katika machafuko, na sijui wanafanya hivyo kwa faida ya nani.

Wito wangu kwa Watanzania, ni kwamba tusiichoke amani. Amani tuliyonayo ndiyo imetutofautisha na mataifa mengi yaliyotuzunguka na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kupigiwa mfano. Tuelekeze nguvu zetu katika shughuli halali za kutuletea kipato zisizoharibu amani yetu.

Tukiiharibu amani tuliyonayo, mwisho wa siku nchi yetu itateketea na sote hatutakuwa salama. Tutakuwa tumekwisha.

Mwisho, namsihi Dk. Slaa ajipe muda wa kuzifahamu vyema siasa za nchi hii. Asidanganywe na mahudhurio ya mikutano ya hadhara akadhani ndizo kura katika masanduku ya kupigia kura. Namsihi ajifunze` zaidi jinsi ya kufanya siasa za kistaarabu bila kueneza uvumi, uongo, chuki na uzushi vyenye kutetelesha amani ya nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania.

Edward Lowassa

Mbunge Mteule wa Monduli

Taarifa hii ya PM aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ya Richmond imesambazwa kwa vyombo vya habari sasa hivi na: AIKA JUNIOR <aika_junior@yahoo.com>
 
Mbona hajaongea kama ataenda Mahakamani kuwa kasingiziwa na DR Slaa,
 
Alafu mbona kila mtu anajitetea lwake CCM hawana msemaji.

Inavyoonekana kikao kilifanyika so far watu watatu wanasema hawakuudhuria
 
Hiyo ni mbinu ya kukwepa ukweli.

Ukweli ni kwamba CCM inajua kuwa kile inachokitaka ndicho itakachopata na ndiyo maana haigopeshwi na kura halali zinazopigwa na Watanzania kwani inajua itazichakachua.

Kauli kama hii ya kipuuzi ilisemwa na Mkapa siku chache kuwa hata mwaka 1995 Mrema alipata mahudhurio makubwa lakini kura kdiogo. Wanajua kuwa walimuibia na kwani wana uwezo huo. CCM kukataa demokrasia ya kweli ni kama mtu kuhairisha kwenda haja!
 
Hivi ni kweli kwamba Nyerere alimkataa Lowasa? Hivi kwa nini alimkataa?
 
Itabidi na Rostam awe waziri wa Fedha. Ridhiwani mambo ya nje na ushirikiano wa kimafisadi
 
sioni jipya angalikuwa muungwana zaidi kuelekeza madai yake kwa mkurugezi wa jiji la mwanza ndugu wilson kabwe kwamba kwanini alimtaja katika kashfa ya uchakachuzi wa matokeo na sio kumshambulia dk slaa kwani misingi ya hoja ya slaa imejengwa katika waraka aliousambaza ndugu kabwe! na kuhusu la arusha ndugu lowasa ana act katika uvumi hivyo si mtu makini hata kidogo dont act on hearsay ndugu lowasa!:nono:
 
Yaani wewe LOWASA unamkumbuka NYERERE?!! bila aibu utalaaniwa wewe.umeibia nchi hii sh ngapi? Watch out FISADI WEWE.

Siku zenu za kutuibia zimekaribia kuisha kabisa ndio mana mna kiwewe.

Presha zitawaua, eti Slaa hajui siasa you wake uuuupppppppppppppppppp. kwasababu hajaiba kama nyie ndio mana hajui siasa.
 
jizi kubwa nyangau.yaani wewe lowasa unamkumbuka nyerere?!! Bila aibu utalaaniwa wewe.umeibia nchi hii sh ngapi? Watch out fisadi wewe.siku zenu za kutuibia zimekaribia kuisha kabisa ndio mana mna kiwewe.

Presha zitawaua, eti slaa hajui siasa you wake uuuupppppppppppppppppp. Kwasababu hajaiba kama nyie ndio mana hajui siasa.

mwisho wao ndio unaelekea hivyo
 
Nyerere nasikia alimwambia Lowasa Kijana mdogo utajiri wote huu ameutoa wapiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

Baada ya kuambiwa hayo Lowasa akaenda kujipanga na kuorodhesha assets zake zote na jinsi alivyozipata then akaenda kwa mwalimu kujidani upya kule Butiama ili mwalimu amsafishe EL.

Baada ya presentation ya mali zake Mwalimu akamwambia EL ata aliyekuandalia amejitaidi then mwalimu akatoa doc yake EL aliondoka bila kuaga.

Alijua mwalimu zuzu kuwa hajui data zake
 
hivi ni kweli kwamba nyerere alimkataa lowasa? Hivi kwa nini alimkataa?

Alimwita akamuorodheshea mali anazo miliki na yeye el akasema kuwa si zake ila watu wanamsingizia.

Nyerere akamwambia kule Roma mke wa mkuu wa Roma alizushiwa kazini akatuma intelijensia yake kuchunguza wakakuta kweli mke wake alikuwa analiwa nje ila wakamnusuru kwa kumwambia bwana mkubwa kuwa mke wake hakuliwa ila anazushiwa! Lakini bwana mkubwa akamwacha kwa kuwa tayari alikua keshaingia dosari.

Kwa hadith hiyo inasemekana kwa maneno kusemwa ina maana ni kweli ana miliki mali hizo na isingekuwa busara kwake kuwania nafasi hiyo!
 
Nyerere nasikia alimwambia Lowasa Kijana mdogo utajiri wote huu ameutoa wapiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

Baada ya kuambiwa hayo Lowasa akaenda kujipanga na kuorodhesha assets zake zote na jinsi alivyozipata then akaenda kwa mwalimu kujidani upya kule Butiama ili mwalimu amsafishe EL.

Baada ya presentation ya mali zake Mwalimu akamwambia EL ata aliyekuandalia amejitaidi then mwalimu akatoa doc yake EL aliondoka bila kuaga.

Alijua mwalimu zuzu kuwa hajui data zake

ha ha ha ha
 
Alimwita akamuorodheshea mali anazo miliki na yeye el akasema kuwa si zake ila watu wanamsingizia.

Nyerere akamwambia kule Roma mke wa mkuu wa Roma alizushiwa kazini akatuma intelijensia yake kuchunguza wakakuta kweli mke wake alikuwa analiwa nje ila wakamnusuru kwa kumwambia bwana mkubwa kuwa mke wake hakuliwa ila anazushiwa! Lakini bwana mkubwa akamwacha kwa kuwa tayari alikua keshaingia dosari.

Kwa hadith hiyo inasemekana kwa maneno kusemwa ina maana ni kweli ana miliki mali hizo na isingekuwa busara kwake kuwania nafasi hiyo!

Aisee
 
haki ya mungu hatutakubali spika awe chenge na lowassa kuwa wairi mkuu mungu angali tunavyoonewa
 
Itabidi na Rostam awe waziri wa Fedha. Ridhiwani mambo ya nje na ushirikiano wa kimafisadi

SALMA waziri wa jinsia wanawake na watoto. Ndiyo maana wabunge wengi wamechaguliwa kihiyo ili familia iteuliwe kuongoza wizara.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom