Mgibeon
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 11,254
- 21,276
U hali gani bosi wangu, shaka sina unaendelea vema kabisa na harakati za ujenzi wa taifa, Naandika waraka huu nikiwa na nia na lengo la kukumbusha tulipotoka ila sio kukukosoa.
Ndugu yangu mshana jr ni dhahil-shahil kwamba katika maisha yako yote hukuwahi kuwaza kukamatia nafasi uliyonayo sasa, yaani kwa kiswahili cha haraka haraka ambacho watu wanaweza kuelewa ni kwamba ulidondokewa na embe chini ya mnazi.
Hata unakumbuka mtu ambaye ilibidi awe hapo ni kiasi gani ameamua kuwa na moyo wa chujio wa kukubali kupoteza kwa maslahi mapana ya amani ya wote waliotaka yeye akalie hicho kiti ulichokalia wewe, ajabu ni kwamba badala ya kuunga mkono yale yanayozungumzwa na ndugu zake ambao umeapa hasirani-abadani kwamba hutaki hata kuwasikia, ndiyo kwanza umekua ukiwakejeli na kuwanyima upenyo kuonekana na kuzungumza.
Imefika mahali unajitapa hadharani kwamba hicho kiti ulikipata kutokana na jitihada zako na wala hakuna yeyote aliyekushauri kwenda kwa seremala kukichongesha! Yaani umewadharau mpaka wale jamaa wawili walioingia msituni, wakatafuta mti mzuri, wakaukata na kuuchana vizuri na kuuleta kwa huyo seremala wako unayejivunia. Huku ni kukosa shukrani sana hasa kwa mtu kama wewe ambaye unapenda sana kuingia kwenye nyumba za ibada na kujifanya wewe ni mpole na huruma sana.
Ulipoanza kukikalia kiti ulikua mnyenyekevu haswa hata ukawaomba wanakijiji wakukumbuke katika dua zao ila sasa inaonekana ushaota mkia na pembe umejiongezea mwenyewe, nikukumbushe tu ndugu yangu mshana jr kua wewe sio wa kwanza kukalia hicho kiti, utakaa na ikiwa mapenzi ya mwenyezi Mungu tunaendelea kua hai basi ishaallah atakalia mwengine wewe utake au usitake.
Hebu mtazame mkalia-kiti aliyepita sasa hivi! Unamuonaje? Anajisikia raha kweli kweli maana kila anapopita watu wanamshangilia na kumsifia ingawa in reality watu walimponda sana wakati akiwa hatamuni, ila kutokana na majigambo na kujiona wewe unakaribia kua Muumba watu wanaona bora yeye kuliko wewe, naam hizo ndio tamaduni na mazoea yetu sisi ngozi nyeusi, tunapenda kulinganisha perfomance.
Hivi bwana mkubwa mshana jr unajua huku kijijini kwa sasa maisha yamekua magumu mnoo, yaani hata ugali umekuja kua anasa kweli? Huku wapi unatupeleka ndugu yangu? Hebu jitafakari mara mbili mbili, inawezekana kuna mahali unakosea au wanaokushauri hawakupi mbinu nzuri, kikubwa braza tunataka unafuu hapa kijijini kwetu.
Najua wale walioleta ule mti uliotengeneza kiti chako kwa sasa wanaonekana wapuuzi tu ila trust me pamoja na uhakika wa mambo ya CHAJE 2020 unashughuli pevu sana, maana matokeo hua hayajipangi, yule mkongwe alipotamka kua "jamani mimi nayasoma kama nilivyoyapokea" sio kweli kwamba hakujua mambo ya Teknohama yalihusika, alijua sana, na mimi binafsi kama Mgibeon naamini kua pale ni zaidi ya pesa ilitumika, mapenzi na upendo ulichochea mtu mzima kupindisha ukweli, Anyway nakutania tu comrade, usichukulie serious kiiiiiiiiiiiiivo! Hivi unajua mimi nimeoa Lembeni pale, kwahiyo wewe ni shemeji yangu, usinune.
Halafu hakuna namna unawezafanya "kisichana cha kizaramo" kikarudi sokoni,? Ni aibu kuweka BAPA/JIBAPA mchana kweupe-pee halafu meza nzima umekaa peke yako! Fanya manuva basi.
Aluta continua.