Waraka wa kusikitisha kwa balozi Kagasheki wasambazwa Bukoba mjini

Nam...

Member
Nov 11, 2011
51
16
Baada ya kuusoma kama mwanaharakati nimeamua kuandika yafuatayo;-

Nakumbuka maneno ya MOHANDAS KARAMACHAND GANDHI aliyefahamika sana kama MAHATIMA GANDHI na baba wa taifa la India, Yeye alisema "SIWEZI KUHUBIRI AU KUPIGIA DEBE HARAKATI ZINAZOHATARISHA UVUNJIFU WA AMANI KWASABABU SI MUHUMINI WAKE, NINACHOWEZA KUHUBIRI NA KUKIPIGIA DEBE NI KUTOKUBALI KUMTII YEYOTE YULE ANAYEHATARISHA MAISHA YAKO"

Hali inayoonekana Bukoba ni suala la utekelezaji wa miradi ya jamii ambayo ipo kisheria lakini wapo wanaotaka kuitumia kama daraja la kujitangaza, katika njia ya kuwaumiza wananchi kwasababu uwezi kufanya mjadala usio na ugomvi kama upande mmoja hauna uhakika au hauelewi kinachoendelea. Sasa je wana wa Bukoba wanajua nini kuhusu mikataba ya soko na mtu akihoji katika hilo amekosea?

Kutokana na sintofahamu hiyo, wapo waliopewa idhini na wananchi kuhoji kwa niaba yao, sasa wanapohoji waliopembeni na ambao hawajui lakini wanataka kutumia daraja hilo kupata uongozi, tayari wanahubiri na kupigia debe harakati zinazohatarisha uvunjifu wa amani kwasababu wanajaza maneno kwa wasiojua mikataba ya soko iko je.

Inawezekana wakasema mengi kutokana na hisia, lakini hii inanipa picha kwamba wasemao wanaweza kuamsha wasiyoyajua au kuyafanyia kazi, ila kwasababu wanataka nafasi watayafanya makubwa ili kutimiza maandiko ya wahenga kwamba "FAHARI WAWILI WAGOMBANAPO, NYASI NDIZO ZINAUMIA".

Mbunge akisimama katika mikutao ya adhara anazungumzia siasa na maenedeleo, mwalimu akiwa darasani anazungumzia masomo na taaluma husika kulingana na kipindi.

Kagasheki kusema amemchonga Meya, kwa mtu mwenye uelewa na akili timamu atajua amemaanisha nini lakini asiyejua chochote atajua amemaanisha sura, lakini kagasheki angekuwa mwalimu, mimi ningeelewa kuwa amemchonga meya kwakumfundisha somo Fulani ambalo limemfikisha alipo.

Hivyo basi kwakuwa ni mwanasiasa Napata picha ya moja kwa moja kwamba amemchonga kisiasa yaani amempa mwanga na mbinu za kusimama mbele ya adhara na kuzungumza kwa kujibu hoja na jinsi gani anaweza kutetea wananchi na hilo halina ubishi jamani waliokuwa bukoba tangu mapema wanalijua, sasa utasemaje MUNGU AKAMUUMBA MTU KWA MFANO WAKE? Tusidanganye wananchi.

Baba wa taifa na aliyeongoza mapinduzi ya taifa la China MAO TSE-TUNG akiongoza chama cha kikomunisti kuanzia mwaka 1935, alisema kuwa "MATABAKA UPAMBANA BAADHI HUSHINDA MAPAMBANO NLAKINI MENGINE HUSHINDWA, NA HIVYO KUTOKOMEZWA NA NDIVYO HISTORIA YA USTAARABU ILIVYO DUNIANI".

Sasa wanaochochea hasira na chuki kwa wananchi wakitumia nafasi ya wananchi kutokuwa na makini au nafasi ya kusoma na kuelewa mambo, wajue kwamba wanayoyakuza siku moja yatafutika kwasababu historia inaonesha hivyo tangu karne zilizotangulia labda kama itakuwa mara ya kwanza kushindikana, na inaonekana yakisha malizika waliokuwa upande Fulani ulazimika kujipendekeza upande wa pili ili wapate nafasi.

Nawasihi kukumbuka maneno ya COMFUCIUS aliyezaliwa mwaka 551 BC na kufariki 497 bc, alisema kuwa "FARAJA YETU KUBWA KATIKA MAISHA NI SI KWAMBA BINADAMU KAMWE HATUANGUKI, BALI KILA TUANGUKAPO TUNAUWEZO WA KUAMKA NA KUENDELEA NA SAFARI", hivyo pamoja na mbunge kuwa ni nafasi mojawapo ya ajira yake katika serikali ya jamhuri, bado anasemea wananchi kupitia matukio anayoyashuhudia ambayo hata hivyo hayako sawa katika maslahi ya mwananchi, kwahiyo wananchi walitaka azungumzie chumbani ili muendelee kulishwa maneno ya uongo?

Kutokana na watu kuhitaji uongozi wa lazima, wanajitokeza wanaoibua habari za uchochezi na kama tunavyotambua masuala ya UDINI hayana nafasi kwa watanzania, kitendo cha mbunge kutoa usafiri kwa shughuli mbalimbali kimekuwa kikifanyika tangu mbunge huyu amechukuwa madaraka ya kuongoza jimbo la Bukoba na si kwa ajili ya kwenda kuhiji MUGANA pekee bali hata kwenye shughuli za mazishi na hata kusafirisha maiti.

Zaidi ya yote mfano wa haraka mbunge ametoa usafiri kwa timu ya mpira BUKOBA VETERAN kwenda Uganda ili kuiunga mkono timu ya taifa, mbona hiyo hawazungumzi kuwa ni makosa? Yeye anapotoa fedha kwa ajili hiyo si nafasi yake kusimamia kama kilichokodwa ni malori au tax hiyo ni kazi ya waliokabidhiwa kitita.

Unaposisitiza kuwa mbona hajaenda MAKA ili aitwe alhaji nadhani ameona gharama hiyo si sahihi kujinufaisha yeye bali wananchi wake kwasababu kipindi hicho ndicho maeneo kadha ya jimbo yalikumbwa na upepo akatoa msaada wa mabati kwa makanisa ya KYAKAILABWA na KILIMAHEWA pamoja na chakula kwa waliokubwa na upepo ambao ulifikia zaidi ya milioni 5 ambapo kwenda MEKA ni dola zaidi ya 900.

Kama kutoa msaada kanisani ni kosa mbona mabati hayajalalamikiwa?
Mwanafizikia wa kale duniani ALBERT EINSTEIN kutoka ULM WURTTEMBER UJERUMANI, alisema "BINADAMU YEYOTE ANAYESOMA SANA NA AMBAYE HUTUMIA KIDOGO MNO UBONGO WAKE MARA NYINGI HUANGUKIA KATIKA TABIA YA KIVIVU YA KUFIKIRI" Nimesema hivyo kwasababu waliowengi wanaoonekana kupinga ni wale wanaosoma sana na kupenda kuiga pasipokujipatia muda wa kufikiri kwamba majimbo yanatofautiana.

Mbunge kupita kila siku anaenda kuudhuria vikao vya madiwani ni kweli kwamba anatatua matatizo ya wananchi wake kama afanyavo Kagasheki? Ni bora asijitokeze kila siku kmwenye vikao kama unavyopenda aige lakini afanikiwe kuwafikia wananchi mapema na kutatu matatizo yao, lakini kama zilivyo sheria za nchi, vikao vikifanyika ni lazima viwe na maandishi ambayo kulingana na taratibu yatakwenda ngazi moja hadi nyingine katika uongozi, je hayo yanafanyika katika vikao vya madiwani Manispaa ya Bukoba?

Itakumbukwa tangu mwaka 2011 mbunge amekuwa akishiriki na hasa akizungumza kupitia mikutano ya adhara kwa kuzungumzia miradi ya maendeleo ikiwamo suala la kuvunja na kujenga soko kuu jipya la Bukoba, ambapo iko katika ushirikiano wa pamoja, lakini kwakuwa kila kitu kina ngazi yake imekuwa ni kawaida Meya akaratibu baadhi ya masuala lakini ni lazima atoe taarifa kupitia vikao na hata kuwasilisha vielelezo kwa mbunge, ila amekuwa hafanyi hivyo na hilo ndo lalamiko la Kagasheki baada ya kuonekana baadhi ya madiwani nao wakihoji lakini wakiogopa kutokana na ubabe wa meya, wakisubiri Kagasheki aulize ambapo inaonekana wamemtoa kama chambo kwa Meya na wananchi.

Hali hiyo inanionesha na kunikumbusha maneno ya mtunzi maarufu wa kale AGATHA CHRISTIE kupitia kitabu chake cha THE MAN IN THE BROWN SUIT, aliyesema kuwa "NI MAISHA MAGUMU NA AJABU, MWANAUME HAWEZI KUOA MWANAMKE KAMA HANA SURA NZURI NA HAVUTII, NA MWANAMKE HATAMPENDA MWANAUME MWENYE SURA NZURI KUMZIDI NA ANAYEVUTIA"

Kupitia maneno hayo, wananchi watajua nani wanamtaka ili awaongoze na wanampenda wala si vema mtu kujipendekeza katika hilo, wakati mambo muhimu yanafichwa nyumbani mwa familia ya Meya, watu watajuaje? Mbunge akiuliza hilo mnamkandamiza?.

Ya Mungu mpe mungu nay a Kaizali mpeni Kaizali, Balozi HAMIS KAGASHEKI unapigana na wananchi wako ila wanaokusakama wanataka nafasi tu, ila kwasababu hawana jinsi wametafuta namna ya kukuchafua.

Mwanafalsafa SOCRETS wa ITALIA katika miaka ya 500-400 kabla ya Kristo, alisambaza elimu kupitia maandiko akiwataka wananchi kusimama kidete katika maslahi yao, lakini waliokuwa na uchu wa madaraka wakiongozaz wananchi mbumbumbu, baada ya kuona Socret anatoa elimu na wananchi wanapata mwamko, walimlazimisha ajiue kwa kunya sumu mwenyewe, lakini kabla hajainywa alisema "VIONGOZI WENYE TAMAA WAMEAMUA KUUA KICHWA KIMOJA, LAKINI WAMESHINDWA KUJUA KWAMBA NIMEKUFA MIMI ILA ELIMU YANGU IMEJAA TAYARI VICHWANI MWA RAIA, HIVYO WATAENDELEZA MAPAMBANO NA KUJIKOMBOA KUTOKA MIKONONI MWA UBWENYENYE"

Kagasheki hata wakikufitini kisiasa hawa wenye tamaa, naamini ujumbe wako tayari wananchi wameupata na kwasasa wanajua kudai haki na ndo maana baada ya tamko lako kwenye mkutano wa hdahara tarehe 24 november 2012 ulisema soko halijafanyiwa upembuzi yakinifu hivyo halitabomolewa kwa haiwezekani ukajenga sehemu usiojua kiasi cha maji chini ya ardhi.

Ndipo siku moja baadaye ikiwa ni jumapili, kampuni isiyojulikana inayojiita GEOPINIUS INVESTMENY iliyoandikwa kwa MAKERPEN ubavuni mwa gari aina ya FUSO T675 AEJ kutoka Dar es salaam kwa mujibu wa (kandayaziwaleo.blogspot.com) ya huko Bukoba, ilikuja na mashine za kuchimba na kupima kiasi cha maji ndani ya soko kuu, lakini kwa akili uliowapa wananchi wakatambua haki yao walizuia gari hiyo kwani Kesi ya soko bado iko mahaklamani, je anayesema soko lazima livunjwe amepanga na mahakama kwamba lazima ashinde kesi hiyo na mbona anataka kulivunja kabla ya machi ambapo kesi inasikilizwa tena?


PEACE AND LOVE JAMANI WANA JF.
 
naona kagasheki mwenyewe umekuja hapa, ningekuwa rais ningeshakufuta kazi mara moja sababu ulishiriki kutoa hati za kusafiria kwa hao watoto wa huyo aliyegeuka kuwa adui yako sasa hivi meya wa bukoba, na ujitamba hadharani kuwa ulisaidia asiyekuwa raia kupata hatai ya kusafiria ya tanzania ujinga wenu na hila mmeanza kuumbuka mapema kweupe, to hell na ujinga wenu.
 
I simpathise with Hon. Kagasheki, I pray that he deliveres the best to people of Bukoba. I pray the evil spirit of the Mayor following go away
 
Hovyo tu! Maneno mengi hakuna la maana, Kagasheki alifanya kampeni za kujengana na meya ili wote wawili wapate ulaji tu, matarajio ya amani yalikuwa kurithi nafasi ya ubunge akidhani mwenzake angemuachia kagasheki nae hataki kufanya hivyo kwa sababu mambo ya uwaziri yamemnogea, kwa uchu walionao 2015 bkb hapatakalika na mbegu ya udini waliyoipanda lazima iwatafune maana walikuwa wanajifanya wanakemea huku wanapandikiza makusudi kabisa, watuachie bukoba yenye amani wao waende tu.
 
Waafrika sisi bado sana. wasomi ndio kabisa wana ujinga mamboleo. hivi inawezekana vipi waziri mzima una msaidia mtu asiye raia kupata hati ya kusafiria ya nchi yako na wala usione umetenda kosa la kukufanya uwajibike?kagasheki ushindwe na ulegee!! wewe ni msaliti wa NCHI yako.
 
Wewe unatumika tu kama kondomu japo umeandika mambo mengi huna jambo la maana nenda kale pilau kwa akina Kagasheki ndio ujira wako.Pia unawakilisha kundi la watanzania wengi wajinga.Nikulize hujui nafasi ya waziri na Mbunge katika utendaji kazi wa Halmashauri?.Kama haujui soma au omba kuelimishwa,toa pumba zako hapa swine.
 
Mleta hoja hakuna kitu ulichoandika bali blaah blaah na kujionesha kwamba umesoma vitabu vingi. Lakini unavi quote out of context inaelekea ume claim.

Tunaomba utoa ufafanuzi, maana ushahidi upo mpka kwenye youtube.

Ilikuwaje Kagasheki akapindisha sheria za nchi, akampatia raia wa nchi nyingine na watoto wake passport ya kusafiria ya Tanzania. Kwa kosa hili Kagasheki anasitahili kuendelea kuwepo kwenye ofisi ya umma?

Kama tabia yake ndiyo hiyo ya kupindisha sheria za nchi kwa manufaa yake binafsi. Je huko Wizara ya Maliasili atashindwaje kupindisha tena sheria na kufisadi maliasili yetu?.

Muwe mnaona aibu kutetea UJINGA, watu watatutushangaa kama kweli huko up stairs nuts zote zipo.
 
When a heart is on fire, sparks always fly out of the mouth. Pole!
 
Its rubbish!!!. Pamoja na usomi wako huna lolote. habari ndefu na quotes za kihistoria lkn hakuna mantiki. Ungejua mtandao huu sio sehemu ya kutafuta sifa usingeandika upuuzi huu. Unafikiri ni nani anayeweza kukuunga mkono kwa upuuzi huu. Tena wewe ndo hovyo na mnafiki mkubwa kuliko kagasheki. Ungejua kwa adha na dhima ya watu kwenda kuhiji usingetetea ***** wa kupinga msimamo wa wakristu kukataa usfiri wa kagasheki, ungejua wakati kagasheki anatoa magari ya kwenda nyakijoga ni waislam wangapi walikuwa wanapanda magari wakidai nao wanakwenda kuhiji. Km umetumwa kusafisha basi hata elimu yako haijakukomboa. Acha kujitafutia ujiko usiokuwa na maana. Otherwise go back to school.
 
naona kagasheki mwenyewe umekuja hapa, ningekuwa rais ningeshakufuta kazi mara moja sababu ulishiriki kutoa hati za kusafiria kwa hao watoto wa huyo aliyegeuka kuwa adui yako sasa hivi meya wa bukoba, na ujitamba hadharani kuwa ulisaidia asiyekuwa raia kupata hatai ya kusafiria ya tanzania ujinga wenu na hila mmeanza kuumbuka mapema kweupe, to hell na ujinga wenu.
kuuliza sio ujinga ...huyo meya anaitwa nani
 
Ukweli utabaki pale pale ya kwamba Waziri Kagasheki ni MDINI SANA. Nina ushahidi wa kutosha kuhusiana na udini wa Kagasheki.
 
It's very sad unapoona watu ambao wamejitambulisha kama wasomi lakini wanatetea visivyotetewa. Uchafu wa meya hauwezi kumsafisha kagasheki ambaye ni very arrogant by all aspects. Halafu usafiri wa kwenda kuhiji Nyakijoga hauwezi kumfanya kagasheki kuwa mzalendo na msafi au kuwa mdini. Watu wamekuwa wakienda kwenye kituo hicho cha sala kwa muda mrefu na kama ni shida ya kufika huko haijaanza leo. Mbona alikuwa hatoi usafiri huo na sasa unatolewa sasa hivi. Alisubiri awe mbunge ndio atoe usafiri. Kagasheki ubunge wake una utata from day one. Ikiwa haijulikani pesa ilitoka wapi akam sio za EPA CCM walianza kununua shahada za kupigia kura kutoka kwa vijana maskini na baada ya kuzinunua wakaona kuwa watashinda. Siku ya kura ikaonekana Lwakatare alikuwa anaongoza tena kwa margin kubwa. Ndipo walimchezea mchezo wa ajabu. Wakachakachua, wakachukua mawakala wa Lwakatare wakawapa hongo na kutoweka huku simu zao za mikononi zikiwa zimezimwa. Kwa mtindo huu Kagesheki alishachafuka na his integrity is questionable. Hivyo kwa kujiingiza kwenye issue ya soko mie naona aache sheria ichukue mkondo wake maana it's obvious there is personal vendetta between Meya na mbunge Kagasheki na sasa natumia loophole ya kushiriki kutengua sheria ili amtishe meya. Wote hawafahi na hapo watu wa Bukoba au niseme wahaya ambao ndio majority yo have put yourselves on the spotlight na hata heshima kidogo mliyokuwa mmebaki nayo is fading. Please don't be dodoki. You have brains to filter what's bad and what's useful. Short of that mtakuwa victims wa msemo wa watu wa Kamachumu "okafa ohyemereire nke emotoka ya Terenti"
 
ukweli utabaki pale pale ya kwamba waziri kagasheki ni mdini sana. Nina ushahidi wa kutosha kuhusiana na udini wa kagasheki.

ogopa m2 ambaye hata familia yake haimuungi mkono kwenye mambo yake! Mnajua mke wake yuko wapi?
 
Back
Top Bottom