Waraka wa kujenga fikra za mapinduzi ya dhati kwenye safari ndefu ya ukombozi wa mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa kujenga fikra za mapinduzi ya dhati kwenye safari ndefu ya ukombozi wa mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, Feb 12, 2012.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Ndugu Wanaharakati,

  Baada ya kutafakari kwa muda mrefu juu ya nini cha kuandika kwenye Waraka huu, nimeona kwamba hakuna cha ziada ila kuandika ukweli. Umefika wakati wa kuutambua ukweli, kuuheshimu ukweli, na kuutamka ukweli, ili vizazi vya sasa na vijavyo vitukumbuke kwamba tulikuwa wa kweli na tulijaribu kuleta Mapinduzi ya Fikra ili kuweza kumkomboa Mtanzania kwenye lindi la Ukoloni Mpya.

  Tukitaka kuutambua ukweli, kuuelewa na kuukubali, lazima tuangalia kwenye historia ya nchi hii. Tuanzie mwanzo.

  Nini kilitokea wakati wa harakati za uhuru kutoka kwenye makucha ya kikoloni ya Uingereza?

  Nani waliokuwa na maamuzi, nini kifanyike, baada ya uhuru kupatikana?

  Nini kilifanyika, nani aliamua, nani aliidhinisha?

  Tukiweza kuchambua na kuchunguza, hatimaye ukweli utapatikana.

  Hata hivyo, yafuatayo nayo ni ya kweli kabisa, wala hayana ubishi wa aina yoyote ile.


  1. Ni ukweli usiopingika kwamba Katiba ya kwanza ya nchi hii, Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika, iliandikwa na kikundi kidogo sana cha Watanganyika, walioitwa “wazoefu” au “weledi” wa kushughulika na mambo ya Katiba. Watu hawa walichambua katiba za nchi ambazo awali zilikuwa makoloni, na kutoa humo mambo ambayo yalionekana kuwa na faida kwa maslahi ya watawala wapya, ndipo yakajumuishwa na kupatikana Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika (1961). Watu walioandika Katiba hiyo wanajulikana.
  2. Ni ukweli usiopingika kwamba katika zoezi zima la kuandika Katiba hiyo, Watanganyika – kwa uwingi wao – hawakuhusishwa, sio tu kwa kuwapa nafasi ya kutoa maoni yao, bali pia, hata kuusoma muswada au rasimu ya Katiba hiyo, ili waweze kuridhia kuwapo kwa Katiba hiyo.
  3. Baada ya Katiba hiyo kupatikana na Bunge la Jamhuri ya Tanganyika kuanza kufanya kazi, Katiba ilitumika katika kile kilichojulijana kuwa ujenzi wa taifa, kwa minajili kwamba, hapo baadaye, Katiba ya Watu wa Jamhuri ya Tanganyika ingekuja kupatikana. Hili halikufanyika, mpaka sasa.

  Maswali yafuatayo ni muhimu kuyauliza:


  1. Je, Watanganyika waliulizwa iwapo wanaridhia/wanaridhika na mfumo wa Serikali ulioanza kutumika mara tu baada ya uhuru?
  2. Je,Watanganyika walishirikishwa kikamilifu katika mchakato mzima wa kuendesha nchi yao, kupitia Serikali iliyokuwapo madarakani, pamoja na mfumo wa uwakilishi?


  Maoni yangu:


  1. Kwanza, mfumo wa Serikali uliopo hivi sasa, kuanzia kabla na baada ya kuundwa kwa Muungano na Zanzibar, umerithiwa kutoka kwa Wakoloni Waingereza, si mfumo wa Serikali ambao umebuniwa na Watanganyika na/au Watanzania
  2. Pili, mfumo wa Uwakilishi (Bunge), haukuridhiwa na Watanganyika/Watanzania, na hauna tofauti sana na mfumo wa Kichifu uliokuwapo hapo awali, iwapo Chifu alikuwa anatokana na familia iliyokuwa inatawala. Sehemu nyingine, Wabunge wamekuwa wakiandaa mazingira ya kuwarithisha ndugu zao, watoto wao, jamaa zao, Ubunge huo, pindi wanapofikia muda wa kustaafu. Hivyo, ingawa upatikanaji wa Mbunge ni kwa njia ya uchaguzi, utendaji wake na mapokeo yake hayana tofauti na Uchifu. Mbunge, mpaka sasa, akienda jimboni kwake, hupokelewa kana kwamba ni mtu mkubwa sana, yaani, mtawala au Chifu.
  3. Tatu, mfumo wa uchaguzi hapa nchini una kasoro kubwa sana, ukiwa umegubikwa na hila, udanganyifu, rushwa kwa kiwango kikubwa, kutoka ndani ya chama tawala hadi nje, ilhali vyama vya upinzani, vingi ambavyo vikiwa havina nguvu ya kutosha – isipokuwa CHADEMA pekee – vikionekana kuwapo kwa sababu ya kupunguza wingi wa kura ambazo zingekwenda CHADEMA, jambo ambalo linavifanya vionekane kuwa CCM B, C, D, E, F, G, H, n.k.


  Nini kifanyike:


  1. Kwenye mikutano ya upatikanaji wa Katiba Mpya, wewe Mtanzania lazima ufikirie yote haya, kisha ubaini nini utakuwa mchango wako, kwani sasa umepewa nafasi ya kutunga katiba YAKO!
  2. Jiulize maswali. Unataka Serikali ya aina gani? Unataka mfumo wa uwakilishi wa aina gani?
  3. Tafakari, chukua hatua.


  Imeandikwa na MwanaHaki
   
 2. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa kamanda! Naamini kati ya watu makini na wewe utakuwemo na vile vile watu makini wataosoma huu waraka wako watautumia ili kuleta ukombozi na mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu hii ya kifisadi na hatimaye tutapata katiba safi kwa maslahi yetu na vizazi vyetu vijavyo!
  Kwa pamoja tushirikiane kukomesha ufisadi na mafisadi wa Chama tawala (CCM)!
   
Loading...