Waraka wa Hussein Bashe kwa NEC, CC na secretariet mpya ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa Hussein Bashe kwa NEC, CC na secretariet mpya ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Apr 14, 2011.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Huu waraka wa Husein Bashe nimeupata face Book


  by Hussein Bashe on Wednesday, April 13, 2011 at 11:16am

  WARAKA WANGU KWA CC NA SEKRETARIETI MPYA CHAMA

  Kwanza nianze kwa kuwapongeza kwa uteuzi mliopata na kuwatakia kila kheri kwa imani hiyo mlopewa na NEC ya chama chetu .

  Pili nitumie fursa hii kumpongeza Mwenyekiti kwa kuendesha kikao ambacho leo kimetuletea PICHA mpya ya vijana na Wazeee katika CC na Sekretariet ya chama na kuzaliwa upya kwa ccm kwa maana ya HISTORIA KUANDIKWA kutokana na maamuzi yaliyofikiwa Dodoma.


  Ningependa kutumia nafasi hii kuwaambia viongozi wetu sasa ni wakati wa chama kukabiliana na changamoto zinazotukabili hatua hii, ya sura mpya haijamaliza bado matatizo yanayotukabili kama chama kinachoongoza taifa hili,na msirudie makosa yaliyofanyika toka kipindi cha 1995 mpaka leo ya chama kubaki na kufanya siasa za PERSONALITIES na kuacha siasa za ISSUE na Nguvu nyingi kuzipeleka katika Formular ya Character assasination ambayo kwa muda mrefu imekiumiza chama na kutufanya kufika hapa tulipo leo ambapo viongozi wote wachama walichafuka na kukosa heshima katika PUBLIC jambo ambalo lilitugharimu kwa Muda Mrefu.


  NAPE na JANUARY ni uwakilishi wa vijana katika nafasi nyeti mlizopewa na mnawakilisha vijana wengi,binafsi nina imani kubwa na nyie bcs sina shaka juu ya uwezo wenu wa kusimamia mambo magumu hata kama wengine hawayapendi,changamoto kubwa mlionayo na kuthibitisha matendo yenu yaendane na vijana wa sasa,mawazo yenu yaendane na vijana wa sasa,fikra na issues mtakazo simamia zifananne na ziwakilishe asilimia 60 ama 70 ya watu wa nchi hii ambao ni VIJANA,msiishi kama waliotangulia hatutarajii na nyie kuiendesha CCM kwa mfumo wa NIDHAMU YA WOGA,ama mfumo wa kiuchaguzi uchaguzi jambo ambalo limekiumiza chama chetu kwa kiwango kikubwa January IDARA YAKO INAITWA IDARA YA SIASA NA MAMBO YA NJE alikukabidhi majukumu alijikita mambo ya nje na kuacha fuction ya siasa.


  CC na Sekretariet huu ni wakati wa kuisimamia SEREKALI ili itimize matarajio ya watanzania wengi,mnawajibu wa kuhakikisha mkataba wetu na watanzania ambao ni ilani ya uchaguzi inasimamiwa na inatekelezwa umefika wakati sasa wa chama kuwa kiranja mkuu wa serekali kwani tuloshinda ni ccm na serekali ni AGENT wa chama kutekeleza yale ambayo tuliwaahidi watanzania,its a high time muwe na utaratibu wa ku evaluate serekali na msisite kumshauri RAIS kumwambia hapa waziri flani hatekelezi wajaibu wake NEC iwe sehemu ya kuevaluate perfomance ya serekali kila QTR mfumo wa utendaji usiwe wa KI IYENA IYENA the world has changed na Variables zimebadilika sana,CC lazima iwe THINK TANK chama na si vikao vya kuchuja wagombea na kupitisha yale ambayo mwenyekiti anataka ama anashauri,lazima dhana ya kuhoji ichukue nafasi chama lazima kikemee pale serekali inapokosea msisite kuiambia serekali hili hapana halikuwa sehemu ya AHADI zetu LAZIMA kila jambo chama kiwe na uhakika serekali inapotaka kutekeleza imejiandaa kulitekeleza tusikosee ku hanlde issue kama tulivyokosea ku HANDLE issue ya katiba, na hapa nipongeze uamuzi wa kufuta HATI ya DHARURA ktk sheria hii inayohusu mchakato wa katiba.


  Chama kina tatizo kubwa la COMMUNICATION STRATEGY we hope JANUARY na NAPE mtabadili mfumo wetu wa kujibu mambo kwa mzaha na kejeli ma na mazoea muubadili ili HOJA ZIJIBIWE KWA HOJA, NAPE usirudie wala kufanya makosa ya kuwatumia watu wasio kuwa na HESHIMA kwenda ktk PUBLIC kujibu hoja yoyte inayohitaji THINKING, usiruhusu jambo litakalo haribu heshima ya chama kwa hoja tu MBONA WAO WANATUZOMEA NA SISI TUKUSANYE WATOTO WAKAZOMEE ,now CCM must act obave diry politics bcs dhamana ya nchii hii ipo mikononi mwetu si lazima kujibu tusi kwa tusi.


  CC na Sekretariet,mnajukumu la kuibana serekali na kuisimamia kuhakiksha uchumi unakua,ajira zinapatikana,mfumuko wa bei unatafutiwa njia za kuudhibiti,mawaziri wanafanya kazi na kutoka LIKIZO,wanasimamia majukumu yao na kufanya maamuzi magumu bila kusubiri kila JAMBO mpaka RAIS alitolee majibu,lazima kuwepo PERFOMANCE APPRISSAL system ambayo chama kitatumia kupima utendaji wa mawakala wake ambao ni serekali,leo bei ya mafuta imepanda,vyakula vimepanda,thamani ya shilingi inashuka,maisha yanakuwa magumu kwa watanzania wengi,sekta ya elimu inachangamoto nyingi za kisera,na kimfumo,chama kinahitaji WELEDI katika kusimamia serekali na hilo ni jukumu ambalo lazima mlifanye.


  Mnawajibu wa kusimamia PARTY COCUS ili bunge litumike katika ubora wake na wabunge wetu muwanoe ili kukidhi standards za kusimamia hoja na ilani ya chama.


  Nidhamu hasa kwa watendaji katika ngazi za wilaya na mikoa ni wajibu wenu kuhakikisha huko chini tatizo la RUSHWA ndani ya mfumo mzima wa chama linakwisha vijana wengi wanashindwa kukipenda chama chetu kwa kuwa huko chini kuna MIUNGU WATU,ni lazima CONCEPT ya utumishi ichukue nafasi ili wenyeviti wetu na makatibu wetu wasiwe wafalme wasimamie COUNCIOUL ili zitekeleze ilani ya uchaguzi kwani HUO NDIO MKATABA WETU NA WATANZANIA.


  Mwisho niwaombe CCM IMEUMIA SANA KWA POLITICS ZA CHARACTER ASSASINATION ,POLITICS ZA PERSONALITIES na kuacha kusimamia mambo ya msingi yanayowaumiza watanzania wengi,RUSHWA,(UFISADI),Tatizo la UADILIFU,UKOSEFU WA UZALENDO,ni udhaifu wetu wa kutosimamia MAADILI YA VIONGOZI na hasa tulipofuta AZIMIO LA ARUSHA,hatuna GUIDELINE juu ya maadili ya VIONGOZI na wanachama,umefika wakati wa chama kulitazama upya AZIMIO LA ARUSHA ambalo tuliamua kulifuta na kulizika chama kiamue kulitazama tena kulirudisha pia kufanya mabadiliko pale tunapoona linahitaji,but MSINGI wa azimio la arusha TUNAUHITAJI TENA.


  Mwigulu una mzigo mkubwa wa ku reforme mfumo wetu wa uchumi ndani ya chama ni wajibu wako kupitia idara yako kuzifanyia audit mali za ccm ili ktk ngazi za wilaya,mikoa,kata,na mashina tuwe na uwezo wa kiuchumi kuondokana na tabia ya kutegemea wafadhili na wafanyabiashara mawilayani na mikoani ili kuwapa uwezo watendaji wetu na viongozi kufanya maamuzi yanayohusu mustakabali wa chama chetu.


  Politics ni uchumi if we are weak economically na sisi kutegemea RUZUKU CCM tutakuwa na hali mbaya ni wajibu wako kufufua miradi iliyowahi kufa na kuisimamia kiukamilifu ,tunaviwanja vingi ni wakati wa kuanzisha Strategic ptnership na mashirika kama NHC na mengine ili kuwekeza ktk real estate, ALL IN ALL LAZIMA MZEE UPAMBANE . ALL THE BEST


  Niwatakie kila la kheri ktika utekelezaji wenu wa majukumu na mfahamu kuwa matarajio ya wana ccm ni kubwa sana ninawaombea kwa mungu kila la kheri MUNGU IBARIKI TANZANIA.MUNGU IBARIKI CC
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Mchokozi wewe Bashe
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Bado tunawatazama tuu hatuna imani na ninyi!
   
 4. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  kwa character assassination anamaanisha wasije kumsulubu RA.?
   
 5. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Waraka umekaa kichaguzi uchaguzi.
   
 6. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  RA ameshasulubiwa, anamtetea JK na wengine, maana Mtanzania lilishaanza jana na leo kumtaja na yeye ni fisadi aondoke. Kazi kubwa.
  Ila jamani mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni, Bashe ameandika vizuri na hii naona kaandika haraka haraka kutoka kichwani, maana yake akitulia anaweza kuandika hata ripoti nzuri si kama ile yenye mambo ya kusema JF imeanzishwa na watu wa Chadema, japo ina mambo mazuri pia. Bashe ni hazina nzuri akipewa nafasi na akiachana na mabosi wake, umri unamruhusu
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..halafu Bashe si alikiri kwamba anafadhiliwa na Rostam Azizi?
   
 8. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huu waraka itakuwa ameuandika RA na kumpa house boy wake Bashe aupeleke NEC.
   
 9. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Well said Bashe, lakini too late now.. mmeharibu mpaka mmepitiliza. CCM ni kama kansa ambayo iko stage ya mwisho. Mkishinda uchaguzi ujao mtashinda kwa kuiba kama kawaida yenu, ila kwa strategy ya kuchapa kazi ili Watanzania wawakubali inahitaji zaidi ya miaka mingine mingi ili mrudi kwenye bongo za watanzania, especially kwa tabaka la watu wenye uelewa wa mambo mliofisadi
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu Bashe bado anauchungu jinsi Ridhwani na timu yake walivyomfanyia mpaka jina lake likakatwa kwenye kugombea ubunge eti hakuwa Raia wa Bongo; ccm kwa mizengwe ndio wenyewe!! Sasa nadhani watampoza kwa kumpa uDC kuziba kule alikoacha Nape.
   
 11. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lugha lugha.......Lugha jamani. Sasa kwani huyu bwana asitumie lugha moja straight kwa kuzingatia ufasaha wa lugha husika. Sasa mara kiingereza mara kiswahili, mara vifupisho ambavyo havijulikali kimataifa. Ah mimi hili limenikera sana hata nikaacha kuzingatia maudhui ya waraka wake.

  Lakini ujumbe ni kwamba tuwe mfano mzuri wa matumizi sahihi ya lugha yeyote tunakayoamua kutumia kufikisha ujumbe
   
 12. J

  Joblube JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bashe naunga mkono baadha ya uliyosema na uchambuzi mzuri ila umesahau serikalini kumewekwa watendaji wengi wabovu lazima kama ni mageuzi ya kweli waingie kwenye viongozi wabovu serikalini wangolewe ambao ni wengi sina haja ya kuwataja
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..hii dhana itazaa ufisadi mwingine.

  ..NHC ni shirika la umma, muachane na mawazo ya kizamani ya mfumo wa chama kimoja.

  ..pia hivyo viwanja mnavyoringia mnapaswa kuvikabidhi serikalini kwasababu ni mali ya umma.
   
 14. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145

  Nami nilitaka kunukuu kipande hicho hicho... Je, anaongelea viwanja vya michezo walivyopora au viwanja vilivyopimwa kwa ajili ya makazi enzi zile za chama kimoja?!!
   
 15. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #15
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  unatapa tapa wewe
  mwisho wako umefika
   
 16. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kumbe ndo maana ccm ni mavuvuzela, kijana kama huyu ambaye kiingereza hajui na kiswahili nacho wasiwasi, anaandika kama vile anapiga soga ndo uvccm wanamtegemea? bwana bashe nenda cdm usiogope ukanolewe na vijana waliokomaa kama kama akina david shilinde, wenje , lema nk. ni vema ukamkimbia rostam mapema kabla hajashindwa kukulipa mshahara, kwa nini?

  1. vodacom imeuzwa kwa vodafone waingereza hawawezi kurithi utapeli wa vodacom ya makaburu wakaendelea kumkumbatia bosi wako fisadi namba wani rostam
  2. makongoro nyerere ameshamwambia kikwete asilipe hata shilingi moja ya dowan kati ya zile 94bn, otherwise jk atafukuzwa kwenye chama cha babake
  3. zitto anataka waliokula stimulus paackage wakamatwe, bosi wako atatumia chapaa kibao kuzima ili asikamatwe, inasemekana ili asihusishwe na kagoda alitoa chapaa ya kueleweka, muulize rose mwakitangwe kilimchotoa kwenye hiyo nafasi uliyorithi, ukwasi!
  4. akina sita na wenzake wana nguvu za kueleweka baada ya rostam kufukuzwa cc
  5. nape amekamata ukamanda hakuna tena ATm mashine za kumwaga fedaha kwa bosi wako kama epa, stimulus package nk
  6. lowasa anapamabana asifukuzwe kwenye chama hana nafasi tena ya kumtetea bosi wako
  7. rostam ndiye adui namba moja wa watanzania wote, kila kona anajulikana kuwa ndiye kisababishi cha matatizo lukuki ya watanzania
  8. kitendo cha kudai kuwa babu wa loliondo hatibu, kimezidi kumjengee matatizo, watz waliopona kwa dawa za babu wanajua wazi kuwa rostam anafurahi umskini na matatizo wa tz na angependa yaendelee ili afaidike
  kwa kuwa wewe ni kbaraka wa mtu huyu basi wewe huna sifa ya kushauri chochote katika nchi yetu, wahi kweu somalia,kudadeki!!!!

  1
   
 17. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyu si walimfurumisha kwa kutokuwa Raia? Ameshakuwa raia?
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..hapa napo ni sawa na kuwategemea Januari na Nape wafanye kazi za Raisi.

  ..kama mawaziri wako LIKIZO kama anavyodai Bashe, basi anayewapaswa kuwashtua ni Waziri Mkuu akisimamiwa na Raisi.

  ..sasa inawezekana Raisi mwenyewe yupoyupo, au anabangaiza, na ndiyo maana mawaziri nao hawafanyi kazi zao.
   
 19. b

  bluhende Member

  #19
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hongera Bashe, tatizo maneno yako hayawiani na matendo. Watz tumekosa uzalendo tumebaki kuwa wanafiki, hivi 'character assasination' na siasa za 'personality' ndio kuchaguliwa kwa JK, kupigwa chini kwa Sitta au Chenge kuwa M/kiti Kamati ya Maadili? Give me a break- Hatudanganyiki
   
 20. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
  house boy ni wewe mwenye wivu na chuki, mtu mzima akili finyu
   
Loading...