Waraka wa CHADEMA-UK kwa Rais, Mabalozi, Taasisi za Haki za Binadamu


MAPUMA MIYOGA

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2013
Messages
3,469
Likes
1,728
Points
280
MAPUMA MIYOGA

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2013
3,469 1,728 280
TAMKO RASMI CHADEMA UK

CHADEMA UK awali ya yote tunapenda kutoa pole kwa waTanzania na wapenzi wa CHADEMA waliopatwa na kukutwa na janga la kurushwa kwa bomu kwenye mkutano wa CHADEMA wa kuhitimisha shughuli za kampeni za uchaguzi wa madiwani huko Arusha. Tunatuma salam zetu kuwafariji wale wote walioguswa kwa namna moja ama nyingine katika jambo hili.

Kama waTanzania, tunapinga vikali na kukemea kitendo hichi kwa nguvu zetu zote. Mazingira na jinsi kitendo hichi kilivyotekelezwa tuna kila sababu ya kuamini kwamba hili ni tendo la kigaidi. Na kwa sababu hiyo ni jukumu la mamlaka (yaani serikali) na vyombo vyake vya dola kulinda na kuepusha matendo ya kigaidi kama haya.

CHADEMA ni chama kinachoongozwa na watu makini (effective and responsible leaders) wenye kuheshimu mamlaka ya sheria za nchi. Wanachama wa CHADEMA wamekuwa watulivu siku zote wakifuata na kuheshimu sheria kama chama kinavyowaelekeza. Hata pamoja na kwamba yamekuwepo matendo mengi sana yanayoashiria kuukandamiza upinzani (hasa CHADEMA) kwa uwazi kabisa, viongozi wamekuwa mstari wa


mbele kuwatuliza wananchi na kuwataka waendelee kuwa na imani na mamlaka. Hii ni dhahiri kwamba imesaidia kuepusha vurugu kusambaa na kuiingiza nchi kwenye balaa la vita baina yetu sisi wenyewe.

Japokuwa chama na hasa sisi wanaCHADEMA UK tutaendelea kutafuta mbinu nyingine katika kupambana na uonevu huu kwa njia ya amani (baadhi kama tulivyoanisha hapo chini), tunapenda pia kuitahadharisha mamlaka kutokujisahau (against complacency) kwamba kama hatua za msingi hazitachukuliwa uvumilivu wa waTanzania utafikia kikomo. Hili ni KARIPIO KALI kwa mamlaka zinazohusika na kwa sababu hiyo tumechukua hatua zifuatazo:

1. Tumetuma barua ya rasmi ya ushauri kwa kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano mh. J.M Kikwete. Pamoja na mambo mengine tumetoa maoni yetu kama ifuatavyo:
Usalama wa taifa ufanyiwe marekebisho makubwa: Tanzania Intelligence Services (TIS) inahitaji kufanyiwa marekebisho na ikibidi ivunjwe na kuwe na vikosi vifuatavyo:

  • Tanzania Secret Intelligence Services (TSIS): Hii iwe ni mamlaka ya kutafuata, kupata na kusimamia siri za kimataifa ikiwa ni katika kulinda nchi na mipaka yake. Kwa kushirikiana na vyombo mbali mbali TSIS itakuwa na jukumu la kupata siri za kijeshi, ugaidi wa kimataifa, n.k.
  • Tanzania Serious Organised Crime Unit (TSOCU): Kitengo hiki kiwe na wajuzi wa maswala mbali mbali ikiwahusisha Polisi maalumu, wataalamu wa computer na mawasiliano, na wajuzi wenye uelewa wa kuchunguza matendo ya kijangili. Kazi kubwa ya kitengo hiki iwe ni kuchunguza na kuwakamata wahalifu wote wanaofanya matendo ya kijangili ikiwa ni pamoja na madawa ya kulevya; wizi ndani ya mashirika na taasisi za serikali unaofanywa na kupangwa na wafanyakazi kwa kushirikiana na watu mbali mbali; Mauaji; n.k. Hata hivyo kazi nyingine muhimu ya TSOCU iwe ni, kwa kutumia njia za kisasa kabisa, kugundua mapema na kuzuia uhalifu kutokea. Kama wakipatikana wana usalama wenye uwezo, kitengo hiki kitaepusha upotevu wa maisha ya watu wasio na hatia kwa kiwango cha juu. Cha muhimu ni kuhakikisha kitengo hiki kinapatiwa vifaa na mafunzo ya kisasa kabisa ili kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuvipa uhuru vyombo hivi vya usalama kutoka kwa wansiasa. Kwa mfano ilivyo sasa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ndiyo wenyeviti wa kamati za usalama za wilaya na mikoa. Hivi vyote ni vyeo (appointement) vya kisiasa. Kwa hivyo kama CHADEMA hatuamini kabisa kwamba vyombo hivi vinaweza kusimamia maswala ya kiusalama kwa haki bila upendeleo wa kisiasa.

Kazi za jeshi la polisi ziwe za kufanya kazi karibu kabisa na wananchi katika kusimamia sheria, kulinda wananchi na mali zao, kuzuia uhalifu, na kuwapunguzia wananchi hofu ya kufanyiwa vitendo vya kihalifu ili kumfanya kila mwananchi ajisikie huru. Hii itakuwa ni kuhakikisha jamii inaishi kwa kufuata sheria na taratibu (maintaining public order), kupambana na wahalifu na kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama.

Hata hivyo jeshi hilo linahitaji kufanyiwa mabadiliko makubwa. Dosari kubwa zinaonekana dhahiri kuanzia kwenye ngazi za mkuu wa jeshi hilo nchini (IGP), kwenda chini kwenye ngazi za wakuu wa polisi wa mikoa (RPCs), wakuu wa vitu (OCSs) na polisi wa kawaida. Kwa mfano mauaji yanapotokea, hakuna uwajibikaji (accountability).

Kwa sababu hiyo kuna umuhimu wa kuzipa nguvu kamati ya ulinzi na usalama ya bunge ili ziweze kuwaita na kuwahoji wakuu wa usalama ili wajieleze mbele ya kamati pale inapohitajika.

2. Tumeandika barua kwenda kwenye ofisi za haki za binadamu (International Human Rights Office) hapa London. Nia na madhumuni ni kuwapa picha ya vitendo vya kinyama vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa manufaa yao binafsi.

3. Tumetuma barua kwenye balozi zaidi ya nane za nchi mbali mbali tukiyaeleza na kuyaanisha matukio yanayoendelea ndani ya nchi huku viongozi wetu wakikaa kimya.

4. Tumevitaarifu vyombo mbali mbali vya habari kama vile BBC, RT Television na Aljazeer kuhusu hali na mwelekeo wa kisiasa Tanzania ambao umeanza kuchukua sura mpya.

Kwa nguvu zote tutaendelea kuueleza ulimwengu na kukaripia uhalifu huu tunaofanyiwa ndani ya nchi. Ni muhimu kwa waTanzania kufahamu kwamba upinzani siyo dhambi . Upinzani ni mawazo mbadala.

Kwa wana-CHADEMA wenzetu
Tanzania ni nchi yetu tunayoipenda na kuithamini. Tunaamini kabisa kwamba amani na utulivu ni vitu muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Sote tunatamani kuwarithisha watoto wetu (next generation) nchi itakayowapa fursa ya kusonga mbele. Hata hivyo amani tunayoiongelea hapa si amani ambayo tumeaminishwa na serikali ya ccm kwa miaka mingi. Amani tunayoisema ni amani ya kweli, amani inayoheshimu utu, amani inayompa fursa kila mwananchi kufanya shuughuli zake bila kuogopa ili mradi anafuata sheria za nchi.

Ni dhahiri kwamba wengi tumechoshwa na uongozi mbovu ambao tumeifikisha nchi hii hapa tulipo leo. Wengine hata tunashangaa kwamba hawa hawa ambao wamekuwa madarakani kwa miaka zaidi ya 50 bila kuleta maendeleo yeyote, leo hii wanaonekana kutaka kung'ang'ania madaraka kwa gharama zozote zile hata kwa kumwaga damu. Watu hawa wanaonesha uchu na jazba ya hali ya juu lakini wakiambiwa wajieleze ni nini wamekifanya kwa miaka 50 hawana jibu. Ikiwa kama haitoshi, wengi tunaona kwamba sasa imetosha, tumeshavumilia vya kutosha (enough is enough).

Pamoja na hayo tunawaomba tuendelee kutetea bila kuchoka juhudi za kulikomboa taifa letu. Endeleeni kuwaelimisha na wengine ambao bado wanahitaji kufumbuka macho. Ukiona hali inafikia hapa ilikofikia, kwa wale wanaojua kusoma nyakati, watajua kwamba ushindi umekaribia.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Nchi Yetu.

17/06/2013Source: Waraka wa CHADEMA-UK kwa Rais, Mabalozi, Taasisi za Haki za Binadamu - wavuti.com
 
G

gem08

Member
Joined
Jun 11, 2012
Messages
40
Likes
1
Points
0
G

gem08

Member
Joined Jun 11, 2012
40 1 0
Safi sana. Hii ni hatua madhubuti dhidi ya matendo ya kigaidi yanayofanywa na baadhi ya watu. Serious issues need serious people and serious actions
 
MVUMBUZI

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Messages
5,076
Likes
808
Points
280
MVUMBUZI

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2011
5,076 808 280
Hongereni vijana kwa kazi nzuri hii message ambayo CCM waliituma jumamosi kwa waTZ imefika. CCM wangekuwa wanaume wangemtuma Nape aje na Mchemba kuliko kutumia Polisi kufanya ugaidi.
 
Medical Dictionary

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Messages
1,053
Likes
7
Points
135
Medical Dictionary

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2012
1,053 7 135
sisi tuliopo nchini tunafarijika sana kuona mnatusapoti,tuunganishe nguvu kuikomboa nchi yetu
 
I

inside-man

Member
Joined
Apr 11, 2013
Messages
12
Likes
0
Points
0
I

inside-man

Member
Joined Apr 11, 2013
12 0 0
Sasa naona magamba wameshikwa pabaya. Viongozi kwenda kujichekesha chekesha wakidanganya eti hii nchi ina amani hii ndiyo dawa yao. Kazi nzuri makamanda UK
 
Chilisosi

Chilisosi

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2008
Messages
3,055
Likes
18
Points
135
Chilisosi

Chilisosi

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2008
3,055 18 135
Naona matamko bila muongozo yameanza kabla hata ya tamko la makao makuu?
Hii ndio tatizo la kuwa na akili nyingi zaidi ya kichwa

Haya wahi kupiga boksi kabla hujachelewa !
 
Wile GAMBA

Wile GAMBA

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2011
Messages
1,809
Likes
4
Points
0
Wile GAMBA

Wile GAMBA

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2011
1,809 4 0
Naona ndiyo kwnza game linaanza, akina Nape wamejisahau sana wanadhani nchi hiii ni yao.
 
P

PERFECT

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2011
Messages
361
Likes
2
Points
0
P

PERFECT

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2011
361 2 0
Well done makamanda, kazeni buti kuijulisha Dunia, mauwaji ya raia wasiyo na hatia.
 
R

Rayman ProphetMcRay

Senior Member
Joined
Dec 8, 2012
Messages
179
Likes
0
Points
0
R

Rayman ProphetMcRay

Senior Member
Joined Dec 8, 2012
179 0 0
Hongereni makamanda dunia lazma ijue unyama unaofanywa na serikal ya ccm.....!
 
I

inside-man

Member
Joined
Apr 11, 2013
Messages
12
Likes
0
Points
0
I

inside-man

Member
Joined Apr 11, 2013
12 0 0
Naona matamko bila muongozo yameanza kabla hata ya tamko la makao makuu?
Hii ndio tatizo la kuwa na akili nyingi zaidi ya kichwa

Haya wahi kupiga boksi kabla hujachelewa !
Watu wanapigania nchi yao.

By the way wewe umesharuhusiwa kutoka hospitali?
 
bily

bily

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Messages
8,054
Likes
4,147
Points
280
bily

bily

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2012
8,054 4,147 280
well done job makamanda hakika kama ni amani na uvumilivu hili sasa basi imetosha kwani uvumilivu una mwisho wake
 
K

kinai

Senior Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
159
Likes
1
Points
0
Age
51
K

kinai

Senior Member
Joined Oct 13, 2012
159 1 0
Ndio maana wanapigania uraia wa nchi mbili ili wakishaharibu Tanzania yetu wao waende wakaishi nchi nyingine. Hawafikirii Watanzania wasioweza hata kulipa ada ya sh 20.000 mashuleni. Tukatae wazo la uraia wa nchi mbili kwasababu viongozi wetu na wapambe wao wanataka kujipatia hifadhi baada ya kutuachia majanga nchini. CDM kazeni buti msihangaike na tume za kina chagonja na mngulu kwani hao wote lao moja. Tena hili suala lazima mlishikie bango mpaka kieleweke maana ccm wanaona Watanzania wanaachaga mambo yaishe kirahisi kila baada ya matukio kama haya. Toeni funzo kwa ccm sasa na ikiwezekana piteni nchi nzima kuwaeleza wananchi ukweli. Wameua mwangosi, wamemtesa kibanda na dr ulimboka wanaona watz wapole hawachukui hatua. TOENI FUNZO KWA CCM WAKOSE KABISA USINGIZI
 
BBJ

BBJ

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Messages
1,183
Likes
11
Points
135
BBJ

BBJ

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2011
1,183 11 135
Kazi nzuri Makamanda wenzangu.Umoja wetu utaleta ukombozi.
 
D

duchi

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Messages
1,766
Likes
3
Points
0
D

duchi

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2012
1,766 3 0
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.
 
kelao

kelao

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Messages
5,880
Likes
2,300
Points
280
Age
40
kelao

kelao

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2012
5,880 2,300 280
Tunawashukuru makamanda mlioko UK,muendelee kuwaweka uchi hawa mafisadi wtz popote mliko.mwisho wao hakika upo karibu.
 
N

Naytsory

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
2,116
Likes
553
Points
280
N

Naytsory

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
2,116 553 280
Ni vema wakaambatanisha na vielelezo, hasa katika nchi ambazo zina uhusiano wa karibu na Tanzania.
 
MAPUMA MIYOGA

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2013
Messages
3,469
Likes
1,728
Points
280
MAPUMA MIYOGA

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2013
3,469 1,728 280
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.
Mmeshaua na sasa mnasubiri 100m ya Lukuvi. Lakini nawaambieni yakuwa 'Usiue" nanyi ccm mmeua, ndivyo hivyo MUNGU atapimia hukumu yenu, nayo i karibu sana.
 

Forum statistics

Threads 1,275,212
Members 490,932
Posts 30,535,930