Waraka wa Bernard Membe kwa Askofu Mwamakula: Sitishiki, sitakaa kimya na kamwe sitaabudu mtu wala miungu wengine

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,908
“Niguse ninuke”

"Baba Askofu Emmaus Mwamakula!

Tumsifu Yesu Kristo!

Napenda nikushukuru sana kwa ujumbe mzito na wenye tija katika Taifa. Nikiri kwamba nami nimekuwa nakufuatilia sana kwa maoni na ushauri mbalimbali ambao umekuwa ukiutoa kwenye mitandao. Endelea kufanya hivyo! Nikiri pia kuwa nimekuwa nafuatiliwa, nazushiwa shutuma za hatari kama vile za uhaini, usaliti, ufisadi, uhujumu, kufanya kampeni ya Urais nk.

Nikuhakikishie hakuna hata chembe ya ukweli kuhusu yote hayo na ndiyo maana huoni na hutaona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi yangu. Labda wanichukulie hatua zingine! Nimepata vitisho mbalimbali kutoka kwenye Chama changu, makundi mbalimbali ya wachawi na Serikali vya kunifukuza, kuniloga, kunitupa Gerezani kana kwamba mimi ni mhalifu. Baba Askofu, kwa kuwa moyo wangu ni safi, na kwa kuwa sijatenda kosa lolote, SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE.

Ninakushukuru sana kwa ushauri na maneno ya busara uliyonipatia. Tusipotokea wachache wa kuyasema na kuyakemea mabaya Baba Askofu, nchi hii itaingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya tunayoyaona! Serikali ya Awamu ya tano imepewa ridhaa ya Uongozi na sisi wenyewe. Lakini leo sisi tunaonekana ni maadui wa Serikali na hakuna jema lililofanywa na awamu zilizopita. Ninawasikitikia washauri wanafiki na waoga wanaokaa kimya au kumshauri vibaya Rais wetu. Wanafiki wanaomlinganisha Rais wetu na Yesu na wanaomwomba Mungu amshukuru Rais wetu kwa yote anayoyafanya. Pamoja na makosa yote yaliyofanywa na Awamu zilizopita, Serikali na Viongozi hao walijitahidi kuheshimu Katiba, Uhuru, Sheria na Haki za binadamu. Huo ndiyo msingi wa Uongozi Bora Duniani.

Baba Askofu, usichoke kutushauri na kutupa moyo wa kuyatenda yale ambayo yatampendeza Mungu. Unifikishie salaam zangu kwa Maaskofu wote! Ubarikiwe sana Baba Askofu Mkuu Emmaus Bandikile Mwamakula na tuzidi kuombeana.

Bernard K. Membe. Mstaafu!"

NB: Waraka huo hapo juu kutoka kwa Mheshimiwa Membe (pichani), umenifikia leo kupitia nami nimeona niuweke hapa hasa ikizingatiwa kuwa ujumbe wangu wa awali kwake niliuweka hapa pia.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches)

-------

****UJUMBE WA ASKOFU MWAMAKULA ULIOJIBIWA NA BERNARD MEMBE****

UJUMBE MAHSUSI KWA MHESHIMIWA BERNARD MEMBE.

Mheshimiwa Bernard Membe!

Pokea salaam za upendo kutoka kwangu mimi niliye mdogo sana miongoni mwa Maaskofu wa Kanisa la Mungu hapa duniani nisimamaye katika zamu yangu sasa! Nimekuwa nikifuatilia kwa makini na kusikia mengi juu yako katika siku za hivi karibuni. Ninatambua kuwa wewe ni mwanasiasa na siasa ni uwanja wa hoja.

Hata hivyo, kwa mazingira yalivyo tumeshuhudia kauli nyingi kukuzunguka wewe ambazo wakati mwingine zinatia hofu na mashaka. Kauli zinazoashiria kuwa siasa za Tanzania zimeanza kuonyesha dalili za watu kuanza kukosa kuvumiliana hasa pale watu wengine wanapoonyesha muono tofauti wa mambo.

Ninapenda nikuhakikishie kuwa pamoja na ukimya wao, Maaskofu walio wengi katika Nchi hii wanafuatilia kwa karibu sana mambo yanayohusu nchi hii ambayo Mungu amewaweka kuwa watumishi na mawakili wa siri zake. Pengine utatiwa moyo kusikia kuwa mimi pamoja na Maaskofu, Wachungaji, na watu wengine wengi usiowajua tunakuombea na kulitaja jina lako mbele za Mungu wetu.

Tunapenda ifahamike kuwa kukuombea kwetu hakutufanyi sisi kuwa lazima tukubaliane na muono wako wa mambo kuhusiana na siasa za Nchi hii, la hasha! Bali tunakuombea kutokana na ukweli kuwa kwa mazingira yaliyopo sasa baadhi yetu tunahisi kuwa unaweza kujikuta unaishi katika maisha ya hofu na wasiwasi mkubwa.

Tunamuomba Mungu ili akupe utulivu moyoni na pia akupe ulinzi dhidi ya watu ambao wanaweza kutaka kukudhuru kutokana na wao kutokupenda misimamo na mitazamo yako. Kwa kuwa na washindani wako na wao pia watausoma ujumbe huu, tunawasihi sana wasije wakaingia katika mtego wa kugusa uhai wako. Lakini pia, na wewe uepuke kuingia katika mtego wa kutaka kuwadhuru washindani wako. Mungu wetu atahusika na mtu ye yote anayejipanga kumwaga damu ya mtu mwingine iwe yeye mwenyewe au kuwatumia watu wengine.

Tunapenda wanasiasa wote wafahamu kuwa Mungu anapotoa kibali kwa mtu, kibari hicho hakiwezi kuondolewa na mtu au mamlaka ye yote ya kidunia. Kupambana na mtu aliyepata kibali kwa Mungu ni sawa na kupambana na Mungu mwenyewe. Tunapenda ifahamike kuwa kama wapo watu ambao Mungu amewapa kibali, wewe ukipambana nao utakuwa unajisumbua bure. Lakini pia, kama wewe utakuwa umepata kibali kutoka kwa Mungu, basi wale watakaoinuka kupambana na wewe na wao watakuwa wanafukuza upepo!

Tunakemea mambo yote ya kutishana na kunyamazishana na hata kutaka kupotezana miongoni mwa wanasiasa iwe ni katika Vyama vya Upinzani au ndani ya Chama Tawala. Kiongozi ye yote atakayeasisi au kushiriki katika vikao au mikakati ya kutaka kumuua mtu mwingine kwa sababu za kisiasa na mambo mengine nje ya mfumo na mchakato wa ki-Mahakama atakuwa anajitoa mwenyewe katika kibari cha Mungu kwa kuwa damu ya mtu haiwezi kumwagika bure pasipo kupiga kelele!

Ninaomba ukipata nafasi uweze kutafakari kwa kina Zaburi 35.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula -
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
 
"Nikuhakikishie hakuna hata chembe ya ukweli kuhusu yote hayo na ndiyo maana huoni na hutaona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi yangu. Labda wanichukulie hatua zingine! Nimepata vitisho mbalimbali kutoka kwenye Chama changu, makundi mbalimbali ya wachawi na Serikali vya kunifukuza, kuniloga, kunitupa Gerezani kana kwamba mimi ni mhalifu. Baba Askofu, kwa kuwa moyo wangu ni safi, na kwa kuwa sijatenda kosa lolote, SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE."
 
"Nikuhakikishie hakuna hata chembe ya ukweli kuhusu yote hayo na ndiyo maana huoni na hutaona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi yangu. Labda wanichukulie hatua zingine! Nimepata vitisho mbalimbali kutoka kwenye Chama changu, makundi mbalimbali ya wachawi na Serikali vya kunifukuza, kuniloga, kunitupa Gerezani kana kwamba mimi ni mhalifu. Baba Askofu, kwa kuwa moyo wangu ni safi, na kwa kuwa sijatenda kosa lolote, SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE."

Kwa msisitizo zaidi...
 
Pesa za libya zirudishwe serkalini zijenge reli
Yeye anasema "Nikuhakikishie hakuna hata chembe ya ukweli kuhusu yote hayo na ndiyo maana huoni na hutaona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi yangu. Labda wanichukulie hatua zingine! Nimepata vitisho mbalimbali kutoka kwenye Chama changu, makundi mbalimbali ya wachawi na Serikali vya kunifukuza, kuniloga, kunitupa Gerezani kana kwamba mimi ni mhalifu. Baba Askofu, kwa kuwa moyo wangu ni safi, na kwa kuwa sijatenda kosa lolote, SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE."
 
Kwa mtindo wa utendaji wa utawala huu wa awamu ya tano, tusije shangaa "wakamzushia" huyo Askofu na Membe wake, kuwa wote siyo raia wa nchi hii!
kweli kabisa, lakini pia naona wewe uraia wako utahojiwa mkuu hivi karibu
 
Back
Top Bottom