Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Felixonfellix, Jun 24, 2012.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Waheshimiwa Wananchi wenzangu,

  Amani iwe kwenu,

  Kwa kipindi cha wiki nzima kumekuwepo na mjadala mkali bungeni, kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na katika taifa kwa ujumla juu ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/13 sanjari na yaliyojiri kutokana na kauli niliyotoa bungeni juu ya udhaifu wa Rais katika usimamizi wa maandalizi na utekelezaji wa bajeti pamoja na mipango muhimu ya maendeleo. Ukweli ni uhuru!.

  Aidha, kupitishwa kwa Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 na Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 bila marekebisho yoyote ya msingi pamoja na michango mingi ya wabunge ya kukosoa kumedhihirisha kile nilicho tahadharisha tangu awali kwamba; kwa kuwa udhaifu wa kikatiba umetoa nguvu kubwa kwa Rais juu ya bajeti na uendeshaji wa nchi, udhaifu wa Rais una athiri maisha ya wananchi. Ukweli ni Uhuru!.

  Katika mazingira haya, udhaifu wa rais na uzembe wa bunge unapandikiza migogoro kati ya wananchi na serikali kutokana ufisadi na masuala ya maendeleo kutopewa kipaumbele cha kutosha zaidi ya matumizi ya kawaida lakini pia inachochea pia migomo baridi ya watumishi wa umma hususun madaktari, walimu na askari kutokana pia na madai yao ya muda mrefu kutokuzingatiwa kwenye bajeti. Ukweli ni Uhuru!.

  Kadhalika udhaifu wa kanuni za Kudumu za Bunge umefanya wabunge kuwekewa mipaka kwa mujibu wa kanuni 97 (2) ya kuchangia mjadala kuhusu hotuba ya bajeti kwa kuchangia tu mambo ya ujumla yanayohusiana na hali ya uchumi wa nchi na kwamba mbunge yoyote haruhusiwi kupendekeza mabadiliko katika makadirio ya mapato na matumizi ya serikali. Ukweli ni Uhuru!.

  Pia, katiba imempa mamlaka makubwa Rais juu ya Bunge kwa kuwa Bunge likikataa bajeti ya serikali kwa mujibu wa Ibara ya 90 (2) (b) moja kwa moja Rais analivunja bunge suala ambalo huwapa hofu wabunge wengi hususani wa chama kinachotawala na kuwafanya wapige kura ya NDIO hata kama waliikosoa bajeti husika. Hivyo, udhaifu wa bunge unachangiwa na ukweli kwamba katiba imeweka nguvu kubwa kwa Rais katika kuvunja bunge linapokataa bajeti wakati huo huo kanuni zimekataza wabunge kupendekeza mabadiliko katika bajeti; kwa hivyo wabunge hawana uwezo wa kubadilisha na wakati huo huo wakikataa bunge linavunjwa, katika mazingira haya udhaifu wa Rais wa kushindwa kutumia nguvu hizo za kikatiba una madhara makubwa sana kwa nchi na maisha ya wananchi. Ukweli ni Uhuru!.

  Kwa mantiki hiyo, katika mchakato wa katiba mpya ni muhimu kwa wananchi kutoa maoni ya kuwezesha ukuu na uhuru wa bunge katika kuisimamia serikali kwenye mchakato wa bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi. Wakati katiba mpya ikisubiriwa, ni muhimu kwa marekebisho ya haraka kufanyika katika kanuni za kudumu za bunge hususani sehemu ya tisa inayohusu utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha kuanzia kanuni ya 94 mpaka kanuni ya 107 ili kuongeza nguvu za bunge katika kuishauri na kuisimamia serikali kwa mujibu wa madaraka ya bunge ya ibara ya 63 (2) na (3) ya katiba ya sasa. Katika muktadha huo, nimeanza kufanya uchambuzi ili kuwasilisha bungeni mapendekezo ya mabadiliko ya kanuni. Ukweli ni Uhuru!.

  Hata hivyo, hata kwa kanuni zilizopo sasa udhaifu wa bunge unaongezeka kutokana na maamuzi ya kizembe mathalani ya kutozingatia matakwa ya kanuni za bunge, mfano Kanuni ya 94 inalitaka bunge ili kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba kwa kukaa kama kamati ya mipango katika mkutano wake wa mwezi Februari ili kujadili na kushauri kuhusu mapendezo ya mpango wa taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali kwa mwaka wa fedha unaofuata, kanuni ambayo toka niingie bungeni haijawahi kutekelezwa kwa wakati hata mara moja pamoja na kuwakumbusha wanaohusika kusimamia kanuni. Ukweli ni Uhuru!.

  Mwaka huu udhaifu umekuwa mkubwa zaidi kwa Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013 sanjari na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 tarehe 18 Juni 2012 na kupitishwa siku moja tarehe 22 Juni 2012 hali ambayo imechangia katika kufanya bajeti ya nchi isizingatie kwa ukamilfu mpango wa taifa wa miaka mitano. Ukweli ni Uhuru!.

  Nashukuru kwamba Spika wa Bunge Anna Makinda amekiri bungeni tarehe 20 Juni 2012 kwamba kulikuwa na udhaifu wa miaka mingi wa kutozingatia kanuni ya 106 ambayo inalitaka bunge kujadili muswada wa sheria ya fedha mwishoni baada ya bunge kukamilisha kazi ya kupitisha muswada wa fedha za matumizi ili kuiwezesha serikali kuongeza vyanzo vya mapato kama wabunge tulivyopendekeza mwaka 2011 na pendekezo hilo kurudiwa tena na kamati ya fedha na uchumi tarehe 18 Juni 2012. Ukweli ni Uhuru!.

  Izingatiwe kuwa iwapo sheria ya fedha ingepitishwa tarehe 22 Juni 2012 kama ilivyokuwa imepangwa awali athari zake zingekuwa kubwa kwa kuwa udhaifu wa kikatiba umetoa nguvu kubwa kwa Rais juu ya utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha kwa mujibu wa ibara ya 99 (1) kwa kuweka masharti kwamba bunge halitashughulikia sehemu kubwa ya masuala ya fedha isipokuwa kama Rais amependekeza kwamba jambo hilo lishughulikiwe na bunge na pendekezo hilo la Rais liwe limewasilishwa kwenye bunge na waziri. Hivyo, michango na mapendekezo ya wabunge bila Rais mwenyewe kupendekeza isingeliwezesha bunge kufanya mabadiliko ya kupanua wigo wa mapato kwa kuwa kwa kuwa mujibu wa ibara 99 (2) (a) (i) udhaifu wa bunge ni pamoja na kukatazwa kutoza kodi au kuongeza kodi. Ukweli ni Uhuru!.

  Hivyo, Kamati ya Fedha na Uchumi itumie vizuri mwanya wa ibara ya 99 (3) kurejea maoni yake, ya kambi rasmi ya upinzani bungeni na michango ya wabunge ya mkutano wanne wa Bunge mwaka 2011 na Mkutano wa nane wa Bunge mwaka 2012 na kufanya marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha kwa kumshauri Waziri. Ukweli ni Uhuru!.

  Aidha, ili kuondoa udhaifu uliopo Rais Kikwete mwenyewe asome kumbukumbu rasmi za bunge (Hansard) za tarehe 18 Juni mpaka 22 Juni 2012 na kuliongoza baraza la mawaziri kumwezesha Waziri wa Fedha ya 86 (10) kuwasilisha muswada wa sheria uliochapishwa upya ukiwa na marekebisho au mabadiliko yanayopaswa kufanyika yenye kulenga kupunguza kodi katika bidhaa zenye kuchangia mfumuko wa bei na kupanua wigo wa mapato kwa kuongeza kodi kwenye vyanzo mbadala tulivyovieleza bungeni. Ukweli ni Uhuru!.

  Izingatiwe kuwa nilipotolewa bungeni tarehe 19 Juni 2012 nilieleza kwa ufupi nilichosema bungeni na nilichotarajia kusema na kuahidi kwamba nitatoa tamko kamili baadaye; baada ya kujipa muda wa kutafakari nimefikia uamuzi wa kutoa tamko husika wakati bunge litakapoelekea kujadili utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012 na makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2012/2013; ambapo pamoja na masuala mengine nitaeleza hatua ambazo Rais anapaswa kuchukua kuwezesha ahadi alizotoa kwa watanzania kuweza kutekelezwa na serikali. Ukweli ni Uhuru!.

  Kwa sasa niwashukuru wananchi wa Ubungo, wakazi wa mkoa wa Dar es salaam na watanzania kwa ujumla walionielewa na kuniunga mkono kupitia maoni yao kwenye mitandao ya kijamii, simu za mkononi na katika vyombo vya habari. Nawashukuru pia viongozi wa dini, chama na asasi mbalimbali nje na ndani ya serikali walionipa moyo wa kuendelea kusimamia ukweli na kuacha unafiki ili kusimamia uwajibikaji wa viongozi kwa maendeleo ya taifa. Ukweli ni Uhuru!.

  Nashukuru pia kwa mchango wa walinipinga na kunikosoa kutokana na kauli niliyotoa juu ya udhaifu wa Rais Kikwete, wapo walioeleza kuwa ilitokana na jazba na wengine wameeleza kuwa ningetumia lugha ya diplomasia kufikisha ujumbe ili kutodhalilisha taasisi ya urais na kwa kuzingatia utamaduni wetu wa heshima kwa wakubwa na wapo wachache waliosema kwamba ni matusi kutamka ‘udhaifu wa Rais'. Ukweli ni Uhuru!.

  Wakati mjadala huu ukiendelea ni rai yangu kwamba rejea ifanyike katika mchango wangu wa tarehe 5 Julai 2011 wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Rais kwa mwaka 2011/2012 na rejea kamili pia ifanyike kwenye mchango wangu wa tarehe 19 Juni 201; na ieleweke kwamba naheshimu taasisi ya urais na umri, naamini katika matumizi ya lugha ya kidiplomasia, hata hivyo nilitafakari na kuamua kuusema ukweli kwa lugha ya moja kwa moja ili ujumbe ufike kwa mamlaka zote zinazohusika na wauchukulie kwa uzito tofauti ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita. Ukweli ni uhuru!.

  Niliamini, naamini na nitaendelea kuamini kwamba kutamka neno ‘udhaifu wa Rais' sio kumtukana Rais na wala sio kulitumia jina la Rais kwa dhihaka; hata hivyo kwa kuwa pamekuwepo na mwelekeo wa propaganda za kudai kuwa kauli hiyo ni matusi na kwa kuwa chanzo cha propaganda hizo ni udhaifu uliofanywa na Naibu Spika Job Ndugai bungeni wa kunihukumu kwa kutumia kanuni tofauti na tuhuma iliyotolewa; nakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wake ili kuwe na mjadala mpana wa kibunge utakaowezesha kumbukumbu sahihi kuwekwa. Ukweli ni uhuru!.

  Katiba ya Nchi ambayo niliapishwa kuilinda pamoja na ubovu wake inatamka katika Ibara ya 63 (2) kwamba "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba". Toka nichaguliwe kuwa mbunge mwaka 2010 kwa nyakati na maeneo mbalimbali viongozi wa vyama, dini, asasi za kiraia, vyombo vya habari na wananchi wa kawaida wakilalamika kuhusu udhaifu wa Rais na kutaka atumie nguvu na mamlaka yake ya kikatiba kuiongoza kwa uthabiti serikali kushughulikia masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yanayolikabili taifa; niliamua kuendelea kusema bungeni kwa mara nyingine ikiwa ni sehemu ya kutimiza wajibu wa kibunge wa kuwakilisha wananchi na kuisimamia serikali. Ukweli ni Uhuru!.

  Tarehe 19 Juni 2012 nilieleza bungeni kabla ya kutolewa sababu za kuikataa bajeti na tarehe 22 Juni 2012 nilipiga kura ya hapana ya kuikataa bajeti kwa kutokuweka misingi thabiti ya kutimiza ahadi ya Rais Kikwete na CCM ya maisha bora kwa kila mtanzania na badala yake kuongeza ugumu wa maisha kutokana na kushindwa kukabiliana na matatizo ya mfumuko wa bei. Aidha, kiwango cha fedha kwa ajili ya miradi ya barabara na maji kwa upande wa jiji la Dar es salaam ikiwemo jimbo la Ubungo ni kidogo tofauti na kile kilichotajwa na Rais Kikwete na kuingizwa kwenye jedwali la Mpango wa Taifa wa miaka mitano kwa upande wa miradi ya maendeleo iliyopaswa kutengewa fedha katika bajeti ya 2012/2013. Ukweli ni Uhuru!.

  Pamoja na utetezi uliotolewa na Serikali juu ya mgongano kati ya tafsiri kati ya kiingereza na Kiswahili, ukweli utaendelea kubaki kuwa tuliamua kuikataa bajeti kwa kuwa ilishindwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao uliwasilishwa na Rais Kikwete na ukapitishwa kwa azimio la bunge ambao ulipaswa kuiongoza serikali kuweka mkazo katika kuendeleza nchi kwa kutumia fedha za ndani kwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwenye miradi ya maendeleo kama zilivyokokotolewa katika mpango husika. Ukweli ni Uhuru!.

  Naamini Rais Kikwete anayofursa ya kurekebisha udhaifu huo kwa kuongeza nguvu zake katika muswada wa sheria ya fedha kupanua wigo wa mapato na hatimaye kumwezesha Waziri wa Fedha kuwasilisha bungeni kwa mujibu wa kanuni ya 107 mapendekezo ya matumizi ya nyongeza ya fedha za serikali yenye kulenga kuongeza kiwango cha fedha za maendeleo. Kwa upande wa Jimbo la Ubungo na Jiji la Dar es salaam, serikali kwenye bajeti ya nyongeza inayopaswa kuwasilishwa iongeze fedha za miradi ya Maji kwa upande wa Ruvu Juu ikiwemo kutenga fedha za kutosha za ujenzi wa Bwawa la Kidunda, kwa upande wa Barabara iongeze fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara za pembezoni za mchujo na za mzunguko za kupunguza msongamano wa magari, na fidia ya ardhi kwa wananchi wa Kata ya Kwembe wanaopaswa kuhama kupisha ujenzi wa Chuo Kikuu Muhimbili (MUHAS) Eneo la Mloganzila. Ukweli ni Uhuru!.

  Kwa Wasemaji wa CCM waliodai kwamba nimetoa lugha ya matusi dhidi ya Rais na mwenyekiti wa chama chao wasome Kitabu cha Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania cha mmoja wa waasisi wa TANU na CCM Mwalimu Julius Nyerere ambapo wakati huo taifa likiwa katika mtanziko alimueleza Rais wa wakati huo kuwa ni ‘kiongozi dhaifu' katika ukurasa wa 50 na kuendelea kusema katika Ukurasa wa 51 na namnukuu "Kwa sababu ya minong'ono-nong'ono ya watu wasiiona mbali kuhusu Rais, na kubabaishwa anakobabaishwa na washauri wake wakuu, nililazimika kuiambia wazi wazi Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kwamba najiona kuwa ninao wajibu wa kumsaidia Rais amalize kipindi chake salama" . Ukweli ni Uhuru!

  Naamini Mwalimu Nyerere hakumtukana Rais Mwinyi, kwa hiyo kunituhumu nimetukana ni kumtuhumu pia Marehemu Baba wa Taifa; narudia tena kusisitiza kuwa udhaifu uliojitokeza ni kutokana na Rais kutokutumia kwa uthabiti nguvu na mamlaka yake kwa mujibu wa katiba ibara za 33, 34, 35, 36, 37, 38 na 99 juu ya utendaji wa serikali na utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo. Ukweli ni Uhuru!.

  Nimalize kwa kunukuu kitabu kingine cha Mwalimu Nyerere cha miaka ya mwanzoni mwa 1960 cha TUJISAHIHISHE, " Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua kuwa hana makosa. Na msingi wa woga ni ubinafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani. Pengine twaweza kuwa hatuna cheo chochote ambacho tunaogopa kupoteza; pengine huwa hatuna wala tamaa yoyote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi wote tunayo tamaa hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza ukamfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni ubinafsi mbaya sana.", mwisho wa kunukuu: Ukweli ni uhuru.

  Wenu katika utumishi wa umma,

  John Mnyika
  22 Juni 2012
  Bungeni-Dodoma
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Ngoja nikipata wasaa ntaisoma kwa umakini...muda huu niko busy..ntarudi
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa maelezo muafaka.Kama Sugu ni 'Rais' wa Mbeya na Lema ni 'Rais' wa Arusha kwanini Mnyika asiwe 'Rais' wa Dar?
   
 4. M

  Mzee Mzima Senior Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  well explained!!
   
 5. M

  Mzee Kabwanga Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa kutoa ufafanuzi wa kina na tafsiri ya katiba na maandiko mbalimbali.
   
 6. Guyton

  Guyton JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Uchambuzi makini kutoka kwa mtu makini.

  Mnyika ni mtu makini ata Nape, Wassira, Lukuvi, Makinda ikiwemo raisi mwenyewe wanalifahamu hili.
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  endeleeni kuichangamsha serikali, ndio wajibu wenu kama wabunge
   
 8. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  huyu ndiye kiongozi makini .... maneno yenye ukweli awia .... siyo kina L.M Nchemba hovyo kabia
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mnyika nilikwambia humuwezi Kikwete, shauri lako, wewe endelea tu.
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Good boy!
   
 11. a

  admiral elect Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  safi mnyika huo ndio msimamo wangu pia kuwa sisi watanzania tumekuwa waoga na hivyo wanafiki na ndo maana tumefika hapa kwa kisingizio cha mfumo wetu ni mbaya na dhaifu wakati sisi wenye mfumo hatukubali kuwa ndio wabaya na wadhaifu nambari wani. mimi binafsi najilaumu na kwa kutofanya jambo la kubadilisha hali hii maana itakuwa aibu kwa watoto na wajukuu zetu.mimi nachukia unafiki sana.wakati nikisoma sekondari(O- level) mama yetu alifariki na baba akaoa mwanamke mwingine baada ya muda wa chini ya mwaka 1,nilimwambia wazi bila kumumunya maneno kuwa amefanya haraka sana na zaidi mwanamke aliyemuoa haikuwa chaguo sahihi nikagombezwa sana na ikafikia hatua ya kuitwa kwenye kikao cha wanafamilia nakutakiwa kuomba radhi kwa kuingilia mambo ya mzazi wangu,lakini nikasimamia ukweli kwa gharama ya kunyimwa ada,baadaya miaka mitatu my father admitted that i was dame right!UNAFIKI NA UOGA NDIO CHANZO CHA MATATIZO YETU WATANZANIA! mnyika hongera na kandamizia hapo hapo no matter what !
   
 12. h

  hans79 JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Ukweli wako utakusaidia sana maishani pia jenga tabia ya kujiamini ndo wote wenye mapinduzi na wapigania haki walipitia mabonde pamoja na magumu kama hayo.Simamia ukweli na iwe silaha yako ktk maisha yako yote.
  Rab akupe maisha marefu kt ukombozi wa taifa hili na ombaomba.
   
 13. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Kwanini unasema hivyo mkuu.
   
 14. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hongera Mnyika. Mnyika usipate shida na watu wanaotumikia matumbo yao na wala hawana uchungu dhidi ya watanzania wengine. Ukweli uko wazi na hata kijijini ukiuliza watu watakuambia tu, Jibu ni moja tu tunaye kiongozi ambaye hana uwezo. Na matatizo yote haya ni kwasababu ya udhaifu tu. Neno dhaifu siyo tusi, mimi niliwahi kuambiwa na mwalimu wangu huko nyuma kwamba fulani, wewe ni dhaifu hivyo inabidi ufanye jitihada. Ndugu yangu, hiyo kauliya wewe ni dhaifu ilinipa nafasi ya kuangalia maisha yangu upya na nilichukua hatua na sasa nayaona matunda ya ile kauli ya mwalimu wangu. mimi sikumchukia bali nilichukulia kama changamoto na nilichukua hatua. Hivyo wanaosema kwamba neno dhaifu ni tusi ni wale ambao HAWATAKI KUAMBIWA UKWELI na badala yake wanapenda UNAFIKI.


  Narudia tena, gharama ya maisha kuwa juu, barabara mbovu, bidhaa bandia kujaa nchini, wamachinga wa kichina wengi kariakoo, wazanzibar kuwabagua watanganyika, madini yetu kutotusaidia na badala yake fedha zinapelekwa Canada, USA, n.k, wanyama wetu (106) kutoroshwa kwenda Qatar, Pesa zetu kujaa kwenye Swiss Bank, Wezi wa EPA kusamehewa, kukosekana kwa huduma ya maji safi kwa waliowengi, hospitali za hovyo bila madawa wala vipimo, mgomo wa madaktari, njaa kwa baadhi ya wananchi wakati tuna ardhi ya kutosha, mikataba mibovu, n.k, n.k.

  HAYA YOTE NI MATUNDA YA UDHAIFU WA TAASISI YA URAIS ambayo ina mamlaka makubwa sana kutokana na Katiba ya nchi yetu.
  TELO.
   
 15. a

  admiral elect Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  come what may,huo ndo ukweli!mnyika amechagua kutokuwa mwoga wala mnafiki na hata mkimua ataishi tena
   
 16. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  HII SIYO KARNE YA KUTISHANA NYAU. na kwa taarifa yako hata hao Usalama wa Taifa unaowasemea wamegawanyika makundi mudamrefu kweli.
   
 17. m

  majebere JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Sasa we mnyika,bla bla nyingi za nini, si ungesema unaomba msamaa kwa maneno machache tu. Cheza na Kikwete wewe, haya wana CDM, jamaa yenu anajitetea na kuomba msamaha baada ya kuropoka.
   
 18. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hongera kwa maelezo ya kina, Rais wetu ni mwelewa sana, sidhani kama alifikiria kama vibaraka wa magamba walivyolichukulia. Nakushauri uchapishe waraka huu kwenye magazeti yote ili ujumbe uwafikie wote.
   
 19. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
 20. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [/QUOTE] tunga kitabu kuhusu mada hii mh. Mh mnyiks. Thx
   
Loading...