Waraka mwingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka mwingine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mutekanga, Aug 29, 2009.

 1. M

  Mutekanga Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waraka wa waislam, tumeyataka wenyewe na tujiandae kwa vurugu hizi. Maaskofu, hawakuangalia mbali kuona wanaanzisha vurugu kubwa. Kila dhehebu likitoa waraka na mwongozo wa namna ya kufanya uchaguzi, hatuwezi kufika! Ni wazi utakuja na waraka wa wapagani, waraka wacommunist nk.

  Hizi ni dalili tosha kuonyesha kwamba Hekima na busara zimekwenda likizo. Dini zikianzisha vurugu, haina mwisho. Bahati mbaya au nzuri, waumini wa Afrika wanaamini kiushabiki. Labda ni umaskini wa mali na fikra. Hivyo tutachinjana wenyewe kwa wenyewe kulinda waraka kutoka kwa viongozi wetu wa dini.

  Katika mambo ya siasa, hakuna haja ya kuwa na waraka kutoka madhehebu mbali mbali. Mwongozo wa kuchagua viongozi utolewe na serikali. Dini zinaweza kusaidia kwa kuhakikisha watanzania wana roho ya Kimungu.

  Ni lazima tuwe makini kabisa, vinginevyo tunaweza kuwa kama Somalia na nchi nyingine za Afrika zinazopigana vita ya kudumu. Ni lazima watanzania tusimame kwa pamoja kukemea mtido wa viongozi wa dini kutoa waraka kuwaelekeza waumini wao namna ya kuchagua. Tukichelewa na kuliacha hili likapiti; majuto ni mkuuu!
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ungechukua muda kusoma threads zote zinazohusu ule waraka, usingebandika hili lako!!!

  Tatizo ni upeo wa wachanganuzi wa mambo!!!


  I am sure you will educate people like me more so that i change my mind kuhusu ule waraka wa katoliki
   
 3. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Msiwe na wasiwasi na kuwatisha watu jamani. Organized religions hazina influence tena katika jamii. Hakuna anayekwenda kwenye voting box akakukumbuka kiongozi wake wa dini amesema nini. Ndiyo maana hata ukimwi unatumaliza maana influence ya dini haiingii bedroom. Leteni nyaraka zaidi.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sure, we should refrain from re-inventing the wheel. We need to avoid discussions which don't make any step forward.

  Mod atusaidie kuweke hii kwenye zile thread za nyuma!
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mkuu BB hapa umenena!

  Viongozi wa dini wangekuwa wanasikilizwa kama wanavyotaka kuonyesha, Tanzania isingekuwa hivi tunavyoiona. Madhambi mangapi wanakemea kila siku lakini watu hawajaacha uzinzi, wizi, nk.

  Hili vurugu la nyaraka haitabadili kitu, ikifikawakati wa kuchagua waTanzania kama kawaida yao wataangalia nani kawakaribisha pilao, kuwagawia kanga na fulana hata wengine hununuliwa pombe za bure na kugawa kura zao.
   
 6. M

  Mwanaluguma Member

  #6
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  Mbona unakuwa na upeo mdogo sana wa kutafakari,hivi wewe ukisoma waraka wa waislamu ndio ushike panga ukaue au ukisoma waraka wa wakristo? kwa nini unapoteza muda kuweka hoja mbovu hapa. Waraka kama unamwelekeza mtu kumchagua kiongozi asiye mfisadi wewe tatizo lako nini? Watu sasa hivi wana akili, labda unachotakiwa ni kuwaonya waislamu kwa kauli zao za kusema kuwa wanataka kiongozi ambaye atalinda maslahi yao wanasahau kuwa kiongozi huyo yupo kwa ajili ya watanzania wote,hiyo ndio weakness ya kuikosoa na si waraka kwa ujumla. Tanzania tuna vyama vingi wakati wa kampeni watu wanasikiliza vyama vyote lakini mwishowe huchagua kiongozi wanayemtaka. Ni vema ukaelimisha watu umuhimu wa nyaraka hizo katika jamii badala ya kuziponda kwa hoja dhaifu.
   
 7. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kama mtu ataleta fujo, alaumiwe mwenyewe! Hatuwezi kuwalaumu wengine kama fujo zitaletwa na watu tofauti. Waislamu walilaani waraka wa Wakatoliki. Kama kutoa waraka kilikuwa kitu kibaya, mbona na wao wametoa? Sasa wanataka tusemeje? Kwamba wamefanya kitu cha maana?
   
 8. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2009
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ninavyoamini binafsi binadamu tunatofautiana katika mengi. Tofauti mojawapo ni katika fikra zinazopelekea katika mang'amuzi kinzani na baadaye maamuzi yasiyoshabihiana. Katika hili ninaona kuna upande ambao haujashirikisha uwezo wa fikra sawia na kupelekea katika mgongano unaoegemea zaidi katika mambo ki-imani ambayo si tatizo letu.
  We have a problem and it is our real problem, for the reasons beyond my thoughts no one is reacting to our problems BUT reacting to ideal problem(s) between themselves. I'm honestly and frank those who talking they are not in a position to know what they are talking. [I do believe a human brain has three parts, for our betterment this parts has to be used in a right proportion when it comes to decision that lead to announcement(s)]
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  To me sioni tatizo as long as waumini wanawekwa sawa.suala la machafuko linatoka wapi kama rc huu sio waraka wa kwanza kuutoa jamani labda bse umekumbana na hali tete ya kisiasa ata pope huwa anatoa waraka.
  After all ata tukifikia kuzipiga mi sioni shida ili tuweze tiana adabu kwa watakaobaki naisi wataishi maisha bora kuliko huu uhuni unaoendelea watu hawana discpline ma resources za nchi.
   
Loading...