Elections 2010 Waraka muhimu kwa wapiga kura wa Tanzania

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Nimetumiwa waraka huu kwa email kutoka kwa jamaa mmoja anayeishi huko mikoani. Nawabandikia wadau ili muone ushauri wake.
Soma kwa makini:
sambaza ujumbe huu uwafikie wapiga kura wote waliopo Tanzania.
Mtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na mtindio wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili, tena asiye na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni, wala asiye mzembe wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na azingatie makala hii na awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake popote pale walipo..

Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.

Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupungzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!

Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa ni nini?

Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma, Tabora, na Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi wanabaki kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa vinatumika kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na akina Carl Peters.

Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wameshazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..

Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anayeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.

Ni Dr.Slaa anayeweza kusimamia mashirika ya umma kuleta tija; achana na CCM wanaofyonza michango yetu.Kwani haya mashirika yameshindwa nini kuwajengea nyumba wanachama wake? Mbona kwingine yameweza? Ni Dr.Slaa anayeweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa sheria bila kuwaonea watu wala bila kulipiza visasi.

Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa muda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? Naomba niwape heko ITV kwa kuturejesha kwenye hotuba za mwalimu. Katika hotuba yake moja alisema waziri mmoja kule uingereza aliandikwa kidogo tu gazetini juu ya kashfa, yule waziri alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.

CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!

Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Si tumeona Mwembeyanga alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa chini? we must be serious! Hivi kweli dunia ya leo watu wanavuliwa nguo njiani kwenda Mwanza, Shinyanaga, Tabora, Kigoma, Mbeya, Lindi na Mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori?

Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo Botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiyejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiyejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu??

Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?

Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, National Parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini tuko maskini wa kutupwa! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania.

Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.

Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi. Peleke ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela.

Ndugu zangu
Nisameheni kwa uhalisia huu.
Kupigia kura CCM ni kukubali kuwa sisi tumelaaniwa. Dalili kubwa ya laana ni mgeni kustawi katika nchi yako na wewe ukabakia lofa, chokoraa, kibarua , mpagazi na manamba. Tuma ujumbe huu kwa watu wote.

Pamoja na maneno haya mazito, hebu endelea kutafakari maneno ya wapenda maendeleo Tz na wanaoungana na Dr W.Slaa kupigania haki ya wanyonge wa Tz. Soma taratibu wakati ukitafakari kwa kina yaliyomo.
1."Kumekucha,kumekucha, kumekucha.JK VS Dr Slaa, jibu ni wazi. Kushindanisha Msanii na mtu Makini, Dola ya Zimbabwe VS USD, FisadiVS Mwadilifu.Nakwambia Tz hadi sasa inaelekea patamu. Mwisho wa Msanii aitwaye JK umefika.
2."Shime wandugu, majira ya usanii yamefikia mwisho wake.Taifa linamtarajia mtu makini aliyejitoa mhanga kufa kwa ajili ya wengi, si mwingine bali Dr.W.Slaa.Its time for change.Waambie watu wajipe moyo mkuu, Mungu amekusudia mema kwa ajili yetu. Hakuna kufa moyo. Marufuku kukata tamaa, tunaye Mungu asiyeshindwa.
3.Wakati umewadia weka vocha za kutosha na piga kampeni kupitia sms na email. Ombea sms kwanza na email kisha sambaza na tuma kwa kila uliye na namba yake hata email bila kujali ni chama gani, kwa uchache ukitumia watu 300 utakuwa umemuonyesha JK mwenye kiburi mlango wa kutokea.
4.Kwa maana jinsi hii Mungu aliipenda Tz hata akamtuma DR Slaa(silaha), ili kila mtanzania atakayemkubali na kumpigia kura na kumchagua kuwa rais apate ukombozi wa kweli. Ni zamu ya CCM kuaga. Tumeonewa na kukandamizwa kiasi cha kutosha, patakatifu ( Ikulu) pamekuwa kituo kikuu cha Usanii, Mungu ibariki TZ, Mungu mbariki DR Slaa.
5.Waambieni watanzania wote kuwa watakuwa kheri kwa kuwa watakula matunda ya matendo yao, hapo tarehe 31.10.2010, watakapompa kura ya NDIYO DR.W.Slaa.
6. Nchi yangu kwanza, chama changu baadaye. Hiyo ndo iwe lugha yetu tunapoelekea uchaguzi mkuu.Wapime wagombea kwa kuangalia kam wana uchungu na nchi ama wanatania.
7.Yaliyojiri siku CCM walipofunga NDOA na UFISADI: Bwana Harusi:Mimi CCM nakutwaa wewe Ufisadi uwe mke wangu wa maisha, nikupende nikutunze wakati wa shida na raha, ndivyo nitakavyofanya kufuata agizo ovu la IBILISI joka wa zamani. Ewe Taasisi ya kulinda na kuendeleza Rushwa (TAKUKURU) unisaidie.
8. Kuna Nchi moja duniani ambayo ukiiba utasamehewa kwa sharti kuwa kwanza urejeshe ulichoiba, sharti la pili ni kuwa uhakikishe umeiba fedha ya kutosha tena uibe banki kuu, iwapo utatimiza mashaarti hayo mawili, una uhakika wa kusamehewa na rais hata ingawa kwa kufanya hyivyo atakuwa amevunja KATIBA.Hiyo nchi inaitwa TZ chini ya chama cha kifisadi CCM kinachoongoza film, wao wanayoiita kuwa ni VITA dhidi ya UFISADI. Ing'oe CCM madarakani hapo tarehe 31.10.2010.
9.Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasikitika kutangaza kifo cha CCM, kitakachotokea kwenye masanduku ya kura hapo tarehe 31.10.2010. Mipango ya mazishi inaandaliwa, habari ziwafikie mafisadi wote popote walipo nchini TZ na nje ya nchi.Ibilisi ailaze mahali pa mateso roho ya marehemu.
10."Maafisa na watendaji wabovu serikalini"huchaguliwa na raia wema ambao hawajitokezi kupiga kura"George Jean Mhariri Daily Sun, USA. Tafadhali himiza watu wajitokeze kupiga kura na kuchagua watu makini na waadilifu. Rejesha heshima ya taifa kwa kumchagua Dr.W.Slaa.Kura yako itaamua hatma ya taifa hili miaka 5 ijayo.
11.Kwa niaba ya mtandao unaoitwa "marafiki wa Dr.Slaa, ninakusalimia na kukukumbusha kuwa mwaka huu usifanye kosa la kukichagua chama cha mafisadi. Utajuta kuwachagua.
12."Kikwete kasema "CHADEMA si chama cha kubeza".Mchague Dr.W.Slaa, alete mabadiliko ya kweli.TZ bila Kikwete inawezekana.
13.Walitudanganya wanaweza, tukawaamini tukawapa kura zetu, tulichokipata ni mateso matupu. wamejipa kila raha waliyoitaka, wamesafiri walivyotaka, wameishi walivyotaka, wanataka tena kura zetu, wakastarehe kwa ARI zaidi, KASI zaidi na NGUVU zaidi. Tuwakatae, tuwanyime kura zetu, chagua Mzalendo wa kweli Dr.W.Slaa.
14.Je wajua utafiti makini umetoa ulinganifu wa wagombea wa urais kwa tiketi za CHADEMA na CCM, kuwa wanalinganishwa na tofauti iliyopo kati ya Dola ya Zimbabwe na marekani. Unaweza kuhukumu mwenyewe, ni nani anasimama kama dola ya zimbabwe na dala ya Marekani.
15.Siku ya kupiga kura, Mungu anataka aone ni watanzania wangapi wana akili timamu na wanaipenda TZ, na si ushabiki wa vyama.Slaa tuko pamoja, huna mpinzani,huu mwaka ni wako na Mungu akubariki.Tuma kwa watu wengi kuonyesha unapinga rushwa na ufisadi, hii ni saa ya ukombozi wa taifa letu. Kutoka kwenye kundi la wezi wa CCM wakiongozwa na mwenyekiti wao JK,
16.YES WE CAN. Make DR.W.Slaa OUR next president and will never regret. Kumbuka KULA ni CCM ila KURA ni kwa DR.W.Slaa.
17.Inzi na nyuki hufa kwa kulazimisha kupenya kwenye kioo angavu, ndivyo watakavyoangamia wasomi, wafanyakazi, na wakulima wanaolazimisha kutimiza ndoto zao kupitia CCM. sasa tuko kwenye kampeni maalum dhidi ya kikwete 2010, aliingia kwa mbinu atatoka kwa mbinu, mtenda hutendwa, tunawasupport wadai haki na operation SANGARA. TZ bila Kikwete inawezekana.Tuma sms hii kwa waliochoshwa na Kikwete hasa Waalimu, NMB, TRL, Wazee wa EAC, na wanafunzi vyuoni.
18.JK ametoa ahadi nyingi hadi anajulikana sasa kama Mr.ahadi. Kuna ahadi moja tu hajatoa nayo ni UZIMA wa milele kwa watakao mpa kura. Chagua DR.Slaa.
19.UFISADI TRAINING COLLEGE, inawatangazia kozi zifuatazo:
a)wizi wa kura b) kutumia vyeti feki c) kuvujisha mitihani d) kulipa mishahara majina hewa e) kuanzisha makampuni hewa,.Chuo kitakupeleka field sehemu nzuri kama vile EPA na BOT.Utaajiriwa na kampuni ya Richmond na TICTS, chuo kimetoa wahitimu kama Lowasa, Karamagi.Jetu Patel, karibu sana nafasi ni chache, fomu zinapatikana kwa waziri mkuu aliyejiuzulu.Je, uko tayari?kama ndiyo wewe uko miongoni mwa CCM. Kama utakuwa unalaani rushwa na ufisadi Mungu awe nawe kwa kujua haki zako. SLAA amechaguliwa kuondoa usanii IKULU. Kura yako ni NGAO kwa Slaa.Maana RUSHWA haikubaliki.
20. wanahaha, wanahemea juujuu, hawana amani, na zaidi hawaamini wanachokiona, au wanachokisikia. Watajuta kushindanisha dola ya Zimbabwe na USA. Mwaka huu tunao.
21.Kampeni ni kwa mtu na mtu (sio shuka kwa shuka kama alivyosema mke wa rais), SMS, Email na MAOMBI,tunawatandika kwa makombora ya ardhini na angani (PRAYER).
22. Swali la msingi hivi umaskini wa watanzania unatokana na NDOA ya Dr.W.Slaa au Ufisadi na uelewa duni wa viongozzi wa nchi chini ya JK?Chagua DR.Slaa.-
23.Mtz shiriki ukombozi wa nchi yako, mchague Dr.W.Slaa, mtu makini, timamu wa akili, na msomi aliyebobea, mwelewa na muumini wa maadili, kiboko ya mafisadi. Mwenye afya njema, siyo kama wengine wanaodondoka ovyo majukwaani. CHADEMA kwa mabadiliko ya kweli.
24. Hivi una taarifa kuwa ongezeko la 100% katika Private sectors na si una taarifa kuwa tayari tamko lilisha tolewa katika media?. Hivi unadhani usisitizaji wake uliishia hapo? Lakini pia nikuulize, Can you manage to double your workers salary? Basi tuseme utaongeza karo, hivi hiyo karo utakayoiongeza MKULIMA ataweza kulipa? Haya bwana ninyi fanyeni mchezo JK apite mi ntakuwa nawauliza maendeleo vipi?
25. Jk ameunda kamati washirikiane na CCM kushughulikia mchakato wa ushindi. Omba Mungu wasielewane, Watumie waombaji wengi haraka waendelee na maombi.
Ndugu yangu na mpendwa,huu si mchezo kabisa, fanya haraka, toka usingizini. Mweleze na rafiki, jirani yako kwa wazi.
Saidia na changia ukombozi wa TZ.
 
ujumbe mzuri ,ila walengwa ambao wote kura zao sawa sidhani kama wako tayari kusoma warak mrefu namna hii kama inawezekana mwenye uwezo make long story short bila ku omit main points
 
Uzalendo wa DR SLAA ni wa maneno zaidi na siyo wa vitendo.Kama ni wa vitendo alichukua hatua gani? mara baada ya kuzungumzia posho za wabunge zipunguzwe.Tulitegemea kwamba SLAA angezikataa zile posho na kulitaka bunge kiasi fulani cha posho zake zielekezwe kwa watanzania masikini.Lakini cha kushangaza aliendelea kuzipokea hizo posho na kuzitafuna yeye na familia yake.Je huo ndio uzalendo wa kweli? wa DR SLAA
 
Uzalendo wa DR SLAA ni wa maneno zaidi na siyo wa vitendo.Kama ni wa vitendo alichukua hatua gani? mara baada ya kuzungumzia posho za wabunge zipunguzwe.Tulitegemea kwamba SLAA angezikataa zile posho na kulitaka bunge kiasi fulani cha posho zake zielekezwe kwa watanzania masikini.Lakini cha kushangaza aliendelea kuzipokea hizo posho na kuzitafuna yeye na familia yake.Je huo ndio uzalendo wa kweli? wa DR SLAA

Ni kwamba huelewi uzalendo wa Dr slaa ? au ni kichwa ngumu cha ufisadi?

Acha upupu.
 
usibishane nae unampa credit; wana paycheck kwa makamba hao; hawana jinsi lazima watoe upupu humu; hao August's and Sept's entries
 
Uzalendo wa DR SLAA ni wa maneno zaidi na siyo wa vitendo.Kama ni wa vitendo alichukua hatua gani? mara baada ya kuzungumzia posho za wabunge zipunguzwe.Tulitegemea kwamba SLAA angezikataa zile posho na kulitaka bunge kiasi fulani cha posho zake zielekezwe kwa watanzania masikini.Lakini cha kushangaza aliendelea kuzipokea hizo posho na kuzitafuna yeye na familia yake.Je huo ndio uzalendo wa kweli? wa DR SLAA
kweli wewe ni bobish.... maana unaonekana hujui kuongoza kimaadili na kuongoza kihuni... collective responsibility ndiyo iliprevail na huwezi hata kama unapinga kitu kazini kikishaamuliwa ukaenda kinyume na wenzako

LABDA UNGESEMA HIVI --- ALIPOKUA AKIZICHUKUA ALITAKIWA AWAPE MASKINI AU AFUNGUE MFUKO WA KUSAIDIA WANAOHITAJI HIZO PESA KWANI KWAKE HAZISWIHI
Bibish you need to go back to school
 
Back
Top Bottom