Waraka: Mambo ya hovyo yanayofanywa na serikali, viongozi wa dini mko wapi?

wanaojielewa wanajua wanachokifanya na kuamua na mtaji mkubwa wa kile chama ni kuendelea kuminya Elimu kwa wachache ili yasitokee kama haya hata mkopo kwa vyuo vikuu unasumbua hizo asilimia kwa hofu hii kuwa wengi wakielimika wataua uhai wa wao kuendelea kutawala hili la mawakili ni Funzo...
 
Amani iwe nanyi wanabodi!
Naam! Mawakili wameonesha kwa vitendo kuwa akili zao ni za kwao hakuna mtu aliye zishika. Wametishwa hawajatishika, wamemchagua wanae mwamini ni kiongozi mwenye msimamo asiye yumbayumba, Tundu Lissu.wasomi wameitendea haki elimu yao,watanzania kuna kitu wamejifunza. Hongereni learned brothers wote.

Kuna kundi lina wasomi wengi sana lakini halitumii ushawishi wake kujenga jamii inayo jitambua na kuheshimu misingi ya kutawala na kutawaliwa. Ni kama wameridhika na mambo yanavyo endelea ndani ya Nchi.viongozi wa dini karibu zote wameridhika na maisha ingawa kondoo wao wanaonewa na kunyanyaswa wakati mwingine bila sababu za msingi.wametosheka na sadaka zetu? Sijui, kimya chao kinatisha.

Kiongozi wa Nchi kupanga matumizi ya fedha za umma bila kupata idhini ya Bunge ni hatari. Kiongozi wa Nchi kupandikiza chuki miongoni mwetu kwa itikadi za vyama ni hatari. Unalazimisha wana CCM wasiwaone wana CHADEMA kwenye shida na mahangaiko mbalimbali na kusema ule ni usaliti! Basi kama ni hivyo uwe unaomba CCM wakuombee! Watanzania wengine utuache!

Kiongozi wa Nchi kutawala Nchi bila kufuata kanuni na taratibu tulizo jiwekea ni hatari.watu hawapati nyongeza za mishahara, vijana hawaja ajiriwa miaka miwili sasa, upendeleo katka ajira hasa kufuata itikadi kumeshamiri sasa kuliko Wakati mwingine wowote, watu kufukuzwa kazi bila sababu za msingi imekuwa jambo la kawaida, upendeleo! Viongozi wa dini wameziba midomo na masikio, wamemwacha Mungu wa Tanzania atawale apendavyo.

Hongereni mawakili, unganeni mtuondolee Bashite kwa heshima ya watumishi zaidi ya 1887 walio ondolewa kwenye ajira kwa kutumia vyeti fake kama Bashite. Haki lazima itamalaki.
Acha propaganda za kijinga, Lisu si suluhisho ya unayoyasema !
 
Akili za humu ni kuigeuza Sheria kuwa siasa ccm na cdm vimeingiaje kwenye sheria?au lisu kabadilisha sasa sheria kuwa siasa ?au ndio mwisho wa mitazamo yenu?
 
Magufuli akutaka achaguliwe lisu ndomana katika kikao chake na majaji alishinikiza wakamchague anae mtaka yeye ila kwakua majaji wanajitambua wamichagua chaguo sahii na nyinyi wabunge mulio itwaitwa na magufuli dodoma na kutishwakutishwa na kuwaambieni chakwenda kufanya bungeni igeni kwa majaji waliagezwa wakatumia elimu yao kufanya kitu sahii na nyinyi tumieni akili zenu kufanya mambo sahii Tanzania si yamtu Tanzania YA watanzania mungu awabaliki sana
 
Sasa lisu ataleta mabadiliko ya kisiasa au ya kisheria au ya kubishana kisheria kama ilivyo kawaida yake.inavyoonekana humu jf tunashabikia kisiasa tu kwasababu tupo huru
 
Pongezi pia ziende kwa mawakili wa serikali ambao pamoja na vikao vilivyowataka wasimchague Lissu, wao bado wametumia akili na utashi wao waliopewa na Mungu, wakamchagua Lissu.
Mawakili wanajitambua siyo wasomi wachumia tumbo. Ni watu wa kupigania Na kutoa haki. Yanayotendeka huku Yuda wanayaona. Inapendeza MTU anapotumia usomi wake kufanya maamuzi ya busara bila Shuruti.
 
Viongozi wadini wamekuwa waoga saana,sijui wengi hawako safi? Hata ibada ya ndoa ilipoingiliwa walikaa kimya,waumini wao tunatupwa jela kwa uonevu wanakaa kimya,ubaguzi unahubiriwa waziwazi mfano kusema wapinzani hawatatia mguu kwenye serikali yake huku akisema hataki wanasiasa anataka watendaji lakini viongozi hawa hawakemei...kwakweli inatia mashaka kuona mhalifu alofoji mavyeti akiombewa makanisani na mashekhe kwanguvu zote!! Ajabu Sana.
 
Amani iwe nanyi wanabodi!
Naam! Mawakili wameonesha kwa vitendo kuwa akili zao ni za kwao hakuna mtu aliye zishika. Wametishwa hawajatishika, wamemchagua wanae mwamini ni kiongozi mwenye msimamo asiye yumbayumba, Tundu Lissu.wasomi wameitendea haki elimu yao,watanzania kuna kitu wamejifunza. Hongereni learned brothers wote.

Kuna kundi lina wasomi wengi sana lakini halitumii ushawishi wake kujenga jamii inayo jitambua na kuheshimu misingi ya kutawala na kutawaliwa. Ni kama wameridhika na mambo yanavyo endelea ndani ya Nchi.viongozi wa dini karibu zote wameridhika na maisha ingawa kondoo wao wanaonewa na kunyanyaswa wakati mwingine bila sababu za msingi.wametosheka na sadaka zetu? Sijui, kimya chao kinatisha.

Kiongozi wa Nchi kupanga matumizi ya fedha za umma bila kupata idhini ya Bunge ni hatari. Kiongozi wa Nchi kupandikiza chuki miongoni mwetu kwa itikadi za vyama ni hatari. Unalazimisha wana CCM wasiwaone wana CHADEMA kwenye shida na mahangaiko mbalimbali na kusema ule ni usaliti! Basi kama ni hivyo uwe unaomba CCM wakuombee! Watanzania wengine utuache!

Kiongozi wa Nchi kutawala Nchi bila kufuata kanuni na taratibu tulizo jiwekea ni hatari.watu hawapati nyongeza za mishahara, vijana hawaja ajiriwa miaka miwili sasa, upendeleo katka ajira hasa kufuata itikadi kumeshamiri sasa kuliko Wakati mwingine wowote, watu kufukuzwa kazi bila sababu za msingi imekuwa jambo la kawaida, upendeleo! Viongozi wa dini wameziba midomo na masikio, wamemwacha Mungu wa Tanzania atawale apendavyo.

Hongereni mawakili, unganeni mtuondolee Bashite kwa heshima ya watumishi zaidi ya 1887 walio ondolewa kwenye ajira kwa kutumia vyeti fake kama Bashite. Haki lazima itamalaki.
Gwajima tu ndie kiongozi wa dini anayetetea wtz
 
Hawa Mawakili walioungana katika kupiga kura Mungu azidi kuwapa roho ya upendo na Ulizi wasipate jambo lolote maishani mwao. Amena
 
Kwa hisani ya Julius S. Mtatiro

Kisheria Tanzania ina Marais watatu tu, ambao wanatambulika kikatiba na wameidhinishwa na sheria ya bunge.

1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anatambulika kupitia ibara ya 33 ya Katiba ya nchi ambayo ni Sheria mama.

2. Rais wa Zanzibar. Anatambulika kupitia ibara ya 103 ya Katiba ya nchi ambayo ni Sheria mama.

3. Rais wa TLS. Anatambulika kupitia sura ya 5, ya Katiba ya nchi ambayo ni Sheria mama. Na anatambulika pia kupitia Sheria ya bunge (Tanganyika Law Society Act, Cap 307 R.E. 2002).

Hawa ndio marais wanaotambulika kwa mujibu wa sheria ya bunge. Marais wote huchaguliwa kwa kura.!
View attachment 483201
Mh mangu sijui atapasukaa!
 
Sasa lisu ataleta mabadiliko ya kisiasa au ya kisheria au ya kubishana kisheria kama ilivyo kawaida yake.inavyoonekana humu jf tunashabikia kisiasa tu kwasababu tupo huru
Watu mna akili fupi sana. Hivi unayajua majukumu ya TLS? Unaifahamu katiba ya TLS. Wanasheria si mambumbumbu wa kuongozwa kwa remote ni wasomi wanaojua wanafanya nini. Hujiulizi kwanini wamepinga mapendekezo ya CCM? Lissu ameonekana anafaa kwa sababu anasimamia utawala wa sheria na siyo kwa sababu ni mbunge wa chadema.jiongeze bwanamdogo
 
Hao viongozi wetu Wa Dini wamekiuka hata viapo vyao ktk imani ya kuhubiri haki na badala yake wanahubiri AMANI badala ya kuhubiri haki, mid nakwamboeni watanzania wenzangu kabla ya mabadiliko ya kweli tutaona mengi
 
Viongozi wadini wamekuwa waoga saana,sijui wengi hawako safi? Hata ibada ya ndoa ilipoingiliwa walikaa kimya,waumini wao tunatupwa jela kwa uonevu wanakaa kimya,ubaguzi unahubiriwa waziwazi mfano kusema wapinzani hawatatia mguu kwenye serikali yake huku akisema hataki wanasiasa anataka watendaji lakini viongozi hawa hawakemei...kwakweli inatia mashaka kuona mhalifu alofoji mavyeti akiombewa makanisani na mashekhe kwanguvu zote!! Ajabu Sana.
Moja ya makundi ambayo nimeyadharau sana na sitokaa niyaheshimu ni hawa viongozi wa dini, hawa sijui hata kama wanaelewa nini msingi wa hizi imani za kidini!
 
Na viongozi wa sirikali bado hawajagundua sababu gani inayosababisha kila kesi inayofunguliwa na sirikali,sirikali lazima igaragazwe mahakamani.
Jibu ni kuwa huenda mawakili wa serikali wanaona mambo mengine ni ya kionevu
 
Moja ya makundi ambayo nimeyadharau sana na sitokaa niyaheshimu ni hawa viongozi wa dini, hawa sijui hata kama wanaelewa nini msingi wa hizi imani za kidini!
hawa wengiwao Ni ma fa fa fa!! Tusiwatarajie sana kwenye kukemea ujinga...Rc wamesoma ila wanamtetea mtu wao kijinga
 
Viongozi wadini wamekuwa waoga saana,sijui wengi hawako safi? Hata ibada ya ndoa ilipoingiliwa walikaa kimya,waumini wao tunatupwa jela kwa uonevu wanakaa kimya,ubaguzi unahubiriwa waziwazi mfano kusema wapinzani hawatatia mguu kwenye serikali yake huku akisema hataki wanasiasa anataka watendaji lakini viongozi hawa hawakemei...kwakweli inatia mashaka kuona mhalifu alofoji mavyeti akiombewa makanisani na mashekhe kwanguvu zote!! Ajabu Sana.
Hao viongozi wa dini hukimbilia kusoma mstari mmoja tu "heshimuni mamlaka......."
Wanataja imeandikwa na nani ipo sura ya ngapi na mstari wa ngapi! KWISHA KAZI.
 
Back
Top Bottom