Waraka mahususi kwa viongozi wa dini wa Tanzania: Kuweni macho na wanasiasa wenzangu, Msigwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka mahususi kwa viongozi wa dini wa Tanzania: Kuweni macho na wanasiasa wenzangu, Msigwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Peter Msigwa, Dec 22, 2011.

 1. Peter Msigwa

  Peter Msigwa Verified User

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 24, 2007
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI

  Salaam za X-Mas na Mwaka Mpya za Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema)


  Waraka mahususi kwaviongozi wa dini wa Tanzania:
  Kuweni macho nawanasiasa wenzangu


  Ndugu Wanahabari,

  Kwa nafasi yangu kamaraia, Mbunge ninayewakilisha wananchi wa Jimbo la Iringa Mjini naWatanzania wote kwa ujumla na mmoja wa viongozi wa dini/dhehebunchini, naomba kutumia fursa yenu na ya vyombo vyenu vya habari kutoaujumbe mahususi kwa viongozi wenzangu wa kidini kwa manufaa ya taifaletu.

  Ninapowasilisha salaam zangu hizi za X-Mas na Mwaka mpya wa 2012, ningependakusisitiza yafuatayo kwa viongozi wenzangu wa dini, kuhusiana na ninihasa unapaswa kuwa wajibu wetu kuhusiana na mwenendo wa viongozi wetuwa kisiasa (mimi pia nikiwa mmoja wao);

  Nianze kwa kuwapongeza viongozi wenzangu wote wa dini waliojitokeza hadharani au kupitia vyombo vya habari hivi karibuni kupinga kusudio au mpango wa kuongeza posho za vikao kwa wabunge. Suala la malipo ya posho za vikao (Sitting allowance) kwa wabunge na watumishi wa umma pamoja na mpango wa kuongeza posho hizo kutoka sh 70,000 hadi sh 200,000 (kwa siku ya kikao), kama ulivyotangazwa na Mhe. Spika wa Bunge, Anne Makinda, hivi karibuni, limegusa hisia za Watanzania wengi wakiwemo viongozi wenzangu wa dini ambao naungana nao kuzipinga nikisisitiza msimamo wa siku nyingi wa chama chetu (Chadema).


  Pongezi hizi zinazingatia ukweli kuwa katika suala hili la posho, Baadhi ya viongozi wa dini wameweza kuchukua wajibu wao kikamilifu wa kuwa juu ya wanasiasa wenye malengo mabaya tofauti na desturi iliyoanza kujengeka hivi karibuni ya baadhi ya wanasiasa hususan wale wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupenda kuwatumia vibaya baadhi ya viongozi wa dini na nyumba za ibada kama sabuni ya kujisafishia uchafu wao na ngazi ya kufikia malengo ya kuutafuta urais au ubunge na udiwani (uongozi mchafu). Ingawa kanisa ni mahali pa kusafishwa uchafu na kila mtu anakaribishwa, lakini tumkumbuke yule Simon Mchawi katika kitabu cha matendo ya mitume, aliyejaribu kununua kipawa cha Roho mtakatifukwa faida yake binafsi, Ndipo mtumishi wa Mungu Petro alipomwambia apotelee mbali pamoja na pesa yake.


  Nawasihi viongozi wa dini wenzangu kwamba kamwe tusikubali kuwa mawakala wa kufanikisha mbio za urais mchafu. Tusikubali kuwa chini ya wanasiasa maana jukumu letu la kuwanusuru wanadamu kiroho kwa kuwaongoza kumcha Mungu, ni jukumu zito na kubwa kuliko uroho wa madaraka unaowakimbiza baadhi ya wanasiasa kwenye nyumba za ibada.


  Ni udhalilishaji mkubwa wa huduma ya kiroho pale viongozi wa dini tunapowakaribisha wanasiasa kufanya shughuli kama za uzinduzi wa makanisa au albamu za nyimbo za kidini kana kwamba wao ndio wenye upako, utukufu na mamlaka zaidi ya kubariki kinachozinduliwa kuliko sisi viongozi wa dini wenyewe.


  Tabia kama hii ya kuwatanguliza mbele wanasiasa kwenye shughuli za kiroho badala ya kuacha huduma hii ijitegemee yenyewe (maana Mungu ni Mkuu na mwenye uwezo kuliko siasa), kwa namna moja au nyingine imekuwa ndio kichocheo cha kufanya wanasiasa kutafuta pesa kwa gharama yoyote, ilimradi wakiitwa kwenye mialiko hiyo waweze kutoa fungu kubwa wakiamini itawajenga kisiasa hata kama hawana nia ya kweli na Mungu.


  Tusikubali kamwe kutumiwa vibaya na wanasiasa wanaojipenyeza kwenye matukio mbalimbali kama ya harambee na uzinduzi wa albamu za nyimbo za kiinjili, kwa lengo la kujitangaza, kujisafisha na kujipendekeza kwa umma uliowakataa au kukosa imani nao.


  Tusikubali nyumba takatifu za ibada zigeuzwe viwanja vya kampeni za kisiasa na wala tusiwe chanzo cha kuiingiza nchi yetu katika mgawanyiko na machafuko ya kidini kwasababu tu ya kuwabeba baadhi ya wanasiasa ambao ama kwa sababu ya uchafu wao au umma kukosa imani nao, wameona hawawezi tena kuwa na uhalali wa kujitangaza wala kujijenga tena kwenye majukwaa ya kisiasa bila kwanza kukimbilia makanisani. Binafsi naamini, mwanasiasa msafi anayejiamini na anayemcha Mungu kwelikweli haitaji harambee au tukio lolote la kujinadi kanisani , maana huko si pahali pake.


  Najua kuwa Watanzania wengi wanakerwa na tabia ya baadhi ya sisi viongozi wa dini kama maaskofu, wachungaji na mapadri kubabaikia wanasiasa kwa kiasi cha kuonekana wanaidhalilisha huduma hii kuu. Kanisa likitakiwa kuzinduliwa – mwanasiasa, uzinduzi wa nyimbo ya injili – mwanasiasa, ununuzi wa magitaa – mwanasiasa, ununuzi wa maspika – mwanasiasa. Hivi hawa wanasiasa wana upako gani kana kwamba kazi ya Mungu haiwezi kufanyika bila wao?


  Tunapokwenda kusherehekea siku kuu hii ya X Mas na Mwaka Mpya, ninawasihi tena viongozi wenzangu wa kidini, kwamba tumkumbuke nabii Baalam ambaye vitabu vitakatifu vinaeleza jinsi alivyoifanyia biashara huduma yake ya kinabii mpaka alisababisha Punda aongee;

  Tumkumbuke mtumishi wa nabii Elisha, aliyeitwa Gehazi, ambaye vitabu vitakatifu vinatufundisha kwamba alipenda pesa na zawadi akasahau mwito wake wa kitume mpaka ukoma wa Nahaman ukahamia mwilini mwake.

  Tumkumbuke Esau aliyeuza haki ya uzaliwa wake wa kwanza kwa njaa ya muda mfupi (dengu, mlo moja tu). Na tumkumbuke Yuda Eskarioti ambaye alimuuza mwokozi wetu, Yesu Kristu, kwa vipande thelathini vya fedha, na kwa hiyo, sisi viongozi wa dini tusikubali kamwe kuwauza Watanzania wenzetu kwa pesa za wanasiasa wachafu.


  Nasisitiza tena, kwamba sisi viongozi wa dini tunapaswa kuwa viongozi na sio wafuasi wa wanasiasa, tunapaswa kuwaonyesha njia wanadamu wote wakiwemo wanasiasa na sio wanasiasa watuonyeshe njia sisi, maana kufanya hivyo ni kulishusha thamani neno la Mungu.


  Naamini kama taifa kwa ujumla tuna hali za duni za kimaisha zinazotugusa pia sisi viongozi wa kiroho, lakini hii isisababishe tukasahau misingi yetu ya kitume kana kwamba Mungu aliyetuita ametuacha. Naamini sisi viongozi wa dini tukisimama imara bila kuyumba, Tanzania yetu inayougua umaskini, ujinga, maradhi na ufisadi, hatimaye itaponywa. Hizi ndio salamu zangu za mwaka mpya kwa viongozi wa dini ambao naamini kupitia wao Watanzania wote wataongozwa vema


  Nawatakia kheri na fanaka ya X- Mas na Mwaka Mpya.  Mungu ibariki Tanzania
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Roho ya tamaa ya fedha imewaingia viongozi wetu wa dini...Wamepofushwa macho...
   
 3. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  haya mambo hata mimi muumini huwa siyapendi sema ndio hivyo nitalalamikia wapi tunabaki tunayaongea vijiweni, wenye imani finyu ndio hivyo kila siku wanahama makanisa
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  Haya makanisa yanajidhalilisha sana. Hivi katika mamilioni ya wakatoliki wanashindwa kumpata mmoja wa kuendesha harambee yao Mwanza hadi wanakwenda kumpigia magoti mlutheri Lowasa? viongozi wetu wa dini wa zama hizi hawana tofauti na huyo mchawi aliyetaka kuunua kipawa cha roho mtakatifu.
   
 5. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nadhani kabla ya mualiko huwa kuna MAELEWANO ya baadae yenye mlengo wa kimanufaa (si taasisi zote za kidini), hivyo ucha Mungu unatoweka na wenye nacho ndio wanaong'ara. Si Lowassa tu, ni wengi wa wanasiasa wanatumia taasisi za dini kwa maslahi yao kisiasa. Nchi hii imekuwa ni mithili ya 'dampo', waila hongera mchungaji kwa kunena kwa vitendo juu ya khulka hii inayoshamiri.

  IKUMBUKWE: Makanisa ni kama yanashindana vile (am sori kwa hili) katika upanuaji wa huduma zao kiroho, na waumini si wazuri sana mifukoni kulinganisha na wanasiasa. Ndio maana makanisa ya tangu ukoloni nayo yameingia katika kujiimarisha ili yasimezwe na utitiri wa makanisa ya MANABII & MITUME wa kisasa.

  Mwenye macho...
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mchungaji Msigwa ahsante kwa ujumbe mzito wa kufungia mwaka.

  Viongozi wa kidini ambao wanaaminiwa sana na waumini wao na wananchi kwa ujumla, wamekuwa wakitumikia wanasiasa.

  Na bahati mbaya sana hii tabia ya watumishi wa Mungu kuwatumikia wanasiasa imezidi kujikita siku za hivi karibuni. Na wanasiasa wanaoonekana kuyatumia madhehebu ya dini ni wale wenye kashfa za rushwa na ufisadi. Ni bahati mbaya sana kwamba watumishi wa Mungu wamekumbwa na upepo wa "kisuli suli" cha siasa chafu na wamekubali kusombwa bila kujitambua.
   
 7. c

  comte JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 844
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 80
  baba mchungaji, mheshimiwa mbunge , raia, na mwana wa adamu mwenzangu MSIGWA,

  KWANINI UMEACHAKUTUSAIDIA KUPATA MAISHA YA MILELE UNATUTAFUTIA MAISHA BORA
   
 8. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Pale CHADEMA hakuna siasa za unafiki, asante Mch Msigwa, G. Lema bado tunasubiri nyingine.
   
 9. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Asante Mch Msigwa kwa ujumbe, mwenye masikio na asikie neno ambalo litasaidia kusafisha kanisa na kirusi cha wanasiasa wanaotafuta uongozi makanisani. Mungu akupiganie
   
 10. Nkwesa Makambo

  Nkwesa Makambo JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 4,765
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mmoja wa watu wanaokerwa na mambo yanavyoenda makanisani,issue huwa ni kupata fedha hawajali hata mantiki ya jambo wanalotaka kufanya, hii ndiyo inasababisha kuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili baada ya kanisa kujiingiza miguu yote miwili kwenye ujasiarimali usio na harufu ya KIROHO zaidi ya kuwinda mambo ya kidunia.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Habari murua kabisa. Kwa wenye mapenzi mema na uelewa mpana ni kwamba sikio lao la tatu tayari limekusikia na tayari kuyazingatia tunapoingia mwaka mya 2012.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 12. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Ujumbe mzito sana kwa mchungaji.Nimeupitisha 100%
   
 13. I

  Ismaily JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana Mh msigwa,viongozi wa dini wamekuwa wakitumika na wanasiasa na kusababisha imani za watu kuonekana zimebase kwenye mali au kujipatia utajiri badala zibase kwenye maadili na imani ya ukweli na matendo mema..
   
 14. J

  JABEZ Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kama vile Msigwa ulikwa moyoni mwangu: naichukia sana hii tabia ya kanisa kupenda kuwaalika viongozi wa siasa kwenye shughuli za kiroho. Na X-Masi inakuja, utasikia...Waziri...kawaasa ....wakati akihutubia kwenye ibada ya XMasi! Lakini, hata wenzetu wa ISLAM, nao utasikia mgeni rasmi wa Idd ni Rais, Makamu wa Rais n.k. Hapa Mchungaji Msigwa umeonesha uongozi: siasa ikae kivyake na dini kivyake!
   
 15. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  KANISA HALIWEZI KUJITENGA NA SIASA KWA AJILI YA FAIDA YA JAMII.

  I agree that religion and politics, to a certain degree, should be separated, but only as far as the day-to-day running of the government is concerned. Religion, however, can't close its eyes, ears or mouth to injustice and corruption. It can and must be a critic to bad governance and injustice. It has to be the conscience to a government that has no conscience

  Kwani hao wanasiasa wanajipendekeza au wanaalikwa? UTAWEZAJE KUKEMEA MAOVU KTK JAMII KAMA UTAWATENGA WANASIASA? Hata hivo yesu alikuwa anakula na wenye dhambi walimdhihaki sana mfano mzuri alipoenda nyumbani kwa Zakayo, Kuwaita hao viongozi ni njia nzuri ya kuwaweka karibu na kanisa ili wajibadili tabia zao.

  Angekuwa kweli mtumishi wa Mungu asingethubutu kuwapinga wenzao wanaowaalika. Hivi anachunga kondoo gani bungeni? Namwona sawa na wale mafarisayo wanavaa mavazi meupe na kusali sala ndefu huku wakikaa viti vya mbele kabisa ktk masunagogi huku wakijiona ni wema kuliko wengine.
   
 16. Luther3

  Luther3 Member

  #16
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We una2mia masabuli kufikiri .mchungaji kanena.labda ume2mwa umtetee.kaz kwako.umma umeshajua hao n wachafu 2.n sawa na kaniki rangi yake haitabadilika
   
 17. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Bora umefunguka kuhusu hilo coz hata mimi linaniboa sana. Pale dini zote mbili zinapo geuka mitaji ya ccm.
   
 18. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  Bado wabongo ni waoga, mchungaji si awaandikie covering letter makanisa aliyoyalenga kuliko kurusha mawe hewani wakati wahusika hawafiki kumi?
  Kila mtu atakwepa na kujifanya waraka haumuhusu, bado ni Dr. Slaa ndio amethubutu na kuweza kuwataja watu kwa majina yao na taasisi zao.
  Pia mchungaji ameshaingia ktk politike ajitoe ktk dini manake kama waraka huu ndio salaam ya xmass basi anaowachunga are in trouble, ngoja salaam za Pengo utaona tofauti.
   
 19. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mwenye masikio ya kusikia na asikie....
   
 20. J

  Jadi JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,402
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  si useme tu EL anaongoza!
   
Loading...